Suala linalonipa ukakasi, hii Mimba alidhamiria kuitoa au ni mpango wa Mungu?

MTINGIJOLI

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
1,344
1,293
Habari za kushinda wakuu,

Poleni na hongereni pia kwa majukumu. Nipo hapa leo kuhitaji ushauri kutoka kwenu maana naona mwenyewe hili kama linanizidi, nina huyu mchumba angu ambae niko nae kwa mda kidogo, ila kazi ilitutenganisha na mimi nilihamishwa kituo cha kazi, mkoa mwengine, so tulipotezana kwa kipindi flani, ila bahati nzuri nimerudishwa tena kituo changu cha kazi.

Bila hiyana nilimtafuta, tuliongea mengi sana, kwa kweli sie yule nilimuacha, ameokoka, hanywi pombe, sio yule niliekua nikienda nae madisco kwa kipindi kile, basi baada ya mda tukajikuta tumerudi upya kwenye mahusiano, tulikua tunakutana ( sijui hii kidini imekaaje) niwe mkweli hatukua tukitumia kinga.

Basi akanipa taarifa kua haelewi siku zake, nikamshauri akapime, kweli akagagundulika ni mjamzito, nikapokea kwa mikono miwili, basi maisha yakaendelea, ingawa mimi sikuwaambia nyumbani.

Vituko vikaanza, mara anune bila sababu, mdogo wangu anaongea nae vizuri, ila nikirudi mimi ni kimya, tukienda kazini asubuhi atakaa kimya hadi namshusha kituo chake, na hata nikimuongelesha, ujibuji wake ni tofauti.

Nikajipa moyo kwa vile nasikia wajawazito wako hivyo, haikunisumbua, ni kweli mi ni mnywaji labda anakereka, ila unywaji wangu ni wa kujiburudisha mimi na sio kero kwa wengine, akaanza kulalamika tumbo linamuuma linamuuma linaacha, linaweza likamuuma usiku asubuhi akawa vizuri, leo nimeamka nimejiandaa kwenda kazini, ananiambia hajisikii vizuri, so hatoenda kazini, basi mi nikaondoka zangu,

Jioni narudi napokelewa na kilio, ila sioni kama ni kutoka moyoni, ananiambia mimba imetoka kwa bahati mbaya, kumbe wakati tumbo linaanza kumsumbua, alimeza flagyl, walimshauri rafiki zake huko ofisini, ingawa mimi hakuniambia, ni mengi tu ingawa nimeshindwa kuyaandika yote hapa,

Suala linalonipa ukakasi, hii mmba alidhamiria kuitoa au ni mpango wa mungu?

Namuangalia hapa hata simmalizi, hapa bila shaka ni sehemu sahihi, hebu naombeni ushauri wenu kwenye hili, amenipa wakati mgumu kweli

Nb: samahani kwa uandishi wangu, hapo nimejitahidi sana
 
Haipaswi kuhukumu

Ila mjamziyo utakubalije kunywa flagyl wakati zinajulikana kwa kutoa mimba?????

Mhoji vizuri

Mkuu,kama ulivyoandika hupaswi kuhukumu

Inawezekana hakujua kama flagyl zinatoa mimba mana hata mie ndio nimejua hapa kumbe zinatoa
 
Hapo tumia akili ya kiume. Huwezi badilisha yaliyopita. Kwani uwezo wako wa kudunga mimba umeisha? Jifanye mjinga siku ipite. Mpe wazo la kumdunga nyingine usikie..

Ndo utajua mbivu na mbichi.

Tuliza akili, katoa mimba tu unapagawa hivi, je akikutema si utajinyonga, au uambiwe kachumbiwa. Jifunze kuwa na roho ngumu. Hawa Viumbe usiwaamini saaanaaa...
 
Umeshasema 'alimeza flagyl alishauriwa na wenzie'.. Mbona tayari jibu unalo mkuu..!?

Btw, Subiri apone kabisa mkae chini akuambie hasa sababu ya yeye kufanya hivyo, kumchukia siyo suluhisho la tatizo ukizingatia imeshatokea iwe bahati mbaya ama kwa kudhamiria, la muhimu wewe mkumbushe tu kutubu.!!

NB; Kukutana kimwili kabla ya ndoa haimpendezi Muumba ni kupotoka kwetu tu wana wa Adam.!!
 
Sasa hamuaminiani sie tutawasaidiaje ikiwa uaminifu ni nguzo ya mahusiano imara pia?
 
Usimhoji nikuhakikishie huwezi ujua ukweli cha zaidi utatengeneza hypohesis ambazo zitakuumiza. Tengeneza akili yako isahau lililotokea...

Akijiskia kusema atasema mwenyewe asiposema iwe sawa kwako.

Kikubwa ni kujua je, uhusiano unaendelea?

Moyo upofu huwezi jua aliwazalo mwenzio.
 
Dogo huo mzigo hukuweka wewe bali ulisaidiwa...

Binti kajiongeza kabla ishu haijabumbuluka...
 
Mi ndio mesikia leo flagyl inatoa mimba, pamoja na kuwa na mtoto tayar, nam huenda ningeumwa tumbo enz hizo na kushauriwa kunywa flagyl yawezekana ningekunywa, so usimuhukumu huenda hakujua. Japo kama mjanja ukiwa mjamzito kabla ya kunywa dawa yoyote atleast angegoogle
 
Nimekuja kujikuta siku hizi nawaogopa haswaa hawa Wadada wanaojifanya wa Kusali sana walio singo
 
Ninachohisi huyo dada hakupendi tena na kwako yupo kujikinga na mvua ikikatika anapita hivi ...Halafu nikuambie hiyo mimba kaitoa hana malengo na wewe kama ambavyo wewe huna malengo nae.
 
Ninachohisi huyo dada hakupendi tena na kwako yupo kujikinga na mvua ikikatika anapita hivi ...Halafu nikuambie hiyo mimba kaitoa hana malengo na wewe kama ambavyo wewe huna malengo nae.
Si Kweli kwamba Sina Malengo Nae
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom