Strabag phase III: Kiama cha parking Kariakoo chaja

Strabag phase III: Kiama cha parking Kariakoo chaja

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,718
Reaction score
830,771
Ule mradi wa mabasi yaendeyo haraka kwenye njia yake maalum sasa unaingia hatua ya tatu

Hatua ya kwanza ilikuwa Mbezi-Ferry, imekamilika kwa zaidi ya asilimia 90

Hatua ya pili ilikuwa Morocco-Magomeni nayo iko mbioni kukamilika

Hatua ya tatu Fire/Bakhresa-Gerezani inaanza mara baada tu ya mapumziko ya Pasaka

Kote huko mradi ulikopita hakuna tena parking za kando ya barabara na barabara za kuchepuka nyingi zimekufa,sasa ujenzi ndio unanza Bakhresa-Gerezani maegesho yote yaliyokuwepo kandoni mwa barabara ya msimbazi hayatakuwepo tena!!! Hivyo wenye magari na ofisi zao waliokuwa wanategemea zile parking waanze kukuna vichwa kuhusu maegesho! Serikali kupitia jiji sidhani kana wana mipango yoyote kuhusu hili
 
Muache magari nyumbani mpande hayo mabasi foleni ipungue. Pia mnaweza kupaki mitaa mingine au parking zipo mtaa wa msimbazi tu?

Shida hakuna ustaarabu kwenye public transport. Wengine wanaona bora wakomae na gari zao tu.
 
Muache magari nyumbani mpande hayo mabasi foleni ipungue. Pia mnaweza kupaki mitaa mingine au parking zipo mtaa wa msimbazi tu?

Kweli kabisa waache nyumbani magari yao wasiyalete katikati ya mji..
Lakini pale jangwani panafaha kujengwa parking
 
Shida hakuna ustaarabu kwenye public transport. Wengine wanaona bora wakomae na gari zao tu.

Basi wacha wakomae na gari zao,ila hatuwezi kuacha kujenga mradi wa kunufaisha wengi kisa wachache na magari yao watakosa parking.
 
kwanini magorofa yaliyopo pembezoni mwa barabara hiyo yasivunjwe ili kuwepo na nafasi pana ya kutosha ?
 
Tuliambiwa wangeanza majaribio mwezi july mwaka jana...hadi leo kimyaaaaa...kwani unaanza lini?

Pesa za mradi zililiwa (zilifanyiwa kazi nyingine), ndio maana hata kipande cha mtaa wa Msimbazi Strabag waligoma kuanza.
 
Poleni wanakariakoo...mm ofisini yangu ipo kimanzichana...poleni sana
 
kwanini magorofa yaliyopo pembezoni mwa barabara hiyo yasivunjwe ili kuwepo na nafasi pana ya kutosha ?

Nafasi iliopo inatosha kujenga bila kuvunja ghorofa la mtu! Seriously unataka ghorofa la mtu livunjwe ujengewe parking?! Lingekuwa ghorofa lako ungeshauri hivyo hivyo?!
 
Parking zipo jangwani na kituo kipya cha basi cha mbagala.
 
Back
Top Bottom