Story ya kusikitisha ya Hudson

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,737
4,252
Kila baada ya chakula Hudson alikua akificha chakula na kuweka kwenye mfuko kisha kuondoka nacho, alikua akikaa huko kwa muda na kurejea, Mama yake alichunguza sana mpaka kujua alikua anapaleka wapi chakula. Aligundua kua mtaa wapili kulikua na kichaa mmoja mzee mtu mzima, Hunson ndiyo alikua akimpelekea chakula.

Kuona vile Mama yake alikasirika na kumkanya kua asimpelekee chakula wala kuwa na karibu naye, Hudson ambaye ndiyo alikua chekechea alilia sana lakini Mama yake hakujali, alimuambia Baba yake ambaye naye alimkataza kuchukua chakula nyumbani na kumpelekea yule kichaa. Lakini Hudson hakuacha aliendelea kufanya vile kila alipopata nafasi ya kuiba chakula.

Baba yake kuona vile alitafuta watu wakamchukua yule kichaa wakampiga na kumuondoa pale, walimpeleka mbali kabisa mkoa mwingine. Hudson alipoenda hakumuona aliishia kulia tu. Siku moja Hudson akiwa anavuka barabara maeneo yaleyale aligongwa na gari na kufa palepale. Wazazi wake walilia sana walihuzunika sana kwani ndiyo alikua mtoto wao wapekee.

Miezi mitano baadaye yule kichaa alirudi eneo lilelile na kuwa anakaa palepale. Siku moja Mama yake na Hudson akiwa anapita maeneo yale alimuona yule kichaa, machozi yalianza kumdondoka kwani alimkumbuka mwanae na alijua kua walimkatisha kufanya wema, alijisikia vibaya kwa kumkatisha mwanae kumsaidia yule kichaa.

Akiwa amesimama anahuzunika alikuja mtoto mmoja nakusimama pembeni yake. “Huyu kichaa siku hizi tangu amerudi amekua mkali sana?” Yule mtoto aliongea, Mama Hudson alimuuliza kwanini? Alimjibu “Mtoto wake amekufa ndiyo maana ana hasira?” Mama Hudson alishangaa kua kumbe yule kichaa alikua na mtoto alimuonea huruma na kumuuliza kama alijuaje kama ana mtoto?

Yule mtoto alimjibu. “Hapana si mtoto wake kabisa sema watu tunasema mtoto wake, kuna mtoto alikua anampenda sana kila siku alikua akija hapa huyu kichaa anakaa katikati ya barabara anasimamisha magari yote mpaka yule mtoto apite, huyo mtoto kwao ni matajiri na alikua anamletea chakula, kichaa alipoondoka mtoto alivuka barabara bila kuangalia Magari akagongwa na Gari na kufa hapohapo”.

Mama Hudson alijikuta anaishiwa na nguvu na kudondoka hapohapo, watu walikuja na kumpepea, alipata fahamu baada ya kama nusu saa hivi akiwa Hospitalini. Watu waliomfahamu walimpigia simu mume wake na alipokuja alimuambia kisa chote kisha akamuambia mume wangu sisi ndiyo tumemuua mtoto wetu! Mumewe hakua na jibu zaidi ya kutoa machozi tu kama mtoto mdogo!

*Ndugu zangu wema hauozi*
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom