Stendi Kuu Bukoba ni aibu tupu

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Nani aliwaroga Wahaya? Inawezeka aliyewaroga alikufa na ndumba zake, ni lini Kagera itarudisha heshima ya NSHOMILE?

Hii ni stendi kuu ya Bukoba. Kwa sasa hali iko ivi ukiingia stendi inabidi ununue mabutusi uvue viatu alafu ukunje nguo yako kwa chini ndio uingie stendi kuu.

Niaibu kwa Wahaya, niaibu kwa Serkali niaibu kwa CCM.

CHADEMA walionesha njia wakaanza kujenga stendi kuu Kyakairabwa lakini sasa ivi tayari CCM wameanza figisu hawataki kumalizia stendi ile kisa ilianzishwa na Baraza chini ya CHADEMA.

Wahaya popote mlipo pazeni sauti mpaka Rais asikie tuondoe matope katikati ya mji ambao ndiyo lango kuu la Kagera.

Nimeambatanisha mchoro wa stendi inayotelekezwa na awa wasaka tonge

Wasomi wetu tafadhali rudi nyumbani tujenge stendi kuu tuondokane na aibu hii.View attachment 1775058View attachment 1775057View attachment 1775056

FB_IMG_1619767549377.jpg

Mchoro wa stendi inayotelekezwa
 
Huko kwa nshomile' niliwahi fika pale stendi, sikuamini macho yangu, kwamba ndio wale jamaa wanaotishia huku mikoa mingine na suti zao. Jamani kumbukeni nyumbani nyie jamaa. Kweli ni aibu aisee.
 
Nafikiri stend ya manispaa ya mkoa Wa Kagera ndo mbovu kuliko mikoa yote Tanzania.

Bukoba tumezidiwa hata Mtwara.

ndo ukweli huo. Bukoba mjini umepambwa na majengo ya miaka tangu ukoloni.

Wahaya hatupendagi kujenga nyumbani kwasababu uchawi ni mwingi yawezekana.

Lakini ukitukuta Darsalama dah tunaendesha Mahama, n.k
Wamejenga huko migombani vijijini mwao kuna mijengo mizuri sana.

Stendi ni mradi wa serikali si wa mwananchi mmoja mmoja. Hata huko kwenye stendi nzuri kama Mbezi, Msamvu, Singida kote zimejengwa na serikali na wananchi kuchangishana na kujenga kwa sababu tu ni wazawa wa huko.
 
Hiyo sio stendi ni kama kijiwe fulani hivi ila yawezekana ni mtaji wa mabwana flan ....make nahisi huwa wanatoza kila gari inayoingia ndani
 
Alaumiwe jiwe tu. Hata mradi wa Omukajunguti wa Tibaijuka wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa, ulihamishiwa Chato.
 
Hiyo sio stendi ni kama kijiwe fulani hivi ila yawezekana ni mtaji wa mabwana flan ....make nahisi huwa wanatoza kila gari inayoingia ndani
Haha, niliwahi kupanda Basi pale njiapanda ya Bwanga, basi lilikuwa ninatoka Dar kwenda Bukoba na watani zangu walikuwa wamevaa makoti utadhani maafisa wa ikulu, wanaongea kilugha tu. Kilichonishangaza, ndani ya Basi walining'iniza mikate ya Bongo. Sasa sikujua, inamaana walikokuwa wanaenda mikate ilikuwa haipo??? Hahahaha wataniii.
 
Back
Top Bottom