STORI YA KWELI: Nimeamini ARV zimepunguza Umaarufu na Hofu ya UKIMWI...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Miaka ya nyuma hofu ya UKIMWI ilikuwa juu sana. Tahadhari zilikuwa kubwa kiasi kwamba kuanzia wazazi hata majirani wakikuona na mtu ambaye haeleweki wanakuonya.

Mara ya Mwisho miaka kadhaa iliyopita nilishuhudia mwanadada mlimbwende, kuna baadhi ya vijana mtaani walishakosakosa kumbaka kwa uzuri wake. Chumba alichopanga kila aina ya mwanaume alionekana. Siku alipoanza kukohoa, kikohozi hakikurudi nyuma kiliambatana na upele,mara ngozi kunyauka, makalio makubwa na ya kuvutia yakapukutika taratibu ila kwa uhakika. Hali ikawa mbaya ilibidi arudi kwao Mnyantuzu yule, kule aliendelea kupukutuka na kudhoofu kwa kasi ya mwendokasi. Wafuatiliaji na marafiki wake waliokwenda kumtembelea siku za mwishomwisho za uhai wake, alikuwa amefikia hatua ya kutosha kwenye beseni la kuoshea watoto.

Hakukua na jinsi binti mzuri wa kuvutia mlimbwende wa kutupwa, hata sisi tuliokuwa wadogo hatujitambui tuliuona uzuri wa mnyatuzu yule. Lakini alitutoka akiwa kapukutika nyama zote, Dada mkubwa na mpana akatukutoka akiwa ameshambuliwa kila kiungo kaisha kabisa macho tu ndio yaliyobaki angavu huku mwili ukikoswa hata sehemu ya kumchoma sindano kuokoa maisha yake. Siku, na muda ukafika dada yule akapumzika bila wasiwasi akiwa ameshiba mateso na uchovu mwingi, hadi sasa hatunae na wengi mtaani wameshamsahau kama aliwahi kuwepo.

Tafakuri na hofu ilitanda vijana mtaani. Tukaanza kuwakumbuka waume wa watu, mabosi ambao tuliwaita shemeji, Hata tukafikia kuwakumbuka machekibobu wa mtaani kwetu wakiongozwa na dogo aliyeitwa SHIJa... waliponusurika kumbaka dada huyu akitokea kazini usiku.

Nikiangalia Leo, Muathirika anatutoka akiwa na afya tele, Mwili ukianza kupukutika ARV zinaingilia kati na kumstawisha haraka sana. Nagundua ni kweli kabisa Mnyantuzu yule angekuwepo zama hizi angekuwa na mnyororo mrefu wa wahanga.

Nikilinganisha tukio lile, na la mwingine ambaye kila asubuhi watoto wake walikuwa wakimtoa nje asubuhi kwenye beseni akioshwa, Tukiwa wadogo akitoka tu tunajipitisha kupata ushilawadu kidogo maana hatukuamini kama ni yeye huku tukiishia kutukanwa kila anapotuona, na kubali kuwa ARV sio tu zimeongeza siku za kuishi bali ZIMEFUTA kabisa UMAARUFU na HOfu ya UKIMWI.

Je? Ni kweli?

Sema chochote maana hii ni Afrika yetu na janga lipo miongoni mwetu tusipokuwa wawazi haitasaidia kitu.

Angalizo: Lengo sio kunyanyapaa bali tunajifunza kupitia jicho la historia
 
You are very right Mkuu. Sayansi inazidi kumsaidia binadamu kukabiliana na Changamoto za maisha yake. Mfano nakumbuka zamani TB ilikuwa tishio kweli kweli. Dawa ilikuwa ni sindano 60! Baada ya hapo TB siyo tishio tena.

Mimi naona hayo ndo maendeleo yenyewe. Ukimwi kwa sasa si issue kihivo..na kama ulivyosema mtu akiwa nao hata akitangulia mbele ya haki..ni mara chache sana aende ameugua sana na kupoteza mwili wake. Mtu anaondoka mzima mzima..na ni nadra hata kujua kilichomuondolea uhai wake.

Mimi nasema hayo ndo matunda ya sayansi. Ni vema serikali zetu zikawekeza kwenye elimu especially sayansi. Naamini vizazi vijavyo vitaishi hata miaka 100 na kuendelea.
 
UKIMWI ni gonjwa hatari sana, namkumbuka Mzee mmoja mtaani kwetu. Alikuwa ni Mwanajeshi, alikuwa mkakamavu aliyejazia misuli katika mwili. Mrefu na aliogopwa sana hapo mtaani.

Maskini, katika harakati za kazi zake akaukwaa. Aliisha, alitia huruma na mtu yeyote aliyemfahamu akimtazama tu anaweza kupiga yowe kwa huruma na kuogopa. Alinyooka na kubaki mifupa, aliteketea. Alibakia na fuvu la kichwa tu, na mifupa yake. Ngozi ikiwa imelemaa haswa.

Aliondoka baada ya kipindi fulani. Hakuna aliyekuwa tayari kumtazama. Alizikwa kwa heshima zote.

Nikimkumbuka huyu mzee, mpaka hata hamu ya kugegeda inaisha.

Kwa sasa mimi sioni kama kuna Hili gonjwa haswa. Hii ni photocopy tu ya gonjwa lenyewe. Watu hawaliogopi. Watu walioambukizwa tayari wana furaha na kufurahia maisha kama kawaida. Wanadunda.
Mungu pitishia mbali nami gonjwa hili hatari.
 
ARV ni kama dawa nyingi nyingine baada ya kumaliza kazi yake mwilini zinatoka kwa njia ya mkojo hivyo hupitia mchujo wa kidneys. Wagonjwa wanachekiwa kidney function levels kila wakienda kwenye kitengo na kama dawa zinaleta madhara mgonjwa hubadilishiwa dawa. ARV zimepumguza maambukizi mapya kwa wanaofuata masharti ya tiba.
 
You are very right Mkuu. Sayansi inazidi kumsaidia binadamu kukabiliana na Changamoto za maisha yake. Mfano nakumbuka zamani TB ilikuwa tishio kweli kweli. Dawa ilikuwa ni sindano 60! Baada ya hapo TB siyo tishio tena.

Mimi naona hayo ndo maendeleo yenyewe. Ukimwi kwa sasa si issue kihivo..na kama ulivyosema mtu akiwa nao hata akitangulia mbele ya haki..ni mara chache sana aende ameugua sana na kupoteza mwili wake. Mtu anaondoka mzima mzima..na ni nadra hata kujua kilichomuondolea uhai wake.

Mimi nasema hayo ndo matunda ya sayansi. Ni vema serikali zetu zikawekeza kwenye elimu especially sayansi. Naamini vizazi vijavyo vitaishi hata miaka 100 na kuendelea.
Sayansi na Teknolojia kweli mkuu, inaondoa mzigo mkubwa kwenye jamii yetu.
Ndio maana tunasisitiza serikali ihamasishe vyuo vyetu viwekeze kwenye Research and Development.
Hakuna haja ya matafiti makubwa yenye kutaka trillions, bali hata za wastani tu kutatua matatizo madogo madogo ya mtanzania. Maana ukimuongezea mtu maisha unaliongezea taifa Man-Hours.
Tukishindwa tuwe na kitengo cha kufuatilia tafiti zote duniani za kisasa, na kuchuja zile zenye faida kwetu na kuziendeleza. Ingawa nchi yetu ni maskini saaana kiasi kwamba hata tunashindwa tuwekeze wapi kwa pesa kidogo kuliko ukubwa wa matatizo yetu.
ndio maana leo wanasiasa wanabishana Tuwekeze kwenye Miundombinu, Mwingine hapana unakosea Kilimo, Mwingine Viwanda ndio kila kitu na mwingine afya au elimu. Kelele zote hizi ni matokeo ya Umasikini wa kutupwa maana tungekuwa na pesa yote hayo yangefanyika bila ugomvi.
 
UKIMWI ni gonjwa hatari sana, namkumbuka Mzee mmoja mtaani kwetu. Alikuwa ni Mwanajeshi, alikuwa mkakamavu aliyejazia misuli katika mwili. Mrefu na aliogopwa sana hapo mtaani.

Maskini, katika harakati za kazi zake akaukwaa. Aliisha, alitia huruma na mtu yeyote aliyemfahamu akimtazama tu anaweza kupiga yowe kwa huruma na kuogopa. Alinyooka na kubaki mifupa, aliteketea. Alibakia na fuvu la kichwa tu, na mifupa yake. Ngozi ikiwa imelemaa haswa.

Aliondoka baada ya kipindi fulani. Hakuna aliyekuwa tayari kumtazama. Alizikwa kwa heshima zote.

Nikimkumbuka huyu mzee, mpaka hata hamu ya kugegeda inaisha.

Kwa sasa mimi sioni kama kuna Hili gonjwa haswa. Hii ni photocopy tu ya gonjwa lenyewe. Watu hawaliogopi. Watu walioambukizwa tayari wana furaha na kufurahia maisha kama kawaida. Wanadunda.
Mungu pitishia mbali nami gonjwa hili hatari.
Amina
 
Mkuu uminitoa machoz ukimwi uliniondolea baba yang nikikumbuka alivyokuwa dk za mwisho za uwah wake aliteseka sana kibaya zaid baada ya kuenda hospital bila mafanikio nafkir hawakumpima mapema

Tukaamia upande wa tiba mbadala hapo ndo kuku wakatafunwa sana na wajanja wa town ikafka kipindi kwenye SM yang kuna namba nying za waganga wa kienyeji kuliko hata ndg zangu

Hatimaye tulikuja kugundua hata ya mwisho kuwa ni ukimwi

Lakin tunashukur mama yangu bado yupo huu ni mwaka 12 anatumia dawa na ana afya nzr

Namuomba mungu aendelee kumpa maisha marefu maana bado ni nguzo katika familia yetu
 
pole sana .
Inasikitisha sana, kuna baadhi ya familia siku alipoanza baba, mama akafuatia, wakaugua karibu nyumba nzima hatua kwa hatua. Ukimwi ule utadhani ni ugonjwa tofauti na huu wa sasa maana unaweza kuishi siku zote kama ukifuata kanuni.
Mungu atamuhifadhi mzazi wetu mkuu...
 
Back
Top Bottom