Binafsi ni mwanachama Hai wa CCM, naomba nimshauri Nape na viongozi wengine wa kada za juu wa CCM, ni ukweli usiopingika kuwa zaidi ya nusu ya vijana waliopo Tanzania wamehamia au wanaunga mkono upinzani, vijana tuliobaki CCM ni wachache mno.
Ushauri wangu:
Tukiwa tunaelekea kwenye chaguzi za kata na wilaya na badae mkoa na Taifa, vijana wahakikishiwe kutowekewa mizengwe kama ambavyo imekuwa ikitokea hili Nape analifahamu, mfano baadhi ya nafasi kutorusiwa kutokuwa na mawakala kule Dodoma ili uhuni ufanyike, eti ni aibu waziri akigombea na kushindwa hivyo abebwe.
Vinginevyo hata sisi wachache tuliobaki ccm mtatukosa! huu ni ushauri sihitaji Nape atoe majibu ya utetezi