Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Mungu yupo na dini ya kweli ni matendo mema

Ila bado hatujaweza kuthibitisha uwepo wake , hilo usibishe dada !
 
Uthibitisho wa kipi ninachosema?

Uthibitisho gani?

Ili kitu kikubalike kwamba ni uthibitisho kwako, kinahitaji kukidhi vigezo gani?
 
amina sana NGUDU YANGU ..HAWA WATU NDIO HAPA TUNAWAKAMATA TUNAWAONA EMPTY KABISA...KUNA MMOJA ANAPINGA UWEPO WA YESU KUA ALIISHI ILA ANAKUBALI GALILEO ALIKUWEPO...HAHAHAHHAHA NIMEFURAHI SANA
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kungekuwa hakuna mtengano huu.

Mtengano huu unaonesha Mungu huyo hayupo, ni hadithi tu zimetungwa na watu.

Ndiyo maana kila utamaduni una hadithi yake tofauti.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kungekuwa hakuna mtengano huu.

Mtengano huu unaonesha Mungu huyo hayupo, ni hadithi tu zimetungwa na watu.

Ndiyo maana kila utamaduni una hadithi yake tofauti.
Teh ....

Mi siwez kumthibitisha ...

Ila naamini yupo ...

Kuna wanasayansi wenzangu wa neuro hapa John Hopkins hawataki kuelewa kabisa story za Mungu kuwepo
 
Uwepo wa socrates unaweza kuthibitishwa

Unawezaje kuthibitisha uwepo wa Socrates ? Au unatumia nyenzo gani kuthibitisha uwepo wake ?
Lakini uwepo Wa Mungu kuthibitishwa ndo umeibua yote haya !!

Unafikiri ni sahihi kuwepo au kuibuka haya ? Je ushawahi kujiuliza ya kuwa wanao kana uwepo wa Muumba wameegemea misingi gani ? Je wako sahihi ?
Kiranga anataka athibitishiwe Mungu yupo , mimi naamini Mungu yupo ila siwezi kuthibitisha
Hapo ndipo wengi hatumuelewi kiranga na hatumsaidii sisi kama watu ambao tunaamini Mungu yupo

Tunamshambulia , na amekuwa victim

Kiranga hajawahi kutaka kuthibitishiwa uwepo wa Mungu ukipima katika mizani ya kielimu. Huwezi kuomba thabati ukianza na kukanusha,na kama angekuwa anataka kuthibitishiwa uwepo wa Mungu asingekuwa anakanusha mpaka leo. Kwa maana yeye ana imani yake tayari,ambayo alitakiwa kwanza athibitishe yeye kuwa Mungu yupo. Ajabu jambo asilolijua ni kuwa hiyo imani yake imejengeka katika ujinga,kwani siku zote swali lakini ni "Kama Mungu ni mjuzi wa yote,......... kwanini ameruhusu maouvu au majanga yatokee ?"

Naendelea ....
 
Kiranga njoo umjibu dada ako

Mi sielewi maswal yake
 
Teh ....

Mi siwez kumthibitisha ...

Ila naamini yupo ...

Kuna wanasayansi wenzangu wa neuro hapa John Hopkins hawataki kuelewa kabisa story za Mungu kuwepo
Kuamini unaruhusiwa kuamini lolote, hata lile ambalo halipo.

Na kifalsafa unaruhusiwa uhuru wa kuamini. Hili jambo halihitaji kwenda na fact. Ndiyo maana uhuru wa kuabudu upo katika katiba na Universal Declaration of Human Rights.

Kuna sababu hao wanasayansi wa Hopkins hawaamini habari za Mungu.

Ukiangalia nchi zenye maendeleo ya elimu kama Northern Europe utaona imani ya Mungu ni ndogo sana.

Halafu ukiangalia nchi zenye kiwango cha chini cha elimu rasmi huku kwetu Africa utaona watu wanasema imani ya Mungu iko juu sana.

Halafu ukiwaangalia hata hao wanaosema wanamuamini Mungu, ukiangalia matendo yao, utakuta kwa sehemu kubwa wanapiga soga tu, hawaishi kama watu wanaoamini kweli Mungu yupo. Kwa sababu hata kwa watu wanaosema wanaamini Mungu yupo, ni vigumu kuishi kama unaamini Mungu yupo wakati hayupo.

Ndiyo maana katika dunia hii, wanaoishi kwa maandiko ya huyo anayesemwa Mungu (ambayo yana contradiction kibao) ni wachache sana. Hata kama unaweza sheria za msingi tu kama kigezo.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kungekuwa hakuna mtengano huu.

Huku ni kufikiri kitoto,ukisema hivyo ungekuwa wapi uhuru wa kuchagua na yangekuwa waoi matumizi ya akili ?

Lakini,Allah anaweka yaliyo bora na anajua kupangilia mambo na taratibu zake hazibadiliki.

Lakini swali kwako ambalo huwezi kulijibu,umejuaje hilo ?
Mtengano huu unaonesha Mungu huyo hayupo, ni hadithi tu zimetungwa na watu.

Lakini kielimu hapa hujaonyesha kama Mungu hayupo sababu majibu yalikutangulia kitambo sana kabla hujukiani kama utazaliwa.

Na kuishia kusema "...ni hadithi tu zimetungwa na watu." bila kuonyesha zilitungwa vipi na kwanini na kwa nani na umejuaje ? Huku nu kukimbia mjadala.
 
Kiranga njoo umjibu dada ako

Mi sielewi maswal yake
I swore off this calcified cretin.

Hana basic qualifications za kufanya mjadala nami.

Namuambia haelewi Socratic method ni nini, ananiambia hana haja ya kuelewa.

Hana hata utashi wa kuelewa asichoelewa, sasa nitajibizana naye ili iweje?

Nimemu ignore, hata anachoandika sikioni.
 
Mwanzon ni kama walkua wanantenga kutokana na misimam yangu ya dini

Ila nikaamua kuacha kuwa na misimamo , nisiwalazimishe waamini Mungu yupo

Urafiki ukarejea !

Wala nao hawanisumbui
 
 
Mungu yupo na dini ya kweli ni matendo mema

Ila bado hatujaweza kuthibitisha uwepo wake , hilo usibishe dada !

Nacheka sana,kuniita mimi "dada" hakubadilishi ukweli na wanaume tuna lugha zetu,na katika wanaume kuna wanaume. Vipi ukitaka kunifedhehesha nini ? Nakupa udhuru na hivi ndivyo nilivyo mimi.

Huwezi kutenda mema bila kujua kwanini unatenda wema na unatenda wema kwa ajili ya nani ? Hapa ndipo wanatoka wote watendao wema huku wana imani potofu,nia batili na hapa wanatoka mabudha,wamajusi,waabudu mizimu,washirikina na mfano wao.
 

Mufti siku hizi unajengeka
_Naona unajenga hoja kwa logic .....hatari sana


Ilabaki kidogo nidhani sio wewe..!?
 
Mwanzon ni kama walkua wanantenga kutokana na misimam yangu ya dini

Ila nikaamua kuacha kuwa na misimamo , nisiwalazimishe waamini Mungu yupo

Urafiki ukarejea !

Wala nao hawanisumbui
Rafiki ambaye atataka kunitenga kwa sababu ya tofauti za kifalsafa kuhusu dini, huyo hakufaa kuwa rafiki yangu tangu mwanzo.

Wajamaica wana msemo wao mmoja naishi kwa kuutumia maisha yangu yote.

Wanasema "Me no beg no friend". Siombelezi urafiki, unatokea tu naturally.

Mimi nina marafiki kuanzia ma Buddhist monks mpaka wachungaji.
 
Sawa

Siku njema
 

Nacheka sana,usikimbie maswali nawajua vizuri sana,kama wakubwa zako walsindwa walishindwa ni muhali wewe kuweza,nimekuuliza maswali mangapi hujibu ?

Ajabu hata kanuni za mijadala huzijui,hakuna kanuni ya mijadala inayokutaka kukimbia maswali.

Socratic Method nilikwambia kuijua kwake na kutokuijua ni sawa,yaani hakunipunguzii chochote wala kuniongezea lolote,sasa wewe ndio ungetumia njia kujenga hoja yako,ajabu ukatolea mfano wa mwalimu na waanfunzi wake na ukasahau nimekuuliza swali katika muktadha gani. Hili ni tatizo la kukaririshwa kabla ya kuelewa,na umekuwa kama punda aliye bebeshwa mizigo ya vitabu na hafaidiki na vitabu hivyo.
 
Mkuu Kiranga na dmatemu na wengine mnaopinga uwepo was Mungu, hebu niambieni, mnachukuliaje Uchawi, Uganga, Elimu ya Nyota na Elimu ya majini?

Na je, nini chanzo cha uhai?
Define uchawi, Uganga, Elimu ya Nyota. Elimu ya majini.

Kwa sababu uchawi unaweza kuushangaa kumbe ni tricks saikolojia imechanganywa na kemia na baiolojia.

Uganga unaweza kuwa baiolojia na tricks za saikolojia.

Elimu ya Nyota unaweza kuwa tricks za saikolojia na unajimu.

Elimu ya majini inaweza kuwa sayansi ya ku navigate baharini, kwenye mito na maziwa ya maji.

Swali lako halina maana sana kama halina definition ya terms.

Hilo moja.

Halafu, kama kweli uchawi upo, kama unavyoaminika na wengi, watu wanaua wenzao kwa uchawi, huo ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeruhusu uchawi au uovu wowote uwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…