Suala linalonipa ukakasi, hii Mimba alidhamiria kuitoa au ni mpango wa Mungu?

Mimba ya umri gani??
Ulimkuta kwenye status gani??anableed or hapana??
Sijawahi skia flagyl zinatoa mimba nachojua zinazuia mimba ngj wakuu waje watujuze zaidi
Mwezi Na Siku Kadhaa, Yeah Kabla Kushika Ujauzito alikua anapata Siku Zake Kama Kawaida
 
Habari za kushinda wakuu,

Poleni na hongereni pia kwa majukumu. Nipo hapa leo kuhitaji ushauri kutoka kwenu maana naona mwenyewe hili kama linanizidi, nina huyu mchumba angu ambae niko nae kwa mda kidogo, ila kazi ilitutenganisha na mimi nilihamishwa kituo cha kazi, mkoa mwengine, so tulipotezana kwa kipindi flani, ila bahati nzuri nimerudishwa tena kituo changu cha kazi.

Bila hiyana nilimtafuta, tuliongea mengi sana, kwa kweli sie yule nilimuacha, ameokoka, hanywi pombe, sio yule niliekua nikienda nae madisco kwa kipindi kile, basi baada ya mda tukajikuta tumerudi upya kwenye mahusiano, tulikua tunakutana ( sijui hii kidini imekaaje) niwe mkweli hatukua tukitumia kinga.

Basi akanipa taarifa kua haelewi siku zake, nikamshauri akapime, kweli akagagundulika ni mjamzito, nikapokea kwa mikono miwili, basi maisha yakaendelea, ingawa mimi sikuwaambia nyumbani.

Vituko vikaanza, mara anune bila sababu, mdogo wangu anaongea nae vizuri, ila nikirudi mimi ni kimya, tukienda kazini asubuhi atakaa kimya hadi namshusha kituo chake, na hata nikimuongelesha, ujibuji wake ni tofauti.

Nikajipa moyo kwa vile nasikia wajawazito wako hivyo, haikunisumbua, ni kweli mi ni mnywaji labda anakereka, ila unywaji wangu ni wa kujiburudisha mimi na sio kero kwa wengine, akaanza kulalamika tumbo linamuuma linamuuma linaacha, linaweza likamuuma usiku asubuhi akawa vizuri, leo nimeamka nimejiandaa kwenda kazini, ananiambia hajisikii vizuri, so hatoenda kazini, basi mi nikaondoka zangu,

Jioni narudi napokelewa na kilio, ila sioni kama ni kutoka moyoni, ananiambia mimba imetoka kwa bahati mbaya, kumbe wakati tumbo linaanza kumsumbua, alimeza flagyl, walimshauri rafiki zake huko ofisini, ingawa mimi hakuniambia, ni mengi tu ingawa nimeshindwa kuyaandika yote hapa,

Suala linalonipa ukakasi, hii mmba alidhamiria kuitoa au ni mpango wa mungu?

Namuangalia hapa hata simmalizi, hapa bila shaka ni sehemu sahihi, hebu naombeni ushauri wenu kwenye hili, amenipa wakati mgumu kweli

Nb: samahani kwa uandishi wangu, hapo nimejitahidi sana

Mkuu kwanza pole kwa yote lakin kabla hujajiuliza mengi nadhan ni bora uanze kufanya uchunguzi ujue kunani...wahenga walisema ni bora kulia leo badala ya kesho
 
Mwezi Na Siku Kadhaa, Yeah Kabla Kushika Ujauzito alikua anapata Siku Zake Kama Kawaida

Nilimaanisha wakati anakupa taarifa ya mimba kutoka alikuwa kwenye status gani??

Ulimwacha nyumbani jioni mimba imetoka alisafishwa hospitali or alitumia dawa if ues ni dawa zipi na kwa maelekezo ya nani?!

Ulimuuliza y hakukupigia alipojiskia tofauti (maumivu ya tumbo) or alishtukia tu imetoka

Njoo ukazie

Cc Kingsmann
 
Dawa Alimeza Jana Yake, Kama Nilivyoelezea Hapo Juu, Na Mimi Nilipofika Kazini, Nilimjulia hali na Alinijibu, Anaendelea Vizuri, Taarifa Za Mimba kutoka Amenipa Jioni baada Ya Mimi Kurudi Kutoka Kazini, Kwamba ameshtuka tu na Kuona Damu Zinamtoka
 
Alafu akafanyeje baada ya kuona damu??
Me nahisi nimchezomchafu umechezewa either mimba haikuwa yako or ni yako lkn hakua teyari kuwa mama
 
mtoa maada anatakiwa atuambie hyo mimba ilikuwa ya miez mingap!!
 
Umeshasema 'alimeza flagyl alishauriwa na wenzie'.. Mbona tayari jibu unalo mkuu..!?

Btw, Subiri apone kabisa mkae chini akuambie hasa sababu ya yeye kufanya hivyo, kumchukia siyo suluhisho la tatizo ukizingatia imeshatokea iwe bahati mbaya ama kwa kudhamiria, la muhimu wewe mkumbushe tu kutubu.!!

NB; Kukutana kimwili kabla ya ndoa haimpendezi Muumba ni kupotoka kwetu tu wana wa Adam.!!
Aliekwambia Flagyl zinatoa mimba nani??
 
Habari za kushinda wakuu,

Poleni na hongereni pia kwa majukumu. Nipo hapa leo kuhitaji ushauri kutoka kwenu maana naona mwenyewe hili kama linanizidi, nina huyu mchumba angu ambae niko nae kwa mda kidogo, ila kazi ilitutenganisha na mimi nilihamishwa kituo cha kazi, mkoa mwengine, so tulipotezana kwa kipindi flani, ila bahati nzuri nimerudishwa tena kituo changu cha kazi.

Bila hiyana nilimtafuta, tuliongea mengi sana, kwa kweli sie yule nilimuacha, ameokoka, hanywi pombe, sio yule niliekua nikienda nae madisco kwa kipindi kile, basi baada ya mda tukajikuta tumerudi upya kwenye mahusiano, tulikua tunakutana ( sijui hii kidini imekaaje) niwe mkweli hatukua tukitumia kinga.

Basi akanipa taarifa kua haelewi siku zake, nikamshauri akapime, kweli akagagundulika ni mjamzito, nikapokea kwa mikono miwili, basi maisha yakaendelea, ingawa mimi sikuwaambia nyumbani.

Vituko vikaanza, mara anune bila sababu, mdogo wangu anaongea nae vizuri, ila nikirudi mimi ni kimya, tukienda kazini asubuhi atakaa kimya hadi namshusha kituo chake, na hata nikimuongelesha, ujibuji wake ni tofauti.

Nikajipa moyo kwa vile nasikia wajawazito wako hivyo, haikunisumbua, ni kweli mi ni mnywaji labda anakereka, ila unywaji wangu ni wa kujiburudisha mimi na sio kero kwa wengine, akaanza kulalamika tumbo linamuuma linamuuma linaacha, linaweza likamuuma usiku asubuhi akawa vizuri, leo nimeamka nimejiandaa kwenda kazini, ananiambia hajisikii vizuri, so hatoenda kazini, basi mi nikaondoka zangu,

Jioni narudi napokelewa na kilio, ila sioni kama ni kutoka moyoni, ananiambia mimba imetoka kwa bahati mbaya, kumbe wakati tumbo linaanza kumsumbua, alimeza flagyl, walimshauri rafiki zake huko ofisini, ingawa mimi hakuniambia, ni mengi tu ingawa nimeshindwa kuyaandika yote hapa,

Suala linalonipa ukakasi, hii mmba alidhamiria kuitoa au ni mpango wa mungu?

Namuangalia hapa hata simmalizi, hapa bila shaka ni sehemu sahihi, hebu naombeni ushauri wenu kwenye hili, amenipa wakati mgumu kweli

Nb: samahani kwa uandishi wangu, hapo nimejitahidi sana
Mkuu kanywe tu Beer utapata majibu ya nini cha kufanya, kuna muda Beer zinasaidia sana kuleta maamuzi ya busara
 
Hapo tumia akili ya kiume. Huwezi badilisha yaliyopita. Kwani uwezo wako wa kudunga mimba umeisha? Jifanye mjinga siku ipite. Mpe wazo la kumdunga nyingine usikie..

Ndo utajua mbivu na mbichi.

Tuliza akili, katoa mimba tu unapagawa hivi, je akikutema si utajinyonga, au uambiwe kachumbiwa. Jifunze kuwa na roho ngumu. Hawa Viumbe usiwaamini saaanaaa...

Fwata huu ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom