Sababu 5 za kwanini bado upo single

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,598
5,979
Katika maisha ya Mahusiano shauku ya kila mmoja wetu nikuwa na urafiki au mahusiano yatakayomfikisha katika Ndoa.

Ikiwa ni mtu uliyekamilika kimwili na kihisia ukiachana na watu waliojitoa na kujiweka WAKFU kwa ajili ya kazi ya MUNGU, ni lazima shauku yako itakuwa, ni kuwa katika mahusiano yatakayokufanya kuoa au olewa.

Ndo maana Maandiko ya Biblia Takatifu Mtume Paul akatukumbusha kwa kusema:

" Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe"
(1 Wakorintho 7:2)

Zifuatazo ni Sababu zinazochangia kwanini uendelee kuwa SINGLE (kuwa mwenyewe).
Hauna mpenzi, hauna mchumba, hauko katika ndoa haijalishi wewe ni wakiume au wakike.

Historia mbaya ya malezi utotoni

Historia ya Malezi kuanzia utotoni ni jambo linalochangia wewe kuendelea kuwa single, yawezekana unaishi na kumbukumbu au fikra za maisha ya nyuma yaliyokutesa na kukuumiza.
Mfano ulibakwa, ulinyanyaswa kijinsia, uliteswa na wazazi wako, uliteswa na mzazi wa kambo, uliteswa na ndugu, ulinyanyaswa wakati ulipokuwa shuleni na kumbukumbu zingine.

Kumbukumbu hizi za maisha yako ya nyuma zimekufanya uwe na fikra hasi kuhusu mahusiano, zimekufanya uwe na mtazamo hasi kuhusu wanawake au wanaume katika mahusiano, Zimekufanya usione sababu yakuwa katika mahusiano.
Nakushauri tatizo hili linauwezekano wa kupona, tafuta msaada wa kisaikolojia kutoka kwa wataalamu wa saikolojia na ushauri.

Majeraha au maumivu ya mahusiano

Majeraha, makovu au maumivu ya mahusiano uliyowahi kuwa nayo, ni jambo au sababu inayokufanya uwe single au uendelee kuwa single. Yawekezana ulisalitiwa au kuumizwa kwa namna yoyote ile.

Nipende kukushauri kuwa, Tafuta msaada wa kisaikolojia na ushauri kutoka kwa wataalamu watakusaidia katika kuondokana na majeraha, makovu au maumivu ya mahusiano yako ili kuondoa mtazamo wako wa kuendelea kuishi Single. Yawezekana sio matamanio yako uishi au uendelee kuwa single ila maumivu hayo yamekufanya uepuke na kuchukia mahusiano kwa hofu ya kuumizwa.

Kushindwa kutawala hisia zako hasi

Hali yako ya kushindwa kutawala hisia zako hasi ni jambo linalokufanya uendelee kuwa single au kuachika katika kila mahusiano yako unayokuwa nayo mfano wa hisia hizo ni:- Huzuni, Hasira, Hofu, Chuki, Kulipiza kisasi, Wivu, Lawama, Kutokujali.

Ikiwa hutojua namna ya kuzitawala hisia zako itakuwa ni ngumu sana kwa mwenzi wako au mpenzi wako kukuvumilia katika mahusiano. Hali hii itakufanya uendelee kuwa single kwa kujenga tabia ya kuyaongelea vibaya mahusiano.

Kukosa mbinu za mahusiano

Kuhusiana na mtu mwingine ambaye ana tabia tofauti na yako kunahitaji mbinu za mahusiano. Usipojua mbinu za kuhusiana au kuishi na mtu mwenye tabia tofauti na yako huwezi kukaa kwa mda mrefu Katika mahusiano yako.

Hali yako yakutokujua namna ya kuwasiliana, hali yako ya kutokuja mwenzi wako nini hapendi na nini anapenda, hali yako ya kutokujua namna ya kujali, Hali yako ya kutokujua kuomba msamaha au kusamehe, Hali yako ya kutokujua umuhimu wa kushukuru. Ni mambo yatakayokufanya uendelee kuwa single au kuachika katika kila mahusiano yako.
Tafuta vitabu vya mahusiano, Tafuta wataalamu wa saikolojia na ushauri kuhusu mahusiano watakusaidia namna ya kujifunza zaidi mbinu hizi kwa ajili ya mahusiano yako.

Domo zege

Domo zege ni ile hali ya hofu au woga wa kushindwa kuziongea hisia zako kwa mtu unaempenda, hofu au woga huu utakufanya uendelee kuwa single maisha yako yote. Haijalishi wewe umelelewa kidini kiasi gani.

Imeandikwa
".. Imani bila matendo imekufa"
(Yakobo 2:26)

Ikiwa utaomba na kusubiri MUNGU, akuletee mchumba wakati huo, wewe mwenyewe huna uwezo wa kuzielezea hisia zako kwa mtu unaempenda ni Sababu itakayokufanya uendelee kuwa single kwa kipindi kirefu au kuchelewa kuoa au kuolewa.

Acha uwoga, jiamini jenga tabia ya kujichanganya kwa kuzungumza na watu wa jinsia zote, hali itakufanya uondokane na tatizo hili la Domo zege.
 

RAYMANU254

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
2,524
4,424
Kukosa pesa za kumhudumia mwenza wako nayo pia Ni mojawapo ya sababu mkuu, vijana wengi has a wa kiume wanashindwa kuingia kwenye mahusiano na wenza wao wa kike maana wanajiona hawapo vizuri kiuchumi kwahyo wanahisi watashindwa kuwahudumia wenza wao
 

babyfancy

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
2,179
5,811
Sababu sijisikii tu kuanza kubanana banana mimi according to mario life is too short enjoy your self
 

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
8,276
19,189
Nilikutana na kina sio kina, ujazo sio ujazo. Afu mvuke wake unakuja unakataa. Nilipojaribu kuzungumza nimejikuta niko single.
 

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
7,657
8,486
Hakuna mwanaume domo zege ila hajakutana tu na mtu aliyemuelewa sio kila demu unatongozatongoza tu ila hyo namba 2 ndio sababu kwa watu wengi.
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
14,737
33,748
Sababu ya pili "majeraha ya mahusiano " is why am single, naogopa kumuamini mtu mwingine sababu ya niliyopitia, kuachwa na mtu unayempenda mmh inauma
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom