Story behind your date of birth

Story behind your date of birth




NYOTA YA KAA (CANCER)

Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12.

  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Juni na tarehe 20 July ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni mwezi (moon).
  • Siku yao ya bahati ni Jumatatu.
  • Namba yao ya bahati ni 2 na 7.
  • Rangi yao ya bahati ni Nyeupe.
  • Asili ya nyota yao ni Maji.

KIPAJI CHA KAA (SENSITIVE):

Wenye nyota hii wana kipaji cha hisia ya kugundua mambo yanayotendeka ikiwa ni pamoja na kubashiri mambo, kumwelewa mtu kwa undani na kujua jambo ambalo mtu anataka kulifanya au jambo litakalotendeka hasa kwenye watu wengi.

TABIA ZA KAA

Watu wenye Nyota hii ni wenye tabia ya hisia nzito ni wapole na wenye huruma. Wakiwa na dhamira ya ulezi na kuwaangalia watu wengine na hiyo inaonekana waziwazi katika nyumba zao na familia zao.
Hata hivyo upande mwingine ni watu ambao wana gubu na wakali ne wenye kupenda kujishughulisha na wanajiamini.
ni watu ambao wanaweza kubadilika lakini wenye msimamo na itikadi na wanaweza kuwa ni wenye wivu mkali na wenye kudhibiti.

TABIA YA KAA KATIKA MAPENZI :

Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa wenye nyota hii pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanapenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu na wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.
Wenye Nyota hii bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo basi huwa hawana raha.
Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.

MATATIZO YA KIAFYA:

Nyota hii inatawala njia kuu ya chakula kuelekea tumboni, mbavu, mfupa wa kidari, tumbo la uzazi, utumbo mdogo na utumbo au sehemu zote za kusagia chakula.
Vile vile inatawala bandana na matiti.
Tatizo lao kubwa la maradhi yao linatokana na ukimya wao wanapoudhiwa. Inapotokea hivyo wao hushindwa kusema na huumia kimya kimya.
Maradhi yao makubwa yanakuwa maradhi yanayosababishwa na gesi , au vidonda vya tumbo au kiungulia au maradhi yanayotokana na mwili kuwa mnene au umbo kubwa.
{mospagebreak}

KAZI ZA WENYE NYOTA YA KAA:

Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi ambazo zitawafanya wao wawe walezi wa wale wanaowatumikia ili kukidhi mahitaji ya nyota yao.
Wanatakiwa wafanye kazi za utabibu kama vile Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini kama vile mabaharia, kazi za huduma ya chakula kama hoteli, migahawa, kazi za kuhudumia watoto kama katika shule za chekechea, kazi za benki au kazi za maneja utumishi au kazi za kuandika.

FAMILIA ZA KAA:

Wenye nyota hii ni wazazi asilia, na wazazi wakiume mara nyingi huonekana wakiwasaidia wake zao kulea watoto.
Wanafanya kwa bidii kuhakikisha familia zao zinapata kila kitu kinachohitajika.
Mzazi wakike ana hisia kiuzazi kuliko mume na kwa mtoto kwa mtoto anyependa kuwa huru kuna muda hujihisi kwamba mama yake anambana.
Wazazi wa nyota hii wana tabia ya kuangalia mambo yaliopita nyuma hivyo hupenda mambo yasibadilike milele.
Hali ya Wazazi hao ya kubadilika badilika huwapa wakati mgumu watoto hasa wale wenye hisia ndogo ambao huhisi wanasukumwa sana na hutaka kujikomboa ili waondokane na baa hilo.
Wazazi wenye nyota hii hupenda sana watoto wao wafanye wanzozitaka wao kinyume na matakwa ya watoto wao .

MADINI YA KAA:

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae madini ya moonstone au jiwe lolote lenye rangi ya maziwa.
madini haya yana uwezo wa kuongeza hisia na kufanya wawe na ari ya kuwatumikia na kuwakinga wenzao.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:

Tabia ya Mbuzi ya ubahili na kutopenda anasa hulainishwa na tabia ya Kaa ya upendo, huba na huruma ambayo humfanya mbuzi atulie na atumie kile alichonacho .

VYAKULA VYA KAA:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vyakula vinavyotawaliwa na nyota yao.
Vyakula vyenyewe ni kama Mapeas, kaa au vyakula vya baharini, na mboga kama kabichi na saladi (lettuce).

NCHI ZA KAA:

Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika miji au nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.
Miji hiyo ni New York (Marekani) na Venice (Ugiriki) au nchi za New Zealand na Scotland.

RANGI ZA KAA:

Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.


  • Ukiwa na Swali au Tatizo lolote usikose kunitafuta kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano



Kwenye hii nyota yangu pamejaa ukweli mtupu, ngoja nitafute na nauli kabisa niende Scotland
 
Hii ni longolongo wote tukaishi york, zealand, ugiriki nk.huku ugaibuni abaki nani? Loooo siamini manyota hata chembe
 
i don't believe katika haya mambo,but kinachochanganya ni kuwa kila kilichosemwa hapo juu kulingana na tarehe yangu ni sahihi na uhalisia wangu,siamini.Is it coincidence?
 
Aisee kweny 3rd ni mie kabisaa,napenda hela balaa halafu ss ni afadhali nizipende afu nitumie,hapana napenda kuwa nazo nikizitazama tu mwee!mh ni selfish vibayavibaya jamani uwii na ni mtu ninayependa uhuru kweli,mh mbona imenilenga
 
Hii kitu imenielezea vile nilivyo pia nimefurahi kwani nimejijua
 
Aisee kweny 3rd ni mie kabisaa,napenda hela balaa halafu ss ni afadhali nizipende afu nitumie,hapana napenda kuwa nazo nikizitazama tu mwee!mh ni selfish vibayavibaya jamani uwii na ni mtu ninayependa uhuru kweli,mh mbona imenilenga

Namba tatu mwenzangu itabidi tuonane as soon as possible
 
Aisee number 3...mmmmh kweli i never get wat i want without working hard...hata kama nikitaka karanga lazima niisotee....
 
MziziMkavu mimi nimezaliwa tarehe 19 February, siku zote nilikuwa najua nyota yangu ni NDOO ila kwa maelezo uliyoweka hapa unasema mimi ni SAMAKI...Naomba ufafanuzi please japo kitabia naendana kabisa na maelezo ya NDOO kuliko hio SAMAKI uliyoitaja kwangu...
Natafuta mke sasa hv hebu niambie mke wa nyota ipi atanifaa kutokana with referring to nyota yangu
 
Last edited by a moderator:
What kind of wizardry is this!? I feel like you have been spying on my life MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu I don't believe in this...
It is just a random human behaviours....

Human beings are creatures of habits!

So they will develop a patern of behaviours based on environment. ..

I disagree. ....

Know thyself!
 
Last edited by a moderator:
Number 3 nina mahusiano nae duh! hujamkosea hata kidogo!!! MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom