Story za mkeo/mpenz wa ndoa

first of all don't salute us coz we have no ranks,okay ni kwamba hamchez na alama za nyakati,hujui mume wako amekumbana na mishe gani instead unaanza kuleta story zako za ajabu ooooh sijui yule mama wa keki leo amezidisha unga wa ubuyu kwenye soda ya bosi aliyokunywa leo ilikuwa na kichupa ndani(hueleweki)unategemea kusikilizwa?na mfumo ndo huo mpaka mtakapokuwa smart,na kwa bahati nzuri na kwenye katiba mpya lipo,no chance for non sense stories.
 
Guys it may not mean that all women and men are like that (Ni kweli kuna wanaume hawapendi mpira wala hawachagui gari) but it is a generalization that will give you somewhere to begin.

Kwanza, hakuainisha kuwa hii ni general view. Pia hata hizo general views zinakuwa na specifications; wanawake na wanaume wa aina gani au wa wapi, kwa mfano.

kuna utofauti wa aina za stori ambazo wanaume wanazipenda na zingine ambazo wanawake wanazipenda.

Hizi generalization zinaweza kumfanya mtu kukosa kujiamini na kujithamini alivyo kwa sababu tu ameambiwa yeye si sawa na wanawake au wanaume wengine.
 
Kwa mfano dada @sakapal, I'm your husband, tuko garini - unanipigia story zako na wadada wenzio wa kazini,umemaliza unaanza kilichojiri harusini kwa fulani, kisha fulani na mumewe then mara dada huyu kaachana na mpenziwe.
Kwa kweli I wont stand hearing you talking all the way!
na ukianza story za kitchen party I will kick you out of the car!

Mwanamme anayejua maongezi anamjibu vizuri mkewe na kuyaongoza hayo maongezi kuelekea kule anakofikiri kunafaa zaidi.

Sasa wewe unaona mkeo anaendekeza gossip, badala ya kuonyesha hufagilii na kuongea habari hizo hizo kwa kina zaidi, unamuacha mamaa anakuwa kama anafanya jitihada za kuwa social wakati wewe ume mute.

Unakosa mvuto.

Unaweza kupinduliwa kwa kitu kidogo tu, katokea kijana mtanashati hana lolote zaidi ya maongezi mazuri, anakufanya mbaya.

Halafu utalalamika wanawake wa siku hizi wasaliti.

Kumbe usaliti umeanza mwenyewe kwa emotional neglect iliyo borderline torture.

Mara nyingine mtu anaweza kuanza kuongelea weather sio kwa maana ya kwamba anataka kuongelea weather, anataka ku crack the ice tu kwa nyepesi nyepesi, sasa kama mwanamme kichwa you take that and run, you build up the convo.

Sasa wewe mtu kaanza na weather tu unasema huyu naye kashaanza story zake za ajabu ajabu.

Utaonyesha humpendi, anakuboa. Mtu kama unampenda kweli hata akikoroma utaona kama muziki.

Na akileta story nyepesi nyepesi unazipeleka kunako, si kumchunia.
 
Kwanza, hakuainisha kuwa hii ni general view. Pia hata hizo general views zinakuwa na specifications; wanawake na wanaume wa aina gani au wa wapi, kwa mfano.

a) Siyo kila kitu ni lazima kiainishwe, you have to figure out some things on your own(Like, that being a generalization is an obvious fact since you can't define human behaviors in few lines)

b) Generalization kuwa na grouped specifications depends on the level of simplicity that the guy decided to use

c) Honestly naongea toka kwenye experience, wadada wengi stori zao ni about other people (Naomba u note nimesema wengi na siyo wote, asante). Which to many men is so boring!

Hizi generalization zinaweza kumfanya mtu kukosa kujiamini na kujithamini alivyo kwa sababu tu ameambiwa yeye si sawa na wanawake au wanaume wengine.

d) Of course you are not equal to anyone, haven't you heard that everyone is unique?
 
Kwanza pole sana my dear sakapal but i salute u again in the name of..

Kwanza na mimi niseme kwamba inaweza kuwa fault ya either mwanamke au mwanaume katika kutojua stori gani mwenzake anapenda au havutiwi nazo. Ni kweli kuna vitu havilazimishiki kwa mwingine..kwa mfano binafsi sipendi gossip..yaan flani kafanya hiki ama kama kafanya kile (the shigongo style)..Ina maana kama mkewangu analeta stori za namna hii lazima nitamtune off..Lakini pia kuna wakati ambao mnahitaji kurelax hamuwezi kila wakati kuongelea mambo ya maendeleo tu mnaweza pia kuongelea social life..As a man lazima umsome mkeo na unaweza kudirect stori ili na wewe upate cha kuchangia. Sishauri tabia ya kukaa kimya all the way!!!
 
Last edited by a moderator:
Mwanamme anayejua maongezi anamjibu vizuri mkewe na kuyaongoza hayo maongezi kuelekea kule anakofikiri kunafaa zaidi.

Sasa wewe unaona mkeo anaendekeza gossip, badala ya kuonyesha hufagilii na kuongea habari hizo hizo kwa kina zaidi, unamuacha mamaa anakuwa kama anafanya jitihada za kuwa social wakati wewe ume mute.

Unakosa mvuto.

Unaweza kupinduliwa kwa kitu kidogo tu, katokea kijana mtanashati hana lolote zaidi ya maongezi mazuri, anakufanya mbaya.

Halafu utalalamika wanawake wa siku hizi wasaliti.

Kumbe usaliti umeanza mwenyewe kwa emotional neglect iliyo borderline torture.

Mara nyingine mtu anaweza kuanza kuongelea weather sio kwa maana ya kwamba anataka kuongelea weather, anataka ku crack the ice tu kwa nyepesi nyepesi, sasa kama mwanamme kichwa you take that and run, you build up the convo.

Sasa wewe mtu kaanza na weather tu unasema huyu naye kashaanza story zake za ajabu ajabu.

Utaonyesha humpendi, anakuboa. Mtu kama unampenda kweli hata akikoroma utaona kama muziki.

Na akileta story nyepesi nyepesi unazipeleka kunako, si kumchunia.

Trust me, sikukurupuka kwenye kuoa mke na sijaweza kumuheshimu na kumtunza kiasi cha kuja kupinduliwa kirahisi kama unavyodhani.
Na wala mke wangu hayuko hivyo
 
Sikuongelei wewe, naongelea a scenario.

Hii case iliyoletwa hapa ni emotional neglect.

Huyu mama anaweza kuwekwa katika majaribu kirahisi sana kama akitokea mtu mwingine akaonyesha kumjali na kumsikiliza.

Tusiwaweke wenzetu katika majaribu kirahisi hivi. Inafaa kusomana tangu mwanzo kabisa na kama mtu hamko compatible, hampotezeani muda kabisa.
 
Wanawake wote wakiwa hivi mfumodume hauishi kamwe.

Mwanamke ni lazima abadilike kumfuata mwanamme, hata kama mwanmme ni an antisocial jerk.
Naona unadandia treni kwa mbele.Na hayo mambo ya gender yamekukaa sana kichwani.Mimi sijatamka kuwa mwanamke ndio wa kubadilika pekee.Nilimlenga aliyeleta mada.Na isitoshe suala la kubadilika ili usimkwaze mwenzio ni la pande zote.Hata wewe Kiranga kama unavitabia vya kulazimisha mkeo awe kama utakavyo badilika.
Halafu tusipende kuhukumu kuwa kila anayeishi kama alivyo kuwa ni antisocial.Tuheshimu interest za mtu.
 
Last edited by a moderator:
a) Siyo kila kitu ni lazima kiainishwe, you have to figure out some things on your own(Like, that being a generalization is an obvious fact since you can define human behaviors in few lines)
Kwenye jukwaa ambalo hatujui wasifu wa wachangiaji (kuanzia umri, na afya ya akili), ni muhimu kuanisha kila kiwezekanacho ili kutotoa fursa ya kutoeleweka. Unaporuhusu watu wa figure out for themselves ndipo unaporuhusu watu kuondoka nadhana ambazo sizo ulizokusudia. Hakuna sababu hiyo wakati uwezo wa kuanisha upo.
b) Generalization kuwa na grouped specifications depends on the level of simplicity that the guy decided to use

Huwezi ukawacha tu kuweka specifications kwa kisingizio cha uamuzi binafsi. Utafiti huwa na specifications for a reason, sio pambo.

Ni sawa na mtu aje asema wanawake wengi wanawaua waume zao kwa sababu ya kutaka fedha za urithi bila ya kusema ni kwa mujibu wa utafiti wa wanawake wa aina gani (eneo, umri, hali binafsi za kiuchumi) itakavyokosa maana kwa mazingira ya Kitanzania, kwa mfano

c) Honestly naongea toka kwenye experience, wadada wengi stori zao ni about other people (Naomba u note nimesema wengi na siyo wote, asante). Which to many men is so boring!

Hii ni experience yako, kwa hiyo siwezi kukupinga kwa sababu sijui hao wanawake unakuwa unakutana wapi au ni wa aina gani. Lakini wakati huo huo naona tayari umeshawazungumzia wanaume wengine pia. Hao "many men" ni wangapi? (kwa sababu hii ni tajriba binafsi unaweza kutuambia)

d) Of course you are not equal to anyone, haven't you heard that everyone is unique?

Ningeweza kujibu kuwa kama everyone is unique hizo general characteristics zinatoka wapi?, lakini sio hoja ya msingi.

Katika darasa lenye watoto wadogo akaja mwalimu akasema watoto hupenda kucheza pamoja, mtoto anaependa kucheza peke yake anaweza kuacha kujithamini na kujilazimisha kuwa kama wengine

Hilo halikomi kwa watoto tu, athari za aina hiyo zinaweza kumpata mtu katika umri wowote. Kuwa specific ni muhimu ili kuondoa mwanya huo.
 
a) Siyo kila kitu ni lazima kiainishwe, you have to figure out some things on your own(Like, that being a generalization is an obvious fact since you can't define human behaviors in few lines)

b) Generalization kuwa na grouped specifications depends on the level of simplicity that the guy decided to use

c) Honestly naongea toka kwenye experience, wadada wengi stori zao ni about other people (Naomba u note nimesema wengi na siyo wote, asante). Which to many men is so boring!

d) Of course you are not equal to anyone, haven't you heard that everyone is unique?

Kama madada wengi kijijini kwenu wako hivyo haimaanishi madada wengi wako hivyo, usiseme madada wengi wako hivyo, kuwa specific useme madada wengi kijijini kwetu wako hivi.

Kuna wengine tuna dada makenika wa magari, tukisikia unawalundika na wasiojua kuangalia muundo wa gari tunaweza kuona unawatusi.
 
Wanawake wote wakiwa hivi mfumodume hauishi kamwe.

Mwanamke ni lazima abadilike kumfuata mwanamme, hata kama mwanmme ni an antisocial jerk.

Antsocial! mtu hafungi mdomo from the word go?! Kuna muda mtu unapenda kuzungumza na kuna muda unahitaji kukaa kimya na mawazo yako, sasa ukiwa na mtu ambaye hafungi mdomo ni kero kupitiliza-moja ya sifa za mke/mume mwema ni kujua wakati gani mwenzangu anahitaji mazungumzo na ni wakati gani inabidi nifunge domo langu. Ukiweza kujua timing hiyo basi maisha yatakuwa murwa la timing hiyo ukiikosea ndoa/mahusiano utayaona mni kero tupu!!
 
Naona unadandia treni kwa mbele.Na hayo mambo ya gender yamekukaa sana kichwani.Mimi sijatamka kuwa mwanamke ndio wa kubadilika pekee.Nilimlenga aliyeleta mada.Na isitoshe suala la kubadilika ili usimkwaze mwenzio ni la pande zote.Hata wewe Kiranga kama unavitabia vya kulazimisha mkeo awe kama utakavyo badilika.
Halafu tusipende kuhukumu kuwa kila anayeishi kama alivyo kuwa ni antisocial.Tuheshimu interest za mtu.

Siwezi kudandia treni kwa mbele wakati ufunguo ninao mwenyewe. Angalia usiweweseke kwa njozi.

Umelenga mwanamke abadilike kumfuata mwanamme subserviently, hata bila kuangalia mambo yaliyoletwa.

Halafu, kutosema pekee hakukutoi kwenye ukweli kwamba umesema mwanamke abadilike bila ya kuangalia upande wa mwanamme.

Mimi naelewa kuheshimu interests za mtu ndo maana nikasema tuchunguzane compatibility. Maana kuwa na mahusiano na mtu ambaye hamna common ground kunaweza kuwa ni kutoheshimu interests za mtu, so you are not introducing this point.

Mie sitaki kumbadilisha mke wangu awe kama mimi, sina hata pa kuanzia kufanya hivyo kwa sababu sijaoa. Na nikioa swagga langu tu, mwenyewe atataka kuwa kama mimi, wala sina haja ya kumlazimisha. Kwa maana mpaka kuoa maana yake kuna compatibility ya kutosha.
 
Last edited by a moderator:
Antsocial! mtu hafungi mdomo from the word go?! Kuna muda mtu unapenda kuzungumza na kuna muda unahitaji kukaa kimya na mawazo yako, sasa ukiwa na mtu ambaye hafungi mdomo ni kero kupitiliza-moja ya sifa za mke/mume mwema ni kujua wakati gani mwenzangu anahitaji mazungumzo na ni wakati gani inabidi nifunge domo langu. Ukiweza kujua timing hiyo basi maisha yatakuwa murwa la timing hiyo ukiikosea ndoa/mahusiano utayaona mni kero tupu!!

Mpaka kufikia hapo utajionyesha hukufanya homework yako mapema.

We hupendi mtu anayeongea, imekuwaje ukaruhusu kuwa naye huyu?

Hukuona hilo mwanzo?
 
Huwezi kumtegemea mtu ajue wakati hujamjuulisha.

Mweleze kwa maneno mazuri au tafuta njia nyengine njema aweze kusoma moods zako.

Kumtaka mtu aweze kusoma mawazo yako kana kwamba ana uwezo wa ghibu ni kujidanganya tu au dalili za kumchoka
 
Siwezi kudandia treni kwa mbele wakati ufunguo ninao mwenyewe. Angalia usiweweseke kwa njozi.

Umelenga mwanamke abadilike kumfuata mwanamme subserviently, hata bila kuangalia mambo yaliyoletwa.

Halafu, kutosema pekee hakukutoi kwenye ukweli kwamba umesema mwanamke abadilike bila ya kuangalia upande wa mwanamme.

Mimi naelewa kuheshimu interests za mtu ndo maana nikasema tuchunguzane compatibility. Maana kuwa na mahusiano na mtu ambaye hamna common ground kunaweza kuwa ni kutoheshimu interests za mtu, so you are not introducing this point.

Mie sitaki kumbadilisha mke wangu awe kama mimi, sina hata pa kuanzia kufanya hivyo kwa sababu sijaoa. Na nikioa swagga langu tu, mwenyewe atataka kuwa kama mimi, wala sina haja ya kumlazimisha. Kwa maana mpaka kuoa maana yake kuna compatibility ya kutosha.

Hapo kwenye red..ni wewe wasema na unaniwekea maneno mdomoni mwangu.Thats not my point.
Hapo kwenye blue ...thats its.Hongera..hata huyo mleta mada anapaswa kuwa hivo sio kulazimisha mtu.
 
Huwezi kumtegemea mtu ajue wakati hujamjuulisha.

Mweleze kwa maneno mazuri au tafuta njia nyengine njema aweze kusoma moods zako.

Kumtaka mtu aweze kusoma mawazo yako kana kwamba ana uwezo wa ghibu ni kujidanganya tu au dalili za kumchoka

Ndio maana ndoa/mahusiano yanatakiwa kwa watu walio-matured sio kuparamiwa na watoto, hii ikiwa ina maana kwamba unaweza kusoma mood za mwenzio bila yeye kukueleza, ukisubiri akueleza ni rahisi kuhisi visivyokuwepo. Wasio na uwezo wa kuyasoma hayo mara nyingi huishia kuumia roho wakidhani hawapendwi/hawajaliwi
 
Sikuongelei wewe, naongelea a scenario.

Hii case iliyoletwa hapa ni emotional neglect.

Huyu mama anaweza kuwekwa katika majaribu kirahisi sana kama akitokea mtu mwingine akaonyesha kumjali na kumsikiliza.

Tusiwaweke wenzetu katika majaribu kirahisi hivi. Inafaa kusomana tangu mwanzo kabisa na kama mtu hamko compatible, hampotezeani muda kabisa.

But then she will drive you nuts with her stories! Kwa kweli kuvumilia mtu akiongea story ambazo huzipendi kila siku ili kuogopa 'emotional neglect' ni utumwa.
Hapa labda tukubaliane aambiwe kama hana story za msingi anyamaze period!
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mpaka kufikia hapo utajionyesha hukufanya homework yako mapema.

We hupendi mtu anayeongea, imekuwaje ukaruhusu kuwa naye huyu?

Hukuona hilo mwanzo?

Mkuu mtu anaunganisha story non-stop? Huyo sina haja naye kwangu ni kero kubwa
 
sakapal, On Point, yaani on point kabisa.

Kuna watu kuongea utadhani analipia, achia mbali humlazimishi akusimulie yake hata kusikiliza yako tu taabu.

Mie nilishafanya maamuzi magumu, Ninaongea kila ninachojosikia, achambue yanayomhusu.
Ila tatizo langu huwa nataka nikiongea mtu anitazame usoni "eye contact'

Kama kuna tv iko on redio kuna wakati nazima ili tuongee.
Can you imagine ukaongelee wapi?? Au uanze kwenda nyumba ya tatu kupiga story wakati kwako kuna watu?? lol
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana ndoa/mahusiano yanatakiwa kwa watu walio-matured sio kuparamiwa na watoto, hii ikiwa ina maana kwamba unaweza kusoma mood za mwenzio bila yeye kukueleza, ukisubiri akueleza ni rahisi kuhisi visivyokuwepo. Wasio na uwezo wa kuyasoma hayo mara nyingi huishia kuumia roho wakidhani hawapendwi/hawajaliwi

Kunyamaziwa kimya japo haelewi ni bora zaidi kuliko kuelezwa kisa "ni rahisi kuhisi visivyokuwepo"?

Hebu tueleze ni rahisi vipi kuhisi visivyokuwepo kama umeelezwa vyema?
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom