State Capture and Treason in Tanzania & Tanganyika -The Port Saga

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,033
3,916
Habari za Wakati huu;

Nimepitia hukumu ya kesi ya IGA ambayo imetolewa na mahakama kuu kanda ya Mbeya.

Nimetafakari kwa uchache tu namna ambavyo hukumu hii imeandikwa. Kwanza nimejikuta najiuliza hivi Mahakimu hawa ndio walioandika hii hukumu au hii hukumu iliandikwa na DPW kisha wakatumiwa waisome?

Kwanza kabisa hukumu kwa ujumla wakili inakubaliana na Ukweli kwamba MKATABA wa DPW ni BATILI. Ila katika hukumu wamejivua uwajibikaji.

kinachoendelea sasa hivi hapa TANZANIA ni kitu kinaitwa STATE CAPTURE-Utekaji wa Nchi.Kwa nini ninasema ni State Capture? Hizi ndio sababu:
  1. Kwanza Sheria kadhaa zimerekebishwa katikamrengo wa kutaka kujenga mazingira ya kulinda maslahi ya DPW
  2. Pili tunaona namna ambavyo mahakama yetu imeshindwa kutimiza wajibu wa kisheria na kikatiba na kubaki na kigugumizi
  3. Tatu tuliona namna Bunge lilivyoendesha Mchakato wa kupitisha na hasa kwa kuzingatia kwamba mkataba huu ulikuja Bungeni kwa kuchelewa na kwa kimya
  4. Nne Tunaona namna ambavyo viongozi wa serikali akiwamo Rais SSH wanavohangaika kuutetea huu mkataba ambao kimsingi hauna maslahi na watanzania
Sasa tufanyeje?
  1. Kwanza kabisa Niwaalike Watanganyika POPOTE pale walipo washiriki katika kupinga jambo hili kwa kadiri ya nafasi na uwezo wao
  2. Pili Tanganyika na Watanganyika wote tutambue kwamba Watoto wetu watakuja kutulaumu na kutulaani
  3. Mwisho kwa wale ambao wanazo nafasi za kuhamasisha tuhamasishane sasa tuangalie namna ya kufanya Demonstration za kitaifa katika kila Mkoa,KIla Wilaya,Kila Mtaa na kila kijiji pamoja na wake zetu na watoto na marafiki tuandamane kwa pamoja kutetea Nchi yetu,Tanganyika yetu na Rasilimali zetu.
  4. Huu ni wito wangu Binafsi,Na mimi Tayari hapa nilipo ninajiandaa kwenda Dodoma kwa ajili ya Kuanza Maandamano Ampapo natarajia kufika Dodoma Tarehe 16 August.Nitaanza Maandamano hayo kutokea Dar es Salaam.Kwa yeyote ambaye yuko Tayari kushiriki anzia Popote Pale Ulipo Tukutane Dodoma Kuanzia Tarehe 16 August.
Karibuni kwa Mjadala zaidi.

Tunataka Tanhanyika yetu na tunataka Serikali isikie sauti ya Wananchi.
 
Niliwaelewa sana cdm kutokwenda mahakamani baada ya dhalimu kupora uchaguzi wa 2020.

Na pia najua ni kwanini wazungu hawako tayari migogoro yao kuamuliwa kesi zao kwenye hizi mahakama kibogoyo.

Machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatarejesha heshima ya mifumo yetu ya kiutawala.
 
Kwanza Sheria kadhaa zimerekebishwa katikamrengo wa kutaka kujenga mazingira ya kulinda maslahi ya DPW
Ni vizuri ukazitaja hizo sheria ziluzorekebishwa, zilirekebishwa lini na vifungu vilivyokuwepo na sasa ni vifungu gani vimewekwa badala yake.
Pili tunaona namna ambavyo mahakama yetu imeshindwa kutimiza wajibu wa kisheria na kikatiba na kubaki na kigugumizi
Mahakama inafanyakazi kwa kuzingatia sheuria na haiangalii matakwa ya ubongokid.

Tatu tuliona namna Bunge lilivyoendesha Mchakato wa kupitisha na hasa kwa kuzingatia kwamba mkataba huu ulikuja Bungeni kwa kuchelewa na kwa kimya
Bunge linatekeleza wajibu bila kuingiliwa, na ndivyo lilivyofanya
 
Ni vizuri ukazitaja hizo sheria ziluzorekebishwa, zilirekebishwa lini na vifungu vilivyokuwepo na sasa ni vifungu gani vimewekwa badala yake.

Mahakama inafanyakazi kwa kuzingatia sheuria na haiangalii matakwa ya ubongokid.

Bunge linatekeleza wajibu bila kuingiliwa, na ndivyo lilivyofanya
Unataka jibu/unahoji/unapinga?
 
Ni vizuri ukazitaja hizo sheria ziluzorekebishwa, zilirekebishwa lini na vifungu vilivyokuwepo na sasa ni vifungu gani vimewekwa badala yake.

Mahakama inafanyakazi kwa kuzingatia sheuria na haiangalii matakwa ya ubongokid.

Bunge linatekeleza wajibu bila kuingiliwa, na ndivyo lilivyofanya
Acha ujinga ndugu yangu. Tanzania hatuna bunge, kama unaelewa maana ya bunge.
 
Huu mkataba watanzania wengi walikataa naposema watanzania wa pande zote mbili bara na visiwani, binafsi nimekutana na wananchi wa kawaida wa visiwani wanasema wazi huu muungano unavunjika sababu ya swala la bandari . Hii inaonyesha tatizo la muungano kwa upande wa Zanzibar lipo Kwa viongozi na sio wananchi wa kawaida.

Hili jambo kilikuwa linatuunganisha site bila kujali dini, kabila au misimamo ya vyama ila Kuna watu Kwa kutaka umaarufu walilivuruga,walilivurugaje?

Maandamano yalitakiwa yafanyike nchi nzima hasa maeneo yaliyoathirika na mikataba. Lakini Kuna watu waliandaa maandamano Kwa kurupuka ndio maana mwitikio ilikuwa Mdogo kama maandamano yangeandaliwa vizuri yangepata sapoti kubwa maana hata hao polisi wanaupinga huu mkataba.

Hata kesi iliyofunguliwa ilifunguliwa Kwa haraka ndio maana baadae wakawa wanaomba michango inaonyesha hawakujiandaa. Mkataba wa Do world unagusa sehemu nyingi ikiwemo ardhi hivyo lilitakiwa jopo la wanasheria wabobezi wa ardhi kama Shivji, wenye utaalamu wa uwekezaji kama Nshala na nyanja nyingine lazima serikali ingebanwa tu wasingepata pa kitokea.
 
ZIMWI WALILOLITENGENEZA 2017 WALITAFUTIA DAWA AGOSTI 2023

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
Simu: +255 026 23222761-5
Fax No. +255 026 2322624
E-mail: cna@bunge.go.tz
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli,
DODOMA

TAARIFA KWA UMMA
_________
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepanga kuujadili MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 2
WA MWAKA 2023 [THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS)(NO.2)
BILL, 2023].

Katika kutekeleza jukumu hilo, kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023, Kamati itasikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya Jumatano tarehe 16 Agosti, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Frank Mfundo, Ghorofa ya 5 Jengo la Utawala, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.

Kamati inawaalika wadau wote wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao. Aidha, maoni yanaweza kutumwa kwa njia ya posta au Barua pepe kwa anuani zifuatazo: -

Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli,
DODOMA.

Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz

Muswada huo unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge: parliament.go.tz/bills-list
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA.
7 Agosti, 2023.

Bunge kukumbana na ruhani walilolitengeneza mwaka 2017

Sheria ya Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya mwaka 2017
1691673607133.png

Bunge limepitisha Miswada ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi ya mwaka 2017.

Miswada hiyo iliyoletwa Bungeni kwa Hati ya Dharura iliwasilishwa Bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi na kujadiliwa kwa siku moja.

Kabla ya kuwasilishwa Bungeni Miswada ya Sheria hizo ilijadiliwa na Kamati ya Bunge ya Pamoja huku wadau mbalimbali wakipata fursa ya kutoa maoni yao.

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa Sheria hizo, Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema Bunge limeshafanya kazi yake kwa miswada hiyo kwa hatua zake zote na kwamba kilichobaki ni kupelekwa kwa Mheshimiwa Rais ili iweze iliweze kusainiwa kwa mujibu wa Ibara ya 97 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

“Niwapongeze sana Wabunge mliofanya kazi bila kuchoka,pongezi kwa Kamati ya Pamoja ya Bunge,Chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Doto Biteko, Miswada ilipelekwa kwenye Kamati Nne, jambo ambalo katika Bunge la 11 ni mara ya kwanza, zaidi ya Wabunge 100 waliipitia kifungu kwa kifungu na hatua kwa hatua,” alisema.

Mheshimiwa Spika pia aliwapongeza wadau wote waliofika Bungeni Dodoma kwa ajili kutoa maoni yao yaliyosaidia kuboresha muswada hiyo.

“Naipongeza pia Serikali na kipekee Mheshimiwa Kabudi kwa ushiriki wake mkubwa katika jambo hili, jinsi ambavyo yeye na timu yake wamefanya kazi usiku na mchana,” alisema

“Kuna maeneo ambayo Serikali ilileta Jedwali la Marekebisho maana yake ni kwamba imeyakubali maoni yaliyotolewa na imeboresha hii ni ‘spirit’ nzuri kwa Serikali, tunaipongeza kwa kukubali kuwasikiliza Wabunge na Wadau,” aliongeza Spika

Aidha, alisema Miswada hiyo miwili imeliingiza Bunge la 11 katika hisrtoria ya kipekee na kwamba kama spika wa Bunge anajisikia faraja kwa kuingia katika historia hiyo mpya ya kuangalia maliasili ya nchi kwa kuweka sheria ya Watanzania kuimiliki na kuweka taratibu za mikataba zilizopigiwa kelele kwa muda mrefu.

“Hatua hii ni kubwa tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kama tukiona kuna matatizo, Serikali ipo na sisi Wabunge tupo,tutakaa na kuona jinsi ya kuweka vizuri zaidi,” alisema.
 
huu mkataba watanzania wengi walikataa naposema watanzania wa pande zote mbili bara na visiwani, binafsi nimekutana na wananchi wa kawaida wa visiwani wanasema wazi huu muungano unavunjika sababu ya swala la bandari . Hii inaonyesha tatizo la muungano kwa upande wa Zanzibar lipo Kwa viongozi na sio wananchi wa kawaida.
Hili jambo kilikuwa linatuunganisha site bila kujali dini, kabila au misimamo ya vyama ila Kuna watu Kwa kutaka umaarufu walilivuruga,walilivurugaje?
Maandamano yalitakiwa yafanyike nchi nzima hasa maeneo yaliyoathirika na mikataba. Lakini Kuna watu waliandaa maandamano Kwa kurupuka ndio maana mwitikio ilikuwa Mdogo kama maandamano yangeandaliwa vizuri yangepata sapoti kubwa maana hata hao polisi wanaupinga huu mkataba.
Hata kesi iliyofunguliwa ilifunguliwa Kwa haraka ndio maana baadae wakawa wanaomba michango inaonyesha hawakujiandaa. Mkataba wa Do world unagusa sehemu nyingi ikiwemo ardhi hivyo lilitakiwa jopo la wanasheria wabobezi wa ardhi kama Shivji, wenye utaalamu wa uwekezaji kama Nshala na nyanja nyingine lazima serikali ingebanwa tu wasingepata pa kitokea.
Kwa hizi mahakama wewe sahau, Jaji anasubiri promotion kutoka kwa mshitakiwa, tubadili kwanza upatikanaji wa majaji
 
TUNAKWENDA MAHAKAMA YA RUFAA

Judgement: Soma kurasa zote 91 ya kesi hii ya kikatiba .....

In the upshot of all this we find this, petition barren of fruits.
Accordingly, the same is hereby dismissed. Since this is a public interest matter, we do not find any justification for granting of costs. We, therefore, make no order as to costs.

Order accordingly.

DATED at MBEYA this 10th August, 2023.

DUNSTAN B. NDUNGURU
JUDGE
10/08/2023

MUSTAFA K. ISMAIL
JUDGE
10/08/2023

ABDI S. KAGOMBA
JUDGE
10/08/2023
Page 91

Endelea kusoma kurasa zone 91 za judgement hii : source :

N.B
Wachambuzi wameona kuwa

Maoni : MTEGO KWA KIKAO CHA BUNGE AGOSTI 2023

Kufuatia maamuzi yaliomo ndani ya hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mjini Mbeya, Tanzania

Sasa mpira umerudishwa bungeni kuona kama vifungu vilivyokiukwa vya sovereignty ya Tanzania zitatetewa visibadilishwe au vitabadilishwa ili uwekezaji wa Dubai kupitia DP World ufanikiwe.

Bunge la Marekani walipinga uwekezaji wa DP World nchini Marekani mbali ya kutetewa sana na viongozi wa utawala waliokuwa White House wakati huo.

Tukumbuke bunge la Muungano wa Tanzania kizalendo lilijadili muswada wa sheria mpya 30 Juni, 2017

Bunge laongeza Siku ili kuchambua Miswada mitatu ya Sheria za Ulinzi wa Rasilimali za Taifa​

Bunge limeongeza siku za Mkutano wa Saba hadi tarehe 05 Julai 2017, ili kupitia Miswada mitatu ya sheria inayohusu marekebisho ya Sheria za Madini na ulinzi wa rasilimali za Taifa.
Akitoa maelezo Bungeni, Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alisema kuwa Kamati ya Uongozi ilikutana tarehe 28 Juni, 2017 Jioni, ili kufanya marekebisho ya Ratiba ya Mkutano wa saba Bunge ambao ulitarajiwa kuisha tarehe 30 Juni, 2017 na kukubaliana kuongeza siku tatu za kazi hadi tarehe 5 Julai, 2017 ili kuliwezesha Bunge kupitia Miswada hiyo.
Kufuatia uamuzi huo Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa ameunda Kamati ya pamoja itakayopitia Miswada miwili ambayo tayari imeshasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni. Miswada hiyo ni; Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms)] Bill, 2017];(iii)Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permmanent Sovereignty)] Bill, 2017].
Mhe Spika alisema kuwa Kamati hiyo ya pamoja itakayochambua miswada hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe Dotto Biteko na itajumuisha Wajumbe wa Kamati nne za Bunge ambazo ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya Sheria Ndogo.

Aidha kwa upande mwingine Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati ya Katiba na Sheria chini ya Uenyekiti wa Mhe Mohamed Omary Mchengerwa itauchambua Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017]

Na sasa miaka mitano baadaye yaani 2023 bunge hili linaona sheria hiyo ya mwaka 2017 inahitaji mabadiliko hivyo kualika wadau wakitazamia mwezi Agosti 2023 wataifanyia mabadiliko ili kuwezesha uwekezaji.
 
Niliwaelewa sana cdm kutokwenda mahakamani baada ya dhalimu kupora uchaguzi wa 2020.

Na pia najua ni kwanini wazungu hawako tayari migogoro yao kuamuliwa kesi zao kwenye hizi mahakama kibogoyo.

Machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatarejesha heshima ya mifumo yetu ya kiutawala.
Wewe ni mafi kbs endelea kila mema huku ukimlaumu marehemu
 
Habari za Wakati huu;

Nimepitia hukumu ya kesi ya IGA ambayo imetolewa na mahakama kuu kanda ya Mbeya.

Nimetafakari kwa uchache tu namna ambavyo hukumu hii imeandikwa. Kwanza nimejikuta najiuliza hivi Mahakimu hawa ndio walioandika hii hukumu au hii hukumu iliandikwa na DPW kisha wakatumiwa waisome?

Kwanza kabisa hukumu kwa ujumla wakili inakubaliana na Ukweli kwamba MKATABA wa DPW ni BATILI. Ila katika hukumu wamejivua uwajibikaji.

kinachoendelea sasa hivi hapa TANZANIA ni kitu kinaitwa STATE CAPTURE-Utekaji wa Nchi.Kwa nini ninasema ni State Capture? Hizi ndio sababu:
  1. Kwanza Sheria kadhaa zimerekebishwa katikamrengo wa kutaka kujenga mazingira ya kulinda maslahi ya DPW
  2. Pili tunaona namna ambavyo mahakama yetu imeshindwa kutimiza wajibu wa kisheria na kikatiba na kubaki na kigugumizi
  3. Tatu tuliona namna Bunge lilivyoendesha Mchakato wa kupitisha na hasa kwa kuzingatia kwamba mkataba huu ulikuja Bungeni kwa kuchelewa na kwa kimya
  4. Nne Tunaona namna ambavyo viongozi wa serikali akiwamo Rais SSH wanavohangaika kuutetea huu mkataba ambao kimsingi hauna maslahi na watanzania
Sasa tufanyeje?
  1. Kwanza kabisa Niwaalike Watanganyika POPOTE pale walipo washiriki katika kupinga jambo hili kwa kadiri ya nafasi na uwezo wao
  2. Pili Tanganyika na Watanganyika wote tutambue kwamba Watoto wetu watakuja kutulaumu na kutulaani
  3. Mwisho kwa wale ambao wanazo nafasi za kuhamasisha tuhamasishane sasa tuangalie namna ya kufanya Demonstration za kitaifa katika kila Mkoa,KIla Wilaya,Kila Mtaa na kila kijiji pamoja na wake zetu na watoto na marafiki tuandamane kwa pamoja kutetea Nchi yetu,Tanganyika yetu na Rasilimali zetu.
  4. Huu ni wito wangu Binafsi,Na mimi Tayari hapa nilipo ninajiandaa kwenda Dodoma kwa ajili ya Kuanza Maandamano Ampapo natarajia kufika Dodoma Tarehe 16 August.Nitaanza Maandamano hayo kutokea Dar es Salaam.Kwa yeyote ambaye yuko Tayari kushiriki anzia Popote Pale Ulipo Tukutane Dodoma Kuanzia Tarehe 16 August.
Karibuni kwa Mjadala zaidi.

Tunataka Tanhanyika yetu na tunataka Serikali isikie sauti ya Wananchi.
Mmeshindwa huko mahakamani na huku kwenye siasa za mtaani mjiandae pia kushindwa. Ni masuala mepesi kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom