LEAH:
Huyu binti nitamsimulia mimi story yake maana hatupo nae tena, :Rest Easy beautifully...gone too soon'....
TONY akisimulia...
Nilimfahamu Leah siku ya udahili wa chuo, alikua amekaa chini kinyonge, mie tena na watoto wazuri , nikamfata nikamuuliza mbona kinyonge mama, akanambia hajisikii poa, na hapo bado hajafanya usajiri, nikiangali hiyo foleni sio poa, maana Kuna watu wa udoso , sijui mawadern , sijui adminstration , sijui wahasibu yaani tafrani, wote hao umalizane nao ndio upewe room, ikabidi niende nikaongee na viongozi wa udoso kwamba pana mwanafunzi anaumwa na hajasajili , yule kiongozi alikua na utu akaja akanisikiliza, akamchua Leah akaenda msajilia...
Alipomaliza kule ndani akaja kunishukuru akaomba namba angu, mie tena sikuvunga...baadae tukaja kua marafiki sana, katika huo urafiki nikaja kugundua kua Leah anaishi na virusi vya Ukimwi, alinambia baada ya kuona namsumbua sana, alinambia tu kwa upendo kua makini Tony pana mabinti wengi tu hapa tuliokuja kwa udhamini wa Mama Salma foundation, sio rahisi kuwatambua kwaio kua makini. Nilipata na hofu maana kwa ule uzuri wa Leah mbona angetaka kuusambaza angetuua wengi.
Leah alikua mrembo jamani daaah, Kuna mda unalaumu maradhi ila unakua hamna namna, nachomsifia Leah alijitunza sana, nilijaribu kumdodosa jinsi alipata maambukizi akanambia kua alizaliwa na hiyo hali, aliupata toka tumboni kwa mama, I felt sorry for her, na hio ikafanya awe rafiki angu sana, Leah alikua ananiasa mara kwa mara kuhusu tabia zangu za kupenda watoto wazuri, nadhani Ile story ya Leah ilichangia sana kua makini na kutouza mechi.
Maisha ya chuo kwa Leah hayakua na mambo mengi sana, alikua ni mfano wa binti anaejitambua sana, alikua anasali mnooo, anasoma kwa juhudi , niliumia tu safari yake haikua ndefu. Angalau Mungu angempa nafasi ya kufurahia juhudi yake ya kusoma. Alikuja kupata mwenza ambae alikua na maambukizi kama yeye, walifunga ndoa punde tu baada ya kumaliza chuo.
Miaka miwili baada ya kumaliza chuo Warda ananipigia simu ananambia Leah amefariki, Ile taarifa ilikua ngumu sana kuipokea, yule binti alikua na juhudi ya kusaka maisha, alikua anafanya biashara mtandaoni tangu tukiwa chuo, anaagiza vitu dar kimtandao anawauzia wanafunzi wenzie na watu wengine mtaani, she was smart and very hard working. Mungu alimchukua mapema mnoo hakumuacha afurahie matunda ya juhudi yake.
Leah Kama angeamua kuingia kwenye mfumo wa Dullah alikua anapata soko sana, she was beautifully indeed, ila alichagua kujiheshimu, hakutaka kuambukiza wengine, kwangu anabaki kua shujaa sana.
Tulimzika Leah nyumbani kwao Morogoro, Ile siku ilinifanya nijitafakari sana, kuna nyimbo zinaimbwa kipindi cha msiba unaweza sema naokoka leo, wale kinamama siijui wanakua wamejipanga kabisa kua tutaanza na wimbo huu tutamalizia na huu, nyimbo zinachoma hadi moyoni. Nikamwambia Dullah nikitoka hapa natafuta kanisa lilipo ndugu angu, Dullah alinicheka balaa ...tukampumzisha Leah na maisha mengine yakaendelea.