Suala la TTCL na Airtel limeishia wapi?

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,975
6,448
Mtakumbuka wiki 2 zilizopita Mheshimiwa Rais alimuagiza Waziri wa Fedha, Bw. Mpango kuwa ashughulikie suala la Airtel na kuhakikishwa inarudishwa kwa shirika la TTCL kabla ya mwaka huu haujaisha.

Sasa yamebaki masaa tu mwaka kuisha, wenye kujua kinachoendelea watujuze jamani
 
Yalikuwa ni mazungumzo baada ya habari? Washauri wa mkuu wa kaya wamezembea kazi!
 
Nani hasa walikuwa ni wahusika wa hili sakata? Yaani mwenyekiti wa bodi kipindi hicho cha 05/08/2005 na hao wenzake wanne walikuwa ni akina nani? Naona walimtaja mmiliki wa hisa moja wa nje lakini ilipikuja kuwataja wabongo Omar Nundu akapotezea hiyo.
 
Wadau, heri ya mwaka mpya 2018.
Naomba msaada tutani; - Ni nani hawa waliokuwa kwenye bodi ya TTCl mwaka 2005? Bila shaka Mkapa Benjamin alikuwa rais wakati huo. Lakini hao board members walikuwa ni akina nani hao watanzania, hasahasa huyo mwenyekiti wa hiyo bodi alikuwa ni nani? Naombea tu asije kuwa joka la makengeza tena.
 
Kuna mwenyekiti mmoja wa TTCL alikuwa anakaa maeneo sikansika lakni kashatangulia mbele ya haki ila cjui alianza lini ila kaondoka kwenye time ya mzee wa msoga
 
Kiki za kijinga tu.
Suala limekaa kimgogoro...badala ya watu kwenda kwenye mahakama ya biashara...wanakimbilia kwenye media...

Wanachoishia kufanya kwenye media ni reputational damage kwa airtel.

Nadhani...of all the terms..hii term imefanya vibaya sana na kuvuruga mambo mengi.

Walichoweza ni kuidhibiti media na kutia hofu watu
 
Back
Top Bottom