Stendi ya Nyegezi Mwanza kulazimishwa Kubaki Nyegezi Badala Ya Kuhamishiwa Usagara "Ni Kosa Jingine la Mipango Miji na Siasa"

Tatizo sio kupatika kwa kiwanja vipi kuhusu fidia?? Umewaza hilo ..pia stand ikipelekwa usagara ....hakutakuwa na maaana maana ni mbali na mji.

Halafu kurudishwa pale pia ni kufanya jini lipendeze kama ilivyo ubungo kwa dar , Msamvu kwa Moro.

Habari za kuhamisha hamisha stand zimepitwa na wakati
 
Kingine mwambie stendi siyo ya jiji ni ya mkoa wa mwanza
Chief Mwanza inakua kwa kasi sana Usagara soon itakua ndani ya jiji na hata miji mingine iliyopo kandokando kama kisesa hata mpaka Magu hivyo Mipango miji wanatakiwa wewe na broad vision plan ya miaka hata angarau 50 years to come.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KANYEGELO,
Eti bwana. Yaani ukienda nchi za ulaya stendi ziko katikati kabisa ya miji. Halafu sisi tunataka tuziweke nje.
 
Eti bwana. Yaani ukienda nchi za ulaya stendi ziko katikati kabisa ya miji. Halafu sisi tunataka tuziweke nje.
Kuna watu Mimi siwaelewi kabisa wanataka stendi ijengwe usagara, sgr station ijengwe fela, ukiwauliza szbabu eti foleni, mfano mzuri kwa sasa stendi iko nyegezi je foleni kubwa iko wapi, jibu ni Kati mza mjini na nyegezi sehemu ambako basi hazipiti, watu wakisikia kupanua mji sio huduma zote zinatoka katikati ya mji, miji ya ulaya stendi ziko mjini na ndio maana hukuti guest house maeneo ya stendi, kwetu wanataka stendi iwe usagara kwa szbabu binafsi,, mwingine anataka aweke guest house au kirestaurant nia ni kuwakamua wasafiri na si kuwasaidia,
 
Ngokongosha,

Nakubaliana nawewe. Hakuna kitu kibaya kama kufikia stendi ya mbali na mji, halafu unaanza kubanana kwenye vidaladala na mizigo yako kutafuta mji ulipo. Stendi zote mabasi na station za reli Ulaya ziko mjini kati. Hao planners wetu hawajifunzi tu?Mbona wengine wamesomea huko lakini? Hivi unajua hata ile stendi ya Msamvu kuna watu walikuwa wameshapanga ihamishiwe huko Mvomero?
 
Mmhhhh mbona makubwa haya , nan aende mvomero sasa?
 
Ukweli ni huu;
Issue ya umbali haikua na mashiko, stand ya jiji tanga ilienda kujengwa Kange unajua umbali wa kange na Tanga mjini?

Ubungo ilikua Kisutu, umbali wa kisutu na ubungo unajua? Na sasa hivi inaenda mbezi mwisho huko.

Kibaha ilihamishwa ikaenda kule nje ya mji.

Hapo walivutana kwakua itaenda misungwi hivyo mapato yote watayakosa! Hii ndio sababu kuu!

Pamoja na hivyo, viongozi wa juu wa Kitaifa hawakuwa wanakubaliana ijengwe hapo nyegezi kutokana na mbanano ila kuna watu wakalazimisha!
 
Ngokongosha,

Nakubaliana nawewe. Hakuna kitu kibaya kama kufikia stendi ya mbali na mji, halafu unaanza kubanana kwenye vidaladala na mizigo yako kutafuta mji ulipo. Stendi zote mabasi na station za reli Ulaya ziko mjini kati. Hao planners wetu hawajifunzi tu?Mbona wengine wamesomea huko lakini? Hivi unajua hata ile stendi ya Msamvu kuna watu walikuwa wameshapanga ihamishiwe huko Mvomero?

Planner wetu hawafanyagi realistic projection au wanafanya ila wanasiasa wanaingilia na kuvuruga!

Kunakua hakuna eneo katikati ya mji lililoachwa kubwa kwa ajili ya stand ikipanuliwa in future, by the time tunapata pesa za mradi inakua hakuna option zaidi ya nje ya mji.

Hao hao wanasiasa wanalazimisha kwa kusema “itasaidia ukuaji wa mji” ipelekwe nje kabisa!
 
Alafu nasikia mwisho wa reli utakuwa usagara afu kituo cha bus nyegezi haileti concert
 
Mzee wa Petro Station Usagara hujambo!
Ni kweli unachosema, ingawa miji inaweza kuamua vinginevyo ndani ya miaka 5-10 ijayo.
Ili maisha yaendelee Stand mpya Nyegezi kwa baadae inaweza kubadilishwa kuwa ni ya daladala alafu stand kuu ya mabasi ikapelekwa Ukirugulu.
Mipango tofauti na kuangalia mambo mengine lakini ni wajibu pia kuangalia na usalama wa Wasafiri/miundombinu/kulala/kula n.k
Vuta subra Nyamsusa usijali kwa sasa fikiria uwekezaji Ukirugulu, Misungwi, na Misasi.
 
Hv mwendazake kenda na mipango yake kwani nini kinacho endelea kwa sasa hapo Nyegezi
 
Back
Top Bottom