Story za Prof. Palamagamba Kabudi

Story za Prof. Palamagamba Kabudi

27 Sep 2019
New York, Marekani

Mahojiano ya Palamagamba Kabudi na Radio Ya Umoja wa Mataifa


Pata taarifa ya habari, makala, habari kwa picha , mahojiano na matukio kuhusu masuala ya kibinadamu, SDGs na mengine mengi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Ni "Habari za UN" kutoka makao makuu ya UN New York, city.

Source : Habari za UN
 
Sept 27, 2019
New York

General Assembly of the UN (New York, 24 – 30 September 2019).

Palamagamba Kabudi, Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation of the United Republic of Tanzania, addresses the general debate of the 74th Session of the

Source : United Nations

Waziri Kabudi ahutubia kikao cha 74 Baraza Kuu La Umoja Wa Mataifa (UN GENERAL ASSEMBLY - UNGA 74)
Mh. Kabudi ktk hotuba yake mbele ya kikao hicho cha 74 cha Baraza la Umoja wa Mataifa - UNGA alielezea mafanikio ya Tanzania tangu Oktoba 2015 kuwa ni:

Mpaka sasa asilimia 66% ya watu Tanzania wana umeme huku 71% ya watu wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama. Huduma za afya zimeboreshwa.

Miundo mbinu kama ujenzi wa barabara ,Ujenzi wa bwawa jipya la Umeme Rufiji , SGR reli na ukarabati wa reli nzima ya mkoloni, upanuzi wa viwanja vya ndege Julius Nyerere Dsm na Abeid Amani Karume Znz vyote zimefanyika kwa kiasi cha kuridhisha.

Tanzania hali ni nzuri kwani Uhuru wa habari /media ni mpana sana kuna vituo 152 vya Radio ambapo vya serikali ni vitatu tu. Vivyo hivyo kati ya vituo 34 za televisheni ni viwili tu ndiyo mali ya serikali. Idadi ya magazeti yenye leseni ni 172.

Kuhusu demokrasia na haki za binadamu uhuru wa siasa za vyama vingi unazidi kukomaa Tanzania ambapo kuna vyama 21 vilivosajiliwa huku vikifanya shughuli za kisiasa kwa uhuru na mpinzani mmoja yupo naye ktk ujumbe aliokuja nao New York akiwa waziri katika serikali ya Maridhiano Zanzibar.

Mazingira ya kuchochea uwekezaji yameboreshwa. Hii ni kufuatia kufutwa kwa kodi nyingi zisizo rafiki ktk kuvutia uwekezaji.

Hata hivyo Mh .Palamagamba Kabudi ametoa (Tanzania imetoa ) angalizo kuhusu kukithiri kwa nchi kujitoa ktk Jumuiya za kimataifa na hivyo kuchelewesha maendeleo kwa ujumla. Lakini ana habari njema kutoka Kusini mwa Afrika, ambapo mwezi Agosti 2019 kulikuwepo kikao kikubwa cha nchi wanachama wa SADC.

Kikao hicho cha SADC kilichofanyika Dar es Salaam, Tanzania kwa mafanikio makubwa kiliweze kuongeza makubaliano ya nchi wanachama kuzidisha mashirikiano ya kiuchumi na biashara na ni habari njema kuelekea kufikia maazimio ya Umoja wa Mataifa ya kufikia maendeleo-endelevu SDG kufuta umasikini duniani.
 
Sept 28, 2019
New York

Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano mkuu wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York,Marekani. Source : http://foreigntanzania.blogspot.com/2019/09/prof-palamagamba-john-kabudi-ahutubia.html?m=1
 
Prof. Palamagamba John Kabudi na story zake nyingi kuhusu masuala ya kimataifa pia kuhusu Julius Nyerere. Palamagamba Kabudi pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari .

Hivyo kolamu / column ya kuzungumzia mapito yake toka zama hizo mpaka sasa hivi itakuwa nafasi murua kuangazia habari motomoto hususan za nafasi yake kama waziri katika serikali.

Leo Azungumzia nafasi ya Tanzania katika dunia na ushawishi wake na kwenda mbali zaidi Prof. Palamagamba Kabudi anafananisha nafasi ya Tanzania ni kama 'nyonga' ya Afrika ktk masuala ya kimataifa.

Source : Zanzibar Ni Kwetu

Hivi huyu Kiongozi ana watoto wangap na mke wake ni nani. Kuhusu hili suala la uraia pacha nimeona watu wanasema jamaa watoto wake wengine hawana uraia wa bongo. Nimejaribu ku tafuta mtandaoni sijaona taarifa zake. Ukweli ni upi jamani???
 
Nyonga [emoji23][emoji23] sema
Kwa sasa mama samia yuko sawa sana na wazungu ndo maana hatak kuonekana yupo upande gani.
 
Fropesa kalamaganda kabugi ni mzee wa mafix

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
UN: Asante Tanzania kwa ulinzi wa amani
image1024x768.jpg

Picha ya UN/ Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi baada ya mazungumzo yao jijini New York, Marekani.

27 Septemba 2019
Amani na Usalama
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aendelea kuwa na mazungumzo na viongozi wanaowakilisha nchi zao kwenye mjadala mkuu wa UNGA74 na miongoni mwao ni kutoka Tanzania na Burundi.

Mjadala mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74 ukiendelea kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi ambapo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu pande mbili hizo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa New York, alhamisi usiku imesema kuwa Guterres na Kabudi wamejadili hali inavyoendelea kwenye ukanda wa Maziwa Makuu ikiwemo Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Katibu Mkuu ameishukuru Tanzania kwa mchango wake wa kipekee kwenye ulinzi wa amani na kusisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia juhudi za kitaifa za kukabiliana na misimamo mikali.
Source : UN: Asante Tanzania kwa ulinzi wa amani, Burundi sakeni suluhu ya janga la kisiasa
Huyu Prof Kabudi naye yupo kwenye orodha ya Dr Vicensia Shule ya wale Lecturers wa UDSM wa "marks for sex". Nakujulisha tu ulielewe, siyo kukaa hapa mnapambana bure
 
Hivi huyu Kiongozi ana watoto wangap na mke wake ni nani. Kuhusu hili suala la uraia pacha nimeona watu wanasema jamaa watoto wake wengine hawana uraia wa bongo. Nimejaribu ku tafuta mtandaoni sijaona taarifa zake. Ukweli ni upi jamani???

Viongozi wengi watoto wao wanaishi ngambo, na uhakika wengi wa watoto hao wana uraia wa nje.
 
Umuhimu wa kuwatumia diaspora ili kupenyeza ushawishi wa uwekezaji na diplomasia ya kiuchumi ifanikiwe zaidi

26 April 2023
Berlin, Germany

JOE CHIALO SASA NI SENETA KTK BARAZA LA SENETI JIMBO LA BERLIN

1685524499369.png

Seneta Joe Chialo atahusika kusimamia masuala nyeti ya Utamaduni, Maridhiano, Ushirikishwaji na Kukuza Demokrasia katika jimbo la Berlin Ujerumani.

Kufuatia mazungumzo marefu ya maridhiano hayo ya vyama vya siasa nchini Ujerumani baada ya uchaguzi wa jimbo la Berlin kuvurugika mwaka 2021 kisha kurudiwa mwaka huu tarehe 12 February 2023, mwanasiasa wa kijerumani mwenye asili ya Tanzania Bw. Joe Isaya Chialo ameteuliwa kuwa senata wa jimbo la Berlin kupitia chama baada ya makubaliano ya kuunda umoja wa mseto ya vyama vya CDU na SPD kuongoza baraza la seneti la jimbo la Berlin.

Vyama vya siasa vya CDU na SPD walikubaliana kuunda serikali ya mseto katika baraza la seneti la jimbo la Berlin baada ya uchaguzi wa jimbo la Berlin mwaka 2021 kutangazwa na Mahakama ya Katiba ya Berlin kuwa uligubikwa na tafrani ya kimfumo hivyo kufutwa na kurudiwa tarehe 12 February 2023.

Bw. Joe Chialo alizaliwa jijini Bonn Ujerumani ambapo baba yake mzee Isaya Chialo alikuwa balozi wa nchi ya Tanzania katika iliyokuwa Ujerumani ya Magharibi mwaka 1970. Baba yake mbali ya kuiwakilisha Tanzania nchini Ujerumani pia mwana diplomasia nguli Mzee Chialo aliwahi kuhudumu kama balozi katika nchi za China na Japan.

===========

A lot of work awaits Berlin’s new Senator for Culture, Joe Chialo​

The new state government Berlin has not yet been elected, surprises are theoretically always possible in the capital – especially among the decimated Social Democrats, the grand coalition is anything but popular.

Cross-shots are therefore conceivable up to the election on Thursday, but even if everything goes smoothly: What Joe Chialo (CDU), the designated Berlin Senator for Culture, intends to do in the new office is still a little nebulous.

The previous indications of the man from the music industry, who will soon bear the title “Senator for Culture, Cohesion, Engagement and Democracy Promotion”, remain vague. Such as his announcement that “the cultural and economic aspects” must be “married even better”.

Does that mean that the publicly financed theatres, museums and opera houses should look more closely at sponsors from business and higher income – or that the future culture senator is also interested in segments of the creative economy for which the state government’s economic department is actually responsible? the gaming industry for example?
 

30 May 2023​

Bungeni, Dodoma
Tanzania

“Nchi Nyingi HAZITAKI URAIA PACHA” Prof. PALAMAGAMBA ACHARUKA KUHUSU URAIA PACHA.


 

30 May 2023​

Bungeni, Dodoma
Tanzania

“Nchi Nyingi HAZITAKI URAIA PACHA” Prof. PALAMAGAMBA ACHARUKA KUHUSU URAIA PACHA.



Anayeelewa hichi kitu anieleweshe vizuri tafadhali, nadhani kwakuwa sikupita shule basi napata tabu kuelewa.

Taifa linafaidika nini watu wake wakiwa ni raia wa Nchi mbili ?
Zipi ni hatari za kuwa na raia wenye uraia pacha?
Taifa linapata hasara gani kama litawanyima uraia pacha?

Kwanini waliukana uraia wa Tanzania mwanzo, kwanini wanautaka sasa?

Wanapitia changamoto gani zinazowafanya watamani kuwa ni raia wa Tanzania kwa mara nyingine?
 
2020 24 January

'BABA WA MIKATABA' PROF. PALAMAGAMBA KABUDI

Nyuma ya pazia aelezea magumu, kuviziana, vitimbi, kuchotana akili na changamoto zingine lukuki za mchakato wa mikataba 9 ya kimataifa na wawekezaji wa kutoka nje :

Profesa Kabudi: Niliandika barua ya kujiuzulu lakini ilichanwa



Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuna wakati aliandika barua ya kujiuzulu lakini alinyang’anywa na ikachanwa.

Mbunge huyo wa kuteuliwa na Rais ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kamati ya madini ya Barrick.

Kabudi anasema alichukua uamuzi wa kuandika barua hiyo baada ya mchakato wa majadiliano na wajumbe wa Barrick kuwa magumu, kwamba aliona aibu kushindwa kazi aliyotumwa.

Amemtaja aliyemnyang’anya barua hiyo ambayo haikuifafanua kwa kina ni Kasmir Simbakuki.

“Nilifikia hatua nikafanya dhambi ya kukata tamaa nikasema jambo hili haliwezekani, niliona ni bora aibu na fedheha hiyo niibebe lakini barua niliyoandika sikufanikiwa kuileta.”
 
4 March 2019

KAZI ZA MKUU WA NCHI NI TOFAUTI NA ZA MKUU WA SERIKALI

Prof. Palamagamba Kabudi ataja kazi za mkuu wa nchi ambazo haziwezi kukasimiwa kabisa yaani Delegatus non potest delegare.” kwa kilatini .....

 
2 Sep 2018
Seattle, the Pacific NorthWest USA

Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Watanzania wanaoishi Ughaibuni katika Maendeleo ya Kijamii na Uchumi. Hotuba hiyo iliwasisimua watu wengi ktk diaspora na kuleta mjadala mpana JamiiForums worldwide.

Prof. Kabudi anakumbuka wanafunzi wenzake ktk darasa lao Chuo Kikuu cha UDSM limetoa watu 'mahiri' siyo yeye tu bali Balozi Wilson Masilingi, Dr. Harrison Mwakyembe, Major General Rwegasira mstaafu Judge Advocat jeshini , pia majaji 7 kati ya hao wako mahakama ya rufaa ya Tanzania

Mmoja wa wana -Diaspora Bw. Deus Rugemalira kwa kumnukuu maoni yake:

'' Hotuba hii ya Prof. Palamagamba Kabudi inafumbua macho ya wengi. Inatoa mwanga (walau kwa ufupi), kama Taifa
1. Wapi tumetoka,
2. Tumetoka vipi,
3. Wapi tumefika na changamoto zake
4. Wapi tunaenda.
Tusipoyajua Haya hatuwezi kujitambua na hatuwezi kuendelea. Ningependa kuona inachapishwa hata gazetini (kama ilivyo) ili wasio na namna ya kuiona, basi wakaisome".

Kabudi, kama uko humu na unasoma au unaangalia hizi post- Mungu bado anakuhitaji kuwatumikia watanzania. Amka sasa , watetee kwenye hili suala la bandari... tafadhari- usiwe kigeugeu, amka sasa, wakati ni wako. Zungumza na watanzania tutakuelewa- ni wengi na bado tunakuaminia. Asante mtoa crip na tunawahitaji watu kama hawa ili tusonhe mbele.. Kabudi.. Njoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo, sema haya ya mikataba ya bandari usikae kimya...njooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo tunaukita kwa mari ya Mungu usiyoiweza kuipinga. Njooooooooooooooooooooooo na sema . Tafadhari
 
Katika watu waliomuangusha marehemu Mzee Magufuli, huyu ni miongoni mwao. Mzee Kabudi, Mungu anakuona.
 
tafadhari- usiwe kigeugeu, amka sasa, wakati ni wako.

Hakika katika wakati huu wa uhitaji nchi imeisongelea miguu ya mzalendo huyu mkubwa ili ipate kuokoka toka mwa minyororo ya wanaCCM wenzie walio madarakani.

WanaCCM viongozi wasioitaki nchi yetu mema ingawa ni taifa lililobarikiwa sana lakini watu wake wanaswagwa katika umasikini na utumwa hata baada ya miaka 61 ya uhuru wake hakuna viongozi wenye uchungu na nchi Tanzania

Prof. simama kwa haki yako ndani ya cha chako tawala CCM ukemee bila kupepesa macho ili uikomboe nchi, bunge, mahakama na wananchi wote bila kujali vyama Tanzania iweze kupata kiongozi bora.
 
10 July 2023
Prof. Palamagamba Kabudi atisha uchaguzi mdogo wa Magubike

 
08 May 2024

mtizamo na msimamo Profesa Palamagamba Kabudi


Profesa kabudi: Yapo Mambo Lazima Yafanyiwe Kazi Kabla Ya Uchaguzi


View: https://m.youtube.com/watch?v=bGvgLlOOW6c

Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimeandaa mkutano wa wa kitaifa ambao umewakutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadili sheria za uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani...


N.B
Fast forward 15 August 2024

Profesa Palamagamba Kabudi ule msemo mtoto mkabidhi mchawi umefanywa kwa yeye kuaminiwa na mheshimiwa rais hivyo kuteuliwa kuwa waziri wa sheria na katiba, hii mitizamo yake ataifanyia kazi chapchap au ni stori zake tu ?
 
Back
Top Bottom