miss mike
Senior Member
- Aug 25, 2015
- 176
- 250
Yani nasubiria maana nimecheka hatari
nasubiria
CHAPTER 1
A. MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU
Kila mwisho wa mwezi mimi na marafiki zangu tunakutanaga kwa ajili ya kupata chakula, inaweza ikawa chakula cha jioni au mchana.. kwa Mwezi Maramoja, inaweza ikawa mwisho wa mwezi au mwanzo wa Mwezi
Nina marafiki 3 wote tumeajiriwa, wote tulisoma pamoja kuanzia form 1 mpaka chuo lakini tofauti kati ya marafiki zangu na mimi ni kwamba wao wameolewa mimi sijaolewa
Kila tunapokutana huwa wananipa wakati mzuri sana, hawanihukumu kwanini nipo singo, hawaniseki vibaya kwakweli wananitia moyo sana kuwa usijali haujachelewa, hakuna kuwahi wala kuchelewa kwenye ndoa, Kila mtu ni Mungu alivyompangia usijiskia vibaya, muda bado unao n.k wa kadhalika
Siku moja rafiki yetu mmoja akawa anasafiri kukazi miezi 3, wakapanga tumuage kwa kupata chakula cha pamoja tukitoka Kanisani, tukapanga kuonana Hotel ya Kempinski Mjini saa 6 mchana
Cha ajabu ni kwamba nilipofika pale, hatukuwa 4 kama tunavyokutanaga yule rafiki yetu aliekuwa anasafiri alikuwa na ndugu yake mmoja ambae nae alikuwa anataka kumuaga... jumla tukawa wa5
Baada ya kusalimiana na kujuliana hali na utambulisho wa ndugu yake na maongezi ya hapa na pale na kupata chakula na vinywaji; ndugu wa rafiki yangu ambaye anasafiri akagundua kuwa mimi sijaolewa akaanza kunihoji maswali Mengi ambayo kwa mtu ambaye sijamzoea sikujskia kujieleza kwake ila kwa kuwa alikuwa amenikazania ikabidi nimjibu
Ndugu wa rafiki: una miaka mingapi
Mimi: 33
Ndugu wa rafiki: una bwana au mchumba au boyfriend
Mimi: bado nipo singo
Ndugu wa rafiki: kwanini upo singo miaka 33? Au unatembea na mume wa mtu wewe ni kimada?!
Mimi: kwani lazima kuwa kwenye mahusiano?!
Ndugu wa rafiki: kwahiyo wewe ni kimada wa mtu?!
Marafiki: wote wapo kimya wananiskiliza wala hawanitetei, nikahisi dunia imesimama
Mimi: hapana sina mtu kabisa
Ndugu wa rafiki: kwahiyo wewe ni bikra?!
Mimi: hapana sio bikra
Ndugu wa rafiki: ukiwa na hamu (genye) unafanyaje sasa? ! Au unatumia dildo (midoli feki iliotengenezwa kama orijino dyu dyu ya mwanaume)
Mimi: Tz hii natoa wapi Dildo?!
Ndugu wa Rafiki: kwahiyo ukiwa na hamu unajikimuje?! Au una rafiki anaekusaidia ukizidiwa?!
Mimi: sina kitu wala mtu wala rafiki wa kunisaidia
Ndugu wa rafiki: unauhakika wewe ni mzima kweli? ! Maana sio bikra sio nini, au na wewe umeokoka Yesu anakusaidia? !
Mimi: hapana sijaokoka ni mkristo wa kawaida
Ndugu wa rafiki: sasa kwanini upo singo mrembo kama wewe una kazi yako, hela zako, ila mamii kuvaa haujui embu ona hii minywele yani upo rafu?! Mwanaume gani Atakusogelea?! Kwanini unajiweka rafu my dia? !
Alafu nyie marafiki zake mko vizuri mmependeza mwenzenu kama ameamkia kwenye banda la ng'ombe kwanini hamumfundishi kuvaa akapendeza akawa fresh safi,
Yani mrembo kama wewe umeshindwa kujipeleka Saloon ukajisopusopu ukapendeza, unakuja kula chakula cha laki 1 Kempinski wakati saloon kuosha na kutengeneza nywele ni elfu 20
Nguo mpaka elfu 20 unapata mlimani city kwa hadhi yako basi
Ivi nyie kwanini mnamwacha mwenzenu anakaa rafu?! Ndio urafiki gani mlionao
Wa kinafiki namna hii?!
Marafiki zangu: wakanyamaza kimya lakini Mimi nilimpenda sana huyu ndugu wa rafiki yangu, Kwanzaa alikuwa smart sana sana sana, Alafu hakuwa ameolewa lakini alikuwa kwenye mahusiano, alionekana ana huruma na roho nzuri na upendo nilitamani angekuwa rafiki yangu; akaendelea tena kuongea
Ndugu wa rafiki yangu: ahahahaha haki ya Mungu, my dia, haya ni maisha, sijui hawa mabwege unaowaita marafiki wanakufundisha nini?! Kama upo na hawa watu kuanzia form 1 mpaka sasa mnafanya kazi Alafu hawana hata mchango wa kawaida kukusaidia sielewi unafanya nini kwenye maisha yao, ondoka katafute marafiki wengine ina maana hawa ni wanafiki kwako hawakuelezi ukweli, rafiki wa kweli anakueleza ukweli, Mimi nimeingia hapana nimekuangalia sana nikajua labda ni house girl wa mmoja wa hawa wadada kumbe rafiki tena una ajira yako nzuri kwanini lakini umejikatia tamaa namna hii?! Kwanini umekuja mchafu mchafu kichwani Nguo hujanyoosha angalia majani kichwani kwani hapa hotelini umeingiaje Kwanzaa? ! Hawajakuuliza kama umekosea njia?!
Mimi: kimya
Ndugu wa rafiki: my dia, hawa sio marafiki zako, hawa ni ma-free mason
Marafiki: wee ushindwe, wakaanza kugomba hapo na kulalamika
Ndugu wa rafiki: ndio nyie ni wachawi wanyonya damu na waiba nyota, mnakuwaje mmerembeka namna hio lakini mwenzenu kakaa kama dada wa kazi? Alafu anapataje mwanaume kwa staili hii?
Au mnafurahia mwenzenu anavyoteseka?!
Marafiki: hapana si tumemwambia lakini hasikii, labda umwulize kwanini kawa hivi maana zamani hakuwa hivi
Sikuhizi ndio kabadilika kawa hivi hana miezi 6 anavaa kiajabu ukimwuliza hasemi na sisi huwa tunamwachaga hivyo
Ndugu wa rafiki: my dia, what happen?! Imekuwaje unakaa kama fundi gereji za magari? !
Mimi: hamna bwana mbona nipo sawa
Ndugu wa rafiki: umetokea kanisani hivi Au umetokea nyumbani?!
Mimi: nikadanganya kuwa nimetoka nyumbani
Ndugu wa rafiki: OK labda uliamka ukasahau kuoga ukaja
My dia ningependa kukusaidia sana, Mimi nimesoma psychology na naweza msoma mtu sana kabla hajaongea na wewe unaonekana una mateso ya moyo yanayokupelekea kukata tamaa, akaingiza mkono kwenye pochi akatoa business card yake akanipa
Ndugu wa rafiki: unitafute kwa wakati wako kama unaona aibu kuongea mbele ya marafiki zako nitakusaidia lakini namna hii ulivyo hapana ukiendelea namna hii utazeeka mwenyewe kama sio kufa siku sio zako... akanyanyuka akaaga anawahi mahali akaondoka
Mimi: nikampenda sana yule mwana psychology (saikolojia) nikatamani tuonane siku hio hio tuongee
Baada ya wiki 1 nikampigia simu yule mwana saikolojia nikamwambia nipo tayari kuongea nae, akaniambia uwa ana darasa la wadada ambao wapo single, kama anataka aniingize huko maana litanisaidia kuchangamka na wezangu, na kufunguka kwa urahisi
Mimi nikakubali, akaniambia darasa kwa wiki mara 1, kila jumamosi, akanipa na bei ya hio programme na itachukua muda fulani wa miezi 10 na malipo yake natakiwa niwe nimemaliza kabla ya miezi 2 kuisha maana mbeleni kunakuwa na programme za kutoka out, kusafiri, yeye atakuwa analipia hotel, chakula
Vinywaji, usafiri,
Ndio hela yake ilikuwa ndefu sana sana sana, lakini sikujali, niliona bora nitoke nikutane na watu, nitengeneze marafiki wapya, nipate connection za maisha, nisafiri, nipanue akili sikujali maana nilikuwa haba na haba lazima nitajaza kibaba hata kama nitabakia kuwa singo
Siku ya siku ikatimia nikaenda kwenye hicho kipindi, nikapokelewana mtu wa mapokezi nikajaza form nikapelekwa sehemu ya kulipia nikalipa mil 8 cash ya Kitanzania sikutaka kuigawanya Au kuilipa kwa mafungu maana hela bwana Leo ipo kesho hamna
Baada ya kupewa risiti nikapelekwa kwenye chumba ambacho nilikutana na wadada 6 na Mimi wa 7 sote tunamsubiria mwana saikolojia aje tuanze shoo
Mwana saikolojia akaingia akatusalimia kwa kutukumbatia na kutubusu kwa furaha tukakaa kwenye masofa mazuri mazuri nakwambia wakaja wahudumu wakauliza mnataka vinywaji gani kila mtu anataja chake hapo saa 10 jioni ya Jumamosi
Baadae tukaanza kikao, mwana saikolojia akajieleza kwa ufupi kuhusu kazi yake na maisha yake kwa ufupi sana na watu aliowasaidia na lile lilikuwa darasa lake la 3
Amesaidia wadada 20 na wakaka 10 waliokuwa singo kama sisi na sasa wameolewa na kuoa na wanafamilia zao wengine ndoa miaka 5 wengine 10
Mimi: nikashangaa huyu dada alikuwa wapi sikuzote sijamwona?!
Mwana saikolojia akaongea sana mpaka alipohakikisha wote tumekuwa relaxed akaanza kutuuliza kila mmoja ajitambulishe kwa majina na kazi (shughuli) anayofanya na kama anawatoto au mtoto
Basi ilikuwa raha sana
Kwakuwa kipindi kilikuwa ni masaa 3 tu
Na hapo tulishaangusha Lisa 1 nanusu mwana saikolojia akaomba mdada m1 aanze kujielezea kwanini yupo singo
Yule mdada aliitwa Kokutona, mwenyeji wa Kagera Mhaya kwa kifupi anaitwa Koku ... mfanya biashara mzuri, hana bwana, hana mtoto, hana mume yupo singo, mrembo sana, ana figa namba nane, bonge la shepu, wema sepetu atasubiria miaka 100.. ana weusi flani unateleza...Black Beauty, Mzuri kisu kweli kweli
Akaulizwa kwanini upo single mrembo
Koku: mimi naomba niwe muwazi na msema kweli, maana msema ni mpenzi wa Mungu
Mimi kila mwanaume ninayempata ananiangusha
Mwana Saikolojia: Kivipi?!
Koku: kila mwanaume ninayempata anakuwa na dudu ndogo, size ya kibamia, machine ndogo
Sasa sijui nina laana au nimelogwa
Mwaka wa 2 huu napata Vibamia tuuu ah nikaamuaga nikae mwenyewe kwa muda
Mtu unakuwa umejiandaa kila kitu wakifungua mlango unakutana na kidole cha mwisho Sasa na hili zigo nachokaa
Wengine nawahairishia kuwa naumwa nimepatwa na tumbo la kubana, Wengine nawaambia naumwa tumbo la mwezi, wengine najidai simu imepigwa nina dharura basi inaisha
Nimeshapata wanaume kama 20 wana machine ndogo, wanene, wembamba, warefu, wafupi, weupe, weusi, vijana, Ben 10, watu wazima ...eh kila mtu me sichaguagi, nikaona nikae mwenyewe huenda sio riski nikaamua kununua Dildo (dudu ya kiume ya mpira) ndio inanisaidia kujikimu ila sio sawa kama ukiwa na mwanaume wa ukweli
Mwana Saikolojia: lakini tatizo sio machine ndogo kama anajua kuitumia Koku
Koku: hamnaaa hata matumizi yenyewe hawajui wala nini kuchoshana ujinga mtupu
Wote: tukacheka huku tunamshangaa Koku maana sio kwa maelezo yale!
Tuonane kesho Tar 16 May 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA kwa Muendelezo mwingine
nasubiria

