Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,312
- 105,648
- Thread starter
- #2,301
Umeuliza swali.Umependekeza mifano ya kimantiki, basi na tuende hivyo.
Kwa hekima yake mtu anaweza kuamua asizae na akaona ni vizuri, lakini kwa walio wengi wanaona utasa, ugumba na namna zote za kukosa uzazi kuwa ni 'mabaya'
Sasa kama kuwa na watoto ndio kitu kizuri ambacho watu wanafurahia, ni kwa nini Mungu hakuumba watu wote wawe na watoto wao tayaritayari?
Wasipitie michakato ya kupevuka
Wasipitie michakato ya utungu
Wawe tu na watoto wao tayaritayari🤔
Lakini hata hilo likiwezekana bado kutakuwa na mabaya.
Watoto wadogo wanalialia
Kulea ni kazi
Mara chanjo, mara waugue
Wasubiriwe wakue ni usumbufu tu. Kwa nini Mungu asingewaumba wakiwa watu wazima.
Sasa hao watu wazima nao (ambao ni watoto) sio vema wangekuwa na watoto wao wakiwa watu wazima tayari? Vivyo hivyo hadi mwisho.... Basi angeumba tu watu wote wanaohitajika mara moja tukaachana na shida. Hapo ndio tutajua kuwa ana upendo wote na uwezo wote eeeeh!?
Sasa bro, huoni kama kwa kufanya hivyo atakuwa effectivelly amefuta kabisa kipengele cha maisha kinachohusisha ukuaji, sex, utoto, utu uzima. Na tayari maisha yamepungua uwanda wake pakubwa tu?.
Vivyo hivyo kama ukienda kwenye 'mabaya' mengine yote yakafutwa moja baada ya jingine ndiyo mwishowe tunakuwa hatuna maisha kama tunavyoyafahamu sie maana hakutakuwa na muda tena.
Maana utauliza kwamba sasa taabu yote ya nini ya milipuko na kujisongasonga kwa nyota, magalaxy na sayari na mavolkano na matetemeko. Si angeumba tu yakiwa mwishoni bila usumbufu huu wenye mabaya mengi. Yaani iwe tu kila kitu kilishasambaa na entropy iwe kamili 100%. Je kutakuwa na uhai tena?
"Sasa kama kuwa na watoto ndio kitu kizuri ambacho watu wanafurahia, ni kwa nini Mungu hakuumba watu wote wawe na watoto wao tayaritayari?".
Hakuumba hivyo kwa sababu hayupo. Ili kuumba hivyo inabidi awepo kwanza.
Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.