Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika??!!

Mtunzi: Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596 email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 4 D : NADHIRI YA MOYO

Nini Salimu aliona??

Tuendeleeee...

...Haaaa, tuondoke hapa hapafai”. Salimu alionekana kupata jibu la maswali yake. Salimu aliongoza njia mkuku mkuku akitazama mazingira huku akitingisha kichwa kama mtu anaye kubalina na jambo Fulani. Karimu nyuma aliendelea kumfata akiwa na mshangao tu hakuelewa kilichojiri ilimbidi awe tu mpole. Salimu alipoteza hamu yote ya kutembea kushangaa shangaa mji alichoamua kuchukua usafiri pamoja na Karimu na kurudi bwenini, tangu hapo Karimu alikuwa mtazamaji tu.

Kibaha High School, Kibaha - Mkoa wa Pwani
Baada Salimu kutuliza akili yake alimuomba Karimu achukue kalamu na karatasi “Kaka naomba uchore kadri vile utakavyo weza kuhusiana na namna nitakavyo kuwa nakuelekeza” “Sawa” Karimu akaanza kuchora taswira za watu kwa mfatano Fulani akisikiliza maelekezo. Ilimchukua takribani nusu saa kumaliza. Salimu aliichukua karatasi yenye mchoro huku akitabasamu kwa namna ya uhalisia aliouona akatingisha kichwa kukubali. Salimu sasa akaanza kusimulia juu ya tukio lile alilolishuhudia kule mjini. Karimu alipatwa na kichaa cha hasira sura ilimfura akaiomba karatasi atazame kwa makini. “Aisee kumbe hawa mbuzi wapo hai sitakubali naapia mpaka wafike pale ninapo pahitaji ama zangu ama zao” Karimu aliongea kwa hisisa kama yeye ndiye anaye husika kwa maamumivu yale. “Kaka tutaweza tu naongelea kesho twende zetu Bagamoyo wale wazee wana busara nyingi hatuwezi kukosa kitu, kuhusu ruhusa niachie mimi.” “Ni kweli” Karimu aliungana na Salimu.

Bagamoyo, Mkoa wa pwani
Mzee Habibu akiwa nje ya nyumba barazani amejikalia huku kiganja cha mkono kakigandasha shavuni mawazo yakimuelemea, Salimu akatokea ndani na kukaa pembeni yake. “Samahani baba nimesikia ukiniita” Mzee Habibu aligeuza shingo yake na kumtazma Salimu, “Ndio mwanangu…ninacho kuomba usije litumia jina la Pius wakati huu ni bado mapema sana, kingine…”. Mzee Habibu akaanza kukuna ndevu zake na kuzivuta vuta “…imeniuma sana kuona bado wahusika wapo hai wakilanda landa kufurahia maisha”, “Mimi pia sikukiamini nilichokiona kwa macho yangu tena mmoja wao ana mkono kipisi na manguo yao meusi” “Mwenyezi mungu awasimamie kwa kweli” mazungumzo yao yakaishia hapo.

KALAGI MUKONO - UGANDA
Majibizano yenye wingi wa mabishano yalisikika yakiendelea ndani ya kijumba cha mbao katikati ya shamba la Migomba. Nje palionekana magari meusi mawili yakifahari yaliyoegeshwa kwa mfatano karibu kabisa na kijumba hicho. Ndani ya usiku huo mzito wa mbalamwezi ang’avu katika kipindi cha kipupwe watu wawili tu pekee ndio walionekana kirahisi wakiwa wamevalia suti nyeusi tii na miwani zao nyeusi wamesimama kwa tahadhari huyu akitazama huku na yule kule kama milingoti iliyosimikwa ardhini bila kutikisika, mikono ikiwa imekusanywa mbele ya vifua kila mmoja akitazama mbele kuihakikisha ulinzi pahala hapo. Licha ya kelele zile za majibizano kufifia na kuzuka hazikufanya kuzuia sauti za wadudu wa usiku pamoja na vyula kuacha kulia. “…Tafadhari naomba acha kunifatilia, mbona hunielewi? kila ninapo kwenda kuweka makazi unanifata, mimi sitaki”. Bwana wa makamo aliongea kwa hasira huku akisimama toka katika kiti cha mbao alichokalia akipiga hatua kumsogelea mtu aliyekuwa akijibizana naye muda mrefu bila maelewano misuri imemtoka mwili umemvimba tayari kwa mapigano.

Haraka walinzi wakawa tayari kumkabili mzee huyo na yeye bira hofu alibenua midomo yake kwa dharau “…eii acheni msifanye lolote, anayo haki muacheni anipige”. Mabwana wale wawili waliokuwa tayari wameshamsogelea mzee huyo wakarudi hatua moja nyuma na kukaa vile walivyokuwa mwanzo. “Komando Ochola nisikilize…natarajia kugombea Uraisi, na mimi ni mmoja ya watu wanaoipenda sana nchi hii”.

Bwana huyo aliongea kwa sauti ya huruma akimtazama Komandoo kwa jicho la kuomba kitu. Kisha akaongea “…naomba rudi ukae kitini kwa heshima yako” Komandoo alihema kwa kutoa pumzi nyingi toka mdomoni mwake akatazama sakafu ya mbao mikono ikiwa tayari kiunoni akajikuna pua yake akijishauri shauri akanyanyua uso wake na kuwatazama jamaa hao kwa zamu kisha akageuka kurudi katika kiti alichokuwa ameketi muda mfupi uliopita akakaa na macho yake yakimtazama bwana yule aliye kuwa akijibizana naye. Yule bwana akajiweka vizuri kola yake kisha akaongea “Hata kama sitafanikiwa kuwa Raisi wa nchi hii najua nitapata nafasi nzuri serikalini na nitafanya kila hila niwe karibu na muheshimiwa huyo mpya nimshauri juu ya jambo hili nakuahidi”. Komandoo kwa jicho la makini akamtazama vizuri bwana yule kisha akauvuta mguu wake wa kushoto na kukunja nne akatabasamu kisha akacheka kivivu alafu akatingisha kichwa chake akisikitika. “Unajua nini bwana mdogo usinilazimishe kufanya kitu nisichokipenda kazi hii naichukia sana, mimi sipo tayari, nakushauri kampe mtu mwengine”. Bwana yule akiwa na macho yakukata tamaa akakusanya viganja vyake vya mikono na kuviweka pajini mwa uso wake akakaa hivyo kwa dakika hivi kisha akavitoa na kumtazama Komandoo pale kitini kisha akaitazama taa ya chemli iliyokuwa imewekwa katika kimeza cha mbao akayatafakari maneno ya Komandoo kisha akakokhoa kidogo “Komandoo hii ni mara yangu ya mwisho kukushawishi sitarudia tena, unakumbuka familia yako ilivyo angamizwa kikatiri ulipo kuwa Israel..”

Itaendelea...

Aiseee usikae mbali stori inazidi kuwa tamu
AKIDA%20S.%20RAMBAO%20%3D%20THE%20HIDDEN%20TRUTH%20(UKWELI%20ULIOFICHIKA)%20(2).jpg
 
Subscribe hapo juu ili iwe rahisi kupata muendelezo kila nikituma.
 
(The Hidden Truth) Ukweli uliofichika

Mtunzi: AKIDA SIRI RAMBAO
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 4 E: NADHIRI YA MOYO

Tuendeleeee...
...Ochola akikokhoa madamu tu mwili ukimuishia nguvu kiza kizito kilianza kufunika macho yake. Bahati kiliingia kikosi cha usalama cha nchi ya India na bwana yule alikimbia kunusuru maisha yake akiamini alishamuua Komandoo Ochola. Na ndipo Komandoo Ochola alipo okolewa na kuhudumiwa kisiri mwisho akatoroka katika Hospitali ile na kukimbilia kusiko julikana.

“Komandooo….” Bwana yule alilitaja jina hilo na kumtoa kabisa Ochola katika bahari ya mawazo safari hii macho yakiwa mekundu kwa hasira “…hebu ona umekuja jificha huku maisha magumu unaikimbia haki yako, uliapia nini siku ile ulipokuwa unajiunga na jeshi?...sasa sita kufata tena lakini kumbuka kwa sasa Tanzania ni kama hiyo chemli inayotegemea mafuta kutoa nuru siku sio nyingi mafuta hayo yataisha na utaghalimika kuyapata”, komandoo Ochola aligeuza kichwa kuitazama chemli pekee iliyopo varandani hapo na kuyarudisha macho kwa bwana yule ambaye alianza kugeuka kuondoka, bwana yule akatembea hatua kazaa kisha akageuza kichwa “…lakini kumbuka pia mauji ya Joka hayakuwa yakawaida na hakuna aliyewagundua wauaji mpaka hivi leo, unakumbuka mchango wake lakini?! Basi jaribu urudi japo kwa ajili ya Muheshimiwa Richard aliyeuwawa kikatili mengineyo ukiyafanya basi itakuwa kwa ajili ya nchi yako hakuna atakaye kuzuia”.

Bwana yule akageuka tena kichovu na wale walinzi wake nao wakageuka tayari kwa kuondoka.

Kabla hajamaliza kutoka katika mlango Komandoo Ochola akasimama “Subiri…” yule bwana akiwa kasha toka nje hakuamini masikio yake “Komandoo Swai ndiye alijaribu kuniua kule Israel na ndiye alimuua Patric…Nitaifanya hii kazi lakini itakuwa ndio kazi yangu ya mwisho katika maisha yangu”. Komandoo Ochola aliongea kwa kujiamini. Bwana yule kwa furaha alirudi ndani na kumkumbatia Komandoo Ochola “Asante sana kaka” kisha akatabasamu kwa dharau akiupindisha mdomo wake alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani Bwana Fanuel Ebarik Mkwasi.

Haya Sasa tunaona Komando Ochola aniingia Mzigoni kufanya kazi ya Waziri Fanuel Mkwasi,

Nini kitajiliiii

Endelea kusoma kwa utulivu mazuri zaidi yanakuja




ITAENDELEA
IMG-20211211-WA0046.jpg
 
(The Hidden Truth) Ukweli uliofichika

Mtunzi: AKIDA SIRI RAMBAO
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 4 F: NADHIRI YA MOYO

Tuendeleeee...
...Ochola akikokhoa madamu tu mwili ukimuishia nguvu kiza kizito kilianza kufunika macho yake. Bahati kiliingia kikosi cha usalama cha nchi ya India na bwana yule alikimbia kunusuru maisha yake akiamini alishamuua Komandoo Ochola. Na ndipo Komandoo Ochola alipo okolewa na kuhudumiwa kisiri mwisho akatoroka katika Hospitali ile na kukimbilia kusiko julikana.

“Komandooo….” Bwana yule alilitaja jina hilo na kumtoa kabisa Ochola katika bahari ya mawazo safari hii macho yakiwa mekundu kwa hasira “…hebu ona umekuja jificha huku maisha magumu unaikimbia haki yako, uliapia nini siku ile ulipokuwa unajiunga na jeshi?...sasa sita kufata tena lakini kumbuka kwa sasa Tanzania ni kama hiyo chemli inayotegemea mafuta kutoa nuru siku sio nyingi mafuta hayo yataisha na utaghalimika kuyapata”, komandoo Ochola aligeuza kichwa kuitazama chemli pekee iliyopo varandani hapo na kuyarudisha macho kwa bwana yule ambaye alianza kugeuka kuondoka, bwana yule akatembea hatua kazaa kisha akageuza kichwa “…lakini kumbuka pia mauji ya Joka hayakuwa yakawaida na hakuna aliyewagundua wauaji mpaka hivi leo, unakumbuka mchango wake lakini?! Basi jaribu urudi japo kwa ajili ya Muheshimiwa Richard aliyeuwawa kikatili mengineyo ukiyafanya basi itakuwa kwa ajili ya nchi yako hakuna atakaye kuzuia”.

Bwana yule akageuka tena kichovu na wale walinzi wake nao wakageuka tayari kwa kuondoka.

Kabla hajamaliza kutoka katika mlango Komandoo Ochola akasimama “Subiri…” yule bwana akiwa kasha toka nje hakuamini masikio yake “Komandoo Swai ndiye alijaribu kuniua kule Israel na ndiye alimuua Patric…Nitaifanya hii kazi lakini itakuwa ndio kazi yangu ya mwisho katika maisha yangu”. Komandoo Ochola aliongea kwa kujiamini. Bwana yule kwa furaha alirudi ndani na kumkumbatia Komandoo Ochola “Asante sana kaka” kisha akatabasamu kwa dharau akiupindisha mdomo wake alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani Bwana Fanuel Ebarik Mkwasi.

Haya Sasa tunaona Komando Ochola aniingia Mzigoni kufanya kazi ya Waziri Fanuel Mkwasi,

Nini kitajiliiii

Endelea kusoma kwa utulivu mazuri zaidi yanakuja




ITAENDELEA
IMG-20211211-WA0046.jpg
 

Attachments

  • IMG-20211211-WA0046.jpg
    IMG-20211211-WA0046.jpg
    21 KB · Views: 35
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika??

Mtunzi : AKIDA SIRI RAMBAO
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU 4 G : NADHIRI YA MOYO

Ngome Msitu wa Magamba, Lushoto- Tanga

Wasichana watatu warembo wakiwa wamevalia suruali nyeusi za kubana pamoja na makoti meusi yaliyoachiwa vifungo yakipepea huku vifua vikiwa vimessitiliwa na sidiria vitovu vikiwa wazi walikuwa bize wakitembea kikakamavu macho mbele wakikatiza baadhi ya majengo yaliyopangwa kiustadi huku kelele za wanaume wa nguvu wakiwa mishughulikoni kimakundi zikiendelea wengine wakipiga miruzi ya shangwee.

Ukomo wao ulifikia katika jengo moja zuri zaidi lililokuwa na walinzi wa kutosha kuzunguka jengo hilo wakiwa wamesimama tayari kushambulia bunduki zikiwa mikononi machoni miwani meusi baada ya ukaguzi walipata fulsa ya kuingia mjengoni. Katika varanda kubwaa iliyonakshiwa kwa epoxy na kupafanya paonekane kama kasri ya kifalme.

Wanaume wawili watuwazima wakiwa wamevalia suti za kufanana walionekana kuwa bize na mazungumzo wakitazama Laptop huku moshi mzito ukiwa umesambaa pahala hapo kutokana na sigara walizokuwa wakizivuta hawakuonekana kujali waziwazi walionekana kustahereka. “Sawa hakuna shida tumekuelewa” aliongea mmoja wao wale mabinti watatu wakasimama na kusalimia kikakamavu salamu yao iliwafanya wageuze viti vyao kuwatazama mabinti hao kila mmoja kwa nafasi yake. Mmmoja wao kwa haraka akaifunga laptop iliyo katika meza kisha akachukua birauli ya mvinyo akanywa kidogo kisha akairudisha glass ya wine katika meza kuubwa ya kioo kigumu na kuikunja miguu kwa kuweka namba nne, bwana huyo mnene mweupe mwenye mvi zilizonawiri sana katika eneo la karibu na paji la uso akatabasamu huku macho yakitembea kuwakagua mmoja baada ya mmoja kisha akaongea “Karibuni sana warembo” mabinti kwa pamoja waliitika kwa sauti zao nyororo. “Naamini mmepumzika tosha katika likizo zenu mlizopewa, karibuni kazini” aligeuka na kumtazama mwenzake ambae muda huo alikuwa akinyoosha nyoosha vidole vya mikono yake kisha akaongea “Unaweza ukaawambia tu mpango mpya” aliongea mwenzake akiisigina pisi la sigara katika kiota chake macho yakirudi kwa wasichana, bwana yule mwenye mvi katika eneo la karibu na uso akajikokholesha kisha kuanza kuongea akiwatazama wasichana mbele yake “Siku zijazo kuna mrusi atakuja hapa nchini na atafikia katika Hotel ya Wave land jijini Dar es salam kinachotakiwa ni kufanya kama kazi yenu inavyo wataka, maelekezo mengine mtapewa na kiongozi wenu wa idara, mnaweza kwenda, mjiandae kwa kazi” alimaliza na kumuangalia mwenzie “…Una mashaka na jambo lolote bwana Peter?” Pater akauminya mdomo kwa pembeni kwa dhihaka “…hakuna shaka niliyonayo ndiyo uliyonayo bwana Samuel” wote wakatabasamu na kuwaacha mabinti wakisindikizwa na wanaume wa nguvu wenye misuri iliyojaa kutoka nje mikononi wakiwa na bunduki za kisasa. “Hivi jamani mlimtambua yule bwana aliye kuwa katika Laptop pale tulipo ingia sauti yake sio ngeni” Mmoja ya wasichana aliongea huku akigeuka kuwatazama wenzake “Wala lisikushughulishe achana nalo dada Meroda” aliongea mmoja wao.

Wave land Hotel, Mbezi-Dar es Salam
Milango ya gari aina ya Jaguar XF 3.0 ilifunguka na warembo watatu wakavichomoza vichwa vyao wakitazama huku na kule kisha wakamalizia viwili wili, loo! Hawakuwa tu wanawake wazuri bali walikuwa wanawake wenye kusisimua kwa mionekano yao, kwa mwendo wa sina habari wote walielekea upande wa mapokezi huku wakikokota mabegi yao. Wave land Hotel moja ya Hoteli maarufu sana katika jiji la Dar es salam maeneo ya Mbezi. Hoteli inayokusanya wageni mbalimbali toka nchi za ughaibuni ikisifiwa kuwa na fukwe nzuri ya mchanga mweupe pee, kumbi za mikutano, sehemu nzuri ya malazi pahala pa kupata vyakula vya kila namna kwa mataifa mbalimbali. Watu wa kawaida choka mbaya wazawa wa nchi walikodolea tu kwa mbali kwa sababu ya gharama kuwa kubwa.
Meroda akaweka mikono juu ya meza ya mapokezi, “Hi” Binti aliye katika mapokezi alituliza vidole vyake vilivyokuwa bize na uchapaji akatabasamu, “Hi” alijibu salamu “Sorry there room paid here for the name Penina Jacob” aliongea Meroda “Ohh wait, that I will watch please” muhudumu alirudisha macho katika Compueter yake “Peninaaa pennii” alilitaja jina hilo na kuacha lipsi za midomo yake kuachana kwa muda “Ohh yes I found, Room number 149 double” aliongea huku akimtazama Meroda kwa tabasamu pana, “Okay thanks” aliongea Meroda dada wa mapokezi alichukua simu ya mezani nakuongea kidogo, “Sorry, Hotel worker will take you to the room, wait a minutes” “Thanks” Meroda alimjibu muhudumu na kutoa simu yake katika kipochi aliyo ning’iniza katika bega lake punde alionekana msichana akisogelea maeneo ya mapokezi hatimaye alifika kabisa, “Ndio dada” muhudumu alitoa funguo katika droo ndogo na kumpatia dada huyo aliyewasili pahala hapo. “You can follow her” Meroda aliwapa ishara wenzake na kuanza kumfata muhudumu nyuma nyuma.

Itaendelea...

Mambo Ni moto

Mmewaona wadada wa kazi????
 
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao

Nani Anahusika??

MSIMU WA PILI

SEHEMU 4 H : NADHIRI YA MOYO

Tumewaona wadada wa kazi watatu wameagizwa na Peter na Samuel kumfatilia Mrusi aliyefika kwa Siri kupeleleza Biashara zao haramu

Tuendeleeee

.... “Ndio dada” muhudumu alitoa funguo katika droo ndogo na kumpatia dada huyo aliyewasili pahala hapo. “You can follow her” Meroda aliwapa ishara wenzake na kuanza kumfata muhudumu nyuma nyuma.
Baada ya kuachwa vyumbani na muhudumu kuondoka, wakaweka vitu vyao vizuri, wakaanza majadiliano baada ya muda wakabadili nguo zao na kuvaa mavazi ya kuogolea na kutoka. Maumbo yao wote yalikuwa waziwazi kabisa sehemu nyeti tu ndizo zilizohefadhiwa na sehemu kubwa ya miili yao ikiwa wazi kabisa tena wakiwa hawana shaka wala wasiwasi wowote, huo ndio utandawazi mwili wazi. Ilikuwa ni jambo la kustaajabisha kwa wale wazawa ambao wamefika hapo kwa mara ya kwanza lakini kwa wale wenyeji wa hotel hiyo walipachukulia kama fukwe kubwa za bahari kama Baia do Sancho nchini Brazil ambayo ilikusanya wanawake wazuri waliotapakaa kwa mavazi ya nusu uchi wakipita huku na kule.

Mavazi waliyoyavaa kwa muonekano haikuwa rahisi kuwatambua kama mabinti hawa walikuwa ni watanzania, wengi waliopishana nao na walio waona kwa mbali waliamini kuwa mabinti hao watakuwa ni watarii tu. Kwa kweli utanda wazi ulitawala na kuharibu jamii nyingi za kiafrika hasa jambo la mavazi. Mabinti hao warembo walitafuta sehemu tulivu ambayo iko wazi mtu yeyote aweze kuwaona na wao kuweza kuwa huru, kwa bahati waliipata wakaweka mambo sawa na wakajituliza katika viti mlalo walivyovikuta pembezoni mwa minazi mingi iliyopandwa kimstari surani miwani za jua zikiwa machoni. Wanaume kazaa waliobahatika kupita pembezoni mwa mabinti hao hawakupita salama shingo walizigeuza kisha kuondoka zao wakisononeka na nyoyo zao kwa uzuri walio jionea, si wake wala si waume wote walikubali kuwa sehemu hiyo siku hiyo imevamiwa na mamalkia wa urembo. Meroda alichukua simu yake ya mkononi akaandika namba akazikagua kisha akazipiga huku mkono wake ukisogea eneo la sikio huku umeshikilia simu kusikiliza upande wa pili kwa yule anaempigia.
Wakati wote huo wenzake walionekana wakiwa bize wakijisomea majarida ya kizungu kana kwamba hawana habari au kujua kinachoendelea. Punde kijana mtanashati aliye valia nguo zinazoonesha kuwa ni mmoja ya wahudumu katika Hotel hiyo akafika pahala hapo huku mkononi akiwa kabeba sahani ya kioo ikiwa na glasi ndefu tupu zikiwa zimezungushiwa tishu kwa ndani huku kopo la juisi ya mchanganyiko wa matunda na mirija yake huku ikiwa imepambwa kuwavutia wateja. “Habari zenu warembo” bila kusikiliza majibu ya wasichana hao aliweka glass za juisi kwa zamu zamu katika kimeza kidogo cha mbao kilicho kuwa pembeni ya kila kitanda mlalo na Meroda huku macho yakiwa kwa Meroda. Meroda na wenzake waliitika huku wakionesha hawana mpango na kijana huyo.

Kijana muhudumu baaada ya kumaliza akaondoka na kupotelea alipotokea.
*****
Meroda na wenzake wote walikuwa nazo habari zote zinazo muhusu Mrusi huyo waliyemfata hapo Waves land, wasifu wote wa Mrusi walikuwa nao mikononi madhaifu yake yote waliyajua ikiwemo tabia yake ya unywaji wa pombe kali na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kujiiba iba na kupenda sana wanawake wazuri wazuri kama wao, ilikuwa ndio maradhi yake. Hivyo kwa mionekano yao waliyokuwa nayo uzuri asilia haitakuwa rahisi kwa mrusi huyo kushindwa kumchombeza mmoja kati yao au kuwataka wote kwa dau nono kama wageni wengi wafanyavyo wafikapo nchi za kiafrika kwa ajili ya anasa za kingono.
Ujio wa mrusi huyo nchini ulikuwa ni wasiri sana na ulikuwa ni wakiserikali, taarifa za ujio huo zilivuja na kuwafikia kina Samuel. Ujio wa Mrusi huyo ulitokana na kuzidi kwa matukio ya kiharifu na kuifanya serikali kuchanganyikiwa.

Wananchi walichoka kwa maovu yaliyokuwa yakifululiza na kutangazwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ambayo asilimia tisisni yalikuwa yakisababishwa na Samuel na Pater. Benki zilivamia mchana kweupe, super market, maduka makubwa na hata wafanya biashara wakubwa waliuuwawa na pesa zao kuchukuliwa. Hivyo basi serikali iliamini kuja kwa mrusi huyo mwenye mafunzo makubwa ya upelelezi toka katika jeshi la Urusi kwa mchango wake kwa kushirikiana na mapolisi wakipelelezi walioandaliwa na serikali basi watafanikiwa kupata mwanga wa kuyatatua matatizo yanayo waandama.

*****
Meroda akiwa amejilaza akageuza shingo huku na kule kutazama kama anaweza kumuona Mrusi, macho yalikazana kutafuta kwa kuwapekua wazungu waliokuwa wamekaa makundi makundi kwa mbali wakiogelea wengine wakiwa wakitembea na familia zao. Mara alishtuliwa na mlio wa simu yake ya mkononi kiasi cha kuwafanya wenzake nao kumtazama, alipokea “Yes…Ohh okay I get you”, alikata simu yake. “Warembo mrusi yupo maeneo haya haya anashangaa shangaa...

Itaendelea

Hayaa tuendeleeee kuinjoy
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao

Contact 0658328596

MSIMU WA PILI

SEHEMU 4 I : NADHIRI YA MOYO

Tuendeleeee...

....“Warembo mrusi yupo maeneo haya haya anashangaa shangaa sasa tunyanyuke kazi imeanza twendeni tukaogelee, lakini macho yetu yawe macho tusijisahau” wenzake walitabasamu tu wakanyuka kuyafata maji ya bahari kwa shangwe. Nyakati hizo upande wa nyuma karibu kabisa na Hotel alionekana kijana mmoja wa kizungu akiwa kavalia singrend na kamptula kubwa mkononi akiwa na glass ya mvinyo machoni akiwa na miwani kuubwa huku cheni ya rangi ya dhahabu ikiwa imezunguka shingo yake. Kijana huyo wa kizungu alionekana kutabasamu kisha akatingisha kichwa kwa kile alichokiona, akaanza kupiga hatua fupi fupi kuelekea sehemu za fukwe huku akinywa kidogo kidogo mvinyo wake macho yakiwa yamekaza kule alipo ona kitu maalumu.
Meroda aliwatazama wenzake taratibu akatoka na kuelekea ufukweni kwa mwendo wa madaha akifata sehemu ile walipo fikia kwa ajili ya mapumziko. Meroda alitembea huku akizikamua nywele zake kitu ambacho kilimfanya kijana wa Kirusi kulamba midomo yake kwa uchu wa mahaba aliokuwa nao, hakuishia kujilamba midomo tu laa bali alijikuta akijikuna kichwa kuonesha kutokuamini macho yake ambayo yalikuwa yakipita yakisawiri mazingira ya umbo la Meroda kuanzia kifuani hadi sehemu za hips. Meroda aliendelea kupotezea maana alimuona kwa kumtazama kwa macho ya chini chini, alisogea alipo pakusudia na kuketi kisha akanyoosha miguu yake akiwatazama wenzake ambao waliigiza kumuita na yeye kukataa kwa mapozi.

Kijana wa kirusi uvumilivu ulimshinda alisogea karibu na kukaa katika moja ya kitanda, alijikohoresha kidogo kitu kilicho mfanya Meroda kugeuza shingo yake kumtazama kwa jicho legevu lililo maliza pumzi yake “Hallow Beuty”, Meroda akatoa tabasamu pana “Ohh, Hallow”, ilikuwa sauti mwororo iliyogonga na kutibua kabisa mishipa ya damu katika mwili wa Jackson. Maana ngoma za masikio zilishangazwa na uzuri wa sauti hiyo matamshi yalitamkikaa na kusikika vema kisha huyo akachukua mafuta yake katika kipochi kidogo alicho kiweka pembeni kidogo ya kiti mlalo na kuanza kujipaka miguuu yake kwa mapozi makubwa kitendo ambacho kilizidi kummaliza sana kija wa Kirusi na kujikuta akishindwa kujielewa aongee nini. “Ahh my name is Jackson …am come from Russia and… am here for short work” aliongea huku macho yakiwa yameganda katika sehemu za mapaja ya Meroda huku uchu wa ngono ukimjaa kama upepo katika mpira. Meroda aligundua hilo alitabasamu na kumgeukia, “Ohh okay welcome, so are you alone here” Kijana Jackson akatabasamu kidogo baada ya kupata fulsa ya kuendelea kupiga domo, “Yes of course am alone…” basi waliendelea kuongea mawili matatu mpaka wenzake wakarudi na kuungana nao wakajikuta wanazoeana stori zikaendelea wee mpaka kigiza kikaanza kusogea. Kijana Jackson hakuzificha hisisa zake alizionesha hata kwa marafiki wa Meroda hukunakiomba usiku wa siku hiyo waende wakapumzike pamoja, lakini Meroda alikataa kata kata na kumfanya kija wa kirusi kukaribia kutokwa na machozi maana alionekana kumpenda ki kweli kweli msichana Meroda huku akiahidii kuondoka nae kwenda naye Urusi baada ya kumaliza kazi iliyo mleta Tanzania.

Ama kweli hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha mrusi wa watu leo amelowa hana ujanja moyo umekosa kuvumilia juu ya kumkosa Meroda toto la Kihaya. Marafiki wa Meroda walimkazania Meroda akubali kwenda kupumzika na kijana wa Kirusi ili wafahamiane vizuri kitu ambacho Meroda aliigiza kukataa kila wakati, mwishowe nae akajifanya kukubali kishingo upande na kunyanyuka kuelekea Hotelini huku Meroda akiwapa ishara wenzake ya kuanza kazi.
Baada ya muda kupita
Meroda akanyanyuka na kutoa kichwa chake kifuani mwa Jackson “Sorry am going to the washroom rignt wayToilet”, “Ok no problem” Jachson akakaa sawa kumpisha Meroda huku akitazama sehemu za nyuma za mwanamke huyo aliyetoka akiwa mtupu kabisa kama alivyo zaliwa akamsindikiza kwa macho mpaka alipopotelea bafuni akailamba midomo yake mawazo yakamchukua alijikuta yupo mbali akiwa na Meroda wakifurahia maisha wakiwa na watoto akajikuta anatabasamu. Upande wa Meroda akiwa chooni alionekana kuwa na wasi wasi sana sura yake ilikuwa na wingi wa mashaka na kuchanganyika na huruma.

Alijitazama katika kioo huku akijiosha uso mara kazaa na kuendelea kujitazama tena mwishowe aliuma meno na kutoka. Jachson bado alikuwa kitandani alipo muona akatabasamu “you are welcome my Beutiful” “Thanks I’m here” Meroda alijisogeza karibu zaidi na kujilaza akiwa kampa kumbatio muruwa akiendela kumpumbaza Mrusi wake. “Ohh, how about Diner” Meroda alijifanya kushtuka kidogo “Ohh let’s ask them” Meroda alijinyanyua kichovu chovu na kusogelea simu ya mezani akabonyeza namba husika na kupiga, aliongea kidogo na kukata akatabasamu na kumgeukia Jachson. Jackson akayanyuka na kutoka kitandani kwa furaha na kumkumbatia Meroda huku akionesha hisia za maombi ya busu Meroda alionesha utayali na kumkubalia hivyo wakajikuta wakiwa wameingia katika sayari ya mahaba mazito. Mara walikatizwa na kengere ya mlango iliyogongwa kwa nje “Shit…” Jackson alionekana kuchukizwa sana lakini alijitahidi kujizuia asionekane na Meroda, Meroda alitoka kifuani wakiwa bado wamesimama, “Excuse me” “Okay” Meroda alisogea hadi katika mlango akachungulia kwenye kioo cha jicho moja kilicho pachikwa katika mlango kwa ajili tu ya usalama, baada ya kuona kuwa ni muhudumu akafungua. Kijana yule yule aliye wahudumia mchana kule ufukweni akiwa na mavazi ya upishi akaingia akisukuma kitololi kidogo kilicho na meza juu iliyo sheheni baadhi ya vyakula na vinywaji, “Welcome” akaingia bila kuongea kitu hadi mezani na kuanza kupanga vitu alivyokuja navyo, akamaliza akaomba ruhusa ya kutoka huyo akaenda zake. Jackson akatabasamu “So….” Meroda alimtazama Jackson “Now take a shower and eat and enjoy the night together” Jackson akatabasamu

Itaendelea
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

MTUNZI: AKIDA SIRI RAMBAO
Contact : 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU 4 J : NADHIRI YA MOYO

Ilipoishia

“So….” Meroda alimtazama Jackson “Now take a shower and eat and enjoy the night together”

Tuendeleeee...

Jackson akatabasamu akaitoa bukta yake na nguo ya ndani peupe bila aibu na kubaki mtupu kisha akaelekea bafuni. Meroda akatabasamu akanyanyua sahani zilizofudikizwa kwa makini, moja kati ya sahani aliona paketi tatu za madawa ya kulevya akazichukua na kuziweka ndani ya sidiria yake. Alisogea kitandani akavua nguo zake chapu chapu na kubakia kama alivyo zaliwa, akalisogelea Taulo lililo tundikwa katika kitundikio akalivaa kuanzia kifuani kushuka chini, baada ya kumaliza akajilaza kitandani. Sauti za mlango ukifungwa zilisikika, “Very beuty full” aljisemea Jackson huku akipiga hatua fupi tabasamu likiwa usoni mwake akitazama umbile la meroda lililompa mgongo “ I feel like I’m already married” aliongea Jackson na kumshika bega Meroda. “Hee! You showered so fast, now let’s eat I’m hungry” Meroda aliongea na kujinyanyua kivivu vivu huku akimshika bega Jackson na kunyanyuka akitangulia sehemu ya meza ya chakula. Walipata chakula pamoja wakileta gumzo za hapa na pale wakicheka kwa sauti mara kazaa.

Kisha wakaingia kitandani, macho ya uchu na kiu ya penzi yalijidhihirisha machoni Jackson akalipokea busu toka kwa meroda huku mikono yake ikipita sehemu mbalimbali za mwili akibinya hapa na pale akisikilizia miguno yahaja toka kwa Meroda aliyekaa juu ya mapaja yake. Ghafla binvuu Jackson alishtuka na macho yaka mtoka haswa bila kutegemea sindano ilikitwa shingoni mwake na kushindiliwa vizuri. Jackson akalegea na kuangukia kitanda bila kufurukuta. “Una masaa mawili tu mpaka kupata fahamu zako Jackson”.

Akanyanyuka toka mapajani hadi katika pochi yake akachukua gloves na kurudi tena kitandani Akamvuta na kuanza kumburuta taratibu hadi bafauni, alichukua dakika tano kumuogesha vizuri na kumfuta kisha akamrudisha kitandani.
Chapu kwa haraka akakimbilia mkoba wake nakutoa paketi yeye kitu kama unga pamoja na bomba mbili za sindano zikiwa na dose ndani yake ‘Pole sana Jackson na hongera kwa kupata busu langu tamu kirahisi nenda kawasimulie wafu waambie hukubahatika kubega apple’ alipo maliza kuongea na nafsi yake alisogea karibu kabisa na sehemu aliyo lala Jackson akachukua mkono wa Jackson wa kuume na kutafuta mshipa akadunga sindano moja ya dose ya madawa ya kulevya akachukua na ya pili akafanya tena. Akaikata paketi ya unga na kumuwekea puani alipotosheka akaiweka paketi juu ya meza ndogo yenye mvinyo aina ya Madiera inafahamika kama Island wine toka Ureno “Kwa kheri Jackson ukifanikiwa kuamka uje unioe bure”
Meroda hakumaliza kazi yake akageukia vyombo alivyokuwa amevitumia tangu alipo fika pahala hapo kwa ustadi akaanza kuvifuta, na kuendelea kufuta kila sehemu aliyo amini kuna ushahidi wake mwishowe akachukua funguo ya chumba na kuiweka juu ya droo ya kitanda akavaa nguo zake na kutazama kila pembe kisha akaondoka zake usiku huo huo. Jackson alibaki pale pale alipo egemezwa akiwa hajielewi wala hajijui udenda ukianza kumtoka mdomoni twee bila kuzuiliwa na mdomo.
Meroda alitoka chumbani na kufunga mlango kwa nje kwa kutumia funguo malaya alitoka kwa kujificha ficha akaitazama kamera ambayo ilikwa ikizunguka katika kordo ya vyumba kutazama ulinzi akaivizia mpaka ilipotazama upande mwengine nae akajitoa katika kipenyo cha ukuta huku akiwa kajificha uso wake kwa kikoi kama alivyoingia mwanzo muda ule alipo ongozana na Jackson kwa wasiwasi wa kutambulika.

Safari ilimpeleka mpaka katika chumba chao walichopanga mara moja akingia.

Asubuhi, Ilisikika sauti ya mluzi ukipigwa katika Kordo, alikuwa ni Muhudumu akiwa kavalia mavazi ya upishi taratibu akiburuza kitololi akasimama katika moja ya mlango na kubisha kwa kubonyeza switch akarudia tena na tena lakini ilikuwa kimya akaamua kuufungua kwa funguo yake “Hallow Morning Mr Jackson” aliita baada ya kuingia ndani “Akirudi atakuta chai yake hapa” alijisemea akapiga hatua kazaa nakuweka alivyobeba katika meza na kuchukua alivyo vikuta lakini alipo geuza kutaka kutoka ndipo alipo pata mshtuko mkubwaa sana, alimshuhudia Jackson akiwa amejiegemeza kitandani hajielewi wala hajijui mkononi bomba la sindano likining’inia na mdomoni na mapovu yaliyomkakuka mdomoni, aliacha kila kitu kwa uoga na kutoka mbio.
*****

Walinzi wa Hotel pamoja na baadhi ya viongozi wa Hotel walipata habari juu ya tukio la kustaajabisha katika chumba alichopanga mteja wao Jackson, hivyo walikusanyana wakitaka kushuhudia yale yaliyo jili. Watu hao walipofika na kushuhudia wakaamua kuita maporisi waje watazame na kutoa taratibu zingine za kiusalama, haikuwa rahsis kufanya haraka haraka lakini iliwezekana baada ya watu wakubwa wanaojua dhamira ya ujio wa mgeni huyo kuingilia kati na kumtoa haraka haraka ili mapolisi wengine na jamii isitambue yale yaliyofichikanwa waliamua kuuchukua mwili na kuupeleka hospital kwa ajili ya uchunguzi wakimchukulia kama ni mtu wa kawaida tu. Walio jua baada ya kujua walishikwa na mshangao maana mazingira ya kijana huyo kukutwa na madwa ya kulevya ili dhihirisha kuwa alikuwa ni mtumiaji na alijiover dose, polisi wa kawaida wasiojua kitu walitaka kuishikilia kesi hiyo na kuichunguza lakini walitulizwa na viongozi wao na kuwaachia watu ambao hawakuwajua ni akina nani lakini walitambulishwa kwao ni maafisa usalama hivyo wao ndio watakao shughulikia kesi hiyo, wakabaki na alama za mshangao na kutii amri. Wageni waliokuwa sehemu hiyo pia walitulizwa na kufichwa fichwa hata wahudumu waliambiwa watulie wasiongee kitu zaidi ya kusema kuwa mteja wao alizidiwa usiku kwa hali mbaya na kupelekea kuzimia na sio kuongelea hali halisi iliyotokea hilo lilikuwa ni agizo la maafisa kivuli walio fika eneo hilo ambao lililowaacha watu wengi na alama za mshangao.

Hivyo taarifa za Jackson zikazimwa chini na Hotelini pakawa kama hapakutokea jambo lolote lile la kuogofya, Ilistaajabaisha sana.

Wananchi bado waliendelea kupata shida hakuna aliyeelewa nchi imepatwa na nini ni laaana au kitu gani, ujambazi uliendelea kuchana mbuga mauwaji yakiendelea kukithiri na utowekaji wa watoto na wake wa watu maarufu nao uliendelea, mateja katika mitaa waliongezeka siku hadi siku.

Jeshi la polisi lawama ziliwaanadama sana. Maafisa polisi wenyewe kwa wenyewe ikafikia hatua wakinyoosheana vidole, baadhi yao walikaa kwenye kipembe na wenyewe wakiulizana baada ya kuona uzito wa mafanikio yao katika pelelezi zao mbali mbali walizojiuhusisha nazo kugonga mwamba. Waungwana waliamua kuomba kustaafu wakastaafu na kutafuta biashara zingine za kufanya maana waliona ni ujinga kuendelea kutazama mambo yakiwa mabaya.

Wanasiasa nao hawakuwa nyuma walipaza sauti wakikosoa na kuendelea kukosoa nchi kwa namna zote wazionazo ni bora lakini ilikuwa kama kutwanga maji kwenye kitu kwa kuzani yatapondeka na kusagika kumbe ni kujichosha tu na kupoteza nguvu.


Itaendelea...
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

MSIMU WA PILI

Sehemu 5 A : PENZI

“Kipindi akiwa katika hatua zakupambana na maisha ya masomo na malengo aliyojiwekea, Salimu anajikuta akiingia katika uwanja wa mausiano ya kimapenzi na binti mrembo toka familia tajiri aliyeficha utambulisho wake, anashindwa zielewa hisia zake na kubaki njia panda, anakosa ujasiri wa kuamini penzi hilo anatamani kumjua zaidi binti huyo, anahisi kitu tofauti na Mapenzi kikiwa moyoni mwake anashindwa jielewa.Je! Hisia zake zinaendana na ukweli uliopo au nikushindwa kuuwelewa moyo wake?”

Kibaha High School, Kibaha - Mkoa wa Pwani

“Ebwana nataka kukuacha kidogo nikaaangaze macho mjini” Salimu aliongea huku akiliweka shati lake vizuri tayari kwa kulivaa. Karimu alisitisha zoezi lake la kufua alilokuwa nalo na kumtazama ndugu yake nje ya vyumba “..aahh basi poa mzee mi nipo kuwa makini tu na uwahi kurudi” ,“hilo ndilo la muhimu mzee haina shida” Salimu huyo akashika njia.
Nyakati hizo hizo kwa upande wa geti kubwa Gari nyeusi ilionekana ikiingia katika lango la shule ya Kibaha boys na kuegeshwa pembeni mwa uzio.

Bwana mmoja mtu mzima mwenye kipara machoni akiwa na miwani kuubwa nyeusi iliyofunika sehemu kubwa ya uso wake kidevuni akiwa ameachia ndevu zilizosheheni mvi huku sura yake ikionekana kula lakini mwili ukionekana kudai, akasimama kikakamavu akajiweka sawa kwa kulivuta vuta vuta koti lake la suti. Huyo mwendo ukaanza safari kuelekea katika upande wa ofisi za shule, kwa mbali alionekana Salimu naye alikuwa anakaribia eneo la geti kuu la kutokea kwa ishara akamuita Salimu baada ya kufika waliongea mawili matatu kisha wakaachana na yeye kuikabiri kordo moja ya sehemu ya mapokezi. Muda mfupi huyo alikata kushoto kuelekea upande wa mashariki na kugota katika mlango uliokuwa na maandishi makubwa “HEAD MASTER”. Baada ya kubisha hodi na kukubaliwa akaingia ndani.

Zilipita dakika chache mlango ukafunguliwa na akatoka akiwa na bahasha ya kaki kubwa ya A4 akielekea katika gari aliyokuja nayo shuleni hapo nakutimka zake.
Katikati ya jiji la Dar es Salam
Salimu alitemebea mpaka akahisi kuchoka na kutamani kurudi ndipo akaamua kukwea moja ya daladala ili kumrahisishia safari yake. Alipoingia tu alikutana na siti moja ambayo ilikuwa iko wazi pembeni upande wa dirishani msichana mrembo sana alikuwa amejikalia na macho yakiwa dirishani, moyo wa Salimu ghfla ulianza kumdunda kiasi cha kumfanya kujishangaa yeye mwenyewe.

Salimu alisogea na kujikalisha huku akiwa bado yumo katika tafakuri moyo ukimuenda matiti akijiwaza ‘mbona si kawaida yangu’, “Habari yako dada angu” alisalimia “Wewe za nini?” akajibiwa. Salimu alistaajabishwa ilimbidi amtazame vizuri na uvumilivu ukamshinda “Kwani ukinijibu ngozi yako itaota upere?” aliongea Salimu “Na wewe ukizijua zitakuongezea umri wa kuishi” akapewa lingine ikawa ni mipasho, Salimu akautia uzi mdomo. Baada ya muda kupita konda wa daladala alipita kwa kila abiria kukusanya michango ya nauli kama ilivyo kawaida huku akiwaita majina mbali mbali wateja wake “…hapo dada angu…shangazi…mjomba…kaka…mama mkubwaa…babu hapo” na kuzirudisha chenchi kuendelea na wengine, taratibu hizo ziliendelea kwa zamu huku baadhi wakishuka na wengine kuingia mwishowe ikafika katika siti aliyokaaa Salimu. “Hapo dogo janja” Salimu alijikunja na kuingiza mkono katika mfuko wa suruali yake ya jinsi lakini hali ya mshangao iliianza kumvaa na kubadili sura yake hakuamini alichokihisi aliamua kuingiza mfuko mwengine na mwengine lakini aliambulia patupu hakupata akitakacho.

Salimu kwa macho ya aibu alimtazama konda huku akitamani kumwambia lakini aliona aibu “Mzee baba vipi mbona jii” Salimu hakuwa na jibu “…mnajua msitufanye wajinga maswala ya kuzarau kazi za watu sisi hatupendi Mzee toa hela kabla haijakuwa mbaya” konda aliongea sura ikiwa imebadalika kwa hasira alilivuta shati lake la sare lililochanika begani na kuliweka sawa huku hela zingine alizoshika mkononi kuzitia katika mfuko wa suruali.

Msichana aliyekaa karibu na Salimu akaifungua pochi yake iliyokusanya noti za elfu kumi kumi pamoja na elfu tano alichomoa elfu tano na kumpa konda na kusubiri chenchi mkono wa kusubiri ukiwa juu juu. Salimu akiwa na mshangao asijue la kufanya konda alihesabu na kuzitoa hela husika na kumpatia Yule binti. “We konda shika hela hii kata nauli ya huyo kijana alafu chenchi mpatie” Mwana mama mmoja kibonge aliyekaa kiti cha nyuma ya Salimu alisikika akiongea kiasi cha kumshangaza sana Salimu mpaka ikambidi ageuke kushuhudia na kuona noti ya Elfu tano akipokea konda huku jicho la asira likiwa kwa Salimu. “Unabahati sana wewe” alizitoa chenchi na kumpa Salimu ambaye alizipokea kisha akageuka kumshukuru yule mama. ‘Sina jinsi zaidi ya kuzichukua mama yangu mana safari yangu bado ndefu. “Manzese darajani” “Shushaa” Yule binti aliyekaa karibu kabisa na Salimu alijizonga zonga na kunyanyuka huyo akashuka huku Salimu akitazama sehemu za nyuma za binti huyo na kutabasamu basi hilo likaanza safari ya kuondoka tena, Salimu alipo tazama chini ya miguu yake aliona kipochi cha Yule msichana akapatwa na mshangao sana aliinama akakiokota haraka huku akipayuka "Dereva Shushaaaaaaa"

Itaendelea
IMG-20211211-WA0046.jpg
 
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

MSIMU WA PILI

SEHEMU 5 B : PENZI

Tuendeleeee...

...akakiokota haraka huku akipayuka “Dereva shusha” huyo akiwa tyayari mlangoni akitazamana na konda “Aisee hii si gari ya baba yako tusisuumbuane unajua” Dereva aliongea kwa lafudhi ya kichaga huku sura akiwa kaikunja kwa usumbufu “Jamani mimi ni mgeni hapa naomba mnisamee nishusheni tafadhari” “Mbona huna kamba mguuni” aliongea konda huku akifungua lango na kuacha watu wakifa kwa vicheko safari hii Salimu aliushika mlango daladala ilisimama na Salimu akashuka kwa tahadhari na kutimua mbio kurudi kule alipo shuka yule msichana. “Mungu wangu pochi yangu” yule binti alishika kichwa chake na kusimama akiwa katikati ya kundi la watu kwenye minada ya nguo na mengineyo aliishiwa nguvu akageuka kutazama kama ataitambua gari ile aliyokwisha shuka.

Hakuridhika akaamua kurudi kabisa akijikimbiza Loo mabasi yalikuwa kama vikombe vya kahawa yalifanana kwa michirizi na rangi kasoro vibao vya viendapo na vitokapo tu. Nguvu zilimuishia masikini alijiskia vibaya akaaamua kukaa katika sehemu ya abiria wanaosubiria magari ya usafiri. Machozi yalimjaa machoni akitamani kulia na kunyamaza kwa wakati mmoja.

Kipindi hicho anawaza na kuwazua atafanyaje sasa kanyanyuka mikono kiunoni akitazama bahati yake asiyoijua ipo au haipo na Salimu akiwa jirani yeye akigeuka huku na kule akifananisha wasichana waliokatiza mbali na karibu kwa bahati akamuona binti akiwa kajiegemeza katika chuma moja la mataa akiwa ni mwenye mawazo, Salimu akatabasamu akaanza kuchapuka kumfata. “Shika pochi yako…” sauti yake ya bezi ilimshtua Shalon na kumtoa mawazoni hivyo ikampelea kunyanyua sura yake kumtazama aliye muongelesha kwa kumshtua. Hakuamini akaduwaa kutazama pochi yake iliyoelekezwa na Salimu na aliponyanyua uso kumtazama mshikaji aibu ikamjia alimtambua akaipokea na kuifungua. Salimu hakuwa na la kusubiri huyo akajichanganya katika mikusanyiko ya watu na kuondoka zake, yule binti mpaka anamaliza kuzikagua hela na kila kitu kilichopo katika pochi kuwa kipo salama akanyanyua sura kumtazama aliye mletea lakini hakuona mtu akabaki mdomo wazi huku akiangaza angaza akigeuka huku nakule huenda atamuona lakini hakufanikiwa.

*****

Wasichana wengi wazuri kuonesha kiburi kwa watu lilikuwa ni jambo la kawida sehemu nyingi, huenda ikawa ni kutokana na uzuri wao au kujikinga na vijana waliokatika baleghe na wanaume wakwale waliojaa tamaa ya kutongoza tongoza wasichana pindi wakutana napo. Wasichana wengine ilitokana na hali za uchumi walizokuwa nazo familia zao hivyo kupelekea kuwadharau watu wengine wasiokuwa nacho kuwa watawapa nini zaidi ya kuwapotezea muda tu.

*****

Kibaha High School, Kibaha - Mkoa wa Pwani
Muda mwingi Salimu alikuwa kimya nje ya baraza ya Hostel alikuwa mawazoni mara akaanza kujichekea mwenyewe Karimu akawasili na kumkodolea Salimu ambaye hakuwa habari “Kaka vipi nakuona unakenua kenua tu hapa vipi sielewi kwema” aliongea Karimu na kujikalisha barazani karibu na Salimu “Mtembea bure si sawa na mkaa bure…Ngoja nikusimulie ndugu yangu ya leo kali nahisi moyo wangu haupo sawa kwa mala ya kwanza yani sijielewi kabisa”. Karimu kicheko kikamtoka alishindwa jizuia “Haa hhaa usiniambie umekutana na mtoto ukampenda kaka?” Salimu alimuangalia tu Karimu kwa aibu “Sina hakikaa kaka ngoja nikusimulie alafu utayapima” Salimu aliongea Basi Salimu alianza kusimulia kila kitu kwa ufasaha na Karimu masikio aliyatega kunasa habari zote kwa makini mpaka masimulizi yalipofika tamati. “Pole sana ndugu yangu ila umejitahidi sana mtu mwengine asinge kuwa na mpango wa kumfanyia wema kama huo”, “ ndio hivyo kaka Wafanyao makubwa huyathamini madogo, nilitokea kuchukia sana lakini niliona haina haja…alafu…isitoshe unajua nilimwangalia kwa wasiwasi sana pale kwenye daladala ohh” Karimu aliendelea kukokodolea macho tu huku akitabasamu. Salimu akaendelea “…yani daah! Alipo nyanyuka sasa nilijikuta natabasamu na kusahau maudhi yote” Salimu aliongea na kutingisha kusadiki maneno yake akaendelea ....

Itaendelea...
AKIDA%20S.%20RAMBAO%20%3D%20THE%20HIDDEN%20TRUTH%20(UKWELI%20ULIOFICHIKA)%20(2).jpg
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika??

Mtunzi: AKIDA SIRI RAMBAO
Contact : 0658328596
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU 5 C : PENZI

Tuendeleeee...

....utayapima” Salimu aliongea Basi Salimu alianza kusimulia kila kitu kwa ufasaha na Karimu masikio aliyatega kunasa habari zote kwa makini mpaka masimulizi yalipofika tamati. “Pole sana ndugu yangu ila umejitahidi sana mtu mwengine asinge kuwa na mpango wa kumfanyia wema kama huo”, “ ndio hivyo kaka Wafanyao makubwa huyathamini madogo, nilitokea kuchukia sana lakini niliona haina haja…alafu…isitoshe unajua nilimwangalia kwa wasiwasi sana pale kwenye daladala ohh” Karimu aliendelea kukokodolea macho tu huku akitabasamu. Salimu akaendelea “…yani daah! Alipo nyanyuka sasa nilijikuta natabasamu na kusahau maudhi yote” Salimu aliongea na kutingisha kusadiki maneno yake akaendelea “…kaka nimewaona wasichana lakini Yule kaka mzuri sana uongo dhambi, lakini ninavyo jisikia sizani kama ni kuhusu mapenzi”. Salimu alimaliza na Karimu akaongea “Enhee na wewe ulipotezaje pesa zako?” Karimu lidokeza Salimu alionekana kuwa na mawazo maana alikodoa macho akitazama chini huku akitabasamu Kalimu akamuangalia huku akicheka “Kaka… vipi kaka” Karimu aliongea kwa kumgusa gusa goti “Naam vipi?... nambie…tumeishia wapi vile?”. Karimu akamtazama mwenzake kwa jicho makini lenye upelelzi huku akitabasamu “…nimekuuliza hivi vipi kuhusu pesa ulizipotezaje” alongea Karimu “Ohh sawa nafikiri ni ule muda niliokuwa nimenunua maji zile chenchi niliziweka katika mfuko wa nyuma wenye leso na kuna sehemu niliitoa kujifuta jasho si unajua joto la kule, naamini ndio sababu ya kuangusha” Salimu alimaliza “Pole sana…na mtu kama huyo kuja kuonana nae utakuta ni uzeeeni” Karimu aliongea wote wakajikuta wakicheka kisha wakabadili mada hiyo na kuzungumza mambo mengine.

Bunju, Kinondini -Dar es Salam

Pembezoni mwa fuke alionekana Shalon akiwa amechuchumaaa maji yakija miguuni mwake na kuondoka huku mkononi akiwa ameshikilia glass ya juisi ya matunda. Akiwa amevalia sketi fupi nyeupe, flana nyeupe kichwani akiwa na kofia ya pama.

Usoni alionekana fika kugubwikwa na mawazo mengi mno yaliyomfanya aendelee kukodolea maji yaliyoipiga miguu yake na kuondoka.

Alijikuta akijisemea “Lakini mbona najihisi kumpenda yule kijana, simjui kwa lolote ndo kwanza nimemuona leo”, alijisimamia na kukitingisha kichwa chake kujisikitikia, ‘Mhh nimekuwa mtu wa ajabu sana, sija muuliza lolote wala namba zake sikuchukua nitampataje’ alijisemea nafsini sura yake ikaingiwa na huzuni. ‘Hapana nitampata ngoja niwe mvumilivu tu’ Shalon alijiwazia kisha akageuka na kupiga hatua kurudi upande wa juu ambapo jumba la kifahari lilikuwa limetawala kwa ukubwa wake likiwa na sifa za kila namna kuthibitisha kuwa lilikuwa ni la kifahari sana.

Jumba hili halikuwa la mchezo mchezo lilikuwa na ghorofa moja lakini lilichukua nafasi na kuonekana kama Hotel ya kitalii. Walinzi walionekana mmoja mmoja kwa mbali wakiwa na siraha zao6 wakiiimarisha ulinzi wa eneo hilo.

Baada ya Miezi

Kibaha High School Kibaha - Mkoa wa Pwani
“Aisee miezi inakwenda sana ndugu yangu si juzi tu tulikuwa katika likizo leo tena likizo nyingine” Salimu aliongea huku akiendelea kupasi shati lake, “Ni kwa sababu tu tulikuwa bize mno ndo maana lakini muda kasi yake ni ilele ile mzee” wote wakaangua kicheko. “Basi sawa yote gheri we jiandae tufanye kama tulivyo panga mzee” Karimu akanyanyuka kitandani na kuchukua taulo huyo akatoka chumbani hapo na mswaki ukiwa mdomoni.

Itaendelea....



Mahaba yameanza huko, Sasa sijui huyo Shalon atapendwaa???

Na yule Mzee mwenye Kipara atakuwa Nani??
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

Mtunzi AKIDA SIRI RAMBAO
Contact : 0658328596
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU 5 D : PENZI

Kariakoo - Dar es Salam
Waliendelea kufanya manunuzi ya viwaro na vitu vingine kama zawadi. Wakaingia hapa na kutoka wakaenda pale wakauliza wakajaribu mavazi wakatoka hivyo hivyo mpaka kila mtu akapata kile akipendacho sasa. Katika mpishano wa hapa na pale kutokana na wingi wa watu ilisikika sauti ya kike ikiita na kupotea. “Wee kaka…wee kaka…jamani nipisheni…we kaakaa”. Dada huyo aliendelea kuminyana na watu aliokuwa akipishana nao wengine wakimtukana wengine wakimuacha tu aende. Salimu alisikia akasimama mara shtukia akishikwa mkono kwa nyuma kumzuia asiende mbele, akageuka na kukutana uso kwa uso na Shalon.

Moyo ulimpasuka Paaa! macho yalimtoka “Mambo”, Shalon alitoa salamu huku akiwa bado kaushikilia mkono, “Ohh…aahh safi tu vipi” aliuliza Salimu na mara Shalon akamvutia kwa pembeni.

Salimu akiwa na uduwanzi Shalon kwa upande wake ujasiri ulianza kumuisha na aibu ikaanza kumtawala alishindwa kumtazama Salimu machoni akauachia mkono na kuinama kwa aibu “Naomba tutoke hapa tukaongee kidogo samahani” Shalon alivunja ukimya wake “Sawa hakuna shida…lakini”. Salimu aligutuka na kuonekana kunyanyua shingo kutafuta “Ahh nipo hap mzee” Karimu akaingia akiwa na uchangamfu akimkodolea macho Salimu “Kuna duka la Ice cream naomba tuongozane twende hapo sitachukua muda mwingi naomba twende tafadhari”. Shalon aliuvunja tena ukimya “Sawa, Karimu twende” aliongea Salimu na kuongoza njia akiwa na Shalon Karimu akiwa nyuma akijichekea, mwishowe wakaingia katika duka kubwa la bidhaa za Azam ikiwemo ice cream na juisi , wakachagua Ice cream kisha ndipo wakatafuta pa kukaa.

Wote walikaa meza moja huku kila mmoja akiwa na kikopo cha ice cream za azam na kijiko, kabla ya lolote Karimu alinyanyuka na kuomba ruhusa akiononekana kama ni mtu mwenye shida Fulani ya dhararura. Akaenda mbali na eneo hilo akiongea na simu yake. “Eti unanikumbuka?” Shalon aliongea huku akiiibana midomo huku akikwepesha macho yake yasikutane na ya Salimu kwa aibu.

Salimu alitulia na kujifanya anajikumbusha kitu fulani “ Yap bira shaka nishawahi kukutana na wewe pahala” aliongea Salimu akimtazama vizuri Shalon akitabasamu akiachilia meno yake meupe kuonekana na kupendezeshwa na mwanya mdogo. ‘Mungu wangu nini hiki’ alijisemea nafsini alijikuta akitetemeka ndani kwa ndani. “Nashukuru kusikia hivyo, kwanza naomba unisamee kwa tukio zima nililokufanyia siku ile, kiukweli si tabia yangu ila sikuwa poa siku ile na sijui shetani gani alitawala maamuzi yangu nikajikuta na misbehave mbele yako” Shalon aliongea akidhihirisha kwa uso wake wenye kutaka msamaha “Usiwaze sana huwa inatokea kama ajari maana binadamu tunaandamwa na mambo mengi sana ya kimaisha, ila nilisha samehe na kusahau” aliongea Salimu na kutabsamu. Tabasamu la Shalon likaongezeka zaidi akionekana wazi furaha imemzidi “Ohh asante sana jamani asante, sikuwa na raha tangu siku ile nilikuwa na wakati mgumu sana kwa kweli nikiwaza nitakutana na wewe lini nikuombe msamaha, asante sana” aliongea Shalon kwa aibu “Karibu” alidokeza Shalon akautoa ulimi wake mrefu na kuilamba Ice cream yake ya chocolate kwa pozi la taratibu huku akimtazama Salimu kwa macho ya wizi. “Kwa jina naitwa Shalon sijui wewe mwenzangu”.

Shalon aliuvunja ukimya “Ohh Shalon ni jina zuri, mi nafahamika kwa jina la Salimu, yule niliye ambatana nae anaitwa Karimu.” Aliongea Salimu akigeuka kumtazama Karimu akiwa meza kazaa nyuma “Ok, asante, ni mapacha sio” Shalon aliuliza “Hapana sio mapacha ila ni indugu lake langu langu lake hivo tu” aliongea Salimu. Karimu alionekana kukaa sehemu ya peke yake akiwatazama kwa mbali jinsi walivyokuwa wakizungumza kwa furaha, “Basi naomba nisiwapotezee muda…” Shalon alipekeua katika hand bag yake na kutoa ka note book kadogo pamoja na pen akaandika namba za simu na kumpatia Salimu, “…samahani nakuomba unitafute tafadhari nina mengi ya kuongea na wewe” aliongea Shalon Salimu akazipokea, “Sawa, asante sana ila nahisi si vibaya kama na mimi nitakuandikia za kwangu” aliongea Salimu “Ni sawa pia” Shalon alimsogezea note book pamoja na Kalamu. Salimu akavichukua na kuziandika namba zake na za Karimu chini yake, kisha akampatia. “Shukrani sana, naomba umuite ndugu yako nahitaji kumuaga”, Salimu aligeuka na kumuita kwa ishara ya mkono kipindi hicho hicho Shalon chap chap akaandika ujumbe mfupi wa maneno “Kiukweli nimetokea kuvutiwa na wewe najiheshimu sana na umenifanya niwe tofauti sana niache nikupende tafadhari” haraka haraka akautuma ujumbe huo kwenda kwenye namba ya Salimu.

Kipindi hicho Karimu teyari alikwisha nyanyuka na kusogelea meza alipo waacha wenzake, “Samahani kwa kuwakimbia jamani kuna mambo fulani Fulani nilikuwa nayaweka sawa” Karimu aliongea huku akikaa baina yao. Kamlio ka ujumbe wa sauti kaliingia na Salimu akakipotezea akaendelea kushangaa shangaa akiutazma zuri wa Shalon vizuri.

Itaendelea..

Shalon amejikuta akimwaga mambo hadharani itakuwajeeee
 
The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)
MTUNZI: Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 1 (C): JINAMIZI LA SIKITIKO.

Mandal Hil Hospital, Kinondoni -Dar es Saalam

Ilipoishia

... daktari aliivua miwani na
kuiweka katika meza huku akiwa bado kashikilia karatasi la Winifrida kisha akaendelea “Majibu kidogo yameenda tofauti na historia yako mama” Winifrida moyo ukamlipuka Puuh!daktari alimtazama Winifrida, Winfrida akajikuta akifumba macho kwa nguvu huku moyo ukimzidi mapigo akaanzakulegea huku mikono ikishika tumbo lake la mshtuko...

Tuendeleeee....

Mheshimiwa Richard akamtupia macho mkewe akionekana kutokuelewa sentensi ya daktari, daktari akauma midomo
yake na kuiachia kwa pamoja, “Mama kizazi kinaonekana kimeathirika sana, na sababu kuu ya uathirikaji huu ni
utolewaji wa mimba kadhaa katika maisha yako hii ni mbaya sana” Winifrida alichukua kitambaa chake kidogo katika
mkoba wake na kujiwekea usoni akilia taratibu. Richard macho yakamtoka asijue la kufanya mapigo ya moyo yakaanza kubadili kasi yake ya kawaida “…na kitu kingine ni kuwa kizazi chako kwa sasa kimelegea, hizo ndio kesi mbili ambazo zimepelekea kutokushika mimba kwa muda wote huo mlio ishi pamoja” aliongea daktari. Richard akashika kichwa
kana kwamba amefiwa na mtu muhimu katika maisha yake, hasira zikampanda maradufu macho yakawa mekundu huku
kajiinamia hakujua afanye nini, ‘Mke wangu kwanini hukuniambia siri hii ya kutoa mimba jamani fedheha gani hii’
Richard alijiwazia, ‘Mume wangu nisamehe sikujua kama itafikia hatua hii mimi najuta bora ningekwambia mapema…lakini ningekwambia usingenipenda nani angenithamini, nani angenisomesha mimi, nani Richard wangu?' walikuwa wakiongea kupitia nafsi zao bila kutambua.

Winifrida alihisi kizunguzungu kwa taarifa hiyo mwili ulishindwa kujizuia kichwa kikiendelea kumuuma na kuwa kizito moyo wote ulichakaa kwa huzuni ya moyo na wasiwasi, daktari akaendelea “Lakini nitamuandikia dawa ambazo atazitumia kwa kipindi huku mkihudhuria maonano na daktari husika mara kwa mara kujua maendeleo yake huendasiku za usoni akapata ujauzito nani anajua, maana Mungu ni mkubwa sana na tuzidi kumuomba maana ni mwingi wa huruma na mwingi wa msamaha” aliongea kwa masikitiko.

Winifrida alitamani ayeyuke atokezee ulimwengu mwingine kabisa kwa uchungu aliokuwa nao na aibu maana aliona
amemvua nguo mumewe mbele ya ulimwengu. ‘Fadhira zote ulizonifanyia mumewe wangu leo nakulipa madudu hivi
maumivu ya aina hii, kwanini nisife?’ Winifrida alijiongelea nafsini, daktari akaendelea “Lakini nawaomba jambo moja msije mkaleta mfarakano kutokana na tukio hili wengi sana wakishamaliza na kuondoka hapa mapenzi na wanandoa wao yanapotea wengi wanaachana, wanasalitiana na hata wengine kujiua kwa sababu tu hawezi kuzaa…” Winifrida alinyanyua kichwa na kumtazama dokta kwa huzuni, ‘Ulijiuaje dokta kuhusu hisia zangu’ alijiongelea tena Winifrida “…Mkaemkijua watoto ni baraka toka kwa Mola, yeye ndiye humpa anaemtaka na humnyima anaemtaka na kumpa wakati anaotaka yeye mwenyewe, vipimo na madawa vipo ilikurahisisha mambo na uchunguzi ili kuweza kujua jinsi ya kutatua matatizo na kuyajua matatizo kama ilivyotokea, hivyo nawasihi sana nyinyi bado ni vijana tena ni watu maarufu
muende na mkawe mfano” dokta Abdi alimaliza, Richard akanyanyuka na kumpa mkono dokta bila kusema kitu akapokea karatasi alimtazama mkewe sekunde kadhaa kama mtu anae tamani kusema jambo huku akiwa kasimama
“Nyanyuka tuondoke” aliongea Richard huku akiwa wa kwanza kutoka, usoni akiwa na hasira ya waziwazi.

Nelson Mandela Road – Dar es Salam.
Ndani ya gari ya aina ya Mitsubish Lancer Winifrida alikuwa ni mtu wa kulia tu alilia mfano wa mtoto mdogo aliye na njaa
na kiu kikali japo hakutoa sauti lakini kilio chake cha kimya kimya kilileta hisia kuwa amezidiwa uchungu. Kilio chake
kilimpelekea macho kumvimba na kuwa mekundu. Richardyeye alionekana kama mtu asiye jali hali ya mkewe wala
hakujigusa, hakujipa nafasi ya kumtazama wala kumuongelesha mkewe tangu walipo toka hospitali na kuitiagari yake funguo, hakutia neno hata moja katika safari hiyo
yeye alikuwa macho mbele kama tochi huku akijinyusa nyusa tu kila wakati. Sura ya Richard ilionekana kukunjamana kama
karatasi iliyo kosa kazi na kukunjwa au kumfananisha na mtu aliyelamba ndimu au kunusa kitu chenye harufu mbaya.
Winifrida mara moja moja alimtupia macho mumewe kiwiziwizi lakini alichokutana nacho aliuona upweke na kuzidisha uchungu unaochoma ndani kwa ndani usioisha wala kupata nafuu huku tumbo likimsokota haswa.

PURPLE in Hotel, Temeke, Kurasini - Dar es Salam.
Kipindi Winifrida akiwa kaegemeza kichwa kwenye kioo cha mlango wa gari akashtushwa na breki kali sana iliyomfanya mwili kusukumwa mbele “Paaap” ilikuwa ni msaada tu wa mkanda wa usalama laa sivyo chochote kingetokea. Baada ya mshituko akaanza kuangaza kupitia katika kioo cha gari na
kuanza kuzirudisha kumbukumbu vizuri mwisho akaishia kusoma kibao kikubwa kilicho kaa pembeni mwa bustaniupande wa mbele ya gari walilopanda, “PURPLE in Hotel …mmh” alijigunia kwa sauti huku akiwa na wasiwasi na mshangao. Richard mikono ikiwa imeshikilia usukani wa gari
kichwa kakiinamisha akihema hovyohovyo, taratibu akatoa mikono katika usukani akajishika kichwa chake nakujiegemeza katika kiti alichokalia, macho akayafumba, zikapita dakika tano nzima pakiwa kimya ndani ya gari. “Naomba unifate tafadhali” Richard aliuvunja ukimya akaufungua mkanda na kutoka katika gari, Wini yeye hakuwa na lakufanya zaidi ya kufata amri ya mumewe huku maswali yakiendelea kumtawala ‘Purple in Hotel kuna nini? kwaniniisiwe nyumbani, na kwanini’ alijiuliza nafsini, Usilo lijua ni
usiku wa giza.

Richard alisogea hadi katika sehemu ya mapokezi huku akipokea salamu za watu waliomfahamu na wasio mfahamu
mahala hapo, baada ya kufika na kuongea maneno mawili matatu na mhudumu akatoa kiasi cha pesa taslim toka
kwenye waleti na kumpatia Mhudumu aliyekuwa mahala hapo akaegema na kuanza kuandika kitu, Mhudumu na yeye
akaikabili simu na kuiweka sikioni akiongea kitu kisha akarejesha sehemu yake. Richard akiwa mwingi wa mawazo
mkewe akiwa hatua kadhaa nyuma akimuangalia kwa kujiiba akiwa “Habari Mheshimiwa…” ilisikika sauti mgongoni mwa Richard na kumshitua akageuka na kumtazama kijana mtanashati aliyevalia sare za Hoteli hiyo “Ooh salama” alijibu “Mnaweza nifata tafadhari” aliongea tena kijana huyo na kuongoza njia huku akifatwa nyuma na Richard pamoja na
mkewe.

Richard aliendelea kujifuta maji kichwani na taulo huku akiwa anaufunga mlango wa bafu kipindi hicho Winifrida kajikalisha
na kujiinamia kwenye kona ya kitanda akiwa kama alivyo kuwa hakuvua wala kuvaa chochote. Richard akamsogelea
mkewe na kukaa karibu yake kwa huzuni kubwa, akamtazamamkewe kwa kumkagua vizuri kana kwamba ni mtu mwenye kumfananisha akabaki kutingisha kichwa chake kuonesha anakataa hali anayoiona au kuihisi kuwa sikweli “Samahani naomba nikuongeleshe tafadhari” alijikuta akiyatoa maneno hayo toka katika kinywa chake huku akimuangalia mkewe.

Winifrida aliyasikia maneno hayo akaunyanyua uso wake na kumtazama mumewe kwa aibu huku akikwepesha macho yake yasikutane na mumewe. “Hivi ni wewe kweli, niWinifrida wangu kweli wewe? Unajua umenikosea sana mke wangu!” maneno hayo yalipenya na kuingia kwenye masikio moja kwa moja hadi katika sakafu ya moyo wa Winifrida na yakatibua fukuto la uchungu lililokuwa limepoa poa kwa vijidakika kadhaa tangu wafike Hotelini hapo yakaleta mchafuko wa moyo. Winifrida alianza upya kulia yani kiasi cha kumshangaza mumewe ambae ndiye aliyekosewa “Wewe una nini unanikejeli au vipi?” Richard alishindwa kuzuia hasira zake alipaza sauti yake nzito juu na kumtazama kwa mshangao akanyanyuka alipo kaa na kusimama huku kajishika kiuno, Winifrida aliteremka taratibu na kukaa katika sakafu huku akilia kimya kimya akayasimamisha magoti yake huku kichwa kakiinamisha, “Nisamehe mume, Rich naona aibu, naona haya mimi kukuita mume wangu kwa dhambi nilizofanya nyuma ya mgongo wako sikukwambia mimi…” winifrida alijifuta machozi na kujikaza kuongea, “Sikujua kama yatafikia hapa, nikweli nilikuongopea historia ya maisha yangu asilimia hamsini sio ya kweli” Richard alimtupia macho ya hasira mkewe “…ila tangu umenioa miaka minne iliyopita, sijawahi kukudanganya nimekuwa nikiishi ndani ya ukweli na uwazi wa kila jambo kwako hiyo ndio ahadi niliyoiweka katika maisha yangu na wewe ni shahidi ” Winifrida akaangua kilio cha chini chini bila kunyamazishwa na mumewe aliye jisimamia pembeni akiwa kampa mgongo “Nipo tayari kuyakubali maamuzi yako mume wangu na hiyo itakuwa ndio adhabu inayo nifaa…” Richard alishtuka na kugeuka kumtazamaa mkewe kwa mshangao, “Ila kabla hujaamua chochote nataka kukupa ukweli mmoja kuwa sijawahi kumpenda mwanaume yoyote zaidi ninavyokupenda… nashukuru nimeweza kufurahia na kuridhika kwa mara ya kwanza ndani ya ndoa yangu”aliongea Winifrida kwa sauti ya mtetemo machozi yakimwagika macho ya Richard yalionekana kupata wingu la machozi uso sasa ukafunguka toka katika mikunjo kunjo ya ndita kwenye paji la uso, “Nilipata ujauzito mara kadhaa na wote walionipatia walipotea wote na kila mmoja alikuja na uongo wake na mimi nilikuwa muhitaji wa pesa kama ulivyokuta hali ya uchumi kwetu haikuwa shwari mzee wangu alivyokuwa mgonjwa gonjwa ningefanyaje?” aliongea tena Winifrida akiwa kapiga magoti akajifuta kamasi na machozi sasa yamekata na sauti imekauka inatoka kama mtu anae
nong’ona akaendelea “Mimi nilikupenda mwenyewe na nilikuvutia mwenyewe na wala sikuwa na tamaa na pesa zako,
na nilitamani uwe wangu maisha yote, sikupenda ughalimike kwa ajili yangu ila uliamua ukanisaidia, nilikufurahia sana
asante kwa hilo” Richard picha ikamjia jinsi alivyomkuta siku za mahusiano yao machanga alipokuwa anahudhuria siku za mwisho wa wiki katika mji wa Tanga, kumbukumbu ilimchosha akatingisha kichwa kuivuruga maana ilimuumiza
taratibu akajikuta anarudi kujikalisha katika kitanda kama zigo lililotupwa kwa kususwa “Puuuh”. Wini akaendelea
“Nilitamani nikuambie ukweli lakini uchafu wangu ungeujua ingekuwaje isingekuwa rahisi kunioa ungenitelekeza tu kama
wale wengine, niliogopa sana kukukosa niliogopa kukwambia niliogopa mimi” Winifrida alijikuta anatingisha kichwa
kusikitika, “Wewe ni mwanaume wa kipekee sana mume wangu, najivunia kuwa nawe, sasa nasubiri hukumu yako na nitaikubali bila kinyongo” Winifrida aliongea nakunyamaza shingo imeinama kama mtu anayesubiri kuchinjwa, Richard
alibaki kuwaza na kuwazua aamue lipi, saa zima na nusu likapita akiwaza tuu. ‘Ni mwanamke uliyenifunza nini maana
ya kupenda na maana ya penzi la dhati sasa mbona umeniumiza kiasi hiki, sijawahi jua uchungu wa penzi kumbe
inauma kiasi hiki?’ alibaki akijiwazia. Ushauri wa dokta kuhusu hali halisi na kukabiliana ilianza kuranda randa katika
kichwa chake ikijirudia rudia ‘Mungu wangu nifanyaje mimi siwezi kumuacha mke wangu siwezi’ Richard alijisemea
moyoni na kunyanyuka haraka haraka na kumkumbatia mkewe kwa masikitiko makubwa sana kiasi cha kumshangaza
sana Winifrida, wote wakaanza kuangua kilio cha huzuni huku wakiwa wamekumbatiana, ama kweli penzi ni kitu kisicho na mfano katika ulimwengu wote. Mabembelezano yalienda na walikuja tahamaki saa tatu usiku, wakaamua kuondoka zao.

Msasani, Kinondoni -Dar es Saalam
Mke na mume wakiwa kitandani wamejilaza kila mmojaakiwa na lake aliwazalo mke akajipindua na kuanza kuongea“Mume wangu unajua nina hofu na uoga sana juu ya dada zako, mama yako, jamaa zako na hata marafiki zako
watanichukuliaje maana dunia hii haina siri” aliongea Winifrida akageuka na kumtazama vizuri mumewe, “Mke
wangu sisi ndio tulio oana sawa? halafu kama Mungu ameamua tusipate hatutapata na kama amepanga tupate
tutapata, tena sasa huwenda tukapata mtoto mzuri mwenye hekima na busara hapo baadae” Richard aliongea na kuachia tabasamu jembamba na kukaza macho kuashiria kumaanishamaneno yake. Winifrida akatabasamu na kujivuta zaidi kwa mumewe, kwa pamoja wakajiweka sawa kuukaribisha usingizi.

Kijiji cha Mtamba, Matombo - Morogoro.
Majira ya saa nne asubuhi hivi, nje ya nyumba ya kisasa kwenye baraza walionekana wanawake watatu, wawili
walikuwa bize wakitembea kwa kupishana huyu akienda na huyu akirudi mikono kiunoni kichwa sakafuni mara wamekaa
mara wamesimama, walionekana wazi vichwa vyao vimebeba mzigo wa hasira kutokana na jazba walizokuwa nazo nyusoni, Lakini watatu wao mama wa makamo ya miaka hamsini mpaka kwenye siti yeye alikuwa kajiegemeza ukutani katika kibaraza hicho, kiganja chake cha mkono wa kuume alikigandisha shavuni mwake mguu mmoja kaukunja na
mwingine kunyooshwa. Mama huyo mtu mzima alibaki kujisikitikia tu aliwatazama wanawake hao waliokuwa mbele
yake kwa wakati huo walikoma kutembea wakabaki wamesimama na kuanza kunesa nesa kama wasoma ngonjera
waliokuwa wakitambiana kwa zamu.“…Mama sisi kesho piga ua lazima twende Dar”, ukimya wa muda mfupi ulivunjwa na
mmoja wao, mama wa watu alitoa kiganja cha mkono shavuni na kunyanyua uso wake kuwatazama kwa zamu wanawake
hao walio mbele yake “Sawa ila nawaomba sana wanangu msiende bila kumtaarifu kaka yenu” mama huyo mtu mzima
alikunjua mguu wake na kuunyoosha kwa mbele, “Nani?..sisi?...aaah mama hilo sahau” mwingine alidakia, alikuwa pande la mwanamke wa maji ya kunde, alionekana kufanana sana na mama huyo, maana alimchukua kila kitu.

“Hakuna cha taarifa wala nini sisi tumeshaaga waume zetu na wewe tumekuletea taarifa tu na sio kutaka ushauri au ruhusa, mwanamke mbaya sana yule bila shaka amempa limbwata
kaka yetu” alimaliza na kugeuza shingo kutazama pembeni mikono kiunoni huku akichezesha mguu kwa hasira. “Sawa
wanangu ila tu nawaomba msiende kumfanyia fujo wifi yenu sawa Ester?” Mama wa watu akageuka kumtazama mwanawe mkubwa aliyekuwa kachukizwa mno amejitazamia pembeni “Mama sikiliza, mimi na dada Ester tumekuletea wajukuu wangapi mpaka sasa je vipi mwanao wa kiume? Je! unajiskia raha sio mtu mheshimiwa eeh anasifa kubwa nchini kazi kumwaga hela za misaada tu kwa watu nani atazirithi mali zake? Sisi tumeshaamua ukitaka ni hivyo usipotaka ni hivyokwaheri” aliongea Ester kama cherehani akashika njia huku akiifunga vizuri kanga yake kiunoni, Eva nae hakukaa akafata nyuma na kumuacha mama huyo akiwasindikiza kwa machoya mshangao wakiingia ndani. Mama wa watu mawazo yakamchukua na kumkumbuka mumewe mzee Edward Kobero, kumbukumbu hizo hazikumuacha macho makavu mama huyo akajikuta akijifuta michozi na utuuzima wake kweli “Ukimuona mtu mzima analia ujue kuna jambo” Mama huyo akiwa bado jamvini alinyanyua kichwa kutazama nyumba anayoishi, ilikuwa nyumba ya kipekee sana na nzuri kuliko nyumba zote kijijini hapo, “Eeh Mungu msaidie mkwewangu dhidi ya shambulio la wanangu” alijisemea.

Ni kweli kilikuwa ni kitu cha kuhuzunisha sana kwa mama huyo wa watoto watatu, masikini alibahatika kupata mtoto
mmoja tu wa kiume kama wa dawa vile ambaye alimsomesha kwa pesa za kuungaunga tena kipindi kile alipo kuwa analimamboga mboga na matunda na kwenda kuuza Morogoro mjini,
alimkumbuka sana marehemu mumewe. Mumewe mzee Edward Kobero alikuwa anajishughulisha na kazi ya ulinzi
alishikwa na umauti baada ya kukosa matibabu stahiki ya jeraha la mguu lililotokana na shambulio la majambazi katika harakati za kujaribi kulinda mali ya bwana Mohammed Seifalijikuta akipigwa risasi ya paja, kwa uhaba wa hospitali na
pesa za kutosha kwa kipindi kile na kesi iliyomkabili toka kwa muajiri wake kwa kuhusishwa na wizi huo ikampelekea
kupatwa na umauti akiwa chumbani kwake.

Msasani, Kinondoni -Dar es Saalam.
Sauti za magari na milio ya ndege wakiimba nyimbo za kushukuru kuingia kwa siku mpya zilisikika kwa mbali toka
katika nyumba ya kipekee mfano wa kasri iliyokuwa ikitajwamiongoni mwa nyumba nzuri kuwahi kutokea nchini, kila apitaye aliishia kuitupia macho ya matamanio na kuishia na ndoto za alinacha. Wapendanao hao wakiwa sebureni pahala pa meza ya chakula Winifrida alilichukua koti la suti lililoegemezwa kwenye kiti kimoja wapo na kumvalisha mumewe ambaye alikuwa kasimama huku mdomo ukicheza cheza kumalizia chakula “Mke wangu basi usisahau kunywa dawa tafadhali sawa” Richard aliongea huku akiendelea kupitisha mkono huu na mkono ule katika mikono ya koti la suti alilokuwa anavalishwa na mkewe “ Usihofu mume wangu nitakunywa” Winifrida aliongea kwa tabasamu pana huku akiendelea kumuweka kola sawa mumewe, “...alafu kama kawaida yako umeacha chai kwenye kikombe” winifrida aliukunja mdomo kwa juu huku macho yakiwa katika kikombe katika meza ya chakula iliyokuwa karibu nao na kusitisha zoezi. “Mmh haya nipatie” aliongea Richard huku
akitabasamu na kukichukua kikombe mkononi mwa mkewe fundo moja tu akamliza chai yote akaitupia macho saa ya mkononi mwake “Saa mbili na robo sasa” aliongea kishaakamsogelea mkewe na kumpiga busu shavuni. “Unajua
siamini kama leo tumeikosa ibada hivi hivi mume wangu”“Wala usihofu sina budi kuufanya huu mkutano ni muhimu
sana… tena leo niandalie ugari wa dona nimeumisi sana,”Richard aliongea huku akiwa tayari ameshaufikia mlango
mkubwa wa kutoka nje. “Haya sawa take care Honey” “You too”. Winifrida akasogea hadi katika mlango akatoa kichwa
kumuangalia mumewe akiondoka, alibaki akitabasamu tuhuku paji la uso likiegemea mlango.

Baada ya Masaa kazaa.
“Habari za Ulimwenguni toka katika izaya ya kiswahili ya DeutscheWellemjini Boni mimi ni Ukhty Zukheirah Abdallah, Katika tarifa ya habari mchana huu, marekani yasitisha mashirikiano yake na Urusi juu ya Syria, wakati Uturuki ikiongeza muda wa hali ya hatari hadi mwakani na ripoti
ya Amnesty International ikifichuwa kwamba ni mataifa kumi tu duniani
yenye uchumi usiozidi asilimia mbili nukta tano...” sauti hiyo ilitokea katika redio ndogo iliyopakatwa kwenye mapaja na
bwana aliyevalia sare macho yakiwa
yameikodoloea redio masikio yamemsimama yakitega kila neno toka redioni akiwa juu ya kiti cha plastiki. Mara
akashtushwa na sauti ya geti ikigongwa kwa nje bira mpangilio kiasi cha kumfanya kukunja sura na kulitupia jicho la hasira geti lakini uso ukiwa hauna uhakika maana si kwa kugongwa huko, akatulia na kutegesha masikio shingo kaipindisha mkono ukiwa katika redio akipunguza sauti kuhakikisha kelele hiyo ya geti anaisikia vizuri, alipotambua kuwa ni kweli kuna mtu anagonga geti sura ikazidi kukunjamana. Akatazama katika kifaa maalumu kwenye ukuta kikionesha wanawake wawili na mabegi yao, alitulia
akabonyeza kitufe pembeni yake “Nyinyi kina nani na mna shida gani? Kwani hamja ona kitufe cha kengere mnagonga
hodi kama kuna ugomvi” aliongea na kusikilizia “Dada zake mheshimiwa Richard tufungulie au sio hapa” ilisikika sauti ikitokea katika kifaa hicho ukutani. “Subirini kidogo…" aliongea bwana huyo na kugeuka tayari kuondoka “Jumaa
kuna nini hapoo” Wini akiwa anarejesha mlango na kusimama aliongea kwa sauti “Kuna wanawake wawili wanasema ni
dada zake kaka Rich…” Wini akiwa amesimama moyo ukamlipuka kiasi cha kupeleka mkono kifuani akijizuia “…Je!
Niwaruhusu?” aliongea Jumaa ‘Mungu wangu wamefata nini tena?’ Wini alijiongelea nafsini, kabla hajapata jibu la swali lake Jumaa akaongea “…niwaruhusu waingie?” Wini akameza fundo la mate la uchungu lililopita kwa tabu kooni, mkono
ukiwa bado katika kitasa “Waruhusu” aliongea na kurudi ndani kinyonge. Juma akabofya sehemu na geti likajifungua
kwa umeme mambo ya teknolojia, wadada wawili hao wakaingia, “Hivi wewee kisa cha kutuweka masaa muda wote
nini hasa” Eva aliongea kwa ukali huku macho yakiwa kwa Jumaa hii ni baada ya kupiga hatua kazaa ndani ya uzio wa
ukuta wa matofali ulio nakshiwa vizuri na kupendeza.“Samahani mnisamehe siwatambui mimi ni mpya hapa
nilikuwa nauliza kwanza” Jumaa alijitetea “Alafu unaonekana mshamba mshamba imekuwaje kaka akakuweka mtu kama
wewe hapa mtu simple simple tu khaa!” Eva aliongea akimtazama kwa dharau, Jumaa kwa makini alibaki kumtazama wazi akionekana kuchukizwa machoni “Wote wapo?” Eva aliuliza “Aliyekuwepo ni dada Winifrida kaka Richard yeye alitoka tangu asubuhi” Jumaa alijibu akificha
macho yake asibainishe hasira zilizomuandama wakati huo,
“Shoga twende zetu” Eva alimgusa bega ndugu yake na kuongoza njia kuufuata mlango. “Ooh mawifi hao karibuni
jamani” Winifrida aliiweka rimoti katika meza akanyanyuka kwa furaha kuwasogelea wageni wake. Ester akamuangalia Winifrida kwa jicho la dharau huku kasimama, akampandisha
akamshusha “Fsyuuuuu…naona unajitanua tu kwa raha zako” Ester aliongea kwa majivuno. Winifrida alihisi mwili kupatwa
na baridi alihisi shari ikimnyemelea lakini akajizuia “Eeh bibi si unajua tena…” Wini alichombeza akinyoosha mkono
kulichukua begi la Ester macho yakiwa kayainamisha chini.‘Eeeh Mungu nipe usalama’ Winifrida alijisemea katika nafsi
yake “Fatuma njoo uchukue begi lingine unifate tafadhari”aliongea Wini huku akianza kulivuta, wakati huo Fatuma
akimfata alipo. Kisha akarudi, “Karibuni wifi zangu jisikieni mpo nyumbani” Wini alisogea pembeni na kukaa “Hivi we
mwanamke kwa kaka yetu ulichokikosa ni nini” Wini alishtushwa “Wifi Ester una maana gani sijaelewa” “Huelewi?
huelewi nini we mwanamke mchawi sana wewe” Ester safari hii aliamua kusimama kwa ghadhabu jicho limemtoka kwa
hasira kidole kakinyoosha kwa Wini, Wini alibaki kabung’aa tu kama mtu asiejielewa. “Sikiliza wewe kinyago cha mpapule tumekuvumilia tumechoka sawa tunataka utuambie kwanini umemroga kaka yetu, unachotaka hasa nini?” Eva nae alijinasua kwenye sofa na kumsogelea Wini akampiga singi
takatifu lililomfanya Wini kuinamia mto wa Sofa uliokuwa pembeni yake. Wini bado alikuwa hajang’amua kitu aliwaza
na kuwazua kipindi akiwa bado kajiegemeza kwenye mtokwenye sofa machozi yakimlengalenga kinachomaanishwa na wifi zake hakukipatia jawabu.

Fatuma alionekana kujiminya katika ukuta akishuhudia kila kitu juu ya mawifi
wakimshambulia Wini, alionekana kujiskia vibaya sana alitamani kwenda kumsaidia kulipiza mashambulizi lakini moyo ulimzuia “Eva mbona unazunguka zunguka tu…” Ester alimsogelea Wini karibu na kumuweka kati kama mwanamke
anae sutwa “…Sikiliza wewe mwanamke sisi tumechoka tunahitaji kuitwa mashangazi haiwezekani miaka kibao hii
umejikalia kama jiwe tu hujiskii vibaya mwanamke wewe” Winifrida alijivuta vuta kichovu na kukaa kitako, alijiinamia,
alijishika kichwa akiwaza maana safari hii tayari alishaelewa maana ya ujio huo nyumbani kwake. Uchungu uliendelea
kumjaa aliona wazi mwisho wake tayari ushafika hana msaada dunia sasa imeshaanza kumtazama alihisi kuchekwa
na kuzomewa na watu wengi, “Mwanamke jeuri huyu halafu hana haya huoni aibu? Hivi hujui Kama thamani ya mwanamke ni mtoto unajua nina hasira sana na wewe na tumekuja kistaarabu tunataka utulete watoto uliowafichamchawi wewe sisi kwetu tuna uzazi ukae na ulijue hilo”. Eva aliongea kwa uchungu sana karibia kutoa machozi, “Hebu fikiria ingekuwa wewe ndio dada yake ungejiskiaje eeh…” Ester aliongea nakumtia singi wifi yake lililopindisha shingo ya Winifrida “Tunachokiamini ni kuwa wewe ni mchawi habari zako tunazo kwa hiyari yako chagua kuondoka au laa sivyo…” Winifrida alinyanyuka kabla Eva hajamalizia kuongea akatoka mkuku mkuku akaziparamia ngazi kupanda juu kwa kasi kiasi cha kuwashangaza wifi zake wakabaki kutazamana.
“Na safari hii utaondoka tu na bado alaaaa” Eva alimrushia maneno na kweli yalimfikia Wini kabla hajaingia chumbani
kwake yalishadakwa na masikio yalikuwa kama mkuki maana yalimuingia moyoni akahisi kuna kitu kimekaa katika koo lake
kinamzuia kuhema aliufungua mlango na kuingia.

Masikini dada wa watu nguvu zilionekana kumuishia alijiona ni mtu aliyepoteza kitu cha thamani katika maisha yake na kutokana na kupoteza kwake basi nae thamani yake imeshuka daraja,hana thamani alijitupa kitandani na kuanza kumwaga kilio, kitanda hakikufaa alijinyanyua na kusogelea kioo cha kabati
huku akiendelea kulia na kujitazama alivyo umbwa “Masikini mimi nimeshajiaribu mimi ooh Mungu wangu” alijisemea kwa
uchungu mara likamjia wazo, alionekana kuanza kuhema hovyo hovyo alikurupuka na kukimbilia katika droo za kabati alitoa kila kitu na kutupa chini hakuambulia kitu akarudi katika nguo alizitoa na kuzikung’uta ili apate kitu ambacho
kinaweza kusaidia kutoa uhai wake. Baada ya kuambulia mikono mitupu akagutuka akasogelea kwenye dressing table
akachukua kisturi na kusogelea kabati akapanda juu yake na kuanza kupapasa papasa kwa makini akatoa tabasamu la
uchungu baada ya kukishika kitu alichokitarajia akashuka huku mkononi akiwa ameshikilia bastola akaiweka kitandani na kusogelea droo ya dressing table akachukua peni na Notebook alishusha pumzi nzito na kuanza kufikiria kidogo kisha akajituliza kitandani na kuanza kuandika huku machozi yakimtirika. Baada ya kufika tamati na kuridhika akaamua kuusoma kwa sauti.

Mume wangu Mpendwa,

Sioni sababu ya Mimi kuishi kutokana na sababu ya kutokuzaa najiskia vibaya sana mume wangu lakini sina jinsi, mawifi zangu ninaowapenda nao hawanipendi tena wananisema vibaya, sitaweza kuwa na amani kuishi na hali hii, kwanini nikupe maisha magumu mimi sitaki uishi kwa masononeko wakati ukweli ni kuwa mimi ndiye niliyekudhurumu hivyo basi sifai kuishi. Buriani mume wangu maisha mema.”

Wini alimaliza kuyasoma kwa sauti, ‘Inaniuma mume lakini haina budi najua hata nikiishi nitakuwa ni kama mti usio nafaida hautoi kivuli wala matunda wala kuni wala mbao wala majani na mizizi isio ponya hata ndege wataukimbia’ Wini
alijongelea nafsini kisha akasimama akaichukua bastola kitandani akaiweka karibu na sikio, jasho jembamba likaanza
kumtoka nyuma ya shingo huku akiwa kafumba macho.

Kipindi chote hicho mawifi hawakuwa na walijualo juu ghorofani, sebuleni sauti ya redio ilipandishwa ikawa juu wakawa ni wenye kucheza taarabu na kurusha maneno ya vijembe kwa wifi yao huku wakipongezana, Fatuma akiwa jikoni chakula hakipikiki kwa raha roho ilimuuma alitamani apande ghorofani akamliwaze dada ake lakini hakuweza kufanya hivyo.

Ghorofani Winifrida wazo la kujiua bado lilikuwa limeutawala mwili, akili na nafsi “qataa” huo ndio mlio pekee uliosikika
masikioni akatulia sekunde kadhaa kusikilizia maumivu ya risasi itakayopenya katika kichwa na kuvuruga ubongo,

Je Nini kitajiri?????

Itaendeleaaaa....

Mijadara muhimuView attachment 1741102
Kabla sijawowa lazima tupime kwanza isijetokea fedheha kama hii mweeeh

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom