Subaru Forester Vs Mazda CX5

Subaru Forester Vs Mazda CX5

Mwezi ujao nataka nihame kwenye Carina Ti na mimi niwe mtu mwenye gari kweli .

Subaru legacy 2015 na subaru forester 2013 hipi itakua nzuri zaidi bei zina tofautiana kwa 3 million
Zote ziko poa ila hapo umefanya comparison ya sedan na SUV vitu viwili vyenye ladha tofauti kabisa
 
Mwezi ujao nataka nihame kwenye Carina Ti na mimi niwe mtu mwenye gari kweli .

Subaru legacy 2015 na subaru forester 2013 hipi itakua nzuri zaidi bei zina tofautiana kwa 3 million
Legacy ni kama Carina TI Tu bado ni gari za chini, sioni sababu ya kutoka kwenye salon na kuingia kwenye salon .... chukua forester 2013
 
Fafanua kidogo hapa mkuu? Ford wanamiliki Mazda au vice versa, au wanashare technology, engine, etc???
Ford walikua na uhusiano na Mazda kwa miaka 40 ambayo walisitisha mwaka 2015 na kubaki na 1/3 ya umiliki na Mazda ila sasa hivi wapo na share na Toyota kwenye Engine na Technology mpya kwa Mazda za miaka ya nyuma Engine na parts zilikua sawa na Ford..
 
Ford walikua na uhusiano na Mazda kwa miaka 40 ambayo walisitisha mwaka 2015 na kubaki na 1/3 ya umiliki na Mazda ila sasa hivi wapo na share na Toyota kwenye Engine na Technology mpya kwa Mazda za miaka ya nyuma Engine na parts zilikua sawa na Ford..
Upo sahihi, na yalikua yanapata kutu sana. Ila sasa Mazda na SkyActiv engine yake ameachana kabisa na Ford.
 
Mkuu hili la matumizi ya mafuta...

Huwa inasemwa na nakubali, kuwa matumizi ya mafuta kwenye gari inategemea vitu vingi...

Ila Kwa navyofaham...Subaru Forester (turbo au non turbo), ikijitahidi Sana sana itaenda 08km/ltr wakati Mazda CX 5 ikijitahidi Sana itaenda 10km/ltr.

Huu ni uzoefu wangu mdogo...naweza kurekebishwa
Subaru ukiacha speaker pia ni jini Kwa kubugia mafuta
 
Matumizi ya mafuta, MAZDA
CX5 nyingi ni Diesel
Who said this. Unajifunza fanya review?? Weka data za petrol na diesel na sio kuandika et nyingi ni diesel

Unajua muagizaji ataagiza ipi? ..ku compare fuel consumption kwa engine za mafuta tofauti si sawa,, Kuna RAV4 za diesel ndo compare na hio mazda
 
Being ndio tatizo, hizi za 2017 zina bei iubwa kidogo. Sa chini ya hapo zina matatizo ya DPFkama zilivyo gari nyingi za Diesel za miaka ya karibuni, hasa kwa mazingira yetu ya bongo ambako diesel ni low quality, inaccurate shida nyingine ya ndogo ndogo ila ukizitibu gari inadumu. Inataka service kwa wakati na kutumia oil sahihi
Hata mafuta yetu zinavumilia? hasa diesel?
 
Hii ndio habari ya mjini Kwa wale wapenda magari mazuri

Hizi ni gari shindani kwa sababu zote zipo kundi moja la COMPACT SUV.

Zinafanana sifa katika utendaji kama vile:

1. Ukubwa wa umbo
2. Nafasi kubwa ndani
3. Ground clearance nzuri
4. Nguvu ya kutosha kustahimili
changamoto za barabara
ngumu

Baadhi ya Tofauti ambazo zinaweza kukusaidia kuchagua kati ya SUBARU FORESTER na MAZDA CX5 ni kama vile:
1. Muonekano, macho
yanatofautiana kila mtu ana
Upendeleo binafsi kati ya
Muonekano wa FORESTER na
MAZDA CX5

2. Matumizi ya mafuta, MAZDA
CX5 nyingi ni Diesel na
zinakwenda mpaka 18KM/L
wakati FORESTER ni Petrol na
zinakwenda 14KM/L. Kuhusu
utofauti wa injini ya Petrol na
Diesel unaweza kurejea somo
hilo lipo humu

3. Upatikanaji wa vifaa na
mafundi, Japo gari zote hazipo
kwa wingi sana, lakini subaru
ipo kwa wingi na hata vifaa ni
vingi na mafundi wapo wengi
pia kulinganisha na MAZDA
CX5

4. MAZDA CX5 zilizo nyingi ni
Non-Turbo lakini zinakuwa na
nguvu kubwa kuliko
FORESTER NON-TURBO (XS)
FORESTER XT inazalisha
nguvu kubwa zaidi kuliko
MAZDA NON-TURBO. Lakini
MAZDA CX5 TURBO inazalisha
nguvu kubwa kuizidi kidogo
FORESTER TURBO (XT)

5. Bajeti, MAZDA CX5 bajeti yake
ni kuanzia TSH 27M mpaka
TSH 30M wakati FORESTER
NEW MODEL zinaanzia TSH
25M mpaka TSH 28M lakini
pia FORESTER OLD MODEL
bajeti ni chini zaidi.

Bila shaka maelezo haya yanajitosheleza kukuwezesha kufanya Uchaguzi sahihi.

View attachment 2789002View attachment 2789003
Mwaka huu ukiniendea vizuri nataka nichukue mazda cx5
 
Inawezekana kabisa ikawa yote mawili. Pamoja na ukweli kwamba zina engine za diesel efficient sana (zina power na zinanusa tu mafuta), ni engine zinahitaji uweke diesel safi na oil sahihi tena kwa wakati.
Tatizo linaanza hapa bongo Diesel hata unayonunua kituo kizuri aje inakuja tayari ikiwa na sulfur ya kutosha, DPF inaziba na usipotibu kwa wakati unaua turbo na hata head kabisa.
Pia zinakuja n mfumo wa upoozaji ambao inashauriwa gari ikifika ubadili coolant junction/bypass uweke ya metal badala ya plastic.

Kupenda vya rahisi (ambalo si kosa) inapelekea watu mara kadhaa kununua gari toka nje zikiwa zishaanza kudevelop hata matatizo.

Kwa kifupi kama unaitaka hii ya diesel, zingatia hayo au la huwezi, tafuta ya petrol
Nchi nyingi sana za ulaya na Asia zimepiga marufuku kabisa matumizi ya magari ya diesel kwasasa, though magari makubwa bado yanatumia since & since
 
Back
Top Bottom