SUA: Wanafunzi walalamika kwa kutopewa pesa yao ya special fucult allowance

paluz

Member
Feb 9, 2016
53
9
Wanafunzi wa chuo kikuu cha sua wakati wakiwa wanaelekea kumaliza muhula wao wa kwanza wa masomo tangu walipofungua mwezi wa kumi na moja mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, kumetokea uhaba wa fedha baada ya kucheleweshewa pesa yao ya special faculty allowance ambayo inatakiwa alipwe mwanafunzi wakati tu akiwa amewasili chuoni.

Tukizungumza moja kwa moja na mwanafunzi wa kozi ya aquaculture na toursim management (majina tumeyahifadhi) kwa wakati tofauti wamesema kwamba kiukweli hali ya kimaisha ni ngumu sana kwani hadi sasa hawajui watakula nini kwani wamekuwa wakishindia mkate na maji kwa ukosefu wa pesa.

Maswa yetu blog tulitinga ofisi za bodi ya mikopo, kuulizia swala hilo na kuambiwa kwamba maelezo yote yapo chuoni kwani pesa zote zilishatolewa.Tutaendelea kufatilia swala hili na kukuletea majibu yaliyosahihi mara tutakapofika chuo husika na kupata maelezo kutoka kwa viongozi husika.
 
pesa ya kula walinunua vifaa,kwa hyo substitute inafanyika hapo,THINK BIG
Kwa kukusaidia special faculty requirement inalipwa moja kwa moja chuoni hapewi mwanafunzi.

Hebu tupe ufafanuzi imekuaje?
 
umefika level gani gani ya elimu?
wakati nipo chuo special faculty hulipwa mwanafunzi husika moja kwa moja
 
Wepesi sana kudai special allowance offcourse ni haki yao, sasa wapewe afu wambie wakuonyeshe hivyo vifaa ndo utajua unafiki wao, nimewahi kupewa special allowance laki nne, nikanunua rular ya efu 5 tu the rest is history.
 
Kwa kukusaidia special faculty requirement inalipwa moja kwa moja chuoni hapewi mwanafunzi.

Hebu tupe ufafanuzi imekuaje?
Vyuo vinatofautiana,kuna vingine hela inaingia moja kwa moja chuoni,vyuo vingine inaingia kwenye account ya mwanafunzi husika.Ila utaratibu wa hela kuingia kwenye accnt ya chuo,umefutwa miaka ya leo.Kwa sasa hela huenda direct kwenye account za wanafunzi!
 
Kwa kukusaidia special faculty requirement inalipwa moja kwa moja chuoni hapewi mwanafunzi.

Hebu tupe ufafanuzi imekuaje?
Ndo madhara ya kuishia darasa la saba alafu unajifanya unajua kuyaelezea mambo ambayo huyajui
 
Utaratibu rasmi ni huu

"Under the new Means Testing System, the whole loan shall be aggregated to one lump sum amount. Out of that, the Tuition Fee and Special Faculty Requirement components shall be paid directly to the Institution of study, whereas the remaining amount shall be paid to the student, quarterly."

Kama ulibadilishwa ni sawa, nashangaa wanaohoji elimu yangu.

Mambo mengi yanafanywa kisiasa kufurahisha watu badala ya kufuata taratibu, je utaratibu wa bodi ulibadilishwa?
 
Wanafunzi wa chuo kikuu cha sua wakati wakiwa wanaelekea kumaliza muhula wao wa kwanza wa masomo tangu walipofungua mwezi wa kumi na moja mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, kumetokea uhaba wa fedha baada ya kucheleweshewa pesa yao ya special faculty allowance ambayo inatakiwa alipwe mwanafunzi wakati tu akiwa amewasili chuoni.

Tukizungumza moja kwa moja na mwanafunzi wa kozi ya aquaculture na toursim management (majina tumeyahifadhi) kwa wakati tofauti wamesema kwamba kiukweli hali ya kimaisha ni ngumu sana kwani hadi sasa hawajui watakula nini kwani wamekuwa wakishindia mkate na maji kwa ukosefu wa pesa.

Maswa yetu blog tulitinga ofisi za bodi ya mikopo, kuulizia swala hilo na kuambiwa kwamba maelezo yote yapo chuoni kwani pesa zote zilishatolewa.Tutaendelea kufatilia swala hili na kukuletea majibu yaliyosahihi mara tutakapofika chuo husika na kupata maelezo kutoka kwa viongozi husika.
Eti wadau SPECIAL FACULTY ni zipiii
 
Back
Top Bottom