Nyamsusa JB
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 568
- 1,562
Habari Wanabodi.
Kuna kinachoendelea hapa Mwanza katika Mradi wa Ujenzi wa Stendi Mpya Kubwa na ya Kisasa Nyegezi Stendi hakika ni Makosa mengine Makubwa ya Kimpango Miji na Taaluma Yake..
Kama inavyo Fahamika kua Mwanza ni kati ya Majiji yanayokua kwa kasi sana Africa na hivyo Kuhitaji Mpango Miji Madhubuti ili kuondoa Misongamano Isiyokua ya Lazima ya Watu na Magari hapo baadae.
Awari ili kuanza kudhibiti Hali hii ya Msongamano kulikua na Mipango ya Kuzihamisha Stendi Kuu Mbili za Jijini Mwanza yaani Stendi ya Buzuruga na Stendi ya Nyegezi na kuzipeleka nje kidogo ya Jiji.
Ambapo stendi ya Buzuruga ingehamishiwa Kisesa ( Hii haina shida kwani mpango wake bado upo palepale)
Shida inakuja hapa kwenye hii Standi ya Nyegezi ambayo ndio stendi kubwa kabisa kwa hapa Mwanza kuendelea kulazimishwa kubaki hapa Nyegezi japo kiuharisia hii Sehemu imekua ndogo sana kuhudumu kama Stendi Kuu ya Mwanza.
Ili Kuipanua Stendi Hii Serikali itahitaji Bilioni nyingi za fedha kama Fidia kwa kulipia mejengo mbalimba ambayo yamejengwa kuizunguka Stendi.
Lakini pia hata Ikilazimishwa Kupanuliwa bado haitaweza kupata Eneo kubwa la Kukidhi Mahitaji yatakayotekea Miaka Miwili baadae.
Pia Hatua hii ya Kuipanua Stendi hii ya Nyengezi haitalisaidia Jiji la Mwanza kuanza kudhibiti Msongamano wa Magari na Watu mapema iwezekanavyo kabla Tatizo la Msongamano halijawa kubwa kama katika Majiji mengine Africa.
Stendi hii ya Nyegezi ilikua Ihamishiwe Usagara ambapo bado kuna Maeneo ya Mashamba ambapo Fidia yake ingekua ndogo sana kulinganisha na Mabilioni ya Kufidia Majengo Nyengezi.
Faida Nyingine ya kuhamishia Stendi Usagara ingekua ni Upatikanaji wa Eneo kubwa kabisa kwa Ujenzi wa Stendi Kubwa Kabisa na ya Kisasa ambayo Ingehudumu kwa Miongo kadhaa tofauti na Stendi kuwepo Nyegezi.
Pia kwa Jiografia ya Usagara ni Sehemu Muafaka kwa Stendi kubwa ya Mkoa kwani ipo njia Panda, Hapa kuna Njia Kuu Kuelekea Mkoa wa Geita, Shinyanga na hata Mkoa wa Mara via Usagara to Kisesa Road. Ni Njia Panda Muafaka kabisa kwa Abiria Kufanya Connection Kirahisi.
Faida nyingine Ilikua ni Kudhibiti Msongamano wa Mabasi na Maroli kwani Ujengwaji wa Standi Usagara ungesababisha Mabasi yote yasipite au kufika Katikati ya Jiji na hivyo kupunguza Msongamano wa Watu.
Lakini pia Ujenzi wa Stendi ungefanyika Usagara ungeongeza Kasi ya Upanuaji wa Jiji kua kubwa zaidi na Miradi mingi ingeanzishwa Usagara tofauti na Stendi kubaki Nyegezi ambapo kwa sasa ni Pafinyu kwa Maendeleo Mapya.
Sababu Kubwa inayosemekana na kusababisha Kung'ang'ania Stendi ya Nyengezi kulazimishwa kubaki hapo ilipo ni Hofu ya Halimashauri ya Nyamagana kupoteza Mapato kutokana kwamba Usagara ipo Wilaya Nyingine ya Halimashauri ya Misungwi.
Sababu Nyingine kuna Tetesi kua Matajiri walio wekeza Mahotel na Vituo vya Mafuta wamecheza Rafu ili kushinikiza Jiji, Stendi hii ya Nyegezi ibaki hapo ilipo japo ni wazi kua Eneo Hilo halina Sifa wala Uwezo wa kubeba Stendi kubwa na ya Kisasa kwa wakati huu.
Sababu Nyingine ni ya Kisiasa na Hofu alioyonayo Mbunge wa sasa wa Jimbo la Nyamagana kupoteza Kula kama hatofanya jitihada za kuzuia kuhamishwa kwa Stendi hii.
Hitimisho.
Naliomba Jiji na Utawala wa Mkoa wa Mwanza liangalie zaidi Faida na Hasara za Sasa na za Baadae za Kung'ang'aniza Stedi hii Nyengezi Kubaki Nyegezi Na Walinganishe na Faida zitakazopatikana Sasa na Baadae kwa Stedi Hiyo Kuhamishiwa Usagara kama ilivyo kwa Stendi ya Buzuruga Kuhamishiwa Kisesa.
Sababu za Kitaalamu na Gharama kwa Serikali zizingatiwe zaidi kuliko hizo sababu za Mapato ya Kiwilaya, Siasa na Watu Binafsi.
Atakae weza Aufikishe Uzi Huu kwa Serikali Kuu au hata Kwa Magufuli Ili Mwanza ipate Kupona Dhidi ya Msongamano Unaokuja Mbeleni.