Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,312
- 105,648
- Thread starter
- #2,281
Mkuu,Angalau nilichogundua ni kwamba, watu wengi, sio wewe tu hawana philosophical background ya hilo swali (Alilouliza Kiranga hapo juu)
"Je Mungu anaweza kuumba ulimwengu usio na mabaya?"
Hapa Kiranga anarejea "Logical Problem Of Evil" kwenye falsafa, kama ungeisoma hii hoja ungejijibu baadhi ya maswali uliyojiuliza mwenyewe.
Hoja yako ni kwamba, kwakua huwezi fikiria (kwa kutumia akili yako ya kibinadamu) au kuvuta picha ya ulimwengu usio na mabaya.
Basi unahitimisha kuwa kwakua haiwezekani kuufikiria (comprehend) ulimwengu wa namna hiyo, basi ulimwengu wa namna hio hauwezekani kuwepo, hivyo huu tulionao ni ulimwengu bora zaidi unaowezekana.
Hitimisho lako ni "total nonsense", huwezi kufikiria au kubuni ulimwengu usio na mabaya kwa sababu wewe sio mwenye "Maarifa yote", wewe sio mwenye "Nguvu zote" na wewe sio mwenye "Upendo wote"
Msingi wa hii hoja ni kwamba, kama kuna kiumbe (au vyovyote utakavyopenda kukiita) chenye hizo sifa tatu (Maarifa yote, Nguvu zote, Upendo wote) na kikataka kuumba ulimwengu, basi hitimisho pekee la kimantiki ni kwamba, "Kingeumbaa ulimwengu usio na mabaya",
kwa sababu tofauti na wewe, kinauweza wa ku "comprehend", "plan", "design", "desire" na nguvu ya ku "create" ulimwengu wa namna hio.
Huwezi kataa hilo hitimisho hapo juu bila angalau kukataa sifa mojawapo ya huyo kiumbe kati ya "Maarifa yote", mfano wenda hajui jinsi ya kuumba huo ulimwengu, ila alitaka na nguvu alikua nazo,
au "Nguvu zote", mfano wenda alikua anajua jinsi gani ya kuumba, na alitaka ila hakua na nguvu za kutosha,
au "Upendo wote" mfano alikua anajua, na alikua na nguvu ya kuumba pia ila hakua na upendo wa kutosha kufanya hivyo
Sasa wewe unakataa sifa ipi kati ya hizo?
Huwezi elezea kwanini Mungu wako (mwenye sifa hizo tatu by definition) aliumba ulimwengu wa namna hii bila angalau kukataa sifa mojawapo kati ya zile tatu, otherwise hatutakua na mjadala wowote wenye maana.
Usilete hoja ya "Freewill" ya kuwa Mungu aliumba ulimwengu usio na mabaya ila akampa binadamu maamuzi binafsi, then binadamu akatumia hayo maamuzi binafsi kuleta maovu
Huo utetezi haujibu hilo swali, kwasababu kuu mbili za haraka haraka
1. Sio kila maovu yanasababishwa na maamuzi ya binadamu, Tsunami, Mafuriko, Magonjwa, Matetemeko ya ardhi n.k
Baadhi ya uovu upo ndani ya DNA zetu, kitu ambacho kipo nje ya utashi wetu, hisia kama chuki, hasira, wivu, tamaa
Hivi sio vitu "unavyoamua" kuwa au kutokua navyo, mtoto mdogo anazaliwa navyo vyote, na kama huamini kwenye Evolution, hizi hisia ni useless na hazina maana yoyote kwenye Creationism.
Fikiria maisha ya mwituni, angalia jinsi gani viumbe vinavyoishi kwa "kulana", Simba haamui "kumla au kutomla swala mwenye mimba", huo ukatili upo kwenye DNA yake.
2. Hakuna Freewill kwenye ulimwengu wa Mungu anayepanga kila kitu kabla, Je Mungu "alishangaa" shetani alipoasi? au alijua kabla? kama alijua kwanini aliumba malaika mwenye mbegu ya uasi?
Unaweza toa utetezi kuwa Mungu anasababu yake nzuri tusiyoijua ya kuumba ulimwengu wa namna hii, lakini swali litakuja, kama hatuijui hio sababu, tumejua vipi ni nzuri? (The greater good argument)
So awali la "Kwanini Mungu aliumba dunia yenye mabaya" ni swali lililoshindikana.
Asante sana. Bora wewe umeisoma na kuielewa "Problem of Evil".
Hapa watu wengi ninaojibizana nao hawajaisoma, na nikijaribu kuwaelewesha kwa falsafa wanajibu kwa ubishi wa imani zao za kidini, bila hata kujifunza kitu katika falsafa.
That is very disappointing.