Suala la zawadi katika mahusiano ya kimapenzi

Tamalisa

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,542
904
Hi all.

Jamani, hivi hili suala la kutoa/ kupewa zawadi na mwenzi wako wenzangu mnalionaje, najua hii inategemea zaidi na
hurka ya mtu binafsi. Lakini sio siri jamani most of girls wanapenda sana kujaliwa haswa kwa njia ya kupewa zawadi na wapenzi wao, wapo wengine nao wanamoyo wa kujitoa nao wanaonesha upendo kwa njia hii kwa wanaume wao,

Japo mara nyingi wanawake wanaona hili suala ni la mwanaume zaidi.sasa pale inapotokea mwanaume yeye hayuko cared kwa njia hii ya zawadi, (suprice ya zawadi), hata kama pipi kijiti ya sh. 100.

Kwa mwanamke ni tosha kabisa anaridhika zaidi hata ya kitandani. inakuaje jamani, unakuta unamwambia mpenzi mimi napenda zawadi na nafurahi sana na kukupenda zaidi nionapo unaniletea hata ndizi, apple, hereni, lakini unakuta respond yake ni ndogo kweli, unaweza kuta binti ni kawaida yake ila njemba hadi akumbushwe.

Kuna wanaume wengi wamepoteza wapenzi kwasababu ya hili, jamani kama masihala tu anatokea jamaa yupo cared kwa zawadi za kawaida tu, taratibu mwanamke anavutika na kukuacha umetoa macho. we jaribu tu kuchangamka mara unaenda kukutana nae beba ndizi mbivu au pipi kimtindo ukifika mpe, sio razima ununue gari, utanambia jinsi upendo utakavyomea.

"Tatizo wanaume mnaangalia sex tu, mwanamke ni zaidi ya sex, wenzangu kila siku wanalalama oh! bora ningempata kama wako oh sijui na nini, aa mara nitambwagwa mimi" wanawake wanateseka kitandani hawaridhiki hata hivi vingine hawapati. Mnaojijua badilikeni basi, muone wanawake watakayowafanyia zaidi ailete fimbo.
 
Dah... Huu pia ni ugonjwa wangu mwingine, unaweza kuniroga kwa haya makitu aisee!!
 
Kujali kwangu ni kihisia zaidi labda niseme sina mazoea ya kutegemea kupata kitu ili nione mtu ananijali.Hata akinijulia hali,hug,busu n.k ni kujali tosha! Naweza niseme ile thought ya kwamba mtu kakununulia kitu ni ishara kwamba alikuwa anakufikiria na huwa anakukumbuka!!!Ila walio wengi wanatumia nafasi hio kama njia ya kujipatia matakwa yao na hii inaenda bothways!!
 
Badala ya ku-concetrate kwenye mambo ya muhimu, eti nawaza nimpelekee Heaven Sent zawadi gani.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo wadada nao hawana appreciation kabisa. Kujua jinsi ya kum treat mwanamke ni bora nipoteze mda wangu kwa mambo mengine. Ukipata mwanamke anaye appreciate kwa kidogo unachompa umekula bingo...!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo wadada nao hawana appreciation kabisa. Kujua jinsi ya kum treat mwanamke ni bora nipoteze mda wangu kwa mambo mengine. Ukipata mwanamke anaye appreciate kwa kidogo unachompa umekula bingo...!

mkuu nikipeleka kama maua kama wanavyofanya wenzetu wa magharibi madada wa hapa si wataniona poyoyo,ila kwa kifupi sijajua caring ya madada zetu ni ipi unaweza ukafanya kila kitu kwake lakini ukaonekana mdebwedo
 
Kujali kwangu ni kihisia zaidi labda niseme sina mazoea ya kutegemea kupata kitu ili nione mtu ananijali.Hata akinijulia hali,hug,busu n.k ni kujali tosha! Naweza niseme ile thought ya kwamba mtu kakununulia kitu ni ishara kwamba alikuwa anakufikiria na huwa anakukumbuka!!!Ila walio wengi wanatumia nafasi hio kama njia ya kujipatia matakwa yao na hii inaenda bothways!!

umeongea pointi ambayo imenivutia kabisaa sijui nikupe zawadi gani?
 
Umeona eeh! Yaani kuna baadhi ya warembo hadi raha wanavyojua kuthamini mtu anapochukua muda wake kumtafutia zawadi nzuri katika tukio lolote lile maishani mwake au zawadi tu kwa kuonyesha mapenzi kwake.

Back
Top Bottom