Stori ya kusisimua-The future is unpredictable

Stori ya kusisimua-The future is unpredictable

Quinn

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
473
Reaction score
1,188
Erick alikuwa kijana anayesoma chuo kimoja nchini uingereza na alikuwa akiishi na mama yake ambaye alikuwa ameajiriwa kwenye mgahawa mmoja mjini london.

Erick alilelewa na mzazi mmoja ambaye ndo uyo mama yake anayefanya kazi mgahawani hivyo maisha yao yalikuwa ya kawaida sana.

Erick aliwahi muuliza mama yake kuhusu baba ake kwani alitamani kumuona ila mama yake alikuwa mkali mno pindi amuulizapo na kumwambia baba ako alinitelekeza na akakataa mimba yake hivyo sitaki uniulize ayo maswali.

Maisha ya chuo ya Erick alikuwa akimpenda sana binti mmoja aitwaye Alice lakin Alice alionekana ni mwanamke asiye endana na Erick kwan alikuwa ni binti mrembo na alikuwa akishinda tuzo nying za urembo apo chuoni.

Alice apo chuoni alikuwa na mvulana wake apo chuoni ambaye alikuwa na hela mnoo na huyo mwanaume wake akitembea uwa ana ambatana na wapambe wake.

Kwenye kila siku ya ijumaa Alice alikuwa akitoka na kampani ya marafiki zake na kuambatana na kampani ya mwanaume wake na kwenda kwenye club za starehe.

Erick alizidi kumpenda sana Alice na kuanza kujisogeza kwake akionesha hali ya kutaka kumsaidia kwenye masomo kwani Erick alikuwa ni mwanafunzi mwenye kufaulu vizuri darasani kwao na ndilo darasa alilokuwamo Alice.

Alice akawa karibu kimasomo na Erick lakini alikuwa hana hisia kabisa na Erick ikafika hatua Erick akawa anafanya assignments alizotoa mwalimu kumsaidia Alice pindi Alice anapokwenda kwa mwanaume wake asa siku ya ijumaa kwani mwanaume wake walikuwa ni chuo kimoja ila madarasa tofauti.

Erick alikuwa anaumia sana moyo pindi awaonapo Alice na bwana ake chuoni na Alice alimtambulisha Erick kwa bwana ake kama msaidizi wake kimasomo.

Erick alirudi kwa mama ake na kumwambia hisia zake kwa Alice...Mama ake akamwambia kama Alice ana mtu wake basi achana naye kwani wasichana wapo wengi na wewe bado kijana.

Erick akiwa chumbani akiwaza maneno ya mama yake kuwa aachane na Alice na kuangalia wasichana wengne akajikuta moyo wake unakataa.

Erick akiwa chumbani siku ya alhamisi nyumbani kwao akatoa karatasi nyeupe na peni yake na kuanza kuandika hisia zake kwa Alice.

Siku ya ijumaa baada ya kipindi cha mwisho kuisha akiwa bado kwenye kiti chake Alice akamsogelea na kumwomba amsaidie assignments zake za wikiendi na Erick akakubali haraka haraka uku kichwani anajiuliza mara mbili mbili kuwa ampe ile barua au hasimpe wakati Alice akiwa mlangoni basi Erick akamwita na kumpa ile barua na kumwambia hasifungue hadi akifika nyumban na Alice akaichukua.

Alice alisoma ile barua akiwa nyumbani na akashangaa kuona ule ujumbe kuwa Erick anampenda na ndipo akatoa simu na kumpigia simu yule mwanaume wake aje nyumbani na alipofika akamuonesha ile barua.

Mwanaume wake alichukia sana na hata Alice akachukia akasema Erick ni maskini,hajui kuvaa na hatuendani, wakaanza kujiuliza tumfanye nn.

Yule mwanaume wake akatoa nakala nyingi akawahi asubuhi siku ya jumatatu chuoni na kubandika zile nakala za barua ya Erick kwenye ubao wa matangazo na nyingine akabandika darasani.

Erick alichelewa kufika chuo siku ya jumatatu na kupita ubao wa matangazo bila kusoma ubao wa matangazo na watu walikuwa madarasani na akaingia darasani, akashangaa kuona wanafunzi wanacheka na kumuuliza jirani anaye kaa naye pemben darasani kuwa watu wanacheka nini ndipo akamwelezea Erick kila kitu. Erick kwa aibu akamuangalia Alice kwa mbali na Alice Akamsonya.

Erick hata kabla ya mwalimu kuingia, muda huo huo akatoka uku akitaka kutoa machozi na kuogoga kuwa baadae wanafunzi wa chuo kizima wakitoka darasani ataiweka wapi sura yake.

Erick alikaa nyumbani wiki nzima uku simu imezimwa na mama ake akimuuliza anasema anaumwa hawez kwnda chuo, siku nyingne anamuongopea mama yake kuwa ameenda kwani mama yake alikuwa anawahi kutoka asubhi na kurudi usiku, hivyo Erick alikaa takribani miezi miwili nyumbani na kupelekea kufukuzwa chuo.

Baada ya muda mrefu alimwambia mama yake ukwel na mama yake alilia sana na kumwambia kuwa nilikuwa nakutegemea wewe mwanangu. Erick akitokwa na machozi uku akimwambia mama yake kuwa akimpatia pesa yuko tayari kurudi shule.

Baada ya miaka mitatu baada ya mama yake kuweka kidogo kidogo ndipo akampatia Erick pesa na Erick akarudi shule uku wale wanafunzi wote waliokuwa wanamjua walikuwa washamaliza chuo zamani sana.

Baada ya miaka ishirini, Erick akiwa london amevaa casual (shati lenye maua maua na kaptura) akaingia kwenye super market kubwa london, akiwa anazunguka kuangalia bidhaa mbali mbali akamuona Alice kwa mbali kwenye sehemu ya bidhaa za watoto.

Akaenda kuelekea Alice alipo na kumsalimia, Alice kwa dharau akaitikia salamu yake uku akishika tumbo lake kwani alikuwa mja mzito na Erick akamwambia hongera.

Alice kwa mashauzi akamwambia bora uondoke tu apa kwani mume wangu ameenda msalani asije akukuta hapa kwani sio yule unayemjua wa chuoni ni mwingine na ana hela sana atakupoteza,analipwa dola 200,000 kwa wiki kazini kwake, tumejenga jengo la kifahari paris kwa sasa tupo hapa london amekuja kikazi na tunaishi kwenye apartment ghali london,je wewe ungeweza?

Mara mume wake akatoka msalani na Alice alipogeuka kumuona mume wake anakaribia akaanza kuogopa kwani Erick alikuwa bado yupo naye anampatia maneno ya kejeli na ya kufedheesha. Yule mume wake na Alice alipofika akashangaa na kustuka kumuona mke wake(Alice) yupo na Erick

Mume wake na Alice akamsalimia Erick na kumwambia mke wake (Alice), mke wangu uyu ni boss wangu anaitwa Erick ndo anamiliki kampuni ninayofanyia kazi natumaini kama mnajuana itasaidia mimi mumeo kuongezewa mkataba wa kazi kwani unaisha mwakani na hii super market ni ya uyu boss wangu sikujua kama mnafahamiana na boss wangu na sijui kama ana nikumbuka kwan ameajiri wafanyakazi wengi....Alice kwa aibu alipigwa na butwaaa na kukosa jibu hadi alihisi mimba inataka kuchomoka.
 
Back
Top Bottom