Stori za radi dhidi ya Kondoo ni za kweli?

Majigo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
5,519
Reaction score
1,831
Toka Udogo Hizi Habari Za Radi kupigana Na Kondoo Nimekuwa Nazisikia Sana Ila Sijawahi Thibitisha Hili. Kwanza Siamini kama Radi Ni Mnyama. Tena Anayeshuka Toka Angani Kuja Duniani. Wakaongeza Huyu mdudu (Radi) Ana Miguu 6, Kondoo Ana uwezo Wa Kumuona Na Kupambana Nae Mpaka Akakimbia Au Kufa Kabisa.

Kwa Yeyote Mwenye Uhakika Na Hili Anisaidie Niujue Ukweli.

Ahsante Jigo
 
zamani kulikuwa na kampuni moja maarufu ya mafuta kutoka italiano inaitwaa AGIP siku hizi tanzania haipo,ila huko uitaliano inaitwaa ENI siku hizi, hawa jamaa walikuwa wana symbol yao ya biashara inakamnyama fulani ,kaka yangu alikuwa ananiambia huyo mnyama ndio radi
images
 
kama radi ni mnyama basi inaweza pia kuwa silaha ya maangamizi maana juzi jamaa kamtumia radi mbaya wake!
 
Hauna uhakika juu ya hili? Ina maana kwa kiasi fulani unaweza kuamini. Back to physics, radi ni umeme utokanao na msuguano wa mawingu/uzalishwaji wa chaji angani. Hakuna mnyama wala mmea
 
kama radi ni mnyama atakuwa analiwa tu
 
Hauna uhakika juu ya hili? Ina maana kwa kiasi fulani unaweza kuamini. Back to physics, radi ni umeme utokanao na msuguano wa mawingu/uzalishwaji wa chaji angani. Hakuna mnyama wala mmea

Radi ni mnyama wewe, kuna mzee mmoja mganga maarufu sana yupo pale Ikwiriri Rufiji, ni mfugaji mzuri sana wa radi. Kama unabisha wewe nenda pale Ikwiriri Rufiji, muulizie mzee Kajunjumele.
 
Back to history, binadamu wa kwanza alikua nyani, ni kweli?
 
Radi ni mnyama?? Labda huko kwenu tu, anaishi wapi? Anakula nini?
 
zamani kulikuwa na kampuni moja maarufu ya mafuta kutoka italiano inaitwaa AGIP siku hizi tanzania haipo,ila huko uitaliano inaitwaa ENI siku hizi, hawa jamaa walikuwa wana symbol yao ya biashara inakamnyama fulani ,kaka yangu alikuwa ananiambia huyo mnyama ndio radi
images

Hii Nembo Hata Mi Niliwahi Ambiwa Ni Radi
Sasa Sijui Ni Kweli!
 
kama radi ni mnyama,tutajie kitabu,tutakitafuta tukisome,msilete habari za kaka yangu,oooo mara babu yangu,hao ni akina nani katika ulimwengu wa wasomi?
 
kama radi ni mnyama basi inaweza pia kuwa silaha ya maangamizi maana juzi jamaa kamtumia radi mbaya wake!

Hizi Habari Nazisikia Sana Huko Mikoa Ya Kusini Maeneo Ya Vijijini
Sijui Kama Kuna Ukweli Juu Ya Hili Pia
 
majigo nitafute tuondoane upweke hii hali sio nzuri

hii Hali Hainifai Hata Mimi
Nashukuru Kwa Kunijari Mpenzi
Nakusaka Sasa Hivi TuWeke Mambo Sawa Ili Tupone Dhidi Ya Hali Hii!
 
Hauna uhakika juu ya hili? Ina maana kwa kiasi fulani unaweza kuamini. Back to physics, radi ni umeme utokanao na msuguano wa mawingu/uzalishwaji wa chaji angani. Hakuna mnyama wala mmea
Ahsante Chief Sasa Vipi Kuhusu Habari Za Vita Vya Kondoo Na Radi?
 
Radi ni mnyama wewe, kuna mzee mmoja mganga maarufu sana yupo pale Ikwiriri Rufiji, ni mfugaji mzuri sana wa radi. Kama unabisha wewe nenda pale Ikwiriri Rufiji, muulizie mzee Kajunjumele.

teh teh teh
Huko Kajunjumele Radi Zimetapakaa Mpaka Kiangazi..Tena Hadi Chooni Unadunguliwa Na Radi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom