Sifa za gari nzuri:
1. Ikidhi mahitaji yako
- mfano kama weye ni mkulima na unaenda kweye mashamba kupitia kwenye bara bara mbaya na mitope, 4xWD is a must.
- Kama weye ni mfugaji unapeleka mapumba kila siku shambani, ya nini ununue gari iliyofunikwa halafu uanze kukodi gari kufanya kazi zako.
- Kama unakaa 20km+ kutoka ofisini kwako hadi nyumbani na hii ni gari ya kuendea kazini cc 3000 za nini?????
2. Iendane na uwezo wako
Kununua gari sio shida sana. Unaweza kuvuta mkwanja benki ukanunua gari na kuendelea kurudisha kila mwezi mwajiri akicheka. swali ni je, utaweza kulipa hiyo monthly bila kuadhiri matumizi mengine - chakula, mavazi, karo za watoto? au ndo utaamua wande kwa kayumba alimradi weye barabarani kila mtu anageukia gari yako?
3. Garama ya spea: nadhani sio issue ya kuangalia juu juu hapa hapa. Kwa mtazamo wangu, angalia rate of consumption of spares vs price yake.
nakupa mfano kimahesabu kulinganisha gari X na Gari Y kwenye spear "S"
Ukichunguza vizuri jedwali hapa chini utaona kuwa aliyenunua Gari X atabadilisha spear "S" mara 2 tu ndani ya miezi 36 (miaka 3) na itamgarimu jumla ya 10,000 ila atatoa 5,000 kununua spea hiyo dhidi ya 2,000 ya yule wa gari Y ambaye atatoa hiyo kila miezi miwili lakini atatumia 36,000 mwisho wa kipindi cha miaka 3.
[TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]
Gari X
[/TD]
[TD]
Gari Y
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Bei ya Spea "S"
[/TD]
[TD="align: right"]
5,000
[/TD]
[TD="align: right"]
2,000
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Spea hubadilishwa kila miezi mingapi?
[/TD]
[TD="align: right"]
18
[/TD]
[TD="align: right"]
2
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Matumizi ya spear kwenye miaka 3
[/TD]
[TD="align: right"]
10,000
[/TD]
[TD="align: right"]
36,000
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]