Steve Wonder (picha inanishangaza kidogo)

Salamander

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
28,538
15,739
Kwenye hii picha anaonekana na mkewe(now x-wife), Kai Millad Morris wakitembea wameshikana mikono. Kinachonishangaza Steve, ambaye ni kipofu mbona katangulia mbele?

1238845_562816113767973_1792051265_n.jpg

Kwenye hii picha anaonekana na mkewe(now x-wife), Kai Millad Morris wakitembea wameshikana mikono. Kinachonishangaza Steve, ambaye ni kipofu mbona katangulia mbele?

Mkuu sijui kama wewe ni mmiliki na muendeshaji wa gari.

Kama ni hivyo basi unaweza kukumbuka kuwa kuna siku nyingine unatoka kazini hadi unafika nyumbani na usikumbuke ulikutana na nini njiani. Ukishaizoea njia basi unakuwa katika auto-pilot na unaweza kufika mahala bila kujua ulifikaje.

Steve ni kipofu tangu alipokuwa mtoto.

Njia zote anazozitumia anazijua kuliko anaeona. Anaweza kukutahadharisha kuwa "hapo mbele kuna jiwe kulia jihadhari" wakati ni usiku na kweli hilo jiwe lipo.

Ukipoteza sense moja ya ufahamu zile nne nyingine zilizobaki zina-compensate.
 
Karibu Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa Lushoto Tanga. Ujifunze, ushangae na kujionea haya ya Steve na mengi mengine ya ndugu zetu wenye ulemavu. Disability is not inability....so we believe!

Nimependa bandiko lako na pengine maneno uliyoyatumia ndio maneno muafaka.

Lakini kwa mtazamo wangu sisi tunaojiita "SIO WALEMAVU (not disabled)" ndio walemavu wakubwa sana.

Sisi "tusio walemavu" mara nyingi hatukumbuki sauti za watu, hatujui kuna ngazi ngapi mpaka mlangoni, hatukumbuki harufu za watu au vitu, nk.

Watu wanapaswa kuelimisha tu. Itachukua muda lakini tutafika.
 
Hakika mkuu, ukiishi na ndugu zetu wenye ulemavu, wa kusikia, kuona, kuongea, viungo au ulemavu wa akili hakika utajifunza mengi na kujua kumbe ulikuwa hujui sana kuhusu uumbaji na uwezo wa mwanadamu regardless ana/hana nini mwilini mwake. Karibu sana ndugu.
 
Steve kweli ni lipofu..mke gani sasa huyo.!!

Mkuu nimecheka (kama mazuri vile), so "ukipofu" wa Steve umepelekea apate huyu "mke gani" duh! Sijui uliwaza awe na mke mwenye nini hasa, au mwenye muonekano gani hasa ili wewe uridhike kuwa "huyu ndiye wa Steve" Naamini Steve alikuwa na vigezo vyake (kama wewe unavyoweza kuwa) ndipo akawa na huyu "mke gani sasa"
 
Salamander Samahani nime/tumeingilia Uzi wako, naweza/twaweza kuwa nje ya mada yako lakini ni katika kuonesha namna gani hatufahamu sana juu ya ndugu zetu wenye ulemavu. Ni topic pana lakini ya kuvutia sana kama mtu ataamua kufuatilia na kujifunza juu ya ndugu zetu wenye ulemavu. Maoni/wito wangu.......kila mmoja wetu ajifunze na ajue kiasi juu ya upande huu wa maisha ya walemavu. Ukweli "mkavu sana" ni kuwa KILA MMOJA WETU NI MLEMAVU MTARAJIWA.
 
Last edited by a moderator:
Karibu Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa Lushoto Tanga. Ujifunze, ushangae na kujionea haya ya Steve na mengi mengine ya ndugu zetu wenye ulemavu. Disability is not inability....so we believe!

Mkuu nakusoma vizuri sana

Nilisoma Mkwawa High School na jamaa vipofu....njia zote walikuwa wanazifahamu....bwenini kwemda chumba chenye vifaa vyao maalum, kwenye chakula, madarasani e.t.c.....

Niliingia chumba cha vifaa vyao maalum kwa mara ya kwanza nikajitambulisha ma kuwasalimu nikaondoka....after 3 days nikapishana nao eneo la assembly na kuwasalimu wakaniambia aah wewe ni *** uliekuja juzi kwetu.....and I was shocked maana hawakukosea wakati mimi nilishasahau majina yao

These people are amazing aisee
 
Nimependa bandiko lako na pengine maneno uliyoyatumia ndio maneno muafaka.

Lakini kwa mtazamo wangu sisi tunaojiita "SIO WALEMAVU (not disabled)" ndio walemavu wakubwa sana.

Sisi "tusio walemavu" mara nyingi hatukumbuki sauti za watu, hatujui kuna ngazi ngapi mpaka mlangoni, hatukumbuki harufu za watu au vitu, nk.

Watu wanapaswa kuelimisha tu. Itachukua muda lakini tutafika.

Salute to you.
 
Na wako very brilliant mi nilifundishwa na Mwalimu pale iyunga ni kipofu yuko nondo balaa yaani kipindi chake kilikuwa kitamu sana .

Saivi nafanya kazi na jamaa mmoja yuko safi sana .

Jamaa wana talents
 
Mkuu yule mwalimu alikua anafundisha civics...Mungu ana maajabu yake..
 
Nimependa bandiko lako na pengine maneno uliyoyatumia ndio maneno muafaka.

Lakini kwa mtazamo wangu sisi tunaojiita "SIO WALEMAVU (not disabled)" ndio walemavu wakubwa sana.

Sisi "tusio walemavu" mara nyingi hatukumbuki sauti za watu, hatujui kuna ngazi ngapi mpaka mlangoni, hatukumbuki harufu za watu au vitu, nk.

Watu wanapaswa kuelimisha tu. Itachukua muda lakini tutafika.
Na pengine vichaa ndo wana akili na maono kuliko hata maprofesa! Nenda kasome novela za Kezilahabi Nagona na Mzingile utapata fununu ya ninachojaribu kukisema. Tunajifanya tunaona kumbe ndo tunaongoza kwa upofu na tunaowaita wajinga ndo wenye maarifa yanayoishi. Karibu kila kitu ni kinyume!
 
Back
Top Bottom