Nimebaini: Siku hizi watu hawatumii tena jina Tanzania bali wanatumia Tanganyika

Exorcist

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
1,236
1,257
Kuna trend nimeona hivi karibuni ambapo watu wameacha kabisa kutumia jina la Tanzania, na kwa sasa wanatumia TANGANYIKA kama mbadala.

Je, ni kwanini Tanganyika imechelewa kutumia mfumo huu ambao wale wa Tanzania visiwani wamekuwa wakitumia miaka yote? Nini hasa kilisababisha watanganyika kuona haya kutumia jina lao, ila wale wa Tanzania visiwani wamekuwa wakitumia jina lao bila haya?

Hali hii imekuwa dhahiri zaidi hasa katika kipindi hiki ambapo viongozi kutoka Tanzania visiwani wameamua kwa makusudi na bila aibu kuiingiza Tanganyika kwenye mkataba wa kitumwa na kimangungo , bila haya kabisa. Hao si wengine bali ni Samia Suluhu, Makame Mbarawa na Jopo lake la wala urojo.

Inaumiza sana, na hoja kuu zinazohitaji majibu kuhusu uuzwaji huu wa Tanganyika ni hizi...

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Haina maana yoyote na ni kama kujifariji tu kutumia neno TANGANYIKA ilihali wanajua hakuna hiko kitu na hakitakuwepo milele. Ndio maana wazungu wanatuona wajinga tusiotumia akili, wenyewe waliotupatia uhuru wanajua ni watanzania na huku hawakuipatia uhuru nchi ya Tanzania.
 
imeonekana Tanganyika inatolewa kafara zaidi kuliko pacha wake kwenye maswala ya kudalaliwa.
 
You must be crazy and hopeless, Mwingereza aliacha Tanzania?
Wewe ndio mjinga usiyetumia akili. Muingereza aliipatia uhuru Tanganyika lakini hao waingereza hawatuiti watanganyika ila watanzania Kwa sababu Gani? Kwa sababu wanajua Tanganyika is no more and there will be no more Tanganyika other than Tanzania ila Kwa akili zenu mnashikilia mambo yasiyobadilika. Mnateseka Bure Kwa sababu HAKUNA YEYOTE HATAKAYEWAPA HIYO TANGANYIKA MNAYOIWAZA. HAIPO TENA
 
Anataka ardhi apewe bure,alafu serikali iende ikachukue kodi ya 1% kama kuna kitu kimewekezwa kama hakuna mtu asisogee hapo
 
Haina maana yoyote na ni kama kujifariji tu kutumia neno TANGANYIKA ilihali wanajua hakuna hiko kitu na hakitakuwepo milele. Ndio maana wazungu wanatuona wajinga tusiotumia akili, wenyewe waliotupatia uhuru wanajua ni watanzania na huku hawakuipatia uhuru nchi ya Tanzania.
hakuna jambo ambalo halina mwisho huu ni upotoshaji.kila jambo lina mwisho wake.hata huu muungano utafikia mwisho wake.
 
Wewe ndio mjinga usiyetumia akili. Muingereza aliipatia uhuru Tanganyika lakini hao waingereza hawatuiti watanganyika ila watanzania Kwa sababu Gani? Kwa sababu wanajua Tanganyika is no more and there will be no more Tanganyika other than Tanzania ila Kwa akili zenu mnashikilia mambo yasiyobadilika. Mnateseka Bure Kwa sababu HAKUNA YEYOTE HATAKAYEWAPA HIYO TANGANYIKA MNAYOIWAZA. HAIPO TENA
Point..
 
Back
Top Bottom