Watu wengi hawajui Gender na hawajui tofauti ya Gender na Sex,
Mtu anakaza misuli ya vidole gumba kubisha kitu hakielewi, anatoa maelezo mengi ya sex badala ya gender,
Kuna sehemu umetoa mfano mzuri sana,
Ulisema Jamii ndio imetengeneza Gender Role na ili kuthibitisha hilo tunaona kuna Jamii ya Pwani Wanaume wanaenda wao Sokoni lakini kuna Jamii ya Bara Wanawake ndio wanaenda Sokoni,
Kuna jamii Wanawake ndio wanafanya kazi zote kama kuchunga, kuleta kuni, biashara, kiufupi yeye ndie anatunza Familia na Mwanaume kazi yake ni kunywa Pombe na Kuoa Wake wengi,
Humu wengi hawana exposure Mtu asema Mwanamke hawezi kubeba Zege wakati Jamii tu ya Wamasai Wanawake ndio wanajenga Nyumba,
Wamakua Mwanamke ndie Kiongozi wa Nyuma yaani ndie Kichwa cha Familia, hao Watoto hawajui wanakuja kukutolea Povu hapa,
Naungana nawe kua Gender Roles zimetengenezwa na Jamii husika kwa kumgawia kila Mmoja Majukumu yake kwa kadri wao wataona,
Na nimekuelewa lengo lako ni kutaka kuweka Usawa kwa Wote na sio huyu anapaswa afanye hili sababu ni Ke na huyu afanye lile sababu ni Me.