Suala la chuo kikuu cha dsm lahitaji umakini zaidi

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
KUSTAHILI AU KUTOSTAHILI KWA MADAI YA WANAFUNZI WA UDSM,
HAKUHALALISHI MTU KUZUNGUMZA CHOCHOTE.

Wanasiasa wamesema, Wanafunzi wamesema, Serikali imesema, Wazazi wamesema, Vyombo vya habari vimesema n.k.

MZOZO WA UDSM HAUTATATULIWA KWA VITISHO, AU JAZBA AU WATU KUWA TAYARI KUFA au MTU KUSEMA CHOCHOTE.

KINACHOHITAJIKA NI MIKAKATI ILIYOPANGIKA KIKAMILIFU AMBAYO ITALETA MATOKEO YA SULUHISHO HATA KAMA ITACHUKUA MUDA.

Exaud J. Makyao
 
Tujiulize haraka haraka...je nini kifanyike kuweza kupata pesa zote zinazohitajika kila mwaka kwa miaka 10 ijayo....tutembeze bakuli au twaweza kwa hela za kodi yetu tu???baada hapo hoja ipelekwe bungeni
 
Tujiulize haraka haraka...je nini kifanyike kuweza kupata pesa zote zinazohitajika kila mwaka kwa miaka 10 ijayo....tutembeze bakuli au twaweza kwa hela za kodi yetu tu???baada hapo hoja ipelekwe bungeni



Kinahitajika major overhaul ya spending ya chuo ambayo itawaathiri wengi pamoja na wahadhili na wafanya kazi wengine.

Kunahitajika kuwe na endowment, wahadhili na watafiti wawe agressive kutafuta grants; najua wanafanya hivi, ninashauri muelekeo wa matumizi ya grants kukazia sana kwenye kusaidia wanafunzi na kasehemu ka ada ya shule na alumni waanze kusaidia kutoa michango.

Nilisoma mahali fulani nje ya nchi kila mwaka napata barua mbili, moja kutoka college niliyosoma inaniomba nichangie, ya pili inatoka kwenye program niliyosoma inaomba mchango chochote nilicho nacho nitoe kiwasaidie wanafunzi fulani fulani. Najua wengi wetu huwa tunapata barua hizi. ( Sijawahi kuchangia) lakini Dar wakianzisha hii niko tayari kukopa kuisaidia.
 
Tujiulize haraka haraka...je nini kifanyike kuweza kupata pesa zote zinazohitajika kila mwaka kwa miaka 10 ijayo....tutembeze bakuli au twaweza kwa hela za kodi yetu tu???baada hapo hoja ipelekwe bungeni

Nani aipeleke hoja bungeni?
 
Ninakubaliana na Makyao kwamba suala la UDSM linahitaji umakini na busara zaidi kuliko vitisho. Na si UDSM tu ni vyuo vyote vya umma. Ila tuanze na chuo mama mabcho ni UDSM.
 
Makyao umetuasa kitu cha muhimu sana.Taifa letu linahitaji wataalamu katika fani mbalimbali. Tunavitegemea sana Vyuo vyetu vya umma kusaidia katika hili. Kwa sasa, hata kama tutategeneza wataalamu, wengi watakuwa hawana mapenzi ya dhati kwa ajiri ya migogoro isiyo isha na hivyo kukosa uzalendo. Kwa mtazamo wangu ni kuwa kama tunataka kuendelea kujitawala na kutawala uchumi na resources zetu, hatuna jinsi isipokuwa kufanya jitihada za makusudi kusomesha watu vile itakavyowezekana. Suala sasa je hizo hela za kusomesha vijana wetu zitike wapi? Tuchangie au tulipe kodi au etc lakini sisi kama Taifa ni lazima tuwe na mbinu na mikakati. Migogoro hii isiyokwisha haina mshindi ila inaweza kuangamiza uwezo wa Taifa kuandaa nguvu kazi
 
Back
Top Bottom