Story: Shemeji Monika

SHEMEJI MONICA

SEHEMU YA 7

?kusema kweli mama, Julieth ni msichana mrembo sana na mwenye kujitambua, mwanaume yeyote akiamua kuruhusu hisia za kimapenzi juu yake ni lazima atampenda, tena sana! Ila mimi sipendi kuziruhusu hisia za aina hiyo, mimi ni mwalimu wake? aljibu James. ?wewe ni mjanja na una akili nyingi sana, naweza kuliona hilo kutoka kwenye majibu yako. Kwa kumalizia nikwambie kuwa Julieth bado ana safairi ndefu sana, sipendi kuona mtu yeyote akiiharibu safari hiyo, kama unampenda Julieth ufuate taratibu za kistaarabu za kumuoa, ila sio sasa, ni mpaka atakapomaliza masomo. Sijui umenielewa?? alisema mama yake Julieth kwa kumaanisha na James akakubali kuwa ameelewa maelezo yale. ?sasa kama umenielewa sitaki kuona kitu cha ajabu kimetokea, nitakuweka pabaya sana? alichimba mkwara mzito mama yake Julieth.

Maongezi yale yakawa yameisha na James akawahi kwenda kuwafundisha wanafunzi wake ambao walikuwa bado wanamsubiri.

Julieth aliweza kuigundua hali ya upole kwa James alipokwenda kwao kwaajili ya kumfundisha siku hiyo, hakujua alikuwa amkumbwa na nini lakini aliiweza kuona alikuwa tofauti. Julieth alipomtaka wakasomee chumbani kama ilivyokuwa siku liyopita James alikataa na kusisitiza kuwa alitaka wasomee pale sebuleni, ikambidi Julieth kukubaliana na matakwa ya mwalimu wake huyo. Katika kumfundisha pia siku hiyo James serious kama mwalimu, ule utani utani wake wa siku zote haukuwepo. Julieth akaanza kujiuliza alikuwa amemkosea nini, lakini hakuona popote alipokuwa amekosea toka waachane jana yake wakiwa na furaha. Baada ya kipndi kuisha James akaaga na kuondoka, Julieth akataka kumsindikiza ila James akakataa na kusisitiza amuache tu aende mwenyewe, ?jamani, nakutoa tu mpaka hapo getini? alisema Julieth ambaye aiona sasa walikuwa wamefika pabaya. ?No, wacha niwahi? alijibu James na kuondoka bila kungoja majibu. James aliamua kupunguza mazoea anapokuwa kwenye mazingira ya nyumbani kwa kina Julieth kwani aliona mazoea yale yangemrudisha tena kwenye maongezi na mama yake Julieth,mpengine wkati huu angekuja vibaya zaidi.

James alifika nyumbani na kumkuta shemji yake, Monica akiwa na mtoto wake wakipiga story za hapa na pale, naye akajumuika nao, kaka yake alikuwa bado hajarudi.

Baada ya kupata chakula cha usiku story zikaendelea mpaka Peter, mtoto wa kaka yake James alipochoka na kwenda kulala, haikuchukua hata nusu saa na James naye akaingia chumbani kwaajili ya kulala, mara akasikia mtetemo wa simu yake ukiashiria kuwa ujumbe ulikuwa umeingia,alipotoa simu yake akagundua kuwa zilikuwepo jumbe mbili, moja ya Monica na nyingine ya Julieth. ?nimekumiss, njoo chumbani kwangu nikuoneshe kitu kizuri? ujumbe wa Monica ulisomeka hivyo, James akaupuuza na kufungua ule wa Julieth. ?hivi James nimekukosea nini mimi? Kama hunipendi kwanini usiniambie tu? Haya ni mapenzi ya namna gani, mara unafuraha mara umeninuia, mimi nitashindwa kwakweli?, ujumbe huu wa Julieth ulimuingia vizuri James, mpaka ndani ya moyo, akajaribu kuvaa viatu vya Julieth ambaye hakuwa akijua nini kimetokea baina ya James na mama yake, akaona kweli binti wa watu atakuwa katika wakati mgumu kulielewa hili swala. ?Julieth kwanini unakuwa mgumu kunielewa? Hapo ni kwenu, tukiendekeza mapenzi utaniletea matatizo, kwanini hulioni hilo? Nakupenda sana lakini sitaki uwe sababu ya kuharibika kwa future yangu? alijibu ujumbe ule James kisha akaamua kurudi kwenye ujumbe wa Monica na kuujibu ?hivi ni kazi sana kumtoa mwanamke bikra?? akatuma ujumbe huo ambao haukuwa na uhusiano wowote na ule ujumbe ambao Monica alitangulia kumtumia.

?James acha kutafuta visingizio, kila mtu anakupenda hapa nyumbani, unamuogopa nani atakaye kudhuru?? ulikuwa na ujumbe mwingine wa Julieth. ?mama yako alinifuata ofisini mchana na akanitaka kukaa mbali na wewe? James akaamua kutumbua jipu baada ya kuona lawama zote zimehamia upande wake. ?khaaa, kwanini mama anaifanyia hivi?, kwakweli sikubali, lazima nionge naye? alijibu Julieth akionesha kukasirishwa sana na alichokifanya mama yake. ?ukiongea naye kuhusu hili unanigombanisha zaidi na mama yako, naomba usifanye hivyo? James kajibu ujumbe ule na Julieth akaona anachokisema ni kweli. ?sasa itakuwaje, tutakuwa tunakutana wapi? Mimi siridhiki na maisha haya? lijibu Julieth. ?kama tunataka kuwa na futurenzui hatuna haja ya kupapatikia mambo, tunaweza kuharibu kila kitu, siwezi kugombana na wazazi wako kama kweli nataka uje kuwa mke wangu baadae? James akajibu. ?yani wewe unataka nikufundishe namna ya kumidhisha mwanamke mwingine? Kwani mimi sina wivu?? ulikuwa ni ujumbe wa Monica ambao James hakuujibu. ?kama unataka nikufundishe njoo? Monica alituma ujumbe mwingine baada ya kuona ule haukujibiwa. ?hapana, nakiheshimu sana hiko chumba cha kaka yangu, siwezi kuja? alijibu kwa kifupi James. ?mara hii umeshasahau mashatri yangu? Tulikubaliana utakuwa unafanya ninachokwambia lakini umenigeuka? alijibu Monica lakini kwa mara nyingine James akapuuza uumbe wake na kulala, kitendo ambacho alijua fika kinamkera sana Monica na kama sio uwepo wa Peter, mtoto wa wake basi lazima Monica angemfuata pale chumbani.

Asubuhi James alidamkia mjini ambapo alienda kununua godoro na vyombo vichache ambavyo alivipeleka kwenye kile chumba chake, alikuwa amepanga kuhamia kesho yake maana hali ya shemeji yake,Monica alikuwa anaelekea kubaya, akaona bora ahame kulinda undugu wao na kaka yake, Paul.

?leo hatusomei nyumbani, nimeaga kuwa umeniambia kuna sehemu tutaenda kusomea, so tafuta sehemu. Na mama akikupigia kuhakikisha ukubali? ulikuwa ni ujumbe wa Julieth kwenye simu ya James. Huyu binti ana akili gani? Alijiuliza James, naye akaandika ujumbe kumjibu ?hapana, tutasomea nyumbani, tumeshaliongea hili swala?. ?nyumbani nimeshaaga na nimeondoka, sahivi nakaribia hapo kazini kwako, nakuja kukungojea umalize kazi tuondoke, na mama atakupigia wakati wowote, andaa maelezo mazuri ya kumpa? alijibu Julieth na kuichangaya akili ya James ambaye alikuwa amekaa na Sir Mdharuba mule ofisini akingojea muda wa kipindi chake. ?please rudi nyumbani kama kweli unanipenda? alijibu James. ?no, safari hii na wewe fanya kitu kwaajili yangu. Nakuja, kama kunifukuza unifukuzie hukohuko? Alijibu Julieth

Usikose sehemu ya 8
 
Back
Top Bottom