Story za mkeo/mpenz wa ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Story za mkeo/mpenz wa ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sakapal, Aug 22, 2012.

 1. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Morning every one!! I salute you all, SALUTE!!!

  Ni hivi , leo nina swali kwa wanaume hasa waliooa au walio kwenye mahusiano na mwanamke kwa muda mrefu, tafadhali naomba mueleze ukweli ili kunisaida mimi na hata wadada wengine wenye shida kama hii.

  Niko na mahabat wangu, tunatabia ya kuondoka wote home kwenda kazini na kurudi pamoja kwa kutumia kabajaji ketu si unajua bongo usafiriwa shida? Na hii imekuwa ikitupa nafasi ya kuongea mambo mengi njiani na tukifika home ni kuangalia watoto kuoga na kulala. Sasa shida iko hivi, mimi napenda sana kuongea na hili analijua utakuta ile nimeingia tu kwenye gari naanza story sometimes za kuchekesha, sometimes za ofisini yaliyojiri ofisini kwetu siku nzima, leo nani kafanyaje, nani kaambiwa nn na bosi, mkutano leo ulikuwaje, na sometime hata siri za ofisi au mikakati ya ofisi yetu namtaarifu nikijua ni maongezi tu looh. Sijui anakuwa anachoka kusikiliza au hapendi tena sauti yangu yaani utakuta unaongea in btw hata hujamaliza anaongeza sauti ya redio like ninyamaze. Unakaa kimya baada ya muda unaanzisha story ingine heee! unashangaa anakuuliza kitu kingine tofauti labda nilikuwa nasimulia kuhusu habari ya watoto utasikia tuu wale mafundi walimaliza jana uliwalipa hela yao yote looh! nachokaje?
  Baada ya kuona shida inazidi na sipati nafasi nzuri ya kusikilizwa nikaona bora nikae kimya na tuwe wote mabubu njia nzima toka mjini hadi home yaani napata shida.
  SWALI;- Hivi kwa nini wanaume hampendi kusikiliza masimulizi ya wake zenu? hii hata kijana mmoja hapa ofisini nilishamsikia akiongea kwamba kunarafiki yake ameoa mwaka jana ila ukifika muda wa kwenda kwake hatamani coz anawaza jinsi ya kusikiliza story za mke wake za siku nzima na mkewe huyo anataka mumewe amsikilize hadi amalize. To me huyu kijana anaboreka na hizi story na amechoka kuzisikiliza, sasa kwa nini nyie wanaume msiwaambie wazi wake zenu kwamba usipige story zako za kutwa nzima? au mwambie kwa upole tu pls nimechoka leo naomba tuongee asubuhi au hata ukamwambia nasikia kichwa kinauma reserve the rest for tomorrow huyu mwanamke atakuwa in good place ya kukuelewa that u need a space ila isiwe kila siku. A u hata ukamsikiliza tu then akimaliza yule mwanamke anafurah basi na wewe unaendelea na mambo yako. Naomba niwaibie siri nyie wanaume...,
  Sikilizeni wake zenu, hii ni kitu ndogo na ya kijinga but ni kubwa na ya muhimu sana hasa kwa wanawake yaani kama mm hapa naugulia coz sisikilizwi story zangu naishia kujikuta naongea mwenyewe na mbaya zaidi kunawakati anakwambia njoo tuongelee kitandani wakati wa kulala akishapata tunda lake ukirudi kuoga unamkuta anakoroma sometimes unamkuta macho but unaanza story ukijastuka mwenzio alishalala saa nyingi, inaudhi kweli muwe mnatuambia kwamba usiongee baby ninausingizi sana.
  Mie napenda sana kuimba hata sometimes unaskia kero kumuimbia coz ukiimba anaona kama unampigia kelele yaani wanaume naomba mnisaidie shida ni nini?
  Hampendi story? je ni story za kipuuzi? mbona hamsemi? maudhiiiiiiiiii??

  Ever remaining,
  Sakapal
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Unapoamua kuwa na mtu ni muhimu kuangalia compatibility na interests. Kuna wanaume wako well rounded na wanaweza kuongelea karibu chochote. Kuna wengine kama si mpira au masumbwi utawaboa tu.

  Mie naamini mpenzi/ rafiki mzuri kabisa ni yule mnayeweza kuongea chochote.

  Halafu mtu kama mlianza kwa kuweza kuongea chochote, akabadilika inaweza kuwa ni ishara ya kukuchoka, mapenzi yameisha unakuwa karma a dreaded chore. Inawezekana ndo maana unaona mazungumzo yake yanazungukia the necessities tu kama malipo ya mafundi etc.

  Wanaume, mwanamke hapewi tunu ya vito na ufundi wa mbinde za uwanjani tu, bali hata kwa nyama tamu ya ulimi. Msifie bila ya kuwa mpambe isivyo, mazungumzo ya kina yanajenga mahusiano mema na ni kuni za kuchochea moto wa mapenzi.

  Mie mtu asiyeongea simuwezi, maana naona kama ana wasiwasi wa kunieleza anachofikiri. Mwanamke anayeongea, hususan anayejua kujieleza, ndiye anayetakiwa dunia ya leo.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hiyo auto-correction Kiranga umetishaa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Freaking different Droid. Nimeibadili settings. Na ku edit post.

  Thank you very much.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Duh! Mi nilitaka kutia neno lakini nikasita....nikadhani labda umeamua kucheza sarakasi za isimu.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ulikuwa unasubiri kutangaziwa zawadi ya atakaeweza kufumbua fumbo lililoandikwa

  I was far ahead of you

  karma= kama
  Kuwait=kuwa

  :A S tongue:
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ungeacha tukachangamsha bongo kidogo....

  Nilifanya makengeza kujaribu kuona neno ndani ya neno

  :redface:
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Wanagenzi wanagenzi na watribu watribu, hawafungamani.
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nafikiri pia kuna utofauti wa aina za stori ambazo wanaume wanazipenda na zingine ambazo wanawake wanazipenda. Hii saa nyingine ni kama nature. Mwanamke hupenda kusimulia matukio yanayohusu watu zaidi, mwenendo wa maisha ya watu, mahusiano, yaliyotokea ofisini, majirani, marafiki, sherehe nk. Kwa wanaume wengi hupenda kuzungumzia vitu, mipango, ubunifu, ujenzi, mafundi nk hata kwenye wakati wa starehe na wakibadilisha labda mpira na aina za magari! Hizi saikolojia ni za ajabu sana, kwa mfano mtu anaweza kupita na gari mbele ya mwanamke na mwanaume. Mwanamke ataangalia ndani ya gari ili aone ni nani anaendesha na yupo na nani, amevaaje nk. Upande wa mwanaume ataangalia model ya gari, ukubwa wa injini nk!

  Katika hali ya kawaida kwenye mahusiano ni vyema ujifunza interest za mwenzi wako. Ni vyema mwanaume ujue mkeo anapenda nini na mke kujua mwanaume anapenda nini. Hii inasaidia kujua nini cha kuongea ambacho kinaweza kuwaweka sawa na kujikuta mnafurahia mazungumzo. Chukulia mfano, mwanaume akimpa lift mdada anayemfahamu, mazungumzo ya ndani ya gari mara nyingi hujaa na vicheko, utani na furaha, jiulize ni kwa nini? Ni vyema mazungumzo kama haya kudumishwa kwenye mahusiano ya kindoa ili kuondoa hali ya mtu kumbore mwenzake.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hii habari ya wanawake wako hivi na wanaume wako hivi.

  Another sweeping generalization.
   
 11. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Pole Saka ,njoo nikusikilize mwayego .
   
 12. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hebu jichunguze na story zako.may be zinaboa kweli.Usitafute kumrekebisha mwenzio jirekebishe wewe kwanza.Kama hicho kitu hakipendi si uache kufanya tafuta kile anapenda???? utapungukiwa nini?
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  HorsePower

  Unadhani wanawake wote na wanaume wote wako hivyo ulivyoeleza?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Talking is Gud kwa kweli,
  Kimtazamo mi nadhani ingebaki tu average talking, muwe na uwezo kwa kukaa kimya pia mkiwa wawili. siyo kila mkikutana mnaongea. Ujue ukiwa muongeaji sana there is a good chance kwamba utaongea na vingine ambavyo siyo
  Mfano
  1)Kusengenya-(i hate this-I hate talking about others while I am with my wife).
  2)Kuudhiana-Increasing chances za mumeo kudisagree na opinions zako.
  3)Kuondoa element ya surprise. Like ukifanya kitu mumeo anajua ulisema utafanya.
  4)And last but not least kuharibu quality ya ur time together...If u bore him then he wont be looking foward to your time together(Pretty hard to embrace, Isn't it?)

  Mi namshukuru Mungu my wife huongea kawaida na hanishikii bango nimsikilize...but then sijawahi kuchoka kumsikiliza
   
 15. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Na mjaribu saa ingine kuja na story za kuongeza kipato ili familia imee sio mastori ya harusin na maofisini mwenu tu kila siku bana yaaani uje na say mpango wa biashara na jinsi ya operationalization mimi ntakusikiliza kila siku hata wa manane ila ya Mke; Honey nikwambie kitu..........
  Mume; Enheee........
  Mke; Jana ofisini ile kikao yooote mpaka jioni ile tukatoka secretary na bosi tumewaacha ofisin ana inasemekana wana uhusiano wa kimapenzi
  Mume; Bad Habit.........
  Mke; Inauma sanaaa

  At Home......
  Mke; Mume wangu
  Mume; Naam......
  Mke; Hivi unajua this weekend ndo ile send-off
  Mume;Owk....ntakupeleka then ukiwa tayari ntakufuata mke wangu.....
  Mke; Sasa utakuta kwenye send-off watu huwa wanajikandika mipoda kama wachawi yaani mi sipendagi...........
  Mume; Ngrrrrrrrrrrrrrrr.........................ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr kalala zamaaaaani as mistory yako inaboa saaaaanaaaaaaa na ni non-constructive

  Tafakari................chukua hatua
   
 16. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Guys it may not mean that all women and men are like that (Ni kweli kuna wanaume hawapendi mpira wala hawachagui gari) but it is a generalization that will give you somewhere to begin.

   
 17. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sorry, sikumaanisha kugeneralize, ila kwa mtazamo wangu naona wengi wako hivyo .... ila si wote ...
   
 18. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kwa mfano dada @sakapal, I'm your husband, tuko garini - unanipigia story zako na wadada wenzio wa kazini,umemaliza unaanza kilichojiri harusini kwa fulani, kisha fulani na mumewe then mara dada huyu kaachana na mpenziwe.
  Kwa kweli I wont stand hearing you talking all the way!
  na ukianza story za kitchen party I will kick you out of the car!
   
 19. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ni baadhi ...
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Wanawake wote wakiwa hivi mfumodume hauishi kamwe.

  Mwanamke ni lazima abadilike kumfuata mwanamme, hata kama mwanmme ni an antisocial jerk.
   
Loading...