STORY: Sitaki Tena

SEHEMU YA 27

Ilipoishia jana usiku...... ...Mara nikawaona askari wanne tena ni wale wale wa treni wakiwa wanakuja kwa mbali eneo tulipokuwa na yule mdada.. Endelea..... ".....Uhh...! uhh....! uhh....! uhh....! uhh...!" Tayari kijasho chembaa kikawa kinanitoka pamoja na kuwa na kaubaridi pale chini ya mti nilipokuwa nimepitiwa na usingizi mzito baada ya wale wadada walipodondosha mitungi yao ya maji na kunikimbia, "Mungu wangu.....! Kwanini tena jamani naendelea kuziota hizi ndoto za mauaji mimi.....?" Nilijikuta nikiilaumu nafsi yangu kwani ni kweli nilikuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu,Eti nimeliona treni limeharibika mpaka nikamuua mzee wa watu na kumvua nguo na kuzivaa mbaya zaidi eti nikaota nimekamatwa na yule mtoto wa huyo Mzee Mhhh...!,

"....Eeeh mwenyezi Mungu niondolee ndoto chafu hizi zisiniandame tena....?" Nikasali kimoyomoyo kisha nikainuka pale chini ya ule mti niliokuwa nimepitiwa na usingizi kisha nikaenda hadi pale wadada walipondondosha ile mitungi yao ya maji na kuanza kukombeleza japo niweze kupata vijimaji kidogo. Jua la Asubuhi likiwa tayari limeshachomoza kabisa na mpaka kufikia leo nilikuwa natimiza siku ya pili bila kupata chochote tumboni zaidi ya hivi vijimaji. Nilikuwa sina jinsi yoyote zaidi ya kuendelea na safari huku nikiwa sijitambui ninapoelekea,nilitembea tena umbali wa kama kilometa sita hivi ndipo nilipokutana na vinyumba vidogo vidogo. Furaha ikanijaa zaidi moyoni mwangu pale nilipowaona watu. "...Wale wadada walionikimbia kulee,mmoja wapo yulee ngoja nimuwahi nimuulize kitu...!" Nikatembea fasta mpaka alipo na nikajua tu hajui kiswahili wala kiingereza kwa hiyo hapa nikutumia njia ya vitendo atanielewa, Safari hii yule dada hakuonesha woga wowote akanipeleka mpaka nyumbani kwao nikakutana na wazazi wao wakanipokea vizuri tu huku wakiongea wenyewe kwa lugha yao. "....Lengula... Pela ine.....!" "...Isa kuno....!" Yule mzee akatoka nje na kurudi na wazee wenzake wakiwa na shauku ya kutaka kunijua kiundani zaidi. "Lengula Mweni.....!" "Pela ine Cilyo.....!" Mara nikashangaa wameleta chakula pamoja na kombe kubwa la maji hivyo nikaanza kuambulia maneno nikajua "kumbe 'Cilyo' inamaana ya chakula...!" Sikukiweza kula kile chakula kwani ilikuwa kama maugali ugali ambayo hayajaiva vizuri yaliyochanganywa na mimboga ya majani iliyoungwa ovyo ovyo tu,Sema kutokana na njaa ya siku mbili niliyokuwa nayo,nilijikuta nafakamia hivyo hivyo na kushushia na yale maji.. "Naomba niongezeni tena maji ya kunywa...." Huku nikioneshea kwa vitendo kuwa nahitaji niongezewe maji, "Pela ine I majie....!" Yule Mzee akamuamlisha mtoto wake aniletee,aliponiletea nikayanywa kisha nikamsikia akimtuma tena kwa mara ya pili yule mtoto. "Ya Na Ubwite Bane Nsansa.....

" Akatoka halafu baada ya muda akarudi na dada mmoja mweupe aliyeonekana kama mtu tofauti na wao kuanzia mavazi hadi nywele zake alivyozitengeneza, "How are you....?" "am fin., wh ar u....?" Nikajua nimeshapata mtetezi wangu kuwa yule dada alikuwa akijua kiingereza lakini nilijiuliza sana ametokea wapi na amejuaje kiingereza maeneo haya,nilijiuliza mara mbili mbili bila ya kupata jibu, "whr ar u cme frm?" "Am frm South Africa to Tanzania..!" Nikamdanganya huku nikiangalia kwa pembeni kwani woga na aibu vilikuwa vimeshakuwa vimenitanda mule ndani huku wale wazee wakitusikiliza kwa ukaribu japokuwa hawakujua chochote pale. "Ar u Tanzanian....?" "Yes of course..." "Waaaooh...! Do u knw how to spk swahil language.....?" "Ndio....." Nikamjibu kwa kiswahili mpaka akashangaa na hakuweza kuamini ndipo nilipoanza kujitambua kuanzia sehemu niliyopo. "Hapa tupo kusini Magharibi mwa Zambia na siyo mbali sana na mpakani mwa Tanzania" "Ulisema unaitwa nani...?" " Brendah BreBre...." Nikamdanganya nikijua kuwa siku akijua kuwa naitwa Levina inaweza ikaleta matatizo yoyote. "Unaskia Brendah...", "Abee...!" "....Hiki kijiji kinaitwa 'Nakonde' ni maarufu sana hapa Zambia na hizi lugha wanazoongea huku ni ki 'Bemba' na ki, 'Njanja' ndicho wanachozungumza sana lakini ki 'Bemba' ndicho tunachozungumza sana,na nadhani umeshakisikia kabla sijaingia hapa..." "Happy..., Nafurahi sana kukufahamu....!" "Hata mimi nafurahi sana Brendah...!" Baada ya pale tukakumbatiana na kutoka na huyo dada anayeitwa 'Happy' na kuongozana naye mpaka kwenye kijumba chao, Jioni ilikuwa imeshatimia huku nakajua nako kakitaka kuzama,nikiwa tayari na ninayemwamini ni mtetezi wangu,nilipewa maji ya kuoga nikajisafisha damu zote zilizogandia mwilini na baada ya hapo alinipa nguo zake nivae kisha akanipa chakula cha usiku, "Kwahiyo Happy...?unasoma au....?"

"Hapana Brendah, Mimi nafanya kazi kulee 'Custom' (Mpakani)tena ni mbali kidogo na hapa huwa nakuja kuchukuliwa na Gari asubuhi sana...!" huku tukiendelea kupiga naye stori nyingi za maisha huku zangu nikizificha ficha asizijue hata kidogo,ilipotimia tena mda wa kulala alinipa shuka na kulala naye katika kitanda chake. Kwa mara nyingine nikafurahia maisha kwani ilipofika asubuhi niliamka kwa furaha zote huku mwili wangu ukisisimka mara kwa mara nadhani ni kutojiamini na mazingira niliyokuwa nayo, Nilivyoamka sikumkuta Happy bali niliambulia kikaratasi kilichoandikwa ujumbe pembeni yangu, Nikakichukuwa na kukisoma. "NAELEKEA OFISINI SAMAHANI SANA BRENDAH KWA KUTOKUAGA.,NISINGEWEZA KUKUAMSHA LAKINI USIHOFU MCHANA NITARUDI TUTAKUWA PAMOJA..UTAJIPIKIA CHAKULA NA MTAKULA HAPO NYUMBANI. Wako Mpendwa HAPPY. Nilipomaliza nilisisimka tena nikatoka nje na kukata mjiti kisha nikachukuwa kikombe cha maji nakuanza kupiga mswaki... *********** * * * Levina kaanza maisha mapya, atadumu hapo? * * * Vipi upande wa Gervas imeishia vipi...?
 
SEHEMU YA 28

Ilipoishia asubuhi... ...Nilipomaliza nilisisimka tena nikatoka nje na kukata mjiti kisha nikachukuwa kikombe cha maji nakuanza kupiga mswaki Endelea...., Kama kawaida yangu nilipomaliza nikaingia jikoni na kutengeneza chai ya rangi kisha nikaingia tena chumbani kupumzisha akili, Mwili wangu sasa ulikuwa umechangamka japokuwa akili haikuwa sawa hata kidogo kwani nilikuwa njia panda kwa vitu viwili,kwanza ni mawasiliano ya wazazi wangu na hofu kubwa ikiwa kama Gervas akienda kumwambia Mama kuwa mimi ndio niliyemuua Mama yake wakati sivyo, Pili ni hatma yangu ya kukaa hapa, "Nitakaa mpaka lini hapa.....?

" Hilo swali ndilo linalonisumbua sana kichwa changu haswaa. Nikiwa pale chumbani kwa Happy nikizubaa huku nakagua huku na kule nikaiona albamu ya picha zake nikavuta na kuanza kuziangalia moja moja, "Daaah kumbe Happy alishaolewa....? Natamani na mimi ningekuwa nimefunga ndoa.....?" Nilizidi kujiumiza sana moyoni,nikaona ile albamu haina tena umuhimu kwangu nikaitupia pembeni na kuanza kupekua pekua mule ndani japo nimjue Happy kiundani zaidi. "...Waaaooh....! Mungu mkubwa kumbe anasimu ya akiba...." Sikuweza kuamini mara moja kwani ni kweli nilishuhudia simu ya ku 'slide' aina ya nokia n95,haraka haraka nikaiwasha nakuanza kupiga namba ya 'Jammy' anayeishi na mama yangu, "....Nakumbuka ni +255713133633 au na 4 mwishoni kama sikosei...." Nikapiga lakini ikawa haipatikani,nikarudia mara mbili mbili bado ikawa vile vile,Nikajikuta nimelegea na nguvu kuniisha haraka haraka halmashauri yangu ikafanya kazi fasta nikafungua sehemu ya internate ili nimtafute Jammy kupitia mtandao wa kijamii wa facebook, "Oooh... My God..! Why....! why....! why.....?" Maskini simu ikakatika chaji nikabaki natafuta sehemu ya kuchajia lakini pale hakukuwa na chaji ya kuchajia japokuwa palikuwa na umeme ule wa Jua,kwahiyo ikanibidi niiweke simu pembeni na kupumzika. "...Brendah.... Brendah..... Brendah.....!" "Ooooh....! Happy....!" Alikuwa ni Happy amerudi toka ofisini na ndiye aliyeniamsha kutoka usingizini pale. "Amka mpendwa...! Vipi ushakula....?" "hapana Happy..., Nilikunywa chai tu nikatengeneza na mihogo kidogo nikala ile asubuhi nimeshiba sana tu mpaka sasa....." "Ngoja nibadili nguo basi niingie jikoni nipike fasta fasta.....!" "Hapana wala usijisumbue Happy mwenzako nimeshiba kweli ile mihogo na chai..." Akabadilisha nguo zake za ofisini na kuvaa za kawaida lakini swala la kupika akawa ameshaghairi tena kupika kwani kiukweli nilikuwa nimeshiba sana.

"Leo nina habari njema kwako Brendah.....!" "Ipi tena hiyo Happy....?" "kutoka ofisini ninapofanyia kazi....!" Nilihisi kama moyo unataka kupasuka kwa furaha ya ajabu niliyokuwa nayo, "Eenhh...Nimejaribu kuongea na mchumba wangu wa zamani ambaye tunafanya naye kazi 'custom' (mpakani) na amekukubali kuwa mwanzoni mwa mwezi ujao ujiandae uanze kazi..." "Kazi gani tena hiyo jamani....!" "Brendah...,ni kazi nzuri na ya kawaida mojawapo ni ya upishi pale ofisini au u 'mesenja' kwakuwa unajua kiingereza itakufaa sana.....", "Ni sawa ahsante sana Happy kwa kuonesha unanijali kama rafiki wa karibu...." "Usijali Brendah na ukijituma zaidi unaweza ukabadilishwa kitengo na kupewa chochote kikubwa pale ofisini....!" Nilijihisi si mtu wa mikosi tena bali ni mwenye bahati ile ya mtende, Niliishi na Happy vizuri sana kama ndugu na rafiki yangu wa karibu,alikuwa akiishi peke yake lakini majirani waliokuwa wamemzunguka aliishi nao vizuri kama ndugu na ndicho kitu nilichojifunza kutoka kwa Happy kuishi na jamii. ~ BAADA YA WIKI TATU~ Siku ya kwenda kuanza kazi ilifika huku nikiwa sijulikani tena kwa jina la Levina pale mtaani bali ni Brendah BreBre, Ilikuwa ni asubuhi sana kwenye saa kumi na moja,Happy akiwa amenipa nguo zake za ziada za kazini, zilizonipendezesha mwili wangu vizuri na ka mwili kidoogo kalikuwa kanaanza kurudi,kichwani nywele zilianza kuniota kwa mbaali hivyo nikazichana huku yale makovu mwangu yakinipungua mwilini kwa kuweka poda nyingi na mdomo wangu nikiupendezesha kwa kuupaka lipsi ya rangi ya pinki na mguuni nikivalia kiatu si kirefu sana,kiukweli ni mda mrefu sikuvaa hivi vitu hivyo ikanifanya nijione tofauti na hata mwenyewe happy.

"Brendah.,kiukweli umependezaa....!" "Ahsante happy...." Tayari mlio wa honi ulikuwa ukipigwa kutokea nje ukiashiria gari limeshafika. "Brendah si upo tayari....!" "Tayari nakusikiliza wewe tu....!" "Haya twende zetu gari ndo hiyo imeshafika...." Tukatoka nje huku nikijiweka vizuri nguo yangu,nakuingia ndani ya gari tayari kwa kuanza safari... Furaha ilinizidi na kusababisha mwili wangu kunisisimka mara kwa mara huku tukipiga story na kujiona kama vile ni ndoto lakini ilikuwa ni kweli kabisa. "Mnama...!, Huyu hapa ni rafiki yangu na ni kama ndugu yangu anaitwa Brendah niliyokuambia kipindi cha nyuma,anaenda kuanza kazi na sisi leo....!" "Aaaa ahaa....! Brendah.....!" "Nafurahi kusikia kuwa tupo pamoja mrembo....!"

Aliongea kwa utani yule dereva 'Mnama' aliyeonesha kuwa mcheshi sana huku akiendelea kuendesha gari. Ilituchukuwa kama lisaa moja na nusu kufika pale custom (mpakani) mwa Zambia na Malawi (LUBA), wafanyakazi walikuwa wamevalia sare za nyeusi na nyeupe kama niliokuwa nimevalia, "Haya Brendah hapa ndipo kazini kwetu na mpaka uko upande ulee....!" Tuliposhuka tu Happy akawa ananionesha mazingira ya pale huku tukiwa tunaelekea kwenye nyumba ambazo zimekaa kama ofisi zipo tatu tukaingia mojawapo kisha happy akagonga hodi.. ******* * * * Levina (Brendah) ameenda kuanza kufanyakazi, itakuwaje? * * * vipi kuhusiana na Mama Levina na Jammy maisha yao? * * * na kuhusu Gervas na mama yake?
 
SEHEMU YA 29

Ilipoishia...., ...ofisi zipo tatu tukaingia mojawapo kisha happy akagonga hodi.. Endelea..... Tulipoingia tu ndani tukamkuta Bosi wa lile eneo keshafika hivyo bila kupoteza mda Happy akaongea naye. "Poka lunda Kumbwa....!" "....Imimonokele..,Pela ine Brendah....!" Akiwa bado Happy anaendelea kuongea na Bosi huku woga ukiwa bado umenijaa na hofu kubwa ikinitanda kutokana na kutojiamini kwamba ndio naelekea kufanya kazi kweli. "Sanguka Brendah....!"

Sikumwelewa Bosi anachosema mpaka Happy aliponielewesha kwa 'Sanguka' inamaanisha karibu kwa ki 'Bemba'. ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ Ndani ya masaa kama mawili nikawa tayari nimeshazoea mazingira ya pale na kitengo kikubwa nilichokuwa nimepangiwa ni u 'Mesenja' na siyo tena usafi kama ilivyotakiwa hapo mwanzo, Nilifanya kazi kwa kujituma zaidi huku malengo yangu nikiyatuliza akilini mwangu, Ilipokaribia muda wa mchana Bosi akawa ametoka na hapo hapo nikapata mwanya wa kuingia tena ofisini mwake nikafunga mlango kwa ufunguo haraka haraka nikaiwahi ile simu ya mezani na kuanza kupiga simu nyumbani, "Yes....! Inaita...! Inaita...! uhh....! Thanx God....!" "Hallow....! Hallow....!" Sauti ya kike ikapokea haraka haraka nikajua tu si mwingine atakuwa ni 'Jammy' tu. "....Levina hapa anaongea, haya niambie fasta fasta mnaendeleaje huko....?" "Wote wazima...? Mama mzima tu...! Tena tupo tunaishi na Gervas hapa nyumbani....!" "Whaaaat.....?" Nilishangaa kwa mshangao mpaka nikajikuta natetemeka na kizungu zungu kikanishika ghafla, Nikiwa bado najishangaa kwa ile simu mara nikasikia hodi inapigwa,nikaanza kunyong'onyea huku nikihisi kama mkojo unajipenyeza kwenye zile sare zangu huku ukitaka kunitoka taratibu,Nikakata haraka ile simu na kuelekea mpaka kwenye mlango kuufungua taratibu huku nikiendelea kutetemeka, "Mhh Brendah....! Nilikuwa nakutafuta sana kumbe bado uko huku....?"

"Nipo rafiki tu yangu,nimeachiwa kazi ya kupanga panga haya mafaili ndio namalizia....!" Nikamdanganya bila hata ya yeye kunigundua nilichokuwa nikikifanya huku nikishusha pumzi taratibu,nikawa katika hali ya kawaida baada ya kuufungua ule mlango na kumkuta ni Happy. "Sasaaaa....! Muda umekwisha na gari ipo tayari twenzetu home....!" "Ok, Poa poa....!" Nikajiweka sawa sawa japokuwa sikuridhika kabisa kutomalizia maongezi yangu kwenye simu. Safari ya kuelekea nyumbani ikaanza na dereva wetu 'Mnama' akaturudisha,nilijitahidi sana kuonesha ninafuraha ili Happy asigundue chochote,nikawa na story nyingi ndani ya gari mpaka kumfanya Dereva Mnama kucheka sana njia yote. ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ Hatimaye tulikuwa tumeshafika nyumbani,jua kali lilikuwa limetawala nikiwa mimi na happy tukashuka ndani ya gari na kuongöza mpaka ndani kisha nikabadili nguo na kuelekea kuoga. Nilipotoka Happy naye akaenda kuoga na aliporudi nikaanza kumdodosa kwa maneno. "Happy hivi kuna simu kama niliona humu ndani jana...?"

"Aaaa haaa....., Eeeh nimekumbuka Brendah si ya Nokia.....?" "Ndio....!" "Aaah...., Si unaona sa hivi natumia hii Samsung..., Ile situmii tena ipo tu...." Akaingia kwenye droo na kunipatia. "Ooh....! Thanx sana Happy.....!" Nilimshukuru sana na kumkumbatia nikionesha upendo wa hali ya juu kwake....." "Lakini hapa huwa hakuna sehemu ya kuchaji mpaka ofisini ndio huwa nachaji simu zangu kwa hiyo kesho tukienda uikumbuke twende nayo.....!" Nilifurahi sana kupata simu huku nikitamani usiku ufike mapema na kukuchwe fasta ili niweze kufika ofisini nikiwa akili yangu yote nikiielekezea ofisini. "Mhh...! Jammy kanitisha kweli kwenye simu., sasa imekuwaje tena Gervas aishi nyumbani kwetu....?" Hilo ni kati ya maswali yaliokuwa yakiniumiza sana kichwa usiku kuchwa bila hata kupata lepe la usingizi huku nikiwa sijui nini kimetokea na kinachoendelea nyumbani. ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ Alfajiri tulivu ilikuwa imeshafika huku nikiwa nafuraha,safari hii nilijikuta naamka mapema na kumuamsha Happy aweze kujiandaa. "....Haya Happy....! Happy....!

Amka kumekucha mpendwa....! Amka mtu wangu....!" Ndani ya dakika chache akawa kesha amka, Nikaanza kuandaa nguo za kuvaa na kitu cha kwanza kabisa kukumbuka ilikuwa ni simu niliyoachiwa na Happy na kuipaki vizuri kwenye kibegi changu na kuingia bafuni. Safari ya kuelekea ofisini ilikuwa imeshawadia huku nikiwa mstari wa mbele kuwahi ofisini pale baada ya kushuka tu. Breki ya kwanza ilikuwa ni kajumba cha mlinzi ambacho huwa kanaifadhiwa mizigo ya watu wale wanaokuwa wamesafirisha vitu vyao kwa njia ya magendo. Haraka haraka nikaiweka chaji na kuelekea ofisini kwa Bosi tayari kwa kuanza kazi. Nilishangaa kumkuta bosi hajafika lakini hilo halikunipa wasiwasi wowote na hata hivyo safari hii sikuwa na hamu tena ya kutumia ile simu ya mezani kwani niliamini tu yangu itajaa chaji na nitaongea na nyumbani muda wowote baadaye.. Nilipomaliza tu kupanga vizuri mafaili kwa Bosi haraka haraka nikatoka na kuelekea kuchukua simu kwenye chaji lakini kabla sijafika eneo lile nikamuona mtu kama Happy akiongea kutumia ile simu yangu niliyoicha kwenye chaji, hofu ikanitawala tena,bila kupoteza muda nikaongeza spidi huku nikimuwahi nisije umbuka, lakini kabla sijamfikia nikahisi kama kuna mtu ananiita nyuma yangu, "Levinaaa....! Levinaaa....! Levinaaa....! Isa kuno....! Isa kuno....!" ******* ¤ ¤ ¤ Je,Kwanini Bosi ameita jina la Levina? ¤ ¤ ¤ Happy anaongea na nani katika simu ya 'Brendah', Levina?
 
SEHEMU YA 30

Ilipoishia.... lakini kabla sijafika eneo lile nikamuona mtu kama Happy akiongea kutumia ile simu yangu niliyoicha kwenye chaji, hofu ikanitawala tena,bila kupoteza muda nikaongeza spidi huku nikimuwahi nisije umbuka, lakini kabla sijamfikia nikahisi kama kuna mtu ananiita nyuma yangu, "Levinaaa....! Levinaaa....! Levinaaa....! Isa kuno....! Isa kuno....!" Endelea.... Nikajikuta nimedondoka chini huku nikiwa sijielewi kwa kile kilichotokea, kwani nikiwa bado nipo pale chini huku nikiendelea kumuangalia Bosi,Mara nikashangaa Mdada mmoja aliyevalia sare kama yangu akimfuata huku akiwa kashika mafaili mkononi. "Aahaa...! Uenda alikuwa anamuita yule mdada anayeenda pale...!, lakiiini....!, Mbona wakati anaita alikuwa ananitazama sana kama ananiita mimi....? Kwanza mimi siitwi Levina naitwa Brendah....!"

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiinuka pale chini kwa ujasiri na ukakamavu wa hali ya juu na kuanza kumfuata Happy eneo alipokuwa. "Brendah vipi tena nikakuona umeanguka pale chini....?" "Hapana nilijikwaa tu jamani....!" Pole sana...,Angalia vizuri huku kuna kokoto nyingi....!" Nilimsikiliza tu huku yale maneno yake yakipita sikio la huku nakutokea kule.., "Kumbe maskini, Happy alikuwa akitumia simu yake ya samsung kuongea na watu...!" Nikabaki nafsi inanishuta baada ya kuona kufuli kubwa pale kwenye mlango nilipoiacha simu yangu. "Happy..., huyu mlinzi yuko wapi....?" Nilimuuliza Happy kwa jazba huku nikiamini labda mlinzi anaweza hata akawa ameichukuwa ile simu. "Kwani nini Brendah....?" "Niliacha ile simu humu ndani kwenye chaji...!" "Basi atakuwa katoka kidogo lakini atakuwa maeneo haya haya wala usijali....!" Happy akanijibu kisha akaondoka na kwenda kuendelea na kazi zake. Nilikaa pale pale nikimsubiri mlinzi mpaka pake alipokuja na haraka haraka nikaiwahi simu na kuiwasha kisha ndani ya sekunde kadhaa nikakutana na meseji kama tatu zote zikitokea kwa Jammy 'Tanzania. "UPO WAPI LEVINA...? FANYA HARAKA URUDI AU UTUME PESA SISI HALI ZETU MBAYA HUKU....!"

Sikutaka kabisa kuiamini ile meseji zaidi ya kuifuta pale kisha nikanyanyua simu na kupiga. "Hallow Jammy....!" "Eeehh.., Levina...? Umepata meseji zangu....?" "Ndio nimezipata,uko na Gervas karibu....?" "Nipo naye ngoja nimpe simu uongee naye....!" "Haya nipe niongee naye...." "hallow Gervas...?" "Levina Mpenzi wangu upo wapiiiiii....?" Nilijikuta machozi yakinitoka niliposikia sauti ya Gervas, Ikanibidi nianze kuamini kuwa ninaye ongea naye ni Gervas. "Mimi nipo mzima tu mpenzi wangu Gervas..., Embu niambie ilikuwaje tangu nilipokuacha pale kwenye treni.....?" "Levina...? Niliteseka na kuumia sana, Tulipofika tu Tanzania huku bado nikiwa katika ulinzi mkali na wale mapolisi wa treni kwa kosa la kufyatua risasi ndani ya treni,tukapitia hospitali kwa ajili ya uchunguzi juu ya kifo cha Mama yangu., ikajulikana kuwa alikufa kwa maumivu makali ya kutokuzingatia dozi za dawa alizopewa,ndipo nikaachiwa huru kwa matatizo yaliyonikuta..., Nikauleta mwili wake mpaka nyumbani,Hivyo tumemzika na sasa mi nimebaki Yatimaaaaa.....!, Yatimaa, yatimaa Levina....? Sina Mama wala Baba....!" "Pole sana Gervas kwa yaliyokukuta....!"

"Levina..,Hapa nilipo sina hata pesa niliibiwa zote kwenye treni,sina kazi na mtetezi wangu aliyebaki ni rafiki yako Jammy..." "Mama yangu yuko wapi....?" "Mama yako yupo na hawezi hata kuongea zaidi ya kutoa macho muda wote,lakini naye amepooza mwili wote,na mimi sasa naelekea kufa kwani miguu yote imeshaoza na inatoa funza wale wakubwa, Jammy kila siku ananiosha na kunipaka dawa lakini haisaidii naendelea kunuka tu,Jammy ni kila kitu yeye ndiye anayemuhudumia Mama yako kwa kila kitu hata pale anapojisaidia hapo hapo,na yeye hana kazi ila tunaishi kwa misaada ya watu,tena wengine wameshatuchoka, nanuka tu Levina nanuka mimi Gervas...? Kuna kipindi nilitaka kujiua lakini Jammy ndiye aliyeniona na kuniokoa..." Nilikata simu kwa hasira,kisha nikaibamiza chini kwa huku nikielekea ofisini kwa bosi nikiwa na akili tofauti... ******* ¤ ¤ ¤ 'Brendah' Levina atafanyaje baada ya kusikia hivyo? ¤ ¤ ¤ Jammy atavumilia kuendelea kuwahudumia Gervas na Mama Levina baada ya kumpata Levina kwenye simu?
 
SEHEMU YA 31


*********

“What's wrong wit u Brendah....?”
Nilipoingia tu nikakutana na maswali kutoka kwa Bosi,
‘’Nothin.....!’
Nikamjibu kioga huku nikijiuma uma na kuonesha kuchanganyikiwa fulani,
‘’Brendah..? I love u...!’’
Sikumshangaa hata siku moja Bosi wetu tangu nimeanza kazi hapa alikuwa akinitaka kimapenzi nikawa namkatalia,
Nikatoka zangu nje na kuzunguka zunguka huku na kule huku nikiwa sijielewi elewi kutokana na hali ya nyumbani.
‘’Brendah...?, Unafanya nini tena hapa.....?’’
Ilikuwa ni sauti ya Happy akiniinua kutoka pale chini nilipokuwa nimekaa huku miguu ikinilegea na kukosa nguvu kabisa.
‘’Happy...., Nashindwa kujielewa kabisa yani......!’’
‘’kwani vipi....?, Embu niambie imekuaje tena.....?’’
‘’Ni ile simu yako Happy....?’’
‘’Imefanyaje tena....?’’
‘’Nimejikuta kwa bahati mbaya nimeidondosha na kuharibika papo hapo..., Ona sasa ilivyokuwa.....’’
Nikamuonesha simu yake ilivyokuwa huku nikamdanganya Happy ili asiweze kujua ukweli wowote kuwa ninachowaza ni nyumbani..,
‘’Pole...Na wala hata usiwaze Brendah.., Tutanunua nyingine kwa muda utumie....!’’
Nikarudi katika hali yangu ya uchangamfu kasha nikaendelea na kazi kama kawaida.


*****************
Baridi lilikuwa kali kiasi kwamba nikabaki najikunyata usiku kutwa,
Mawazo mengi yalinitawala huku nikimfikiria Gervas na sana sana mawazo yalienda moja kwa moja mpaka kuanza kumkumbuka Mama.
‘’Noooo....! Noooo....! Mama....! Mama.....!’’
Nilijikuta nashtuka peke yangu pale kitandani nikipiga kelele zilizofanya Happy aamke kwa kushtuka pale kitandani,
‘’Vipi tena Brendah usiku huu....?’’
‘’Nisamehe Happy.....?’’
‘’Nikusamehe kwa kipi...?’’
‘’Nimekushtua usingizini jamani....!’’
‘’Usijali...,Kwani nini kimetokea....?’’
‘’Happy....!, Nampenda sana Mama yangu,hivyo nimemkumbuka sana....!’’
‘’Kwani ulisema yupo wapi vile....?’’
‘’Yupo anaishi 'Afrika kusini' lakini Baba alishafariki siku nyingi....’’
‘’Pole sana Brendah....!’’
‘’Ahsante Happy....’’
Nikaendelea kumdanganya ili asiweze kujua lolote linaloendelea katika halmashauri ya kichwa changu.
Usiku huo sikuweza kupata hata lepe la usingizi mpaka kunakucha nikaingia bafuni kuoga na nilipotoka nikamuamsha Happy ili naye ajiandae,
Kama kawaida nilivalia mavazi yale yale ya ofisini, gari ikaja na kuondoka zetu,
Siku hiyo nilikuwa nimerudia mambo yangu ya zamani kwani malengo yangu makubwa ni jinsi gani nitaweza kuzipata pesa nyingi ili niweze kuwatumia nyumbani,Hivyo tulipofika ofisini niliingia moja kwa moja mpaka ofisini kwa bosi nikamkuta bado hajafika hivyo furaha yangu ikaongezeka huku nikiamini malengo yangu yatatimia kwa asilimia mia kabisa,
Haraka haraka nikaingia na kujifungia na ufunguo, kilikichofuata nikavua shati na sidiria nikavirushia juu ya meza kisha nikavua ki sketi na taiti niliyokuwa nimevalia vyote nikaviacha juu ya meza ya Bosi,
Na kilichofuata nikaanza kujipapasa mithili ya wale waigizaji wa muvi za utupu Ulaya. Huku nikijipapasa kuanzia shingoni kupitia kwenye chuchu zangu na kumalizia tumboni kwenye kitovu na kisha nikatanua mapaja yangu na kuendelea kuyapapasa kwa hisia kali huku nikisisimka mwili wangu wote,
Mara nikasikia kitasa kinatingishika sikuwa na wasiwasi wowote nikajikongoja kwa mwendo wa madoido nikiwa vile vile utupu na nilipoufikia mlango kabla sijaufungua, Nikalipenyeza jicho langu kwenye tobo la kitasa na kumuona Bosi,kisha nikaufungua fasta fasta,
‘’Supri.i.i.i.i.i......!’’
Nikamvuta tai yake na kuingia naye ndani kisha nikaufunga ule mlango kwa ufunguo.
‘’Ulikuwa ukinitaka kimapenzi siku nyingi Bosi wangu..... Lakini leo nipo ‘spesho’ kwa ajili yako....?’’
‘’Is t true Brendah.....?’’
‘’yeah...!Come an take i t...’’
Nikamshuhudia Bosi akivua nguo zake haraka haraka huku akionesha kuwa na uchu, Nami nikamsaidia kumvua viatu na soksi,kisha suruali na hapo akawa mtupu kabisa kama mimi nilivyokuwa..
‘’Kabla hatujafanya chochote Bosi.., Tukubaliane kwanza!
‘’Sema..., Mimi nipo tayari kwa lolote Brendah....! ‘’
Nikamshuhudia bosi akiwa yupo 'hot' huku akionesha kusisimka sana na kuniangalia sana eneo la sehemu zangu za siri.
‘’Utanipa 'kwacha' ngapi....?’’
Haraka haraka akavuta koti la suti yake na kuchomoa Cheque ya 'kwacha' 700,000.
‘’Thanx bosi wangu, mwaaah...! mwaaah...! mwaaa!’’
Nilifurahi sana na kuona sasa nitakuwa nimepunguza matatizo ya nyumbani,
Hapo hapo bila ya kupoteza muda nikaichukua ile 'Cheque' na kuiweka kwenye sketi yangu na kuirudishia pale juu ya meza na kilichofuatia ni kuanza kumpa utamu wote kutoka mwilini mwangu Bosi,
Nikiwa ndio kwanza najiweka vizuri tuanze kufanya mara tukasikia sauti ya mtu anapiga hodi.
‘’Let' us continue Brendah!’’
Nikaendelea kumshika shika eneo la kifuani kuelekea chini kwake huku akinogewa kwa kufumba macho na kupumua juu juu lakini ile sauti ya mtu iliendelea kubisha hodi na kwa mara hii ilikuwa inaboa,
‘’Mr...? Mr...?
Brendah....! Brendah....!’’
Halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua kuwa ile ni sauti ya Happy,
‘’Happy....?’’
Nikaita kwa nguvu huku Bosi akinitolea macho,kisha nikamuacha pale utupu tukiwa bado hatujafanya mapenzi,nikatoka pale kifuani kwake nakuelekea kuufungua ule mlango,
‘’Nooo...! Noooo....! Brendah dnt do that...?’’
 
SEHEMU YA 32


Sikumsikia chochote alichoongea Bosi, Nikakifikia kitasa na kushika ufunguo na kuanza kuufungua nikiwa namalizia tu kuufungua mara nikasikia sauti ya viatu ikiashiria kuwa yule mtu anaondoka zake, hivyo bila kupoteza muda nikaufunga ule mlango na kurudi kuendelea na Bosi.
Nilipomaliza pale nikachukuwa nguo zangu na kuzivaa kisha nikahakikisha ile 'cheque' ipo kwenye sketi 'then' nikamwaga bosi.
‘’Bye....! Boss....,’’
‘’Ok..., Thanx Brendah.....!’’
‘’Usijali utakuwa unapata zaidi ya hapa!’’
Yale maneno yalimkosha sana Bosi na kumfanya aniangalie nyuma mara mbili mbili nikiwa natoka kuelekea nje.
Nilipourudishia tu mlango wa Bosi nikiwa kwa nje furaha ilinijaa tele moyoni huku nikiamini zoezi la kwanza limeishatimia na kinachofuatia ni jinsi gani nitazituma zile pesa.
Muda wa kurudi nyumbani ulifika huku nikiwa mtu wa kwanza kuingia katika gari ya Mnama.
‘’Happy bado hajafika tu!’’
‘’Mimi nilijua mtakuja naye kama kawaida yenu!’’
Nilimuuliza dereva Mnama kwa mshangao lakini ikabidi tumsubiri kwa muda mpaka atakapokuja ndio tuondoke.
‘’Naona yule anakuja!’’
Tukamuona anatokea kwa chooni,
Akafika nakuanza safari ya kurudi nyumbani.
Muda wote tuliokuwa njiani Happy alionesha kama kukasirishwa na kitu kwani hakuniongelesha kitu chochote zaidi ya kuongea na dereva Mnama mpaka tunafika,
Na hata tuliposhuka bado Happy hakuonesha furaha yoyote kwangu, ila sikutaka nimuulize chochote kwa muda ule nikaendelea kufurahia zoezi nililolifanya la kujipatia hela kutoka kwa Bosi.
Muda wa kulala ulifika bado Happy hakuonesha na furaha yoyote,
‘’Happy vipi mbona leo upo hivyo....?’’
‘’Brendah.....?’’
‘’Abee....!’’
‘’Tangu tumeanza kazi..Bosi amewahi kukwambia kitu chochote kuhusu mapenzi...?’’
‘’hh...! Happy hapana sijawahi kumsikia na hata kama akiniambia siwezi kufanya chochote kwanza mimi najiheshimu sana Happy...!’’
‘’Unajiheshimu...? Kwa kipi?’’
‘’Yani..Nilikuwa nakuangalia tu siku zote, huna haya wala aibu mwanamke wewe? Yani nimekusaidia unanigeuka brendah....?’’
‘’Kwani ni nini Happy..?’’
‘’Usijifanye hujui, hizi mali zote unazoniona nazo mimi,zote ameninulia huyo huyo Bosi?’’
‘’We unajua kabisa natembea na Bosi,halafu na wewe unaenda kunip ‘replace’ hapo hapo?’’
‘’Haya nakuanzia kesho uende huko huko sitaki kukuona tena na hiyo kesho tukiondoka utafute sehemu ya kwenda kulala na kuishi....!’’
‘’Nooo....! Nooo.....! Happy usifanye hivyo mimi sitembei na Bosi jamani....’’
‘’Ni.i.i.i.i.i.i.i.i.i.ni.....? Na ule ujinga uliokuwa ukifanyanaye mule ofisini leo...? Ulidhani sitajua...? Nilikufuatilia mpaka nimejua malaya wewe...? Na uondoke na pepo lako la ngono uko.....?’’
Nilibaki nikiumia sana na kuilaumu nafsi yangu kwa kile nilichokifanya
‘’Lakini ilinibidi nifanye vile.., We hatakama Bosi angenipa pesa, asingenipa za kutosha mpaka kwa njia ile....!’’
Nilijikuta nikijisemea kimoyo moyo huku nijiendelea kuilamu nafsi yangu na kisha nikamwangalia Happy kwa hasira kali huku akiwa amegeuka upande wa pili akijiandaa kulala.
Nikakaa kwa muda takribani nusu saa pale kitandani huku Happy akiwa keshapitiwa na usingizi na alikuwa akikoroma tu kwa muda ule,
Nilitafakari ni jinsi gani nitaweza kwenda mpaka Zambia mjini na kuibadilisha ile 'cheque' nakuwa pesa ili niweze kuituma nyumbani,nikainuka kwa kunyata pale taratibu mpaka kwenye sketi yangu nakuanza kuisachi kwa nia ya kuitoa ile 'cheque',
Niliisachi mara mbili mbili huku nikiwa siamini macho yangu kuwa siioni,
Nilisachi mifuko yote lakini sikuona chochote,nikavuta na sketi ya Happy ya kazini nayo nikaisachi bado sikuambulia kitu,kijasho kikanitoka huku nikitetemeka,
‘’Nikisema nimwamshe Happy nimuulize lazima atanipandishia na kukasirika zaidi....’’
Haraka haraka nikapekua pochi ya Happy napo sikuambulia ile 'cheque' zaidi ya vijihela vyake kama kwacha 600 tu...!
Sikupata usingizi usiku kutwa huku akili ikinichemka sana.
‘’Basi bwana...!, Huenda Happy ameichukuwa na kuificha.....!’’
Nilijisemea kimya kimya huku nikijiegeza kwenye kitanda japo nipate kausingizi kwani yalibaki masaa machache niamke,


* * * * * * * *
 
SEHEMU YA 33

Asubuhi na mapema ilipofika nilikuwa tayari katika gari ya Mnama huku pembeni yangu alikuwapo Happy japo mpaka ilipofika asubuhi bado hakubadilisha msimamo wake kwani hakuniongelesha chochote,
Nilitamani nimuulize dereva kama ameiona ile 'cheque' lakini ilinibidi niwe na subira mpaka tukifika ofisini,kwani Happy atajua kila kitu,
Tulifika eneo la kazi lakini bado Happy alikuwa yupo karibu sana na dereva nikahisi tu kunakitu wanataka kuongea, nikawaacha na kuelekea ofisini tayari kwa kuanza kazi,
Safari hii nilimkuta Bosi keshafika lakini sikutaka kabisa kupoteza muda nikakaa pale nje ya ofisi ili niendelee kuwaona Happy na dereva, nikiwa bado naendelea kuwaangalia mara nikashuhudia dereva akifungua mlango wa gari yake kisha akatoa ile 'cheque' kwa mbaali nakumpatia Happy..
"Happy....! Happy....!’’
‘’Please....! 'Cheque' yangu nirudishie please....!’’
Nikauvaa moyo wa kiujasiri na kuanza kumfuata eneo alipo kwa hasira.Lakini ile namkaribia tu Happy akaiweka ile 'cheque' vizuri mikononi mwake nakuanza kuichana chana vipande huku akipangusa mikono yake kuashiria amemaliza kuichana,
Mishipa ya shingoni ilizidi kunitoka ikiambatana na macho yaliokuwa yamenitutumka mithili ya mjusi anapobanwa na mlango,
‘’Kwanini umechana 'Cheque' yangu...? Kwanini Happy....?’’
‘’Ndio nimechana...! Amua unavyotaka sasa....?’’
Nilimshika shati lake kwa nguvu huku Dereva Mnama akimsaidia kumtoa lakini haikuwezekana kwani Mungu aliniumba tofauti nikiwa na nguvu nyingi sana kuliko baadhi ya wanaume,
‘’Nadhani hunijui ila umenifahamu enh....?’’
‘’Kwenda zako uko.....!’’
‘’Happy unasemaje.....?’’
‘’Malaya mkubwa we utanifanya nini....?’’
Akizidi kunijaza hasira na kunifanya nimrukie kwa vichwa, nikamuunganisha na dereva wake mnama wote mpaka chini,
‘’Brendah....! Brendah....! Brendah stoooop....! Stooooop.....!’’
Ilikuwa ni sauti ya Bosi aliyekuwa ameshaambiwa juu ya timbwili niliokuwa nalifanya na sasa alikuwa ameingilia kati na kunifanya niwaache pale chini wakigala gala,
‘’Kwa heshima yako Bosi nawaacha la sivyo ungezikuta maiti hapa’’
‘’Haya wote twendeni ofisini kwangu!’’
Bosi alituamrisha tumfuate mpaka ofisini kwake tukasuluhshe, lakini hata tulipofika ofisini bado hakuna alionesha kumwelewa mwenzake chochote,
‘’Haya Mnama na Happy nyie nendeni na wewe Brendah kuanzia sasa kazi huna, Na urudi kwenu’’
‘’Unasemaje Bosi?’’
Nimekwambia sitaki kukuona tena hapa ofisini?’’
Mchozi ukaanza kunitoka huku nikiwangalia dereva Mnama na Happy wakitoka nje na kufunga mlango,wakiniacha mule ndani na Bosi.
‘’Unasikia brendah,Nimekwambia hivyo kwa sababu zangu kwani najua nimeshaharibu? Sikukwambia kama natembea na Happy!’’
‘’Kwanini sasa ulikuwa ukinitaka kimapenzi?, Kwanini? Kwanini bosi?’’
‘’Brendah! Tulia, Hapa kwangu umefika mimi Happy simtaki yeye ndio alijipendekeza kwangu isitoshe nimegundua anatembea na yule dereva ndio mana nikamua niwe na wewe, pliz niamini!’’
‘’Lakini sina pakulala Bosi,kwani nilikuwa nikiishi nikimtegemea Happy kwa kila kitu na ndio keshanifukuza kwake sasa?’’
‘’hilo usijali brendah! Nina nyumba kubwa tu ipo kule karibu na mjini na naishi na mfanyakazi wa ndani tu,
Kuanzia sasa nitakuwa naishi na wewe na hapa kazi utaendelea kama kawaida wala usihofu!’’
‘’Kweli bosi?’’
‘’Mimi si ndio Bosi? Niamini mimi sasa!’’


¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤
 
SEHEMU YA 34

Sikufanya kazi yoyote siku hiyo zaidi ya kutulia nje ya ofisi ya Bosi siku nzima, Muda wa kuondoka ulifika huku nikiwashuhudia Happy na dreva wakirudi zao nyumbani,
Bosi alipomaliza kazi zake alinichukuwa na kwenda kuanza maisha mapya kwake,
Huku akilini nikiwa na lengo moja tu la kuhakikisha nimemchuna pesa za kutosha na kuhakikisha nyumbani wanaishi vizuri bila matatizo yeyote,
Ndani ya dakika chache Bosi alikuwa tayari ndani ya gari huku nami nikingia tayari kwa safari,
‘’Brendah? Mbona bado umekasirika wewe?’’
‘’Hapana bos!’’
Tabasamu basi mpenzi wangu enh’’
Nikaonesha kufurahi kidogo japo nimfurahshe Bosi,
Hatimaye ndani ya nusu saa tukawa tumeshafikia nyumbani kwa Bosi,ilikuwa ni jumba kubwa lilokuwa na fensi ya kuvutia,walinzi waliokuwepo pale getini ilikuwa ni jibu tosha kuwa kuna ulinzi mkali mule ndani.
‘’Karibu Brendah! Jisikie upo nyumbani’’
‘’Thanx Bosi’’
Nilimuitikia na kumpiga busu kuonesha kuwa nampenda kiukweli huku moyoni nikiwa najua dhamira yangu kwake.
‘’Hapa sebuleni 'Dining' palee na upande wa huku kuna sehemu ya kupikia twende na chumbani ukapajue!’’
Palikuwa ni pazuri sana kwakweli, ikanifanya nisahau machungu yote yaliotokea kule ofisini.
Usiku ulifika nikiwa nimetoka kuoga na taulo langu moja tu huku ndani nikiwa mtupu kabisa, Bosi alikuwa sebuleni akifanya kazi zake kupitia 'laptop' yake.
Nilipomaliza kujiandaa nikavalia zile zile sare za kazini kwakuwa sikuwa na nguo yoyote ya kubadilisha,nikaelekea sebuleni kuongea na Bosi.
‘’Sema Brendah ushaoga?’’
‘’Yeah!, nimemaliza muda mrefu na hapa naelekea kulala!’’
‘’Keshooo! Inakubidi usiende ofisini naenda mimi,
Hivyo utaondoka na mlinzi mmoja mpaka mjini kwenda kufanya 'shopping' ya nguo zako!’’
Akatoa cheque nyingine ya kwacha 800,000 na kunipa.
‘’Oooooh thanx Bosi wangu!’’
‘’Kuanzia sasa usiniite Bosi tena niite 'Your husband to be...?’’

******

‘’Haya basi Mme wangu nimekuelewa ehh Sasa? Mi natangulia kulala’
‘’Haya we nenda, Mimi wacha nimalizie hapa kidogo nakuja....!’’
Usiku huo kwa jinsi nilivyokuwa na furaha na ile 'Cheque' niliyopewa
Nililala kwa furaha sana japo kidogo sikuwa na amani kwani ilinibidi nimsaliti Gervas,
Nikiwa kama mwanamke mwenye hisia kama wanawake wengine,nilishindwa kabisa kuzuia hisia zangu kwa kulala tena na bosi usiku mzima na kufanya naye mapenzi tena huku nikifurahia kabisa..



¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤
 
SEHEMU YA 35

Asubuhi na mapema tulivu,nilijikuta nikishtuka pale kitandani kwanza kwa kutoamini kama kweli nipo sehemu nyingine tofauti na kwa Happy,
Kipupwe 'Air Condition' iliyovuma chumba kizima ndiyo iliniamsha kutoka usingizini, Bosi alikuwa ameshaondoka na kuniachia ujumbe kwa njia ya kijikaratasi kuwa atachelewa kurudi na kurudi jioni ila nisisahau kwenda kufanya 'shopping',
Ule ujumbe ulikuwa umeambatanishwa na pesa nyingine kama kwacha elfu 20, pamoja na funguo za gari lake jingine la matumizi ya nyumbani..
Furaha iliyoambatana na kusisimka mwili mzima kuanzia kichwani vilinijaa mwili wote na kuona kama napoteza muda hivyo haraka haraka nikaingia bafuni, nikatoka na sare zangu tena zile zile za ofisini kisha nikamwaga mfanyakazi wa mule ndani nikampitia na mlinzi getini.
‘’Lingana Tala Pe’’
‘’Bubuko Babwino ende la Mujini!’’
Nilimuongelesha kwa ki 'Bemba' japo sikuwa nakijua kiviile, nilimuulizia barabara ya kwenda mjini.
Kwakuwa alikuwa na heshima na utii tena mbele ya mke wa bosi akanielewa hivyo akanielekeza tu njia ya mjini ili niende peke yangu, hapakuwa mbali sana, hivyo sikuona umuhimu wa kufuatana naye, nikahakikisha nimebeba zile hela na 'Cheque' nikatoka pale na kuongoza mpaka mjini,
Sikutaka kabisa kupoteza muda fasta nikawa tayari nimefika mjini.
‘’African Development Bank in Zambia....’’
Nikaibadilisha ile 'Cheque' kuwa pesa na zoezi lililofuatia hapo nikutafuta maduka ya nguo hivyo nikatumia ile kwacha elfu 20 tu kununua nguo huku ile kwacha laki 8 nikiwa nayo kwa ajili ya kwenda kutuma nyumbani.
Ndani ya kama nusu saa nilikuwa tayari nimefanikisha karibu kila kitu huku nikibakiza zoezi la mwisho la kutuma hela nyumbani,
Nikaanza kutafuta huku na huku hatimaye nikapata baadaye sana 'WorldRemit Money Transfer'
Lakini kabla sijazituma zile pesa ikanibidi nipige kwanza simu nyumbani.
‘’Hallow! Hallow Jammy?’’
‘’Eeh Levina!’’
Nikaanza kumsikia akilia kwenye simu na kunifanya akili ianze kuhisi kitu mbele ya hisia zangu,
‘’Levina....? Mama hatunaye tena!’’
‘’Unasema nini Jammy?’’
‘’Leo ni siku ya tatu toka amefariki ghafla, tena alifia mikononi mwa Gervas...! Tulijitahidi kukutafuta kwenye simu lakini ilishindikana kwani kila tulipojaribu kukupigia simu ulikuwa hupatikani...."
‘’Kwa hiyo Mumemzika? Au mwili wake uko wapi?’’
‘’Tumeuhifadhi monchwari’’
‘’Musimzike mpaka nije,Niko njiani nakuja’’
Nikakata simu kwa hasira huku nikionesha kuchanganyikiwa, nikaingia kwenye gari na lile fuko langu la hela huku nikitoka pale kwa kasi ya ajabu kuelekea nyumbani.
Ilikuwa imeshatimia kama saa sita mchana huku nikiwa njiani kurudi kwanza nyumbani kwa Bosi kisha nijue ni jinsi gani nitafika Tanzania.
Fasta fasta nikamkuta Bosi bado hajafika nyumbani nikapitiliza mpaka breki ya kwanza chumbani na kuanza kusachi kama kuna hela sehemu yeyote,
Droo kama mbili zilikuwa zimefungwa nikazivunja ile ya kwanza nikakutana na bastola nikaichukuwa, nikavunja na ile droo inayofuatia nikakutana na hela nyingi sana sikutaka hata kujua idadi yake nikaziweka kwenye mfuko nakuzisomba zote bila kubakisha hata senti, kisha nikachukuwa ufunguo wa gari na kutoka nje,
Nikaliwasha gari bila hata ya kuwaaga wale walinzi ninapoelekea nikatoka spidi, ile nakunja tu kona ya nje ya geti mara
Macho yangu yakakutana uso kwa uso na mfanyakazi wa ndani niliomwacha muda si mrefu ndani,Na kwa muda huu alikuwa katoka nje ya geti huku kashikilia viatu vyangu mkononi,
‘’Pe nape Sekesha?’’
‘’Esha Akaso!’’
Nilimjibu kuwa akae navyo kwani sikuona tena umuhimu wa kuvaa viatu vile kwa muda huu,Nikaliondoa gari kwa kasi huku nikibadilisha barabara ya upande mwingine nisije kukutana na Bosi,
Hivyo nikaingia barabara ya vumbi na kulikimbiza gari,
Ndani ya kama dakika ishirini na tano nilikuwa tayari nauona mpaka niliokuwa nafanyia kazi ulee,nikageuza gari na kunyosha njia upande mwingine nikienda sambamba na ule upande niliouacha,
Huku akili yangu nikilekezea zaidi nyumbani haswa Mwili wa Mama na hali ya Gervas huko aliko anaendeleaje,
Nilikuwa kama mtu aliyepigwa ganzi huku anafanyakazi kwa bidii kwani kiukweli nilijivika moyo wa jiwe tena lile jiwe sugu lililolaliwa na mawe makubwa zaidi ya uwezo wake huku nikikatiza kwenye kibarabara chembamba cha vumbi kilichokuwa na misitu mikubwa na mirefu iliyozunguka lile eneo lote.
Nilitembea mwendo mrefu sana wa kama zaidi ya kilometa mia na hamsini nikiwa ndani ya lile pori refu nikiendelea na barabara ile ile ya vumbi na nilikuwa sielewi kama niko sahihi na ile njia au la! kwani upande niliokuwa nikiufata bado ulilingana na ule wa mpakani niliouacha.
‘’Ooooh Mungu saidia nisipotee......’’
Saa ya kwenye gari tayari ilikuwa ikinionesha imetimia saa Nne na robo ya usiku huku mvua ya rasha rasha ikiwa inanyesha kwa nje,
Kadri nilivyokuwa nafuata ile barabara ndivyo mvua nayo ilikuwa inazidi kunyesha mpaka ikanifanya nisiweze kuona tena mbele,
Hivyo nikapaki gari pale pale njiani nakupumzika kwanza mpaka mvua itakapotulia ndio niendelee na safari,
Lilikuwa ni pori kubwa sana kwani giza lilikuwa ni nene sana huku mbele hakuonekani kabisa japokuwa niliwasha taa full,
Nikiwa bado ndani ya ile gari aina ya 'Toyota Harrier' Huku vioo vikiwa vyeusi tupu 'Tinted' ndani nilikuwa nimefungulia redio ya 'CD' huku nikisikiliza nyimbo laini 'Slow Music' na wimbo wa 'End of the road' wa kundi la 'Boyz 2 Men' ulikuwa ukipigwa taratibu huku ukikonga moyo wangu nakunifanya nianze kupata usingizi taratibu huku niking'ang'ania 'mstering' na nikiamini milango yote nimeiloki hawezi kuingia mtu au kitu chochote,
Nilipokuja kushtuka ilikuwa tayari imeshatimia saa nane za usiku huku mvua ikikolea na kuwa kubwa zaidi,
Nikaona kama nitaendelea kusubiri mpaka mvua iishe nitachelewa kufika,
Hapo hapo nikaliwasha gari langu ili niendelee na safari lakini gari liliwaka ila kutembea likawa haliendi,
‘’Ooh Jesus...! Help me..! Help me...!’’
Nilijikuta nikisali huku mapigo yangu ya moyo yakibadilisha mwelekeo nakuwa na kasi ya ajabu,
Nilijaribu kama mara tatu kubadilisha gia lakini ikashindikana kuondoka, likaendelea kung'ang'ania pale pale,Fasta fasta nikachukua tochi na ile bastola kisha nikashuka na kuanza kulizunguka gari nikimulika kwa tochi mpaka mbele ya gari nikafungua 'boneti' (mlango wa mbele ya gari )sikuambulia chochote zaidi ya moshi kwa mbali huku injini ikichemka tu kwani nilikuwa sijui matatizo yoyote ya gari hivyo nikarudishia nakuendelea kuilikagua tairi moja baada ya jingine huku nikipigwa na ile mvua na kulowa tepe tepe hadi nilipokuja kugundua upande wa kushoto tairi moja limenasa kwenye matope mazito kwasababu ya ile mvua kubwa iliokuwa ikiendelea kunyesha.
Nikarudi na kuingia ndani ya gari kuchukua kisu kisha nikakata miti mirefu mirefu yenye majani na kuweka pembeni ya lile tairi lililonasa.
Iliniwia kama nusu saa bila kuogopa kitu chochote pale msituni huku nikilowana nguo zote tepe tepe nikaingia ndani ya gari nikapiga 'For wheel' na kuchomka kwa nguvu hatimaye nikafanikiwa japo nilikuwa nimelowa sana zile nguo nikazivua na kuzitupa halafu nikavuta zile nguo nilizokuwa nimezinunua na kuzivaa kisha nikaendelea na safari,
Nilitembea na gari mwendo si mrefu sana huku nikiwa bado ndani ya ule msitu na nikiwa sijakutana na mtu wala aina yeyote ya gari na tayari ilikuwa imetimu kama saa kumi alfajiri kwani na sauti za ndege nilikuwa nimeshaanza kuzisikia kwa mbaali,
‘’Oooh My God....! Nini tena.....!’’
Mti mkubwa ulikuwa umedondoka katikati ya barabara tena mbele yangu huku ukizuia njia yote gari nisiweze kupita,Akili ndio ikachoka kabisa kwani nilihisi kama mtu kauweka lakini ukweli ulibaki pale pale kuwa umedondoka kwa bahati mbaya ikanibidi nilizime lile gari lisije kuisha mafuta kisha nikakilaza kichwa changu kwenye 'msteringi' nikabaki natafakari ni jinsi gani nitapapita pale,
Mwili wote ulikuwa umenyong'onyea na kukosa nguvu kabisa huku macho yakiwa hayafanyi kazi kabisaa yakiambatana na kichwa kilichokua kikianza kuniuma kwa mbaali,
Nilijikuta nakata tamaa ya kuendelea na safari huku nikitamani nirudi nilipotokea,nikabaki nimeuegemea msteringi kwa hasira ya kushindwa kupita pale mbele kulipokuwa na gogo kubwa,
Mara nikashangaa mwanga mkali unamulika mbele yangu ukiambatana na mlio mkubwa ulioashiria kuna kitu tena kikubwa kinakuja mbele ya macho yangu.
Furaha na uoga kwa mbali vilinijia kwani niliamini lazima njia mbadala ya kupita pale nitaipata,
Ilikuwa ni gari aina ya 'One Ten ' nyeupe kama zile za kazini nilipokuwa na Happy,
‘’Sakamika Tama!’’
‘’Tama..!’’
Nikawaona wakiongea ki lugha huku wakishuka ndani ya gari watu wawili wakiwa wamevalia nguo za kiaskari tena wale wa mpakani halafu wakaliangalia lile gogo lililoanguka katikati ya barabara kisha wakaanza kunifuata eneo nililopo,
‘’Ukisikia kukamatwa ndio leo Levina wa watu mimi!’’
Haraka haraka kabla hawajanifikia nikachukua lile fuko la mahela na kulificha chini ya kiti cha dereva,nikachana kipande cha nguo yangu nakujifunga mguuni kisha nikaichukua ile bastola na kuiweka kwa ndani ya nguo zangu karibu kabisa na sehemu zangu za siri baada ya hapo nikafungua ule mlango na kutoka kwa nje huku nikichechemea upande mmoja nakujifanya kama mtu aliyejereuliwa na mtu au mnyama mkali.
‘’Lupese...! Lupese!’’
Niliomba msaada kwa kutumia lugha yao ya ki 'Bemba' kwani niliambiwa eneo lote la kuzunguka Mpaka huwa wanazungumza lugha hii ya ki 'Bemba' au ki 'Njanja'
Pale pale mmoja wao akaniwahi haraka na kunishika mguu akidhani labda nina matatizo hapo hapo nikatumia mwanya huo huo kujiangusha mpaka chini huku nikiachia mapaja yangu wazi nakuanza kupiga makelele yakulia kwa maumivu,
‘’Ubuuuta Mokola...!’’
Kisha nikawaona wakibishana halafu baada ya muda wakaelewana na kujigawa huku mwingne akielekea kwenye gari yangu mwingine akafungua zipu ya suruali yake tayari kwa kunibaka,
 
SEHEMU YA 36


‘’Eeeh Mwenyezi Mungu...! Mkosi gani tena huu jamani Levina mimi aaaaah....! Liwalo na Liwe....!’’
Nilijikuta nailaumu nafsi yangu kisha nikajijaza moyo wa kijasiri,
Ikanibidi nijilegeze ili aamini kuwa nitafanya naye mapenzi,
Hapo hapo nikatelezesha mikono yangu hadi kwenye nguo huku nikijifanya namvulia nguo,nikaendelea kuvua ile nguo yangu ya ndani hadi nikafikia pale nilipoificha ile bastola nakuichomoa kisha nikamzungushia mkono kama namkumbatia hapo hapo nikamfyatua risasi kama tatu na kufa hapo hapo,
Nikainuka pale fasta fasta na kumfuata yule aliyekimbilia ndani ya gari langu,
Nikamkuta anafurahi peke yake huku kashikilia lile fuko la hela,
‘’Ibele Omupu....?’’
Pale pale na yeye nikamfyatua akafa kisha nikachukua lile fuko langu la hela,Nikazichukuwa na zile nguo zangu kwenye gari kisha nikaviamishia upande wa gari ya wale watu niliowaua na kuligeuza lile gari na kuendelea na safari yangu,
Ile kasi niliogeuza nayo na mtikisiko wa vijibonde maeneo yale vilinifanya nisikie sauti kubwa ya kiume ikitokea ndani ya gari niliokuwa nikiliendesha huku mkono wake mmoja ukinishika kwa nguvu shingoni mwangu na mkono wake mwingine ukinishikia kisu kikubwa mithili ya panga au shoka.
‘’Who ar u....?’’
Kwa uoga wa uliokuwa umenitawala haraka nikajikuta nimefunga breki ghafla, kisha yule mtu akachukuwa lile fuko la hela akanisukumiza kwa pembeni nakuingia mwenyewe upande wa dereva ili aendeshe yeye gari,
Sikujua ni wapi tunapoelekea kwani alizidisha spidi nadhani alikuwa akinipeleka ofisini kwao,
Sikutaka kabisa kufanya makosa kwani nilijua kabisa nachezea kifo fasta fasta nikaivuta ile bastola yangu nakumlengeshea usawa wa kichwa chake,kabla hajaongea chochote nikawa tayari nimeshamfyatua,nikamfuta damu damu baada ya hapo nikamlaza pembeni yangu na kuendelea na safari yangu.
Kwa muda huu kulikuwa tayari kumeshapambazuka kwani ilikuwa imeshatimu saa Mbili asubuhi na nilikuwa nimeshatoka eneo la ule msitu na kwa sasa nilikuwa kwenye vinyumba nyumba tu nikikatisha barabara ya lami bila kuogopa kuwa niko na gari tofauti,
Niliendelea kufuata barabara hadi nikafika sehemu nikakutana na wakulima wametoka shambani nikalisimamisha gari langu nakuwaongelesha.
‘’Ubulalo...?’’
Niliwaita kwa ki 'Bemba' lakini hawakunielewa hata kidogo zaidi ya kutizamana.
‘’Huyu mtu vipi....? Sijui anaongea lugha gani....?’’
‘’Aaaah....! Kumbe mnajua kiswahili.....?’’
‘’Ndio tunajua...! Kwani wewe ni nani....?’’
‘’Kwanza mniambie hapa ni wapi jamani....?’’
‘’Unapaona paleee.....?’’
‘’Wapi...? Pale kwenye lile geti la nyavu nyavu....?’’
‘’Eeenh...! hapo hapo ni mpakani mwa malawi na Tunduma....!’’
‘’Unamaana hapa ni Malawi na kule ni Tanzania....?’’
‘’Eenhe...!,Haya tuambie wewe unaitwa nani....?’’
‘’Mimi naitwa 'Mamamia Mango....!’’
Nikawadanganya jina huku nikiwaacha wakiangaliana na kunicheka jina langu.
‘’Bye...! Ahsanteni sana....’’
Nikatoka kwa mwendo wa taratibu huku nikitafakari ni jinsi gani nitapapita pale mpakani,Halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugeuka pembeni ya gari nakuucheki ule mwili wa mtu niliomuua kwa risasi,Nikamvua nguo zake zile za kiaskari kisha nikazivaa kuanzia suruali yake na shati kisha nikamalizia na kofia kwa juu ikinifunika karibu eneo lote la sura yangu,nikacheki kwa nje sikumuona mtu yoyote nikauchukua ule mwili wa yule mtu ukiwa uchi vile vile kisha nikauburuta hadi nyuma nakuufunikia na turubai.
Nikaliwasha gari na kuanza kuingia lile eneo la mpaka taratibu bila kuonesha woga wowote nilipofika askari mmojawapo akanifungulia geti haraka haraka huku akiamini kabisa lile gari ni la pale pale ofisini kwao.
‘’Salama afande....!’’
Nikamwitikia kwa kichwa kwani sikutaka hata nimwitikie kwa sauti angenigundua kiurahisi hivyo nikatoka spidi huku nikikwea ile barabara ya lami kwa mwendo mrefu zaidi huku nikiamini sasa niko Tanzania lakini ni Tunduma.
Ndani yapata kama masaa mawili kwenye na nusu hivi huku njaa ikianza kunitawala na nguvu kuniisha kwa mbele yangu kwa mbaali nikaona kama kuna mpaka mwingine nikapunguza mwendo.
‘’Oooh shiiiit....!’’ Nini tena kile....? Kumbe kunampaka wa kutokea na kuingia...?’’
Nilifumba macho kwa dakika mbili kisha,

********
 
SEHEMU YA 37



‘’Eeeh Mwenyezi Mungu ninusuru nisikamatwe.....!’’
Nikaendelea na safari yangu nilichokuja kushangaa hata pale getini nilifunguliwa vizuri tena bila hata ya kuulizwa chochote na askari wa pale wala kukaguliwa kwa maana ile gari ilikuwa inafahamika kule nilipotoka.
Nikiwa namalizia kutoka pale mpakani mmoja wa wale askari pale getini ambaye ni wakike akabadilisha mawazo na kuniita huku akinifuata haraka haraka,
‘’Hey....! Hey....! Hey stoooop.....!’’
Nikasimama na kumuangalia akinifuata huku mkono mmoja kashkilia 'Radio Call' akiongea na mtu,
‘’....Lakini anayeendesha ni Mdada aliyevalia sare za askari wa huko kwenu....?’’
‘’Eenhe....! Huyo huyo ndio anayetafutwa kwa kosa la mauaji ya askari wetu wawili msituni na kaiba gari ya ofisi hiyo alionayo mkamateni haraka muuaji huyo msimruhusu....!’’
Mwili ukaanza kunilegea huku nikishindwa nifanyeje kichwa nacho kikaniuma ghafla huku meno yakiumana na kusababisha nianze kutetemeka kwa hofu na sana sana ile maiti niliyoivua nguo nakuifunikia turubai nyuma ndio ilinitetemesha sana



¤ ¤ ¤¤ ¤ ¤ ¤ ¤ ¤


Nikabaki namwangalia tu,
‘’Are u criminal....?’’
‘’Mimi siyo muuaji na wala sina hatia....!’’
Nikamjibu kwa kujiamini tena kwa moyo wa kijasiri huku nikiamini lazima atanielewa kuwa ni mtanzania kwa sababu nilisikia akiaongea kiswahili.
‘’Unaitwa nan?’’
‘’Mamamia mango....’’
‘’Huko umetokea wapi na unaelekea wapi....?’’
Kwa kawaida ukiniachia nafasi ya kuongea huwa sifanyi kosa hata siku moja,
Pale pale nikachomoa fuko langu la hela nakutoa kwacha kama za laki Mbili kisha nikampatia
‘’Chukua hizi naomba uniache niende...!’’
‘’Hapa siwezi kuchukua, wenzangu si unawaona pale wanavyoniangalia..? hebu pisha huko...!’’
Akafungua mlango akapanda siti ya pembeni ili nimpeleke kwa mbele kidogo ndio achukue zile pesa.
‘’Haya twende mpaka pale!’’
Nikaliwasha gari nakuendelea na safari lakini tulipofika tu pale aliponiambia ikawa ndio safari yake ya maisha imeishia hapo, kwani niliposimama tu nilichukuwa ile bastola yangu kisha nikamwekea kichwani mwake.
‘’Hapo hapo usitingishike?’’
Nikaikoki na kumfyatua kisha nikachukua ile 'Radio call' yake nikaiweka ndani ya gari,
kisha nikaendelea na safari tena kwa kasi ya ajabu kutoka pale.
Haikunichukuwa muda kwani ndani ya masaa matano nilikuwa tayari naingia mbeya mjini na breki ya kwanza ilikuwa, 'SOUTHERN BUREAU DE CHANGE' sikufanya kosa nikaingia na kubadilisha nusu ya zile pesa nikawa na kama milioni thelathini nikaingia kwenye kiduka cha nguo na kununua kibegi kidogo cha mgongoni cha kuwekea nguo zangu pamoja za zile pesa kisha baada ya hapo nikitafuta kasehemu cha kupata chakula.
‘’Unauzaje chips mayai?’’
‘’Elfu moja na mia tano!’’
‘’Fanya kunitengenezea fasta fasta niondoke....’’
‘’Usijali bosi wangu...’’
Alikuwa ni kijana machachari akinitengenezea chipsi katika mgahawa wa 'Mmeru kiosk'.
Fasta zile chips zikawa tayari nikampatia pesa kisha nikaingia 'supermaket' na kuchukuwachukuwa maji na soda za kopo bila kusahau 'red bull' kwani huwa nazipenda kwa kuondoa uchovu mwilini mwangu.
Nikaingia ndani ya gari nakula fasta fasta kisha nikashushia na maji na safari ya kuelekea dar ikaendelea.
Ndani ya masaa matatu na giza lilikuwa limefunika kwani ilikuwa kwenye saa tatu za usiku nikawa tayari nipo kwenye lile pori la 'Liamkena' nilipomuua 'Pendo' kipindi kilee,
Pale pale nikakunja kona nakuiacha barabara ya lami nakuingia porini palipojificha nikazima taa za gari kisha nikautupa ule mwili niliouficha kwenye turubai na baada ya hapo nikalala mule mule kwenye gari.
‘’Hallow...! Hallow....! mpakani hapo...! mpakani hapo...! Huyo muuaji kapatikana au bado, uko wapi tuwafate....? ....Hapa Tunduma mpakani tupo?’’
Sauti ya 'radio call' ya yule askari niliyomuua ndio iliniamsha kutoka usingizini pale pale nikacheki saa ya kwenye gari ikawa inaonesha imefika saa kumi alfajiri hapo hapo nikashtuka nakubadilisha zile nguo za kiaskari kisha nikachukuwa nguo zangu zilizobaki pamoja na zilepesa zangu nikazidumbukiza kwenye kile kibegi nakuliacha gari nikikimbia kwa miguu huku nikitafuta barabara ya lami.
Nilikumbuka mengi sana hapa porini kwani ndicho kipindi nilichomuua 'Pendo' na hata kuna wanakijiji walinihudumia huku nilivyoumia mguu.
Ndani ya kama dakika kumi nikawa barabarani na begi langu mgongoni huku nikisubiri gari ya kuondoka nayo kwenda Dar es salaam.
Baridi lilikuwa kali sana lakini ilinibidi kulizoea sikukaa sana likapita basi la 'HOOD' nikalipungia mkono nakuingia ndani ya basi, Abiria karibu wote walikuwa wakinishangaa nadhani ni kwasababu ya kupandia pale msituni tena nikiwa mwenyewe bila ya mtu yeyote, sikuwa na wasiwasi wowote,
‘’Nauli shilingi ngapi....?’’
‘’Kwani wewe unaishia wapi...?’’
‘’Naenda mpaka Dar...!’’
‘’Elfu kumi na Nane...!’’
Nikampatia noti ya elfu ishirini kisha akanirudishia elfu mbili nakunipatia siti.



* * * * * *
 
SEHEMU YA 38

Ndani ya masaa kama matano kwenye na nusu tayari nilikuwa nimepapita Morogoro na tunaitafuta Chalinze,
Moyoni sikuwa na wasiwasi wowote kwani nilijiamini kwa asilimia mia sitakamatwa wala kuulizwa na mtu yeyote juu ya kilichotokea huko nyuma nilipotoka.
Hatimaye nikawa tayari nimeshafika 'Ubungo' Dar es salaam nikachukuwa teksi ya kunipeleka mpaka nyumbani kurasini lakini hali niliyokuta pale ilikuwa ya kawaida kwani hakukuwa na dalili yoyote ya msiba,
Mlango ulikuwa umefungwa, Nilipiga sana hodi bila ya kusikia chochote hakukuwa na mtu yeyote halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta nakuelekea nyumbani kwa kina Gervas, Lakini nilipofika nilikuta pamebadilika sana kwani kulikuwa na geti huku fensi ya ukuta iliyopendezesha na rangi ya pinki na nyeupe,
‘’Hodi...! Hodi....!’’
‘’karibu...!’’
Nilikuta watu wengine tofauti na nilivyodhani labda ningeweza kumkuta hata Gervas au Jammy lakini akatoka dada mmoja mweupe mfupi aliyevalia kanga za kijani.
‘’Wenyewe nimewakuta....?’’
‘’Ndio wenyewe wapo! Kwani ulikuwa unamuulizia nani? Mama au baba?’’
‘’Hapa si kwa akina Gervas?’’
Akashtuka na kunifanya niingiwe na wasiwasi nakudhani labda nimekosea sio pale,
‘’Gervas? Gervas yupi?’’
Moyo ukanilipuka nakushindwa kuelewa elewa kama ni pale au nimekosea njia.
‘’Samahani embu naomba niwaone waliopo niwaulizie?’’
Nikaingia moja kwa moja lakini niliokutana nao kweli ni watu tofauti na nilivyodhania.
‘’Za hapa jamani!’’
‘’Safi karibu binti...’’
‘’Ni muda mrèfu sijafika hapa nilikuwa nataka kujua Gervas kwa sasa yupo wapi?’’
‘’Tangu alipotoka Marekani na mwili wa marehemu mama yake nakumzikia pale makaburi ya kurasini na kwa sasa anakaa nyumba ya pale mbele kwa Mama Levina....’’
‘’Ndio nyumbani kwetu...’’
‘’Na yule aliyefariki ni mama yake Levina wamempeleka monchwari wanamsubiri mpaka....’’
‘’Mimi ndio Levina wanaomsubiri...’’
Nilijikuta nikiupangusa mchozi uliokuwa umeanza kunidondoka alipokuwa anaelezea kuhusiana na mama yangu..
‘’Kwani ndio wewe levina....?’’
‘’Ndio mimi....!’’
Nikashuhudia yule mzee na mke wake wakiingia chumbani kisha bada ya muda wakatoka wakiwa wamebadilisha nguo.
‘’Haya twende binti...’’
Aliongea yule mzee huku nikiongozana nao mpaka stendi ya daladala kuelekea hospitali,
Muda wote sikutaka hata kuvua begi langu wala kuruhusu mtu yoyote anisaidie kwani niliamini ndio uhai wangu hivyo kama litapotea nitaathirika kwa namna moja au nyingine.




* * * * * *
 
SEHEMU YA 39

‘’Fire..,Msimbazi..,muhimbili....!’’
‘’Haya wakushuka fire....?’’
Tayari tulikuwa tumeshafika maeneo ya fire huku tukikatiza njia ya kuingilia muhimbili,
Kwa bahati nzuri tulipofika muhimbili moja kwa moja tukaongoza mpaka monchwari na kumkuta Jammy akiwa nje na nesi huku amejifunika mikanga mwili wote, sikuelewa walichokuwa wakiongea.
‘’Jammy...? Jammy...?’’
Nilipomuita pale pale akageuka nyuma na kunikimbilia kisha akanikumbatia kwa uchungu huku akilia na kunifanya na mimi mchozi uanze kunidondoka huku nikitoa maneno kwa ukali.
‘’kweli Mama kaenda Jammy? Mama hatunaye Jammy?’’
‘’Kweli na mwili wake wameuhifadhi humu ndani na una wiki moja sasa!’’
Akataka kunipokea kile kibegi nilichokuwa nacho mgongoni lakini nikamkatalia.
‘’Twende sehemu wanayolipia tuutoe leo leo Jammy.., Na Gervas yuko wapi....?’’
‘’Gervas yupo 'Ocean road hospital' kalazwa na yeye kutokana na mshtuko alioupata wakati Mama amefariki’’
.. Iliniuma sana lakin nikawa sina jinsi kwani ilinibidi nitatue tatizo moja moja,
‘’....Embu twende zetu huku, kwani umeshalipia hela yeyote ya kukaa mwili wa marehemu hapa monchwari....?’’
‘’Hapana niliomba wakanielewa na kumuhifadhi....’’
Nikamchukua Jammy na kuwaacha midomo wazi kwa mshangao kwani kiukweli nilikuwa ni kama zaidi ya mtu aliyechanganyikiwa tayari kuekaelekea mpaka sehemu wanapouza majeneza.
‘’Jammy unaweza kukumbuka Mama alikuwa na urefu futi ngapi...?’’
‘’...5.5....!’’
Haraka haraka tukachukuwa jeneza pamoja na gari ya kubebea maiti na kuongoza mpaka ndani tena hospitali kuuchukuwa mwili wa marehemu Mama yangu.
Ilinibidi kuendelea kujikaza pale mpaka nilipoamini ni kweli Mama yangu sinaye tena Duniani.
Tulipofika tu nyumbani sikutaka mtu yeyote kujua kuhusiana na swala la mazishi, hivyo nikatafuta vijana kama kumi wakanifanyia kazi ya kuchimba kaburi pale pale pembeni na lilipokuwa kaburi la marehemu Baba kisha tukamzika na baada ya hapo nikawapa kazi ya kulijengea ikiwa ni pamoja na kaburi la Baba kwani nilikuwa limeharibika.
Kisha nikamchukuwa Jammy na kuelekea hospitali kumuona Gervas.
‘’....Umesema amelazwa Ocean Road....?’’
‘’Ndio Levina...!’’
Ndani ya dakika kama kumi tulikuwa tunaingia geti la 'Ocean Road hospitali, Nilijitahidi kusahau yaliotokea nyuma lakini bado nilikuwa kama natokewa na picha ya marehemu Mama.
Tulipofika hospitali breki ya kwanza nikaingia kwanza chooni kujisaidia na kisha tukaingia wodini, Maskini tulimkuta Gervas akiwa kapitiwa na usingizi huku miguu yote miwili akiwa hana imetolewa yote, Nilitaka kupiga kelele kwa mshangao lakini Nesi akawa tayari ameshafika pale.
‘’Nyie ndio ndugu wa huyu mtu...?’’
‘’Ndio sisi....!’’
‘’Mlikuwa wapi siku zote mpaka hospitali inachukuwa jukumu la kumsaidia huyu mgonjwa siku zote mpaka mnavyomuona...?’’
‘’Matatizo nesi..., Matatizo...?’’
‘’Kwani na haya siyo matatizo...?’’
‘’Nesi kwanza inabidi mtuelewe kuwa hapa unapotuona tumetoka kumzika marehemu Mama yetu....!’’
Kabla sijamalizia kumwelezea yule nesi mara akatokea Nesi mwenzake huku akiongea maneno kwa ukali.
‘’...Wanafiki wakubwa hao...! Wanakuambiaje....?’’
‘’Eti wamefiwa....!’’
‘’Nani aliyefiwa...? Huyu levina....?’’
Alipotaja tu jina langu nilipatwa mshtuko ghafla kisha hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua kuwa yule ni Nesi aliowahi kunitesa kipindi cha nyuma nilipolazwa hapa,haraka haraka nikalizungusha begi langu upande wa mbele na kulifungua zipu kwa nia ya kutoa bastola na kumfyatua, Ile naitoa tu
Bastola tayari Jammy alikuwa kaniwahi na kuishikilia,
‘’Jammy niachie...? Niache Jammy nimfyatue huyu mpumbavu...!’’
‘’Nani mpumbavu...? Mpumbavu wewe mwenyewe...! Huu mzoga uliolala na mama yako....?’’
‘’Jammy unamsikia huyu mtu lakini...?’’
Tukiwa bado tunagombana pale mara Gervas akashtuka kutoka usingizini.
‘’l.e.v.i.n.a S.t.o.o.o.o.o.p please...?’’
Nikashusha pumzi zangu huku nikimtolea macho makali yule Nesi na kusababisha umati wa watu ukijaa pale ikiwa ni pamoja na jopo la madokta na manesi wakienea katika eneo lile kutuzunguka pale.
Pale pale dokta mkuu akaja kutuchukua mpaka ofisini kwake kisha akatuandikia maelezo mafupi juu ya mgonjwa na dawa anazohitaji,
‘’Operesheni ya kumuondoa miguu yote tumemfanyia bure na gharama zote za kukaa hapa hospitali nazo tumezifanya bure...’’
‘’Ahsante sana dokta....’’
‘’Hivyo mchukueni mgonjwa wenu muendelee kumtibia nyumbani kwenu....’’
‘’Ahsante sana dokta...’’



* * * * * * * * *


Sikuwa tena na hasira kwani tangu tulipomtoa Gervas hospitali alikuwa anaendelea vizuri na juhudi alizozionesha Jammy akisaidiana na mimi zilimfanya Gervas apone haraka ila akawa anatumia magongo katika kutembea kwake.
Pesa zangu hazikuwa tena za kuridhisha kwani nilipozihesabu kwa mara ya mwisho zilikuwa zimesalia kama milioni ishirini na moja,
Ilifika kipindi Gervas anatakiwa awe na miguu ya bandia ili aweze kutembea, hivyo ikanitoka hela karibia milioni tano yakuwekewa miguu ya bandia tena ile inayoumana na vyuma vyuma kwenye mwili ili vishike, tukawa kila siku tunamfanyia mazoezi hadi akawa anatumia magongo mara moja moja sana.
Furaha ndani ya nyumba yetu iliongezeka maradufu japo hakuna hata moja kati yetu aliyekuwa akifanya kazi lakini kwa zile pesa zilizobakia zilitusaidia sana kutusogeza.
‘’Gervas mpenzi wangu..’’
‘’Sema levina wangu...’’
‘’Salio lililobakia ni kama milioni tisa tu, Embu tushauriane tunafanyaje.....?’’
‘’levina....?’’
‘’Abee...!’’
‘’Inanibidi nikusanye vyeti vyangu vyote kuanzia vya shule mpaka vile vya kazini...’’
‘’Utavipataje sasa...?’’
‘’Aah ah ah..Levina mpenzi siku hizi ni utandawazi tu kwani we hujui kuna 'Internate'?,kwa hiyo uwezo wa ku'download' au hata nikaviagizia kwa njia ya 'fax'...’’
‘’Ok fanya hivyo basi 'as soon as possible' si unaona maisha yetu yanapoelekea....?’’
‘’Usijali Mama...!’’
Akanikumbatia na kunipa busu huku akiuacha mwili wangu usisisimke kwa muda mrefu sana.
Gervas alijitahdi kwa njia zote ili afanikishe suala la yeye kupata kazi, hivyo ndani ya mwezi mmoja alikuwa tayari kafanikisha zoezi la kukusanya vyeti vyake vyote hivyo kila siku kazi yake ikawa ni kwenda mjini kuzurura maofisini kwa ajili ya kufanya usaili 'interview',
Nilijitoa mpaka hela ya mwisho huku tukihonga huku na kule kuhakikisha gervas anapata kazi tena kazi ya kueleweka,na sasa akaunti ilikuwa imefikia hadi laki 1 na elfu themanini huku tukizidi kuchanganyikwa zaidi.
Hatimaye akapata kazi katika kampuni ya 'GEA STAR COMPANY LIMITED' tena kama meneja msaidizi wa kampuni.
Hatimaye hali ikaanza kuwa nzuri kwani matumaini yakarejea tena kwa kasi ya ajabu,
Mshahara wa kwanza kabisa wa gervas ambao ulikuwa ni laki Nane hakuutumia zaidi ya kunikabidhi na kuniachia niutumie kwa matumizi ya hapa nyumbani.
Akili niliyoitumia mi kumkazania Jammy anapata na yeye kazi.
 
SEHEMU YA 40



~ BAADA YA MIEZI SITA ~




Tayari mambo yalikuwa yakienda sawa kwani upendo wa mimi na Gervas ulizidi maradufu huku Jammy akifanya kazi katika kampunialiyokuwa akifanya Gervas lakini yeye Jammy alikuwa katika kitengo cha usafi kwa kuwa hakuwa na elimu ya kutosha hivyo mshahara wake ukawa shilingi laki Moja na Nusu,
Kwa upande wangu nilikuwa nakajisehemu ambapo nilifungua Duka la kuuza vipodozi mchanganyiko, Kiujumla maisha yalikuwa mazuri hadi ikafikia hatua ya Jammy kujipangishia chumba chake na kuanza maisha ya kujitegemea akiwa peke yake hivyo nikabaki mimi na gervas katika ile nyumba yetu huku ya kwakina gervas tukiipangisha na kuwa nachukuwa hela ya kodi kila baada ya miezi Sita shilingi laki Sita hivyo tukawa na uwezo wa kufanya maisha yakawa bora kila siku.
nakumbuka siku moja nikiwa najianda kulala na mpenzi wangu gervas nikamwona yuko tofauti kidogo toka ametoka kazini.
‘’Levina...?’’
“Abe Mme wangu....!’’
‘’Siku ya leo imekuwa nzuri sana yani...’’
‘’Aaah kwani nini kimekutokea mpenzi wangu...?’’
‘’Nimeongezewa mshahara na kuwa kiwango cha juu zaidi...’’
‘’..Eenh kwa hiyo unalipwa milioni mbili....?’’
‘’Umejuaje...? Ndio nimepanda mpaka milioni mbili hiyo ni 'Bonasi' niliyopewa kutoka ofisini kutokana na kufanya kazi kwa bidii....!’’
Nikamkumbatia kwa hisia kali huku nikiamini maisha yetu yataendelea kubadilika na kudumu zaidi ya pale.
‘’...Lakini Levina...?’’
‘’Nini tena Gervas wangu...?’’
‘’kuna kitu kimoja huwa kinaniumiza sana moyoni kila ninapokifikiria...!’’
‘’Jamani kitu gani hicho tena Gervas....?’’
‘’Embu ona jumba tulionalo, ona mali tulizonazo pia angalia na miradi tulionayo..!’’
‘’ndio tunayo kwani vimefanyaje...?’’
‘’Levina maisha hayaendi bila ya mtoto mpenzi wangu...!,embu ona mimi na wewe ni muda gani mpaka sasa hata mtoto wa kupandikiza hatuna...?’’
Hilo swala lilinifanya ninyong'onyee na kuanza kusikia kizungu zungu kwani yote anayezungumza Gervas tena kwa hisia ni kweli lakini ukweli nilionao kutoka moyoni ni kwamba siwezi kuzaa maishani mwangu,mgumba mimi...! mgumba Levina mimi....!

*******

‘’nakuahidi Gervas ipo siku utafurahi tu mpenzi wangu kwani tutapata mtoto tena naimani tutapata hata mapacha cha msingi ni kuwa na subira mpaka siku nitakayoshka mimba...!’’
‘’haya mpenzi wangu tulale sasa yameisha naimani Mungu atafungua njia siku moja...’’
Gervas alinielewa japokuwa nilimdanganya akawa kaamini kabisa na kunifanya nisisimke mwili wote huku nikimkumbatia na kupata usingizi mpaka asubuhi.
Kama kawaida asubuhi ilipofika nilimwandalia Gervas chai ili awahi ofisini na mimi niendelee na shughuli zangu za dukani.ndani ya nusu saa Gervas alikuwa yupo tayari akinishusha maeneo ya dukani kwangu maeneo ya k.koo hivyo na yeye kuendelea na safari yake ya kazini msasani,kiukweli niliyamisi sana haya maisha na niliamini tu ipo siku nitakuja kuishi maisha kama haya na ndio sasa nayaishi tena kwa uhuru na amani tele.




********
 
SEHEMU YA 41


Ndani ya masaa kama matatu ghafla simu yangu ikaita tena kwa namba za simu ya mezani kwani zilijiandika kwenye simu yangu +255 242350304.
‘’Hallow....?’’
‘’Gea star Company hapa. Samahani unamfahamu Gervas?’’
‘’Ndio ni mume wangu kwani vipi tena....?’’
‘’Sisi ni wafanyakazi wenzake,Gervas kadondoka ofisini kwetu na kaumia vibaya sana na kwa sasa yupo hospitali ya 'Regency' upanga...’’
Kabla hajamalizia kuongea nikakata simu.
‘’Ooh My God mkosi gani tena huu tena....?’’
Nikaacha kila kitu na kuelekea mikocheni kumwangalia mpenzi wangu Gervas.Ilinichukuwa kama Dakika ishirini mpaka kufika 'Regency' pale upanga,moyo ulinienda mbio sana huku nikiwa kama mtu aliyechanganyikiwa.
‘’Namuulizia mgonjwa aliyeletwa kutoka ofisi za gea star...?’’
‘’Dada hata salamu...?’’
Nilikuwa sijielewi elewi hata nilipofika mapokezi nilishndiwa kusalimia.
‘’Ooh sorry jamani, samahani sana nimechanganyikiwa...’’
‘’tunasikitika muda wa kuwaona wagonjwa umeisha.,labda ujitahidi uwahi kesho saa kumi na mbili mpaka saa moja na nusu’’
‘’unasema nini...?’’
‘’Dada muda wa kuona wagonjwa kwa leo umekwisha, hatuwezi kukuruhusu...’’
‘’hivi unajua ni nani aliyelazwa....?’’
‘’hata angekuwa ni Rais, hapa kuna utaratibu kama zilivyo sehemu nyingine za kazi’’
‘’Ok, basi nakuomba sana unielewe pliz..! pliz..! pliz..!, Japo niione sura ya mume wangu tu’’
‘’Ok,kwa kukusaidia tu embu jaribu kumuomba mlinzi wa zamu pale pamoja na Nesi wa zamu wakikukubalia nenda ukamuone mgonjwa wako’’
Hapo hapo nikawahi kwenda kuwaomba na wakanielewa hivyo nikaongoza moja kwa moja mpaka wodi aliyolazwa Gervas.
‘’Gervas mpenzi wangu,nini tena Gervas kimekupata jamani...?’’
Nilimkuta gervas akiwa katundikiwa dripu huku kawekwa mirija ya kuvutia hewa 'oxygen' pembeni yake alikuwepo rafiki yake Omari kwa ajili ya kuwanaye karibu usiku wote.

*********

Sikuwa na jinsi tena kwani Gervas ni kweli alikuwa hawezi hata kuongea hivyo nikambusu na kuelekea nyumbani huku nikiendelea kutokwa na machozi, njia nzima ilikuwa ni kilio tu huku naongea peke yangu,hata nilipokuwa katika daladala bado nilikuwa nimezidiwa kwa kwikwi huku mkamasi ukinitoka na kufanya abiria wa daladala wanishangae.
Nilipofika tu nyumbani nilivuta simu yangu na kumpigia Jammy kwani ni mtu wa karibu kwangu.Naye ndani ya dakika kumi alikuwa kishafika kwani hakai mbali sana na maeneo ya pale kwetu.
vipi tena levina kulikoni....?
‘’Jammy levina yupo hoi kalazwa hospitali mikocheni.....!’’ kipi tena kimemsibu....?
‘’sijui ila nilichoambiwa ni kwamba amedondoka ghafa na ameumia eneo lote la usoni’’
Nilimwelezea Jammy na tukapanga nae kesho yake saa kumi na mbili twende tukamwone.


**********
 
SEHEMU YA 42

Asubuhi na mapema tulikuwa tupo getini pale hospitali ya 'Regency' nikiongozana na Jammy.
Watu wengi wakiwa ni pamoja na rafiki zake na Gervas walikuwa wodini wote wakitaka kujua kilichomsibu Gervas.
Hatimaye Dokta akawasili huku kashikilia faili lake akionesha kuwa kuna taarifa anataka kutupa juu ya mgonjwa wetu Gervas.
‘’Jamani habari zenu....?’’
‘’Salama tu Dokta..!’’ poleni sana ila nipo hapa kuwapa majibu ya mgonjwa wenu nani muhusika mkuu hapa....?’’
‘’Mimi hapa na hawa ni wafanyakazi wenzake...!’’
Nikajifanya kiherehere kumwambia daktari huku akinitolea macho.
‘’kwa mujibu wa vipimo vyetu tumegundua kuwa Gervas anamatatizo tena makubwa....’’
‘’yapi tena hayo dokta uwii....?’’
‘’Levina kuwa mtulivu tujue ni nini...?’’
Aliropoka Jammy akiniambia kwa kuniweka niwe msikivu kwani dokta alianza kama kunichanganya.
‘’tumegundua kuwa mzunguko wa damu katika mwili wake hauna tatizo ila inamuonesha kuwa upande wake wa kushoto figo yake imeanza kuharibika tena imerika sana, alishawahi kuwa na tatizo hili kabla ya hapa...?’’
‘’hapana Dokta, hapana sijawahi kusikia hata siku moja tatizo kama hili kwa mume wangu’’
‘’hospitali kwetu hatuna uwezo wa kumfanyia operesheni kwani upungufu wa vyombo na madaktari wa sekta hii hakuna hivyo inategemea na kipato mlichonacho mnaweza kutafuta hospitali kubwa zinazohusika na mambo haya...’’
Pale pale Dokta akaondoka zake na kutuacha nikiwa mimi, Jammy na wafanyakazi wenzake na Gervas tukijadiliana juu ya kutafuta njia mbadala ya kutatua matatizo tuliyonayo.



********
 
SEHEMU YA 43

‘MACHA MISSION HOSPITAL & KIDNEY INSTITUTE IN ZAMBIA’
Ndio hospitali waliokuwa wameelewana wafanyakazi wenzake na Gervas, pia ni kati ya hospitali zilizokuwa karibu sana katika kusaidiana na kampuni ya kina Gervas na kwakuwa Gervas alikuwa kama Meneja msaidizi wa kampuni ya Gea Star hivyo wakapendekeza gharama zote za usafiri wa ndege mimi Gervas na mfanyakazi mmoja zitalipwa na kampuni pia Gervas atafanyiwa operesheni bure pale hospitalini.
Usiku wote sikupata usingizi zaidi ya kuumia sana moyo huku nikitetemeka,nililala na Jammy lakini usiku wote niliuona kama mwaka mzima, nilizunguka jumba lote kuanzia jikoni nikitokea stoo kisha naingia tena sebuleni mara nishike hichi niache mara nishike kile yani ni kama mtu aliyechanganyikiwa,
Ilipofika saa kumi na mbili asubuhi nikasikia mtu anagonga mlangoni haraka haraka nikaenda kufungua
‘’Karibu pita mpaka ndani’’
‘’Hata, Mimi si mkaaji ila nimetumwa na ofisi nikuwaishie hii hapa’’
Akanipa kiasi cha shilingi milioni moja kama akiba safarini na kunipa taarifa ya kuwahi kuondoka,
‘’Unahitajika ufanye haraka iwezekanavyo kwani ndege itaondoka saa saba za mchana hivyo kuanzia asubuhi hii ningekushauri uende kwanza hospitali kwani ndipo mtakapotokea hapo...’’
Nikaingia bafuni na kuoga fasta kisha nikachukuwa kibegi changu cha nguo mbili tatu na kuongoza mpaka 'Regency hospitali' alipolazwa Gervas, Njia nzima nilibaki naongea mwenyewe kama chizi kwani sikuwa na Jammy nilimwachia aendelee na miradi yangu mpaka nitakaporudi.
‘’Karibu binti’’
Ilikuwa ni sauti ya yule dokta niliyemkuta na Omari yule mtu wake wa karibu na Gervas aliyekuwa akimsaidia kwenye kumuangalia na ndiye tutakaeondoka naye kuelekea Zambia.
Walimbeba kwenye kitanda cha wagonjwa mpaka nje kisha wakampandisha kwenye 'ambulance' tayari kwa safari ya kuelekea 'air port',
Tulipotoka pale hospitali woga ulinipungua lakini tulipofika woga ukazidi kunitanda kwani niliamini kabisa huko ninapoelekea sitanusurika na uwezekano wa mimi kunusurika ni mdogo sana yani ni kama tembo kupenya katika tundu la sindano.
Ndani ya dakika kama arobaini na tano hivi tulikuwa tukiingia eneo la uwanja wa ndege lakini tahadhari kubwa nilikuwanayo kwani uso wangu wote nilijifunika kwa mtandio huku nikiachia kidogo kasehemu ka uso wangu.
‘’Levina mshike vizuri upande wa huko...?’’
Aliniita Omari kwa nguvu na kunifanya moyo wangu uende mbio nikatazama huku na kule kisha nikamshikilia vizuri na kumpakiza ndani ya ndege.
Tukiwa bado kwenye juhudi za kumpakiza mara akatokea dada mmoja wa kampuni ya usafi akiwa amevalia suruali nyeusi na shati la bluu pale pale akatupa ufagio wake pembeni na kutufuata kwa nia ya kutusaidia pale kumpakiza gervas kwenye ndege.
‘’lete hiyo dripu nikusaidie...!’’
Aliita kwa sauti ya upole huku nikimpa ile dripu nakumtolea macho.
"Mungu wangu kumbe ni huyu filauni....? Amefuata nini huku....?’’
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikimtolea macho yule mama aliyewahi kuharibu maisha yangu kipindi cha nyuma, Yule aliyekuwa Nesi kipindi kilee pale 'Ocean road hospital' nadhani alifukuzwa kazi na sasa anafanya kazi za usafi hapa uwanja wa ndege.
‘’Jamani huyu kama Gervas....?’’
‘’ndio yeye..!’’
Aliongea yule mama na hapo hapo Omari akawa ameshamjibu.
‘’Nini tena kimemsibu au ni miguu inamsumbua tena....?’’
‘’Hapana anasumbuliwa na figo...!’’
‘’Mungu wangu sasa Levina yupo wapi? Au hayupo naye tena...?’’
‘’Levina si huyo hapo humuoni...?’’
Pale pale nikautoa mtandio wangu kichwani na kumtolea mijicho na mdomo nikimkazia.
‘’Unasemaje....?’’
Niliongea kwa jazba huku nikimwacha yule Mama aendelee kunitolea macho.
‘’Levina mwanangu yale ya nyuma yalishaishaga na sasa tuendelee na mapya, niko hapa kukusaidia...’’
‘’sihitaji msaada wako hata kidogo.., kwanza unisaidie kwa kipi...?’’
‘’Usiseme hivyo Levina embu muelewe Mama anasemaje...?’’
‘’Omari wewe embu yaache tu huyu muone hivi hivi huyu Mama alishanitia kidonda cha maisha kipindi cha nyuma, alitaka kuniua kama mara mbili hivi hivi najiona....?’’
‘’Haya basi yameisha msamehane Levina...’’
‘’Levina mbona mimi nilishaku samehe,unajua toka tulivyogombana niliachishwa kazi pale hospitalini nikatanga tanga sana kutafuta kazi na sasa nimepata kazi ya usafi hapa 'airport' na huwa nasaidia kwenye ndege 'private' kama hizi’’
‘’Nimekuelewa mama haya nenda zako...’’
Bado nilikuwa na hasira naye sikutaka kabisa kumsamehe lakini baadaye kabisa moyo wa kusamehe ukanitanda mwilini mwangu nakujikuta namkumbatia na kukubali tuongozane naye.
Ndege ilikuwa tayari kwa safari ya mpaka Zambia ambapo ilituchukuwa ndani ya masaa 24 mpaka kufika Zambia na tulipofika tukakuta ambulance ya hospitali tayari inatusubiri hivyo tukampakiza gervas na kuelekea mpaka hospitali, muda wote bado gervas hakuweza hata kufumbua macho,kwani alikuwa anahemea mirija,
Ilikuwa ni hospitali kubwa na nilikuwa muoga kila ninapomuona polisi maeneo yale nilikuwa najiwahi kujifunika na mtandio wangu,tulimpomfikisha Gervas tu wodini nilibanwa sana na mkojo hivyo nikakimbia chooni kukojoa fasta ile natoka tu nakutana na karatasi kubwa la rangi lenye picha yangu.
‘’IKATA BRENDAH’’
Iliandikwa ki ‘Bemba’ ikimaanisha kuwa natafutwa huku picha yangu kubwa ya rangi ikitanda ukutani,
‘’Kwanza mimi siitwi Brendah nikatoka spidi kurudi wodini alipo Gervas lakini ile nakatiza tu kona ya kuingilia wodini macho yangu yakakutana uso kwa uso na Bosi wangu wa kipindi kile akiwa na Dereva Mnama huku wamemkokota katika kibaiskeli cha wagonjwa ‘Happy’ , Aliönesha kakonda sana huku wakinikaribia haraka haraka halmashauri yangu ya kichwa ikanituma nichukuwe mtandio wangu nijifunike ile nauvuta mabegani nianze kujifunika nikawa siuoni nikageuka fasta na kukimbilia choòni nikidhani labda nitakuwa nimeusahau nilivyoenda kujisaidia napo nageuka tu nyuma nakutana na polisi akitoka chooni huku akijiweka vizuri bastola yake kwenye suruali
‘’Mama yangu nimekwisha Levina mimi....!’’
Nilichokifanya nilikaza moyo na kupishana na yule polisi na nilipomkaribia kichwa changu nikakielekezea ukutani huku nikiongoza mpaka chooni, lakini nilipofika napo sikuuona hivyo ikanifanya kuchukuwa muda mrefu sana mule chooni ndani.








*******
 
SEHEMU YA 44

Nilivumilia mule chooni kwa dakika kama kumi hivi ndipo nikatoka huku nikihakikisha pako shwari kabisa, Nikachomoka moja kwa moja mpaka wodini.
‘’Levina umetutisha...? Ulikuwa wapi muda wote huo...?’’
Aliongea yule Mama lakini sikuwa ma wasiwasi wowote kwani nilipofika tu nikauwahi mtandio wangu na kuuvaa kichwani huku nikijifunika eneo lote la kichwani.
‘’Nilibanwa tumbo la kuhara, nadhani ni kutokana na kubadilisha hali ya hewa mara nyingi huwa nabanwa sana na kichefu chefu’’
‘’pole sana...!’’
‘’Ahsante Mama’’
Safari hii nilikuwa mtu wa kumpenda sana yule Mama kwani niliamini atakuwa msaidizi na mtetezi wangu kwa chochote nitakachokutana nacho mbeleni.
‘’Dokta amesemaje..?’’
‘’Tena tumekumbuka anakuhitaji ofisini na amenielekeza twende nikupeleke...!’’
Aliendelea kuniambia yule Mama, hapo hapo nikaurekebisha mtandio wangu vizuri huku nikijifunika eneo la usoni na kuongoza mpaka ofisini kwa yule Dokta,
Ndani ya kama nusu saa tulikuwa bado ofisini tunaongea na bosi na makubaliano yakawa ni ni kumfanyia Gervas operesheni na mimi kwa kuwa ni mke wake japo sio wandoa tukakubaliana nijitolee figo yangu moja na kumpatia Gervas.
Sikuwa na jinsi zaidi ya kulazwa na kupigwa nusu kaputi kisha nikaambiwa nisubirie kwa ajili ya operesheni.
Yule Mama tuliekuwa naye alinionea sana huruma mpaka sikuamini kwani na mchozi alikuwa akiutoa kana kwamba labda mie ni mtoto wake wa damu tena wa kuzaliwa naye.



********


Operesheni ilikuwa imekamilika kiukamilifu ndani ya masaa 24 nilipigwa nusu kaputi lakini nilipokuja kuzinduka sikuhisi kitu chochote kwani ni kweli nilikuwa ndani ya kitanda bado huku nimezungushwa dripu iliyojaa damu ikipenyeza kwa kupitia mirija yake mpaka mwilini mwangu.
Sikuweza kuongea kitu chochote kwani mdomoni niliwekewa kitu kama plasta kilichonifanya nishindwe hata kutoa neno moja, nilitamani japo kuuliza Gervas anaendeleaje lakini nilishindwa.
‘’Ohh Mungu ushukuliwe..! Ametoa macho sasa...?’’
Ilikuwa ni sauti ya yule Mama tuliekuja naye na kwasasa alikuwa akifurahi baada ya mimi kurudishwa tena wodini nikiwa hai.
‘’Levina...? Levina...?’’
Sasa walikuwa wakiniita lakini kwa mbaali niliweza kuzisikia sauti za Omari na yule Mama.
Muiite tu waje wamuangalie tayari kesharudishwa wodini..!’’
Ilikuwa sauti ya yule Mama akiwaita watu waje waniangalie lakini sikuwafahamu ni kinanani hapo hapo woga ukaanza kunitawala tena huku halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta nikifungua jicho langu la upande wa kulia nikitaka kujua watakuwa ni kinanani? Mara jicho langu kwa mbali likakutana na yule bosi wangu akiwa na dereva Mnama wakinifuata mpaka eneo la kitanda changu nikicholalia, hapo hapo nikapindua kichwa changu na kujifanya nina usingizi mzito huku nawasikilizia kwa mbaali..
‘’ Mmesema anaitwa Levina...?’’
‘’Ndio na jina lake kamili ni ‘Levina Christian’ na Mume wake anaitwa ‘Gervas Phota’ yupo chumba cha upasuaji..’’.
‘’Aaah basi sisi tulikuwa tunamtafuta ‘Brendah Brebre ‘ kwa kuwa alitoroka tena alifanya mauaji makubwa na inasemekana katokomea Tanzania, Sasa tulivyosikia mnatokea Tanzania ikatubidi tuje kumwangalia.,Samahanini sana kwa usumbufu uliotokea..! Na poleni kwa mgonjwa wenu..!’’

‘’msijali mnakaribishwa Tanzania...’’
Hapo hapo nikarudisha kichwa changu na kuwaangalia wakitokomea huku wakiwa na mapolisi wawili.
‘’Hamnipati ng'o!’’
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikiwasindikiza kwa macho yaliyokuwa na hasira.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom