STARTV: Maamuzi ya NEC-CCM kuelekea 2015

*Kwa walio mbali na Tv *Nape anajaribu kufafanua yale maazimio 27 ua CC ya CCM*
 
NAOMBA MUMKATAZE NAPE KUITA CHADEMA KUWA NI WATANI WA CCM.

Kwenye ukombozi wa mali za uma hakuna utani watu wamedhamiria kutokomeza ufisadi na asifananishe wakati wa chama kimoja na sasa.
 
Swali kwa Nape:

Kikundi cha uamsho Zanzibar wanahubiri kuvunja muungano na hawautaki lakini CCM hamtaki kuwapa haki yao ya msingi kuamua juu ya taifa lao kama waendee na Muungano au la. Kwanini msiwape haki yao kama chama kinachotawala?

La Pili; inaonekana sera za CCM zinalenga kuikomoa CHADEMA?

Tatu; napenda kusema CCM inafanya siasa vyuoni mimi ni mwanachuo najua mnachokifanya, ni wazi mnavyowakataza wenzenu wakati nyie mnafanya sio haki

Mwisho: Rais ni wa CCM na baraza la mawaziri ni la CCM iweje nyie viongozi wa CCM mtoe maamuzi huku mkiwa na nguo za kijani wakati huohuo wanaotoa maamuzi hayo ndo hao hao viongozi wa serikali nao wamevaa nguo za kijani?
 
Namuuliza Nape:

1) Mh Nape amekuwa akishtumiwa na baadhi ya Makundi ndani ya CCM kwamba anaifanya ccm kama kampuni yake. Haya yaliwahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari. Jee hili haliwezi kuiyumbisha CCM kuelekea 2015?

2) CCM imebuni mpango wa kutumia vyuo vikuu kama sehemu ya kujijenga kuelekea 2015. Tayari serikali ilitamka wazi kwamba Vyuo vikuu visitumike kisiasa, Jee haoni CCM inaenda kinyume na serikali yake? Pia haoni kwamba mbinu hii mbinu hii inaweza kuleta vurugu vyuoni na kuifanya elimu yetu kushuka endapo kila Chama kitatumia vyuo vikuu kama matawi ya kisiasa?
 
Kumekua na mijadala kuhusu vyama kupewa ruzuku au hapana, wengine tumekua tukipinga vyama vya siasa kupewa ruzuku.

Hoja yetu ni nyepesi, pesa wanazopewa vyama ni zetu kwa sababu zinatokana na kodi, kinachofanyika ni kwamba vyama vinapewa vingine pasipo ridhaa yetu, sasa kodi ifanye kazi za maendeleo, vyama vitoke, vije kwetu na hoja, tukiridhika tutavichangia tusiporidhika tutaviacha vife. hatuhitaji vyama 20 katika nchi!

swali kwa Nape, nini msimamo wake/wao kuhusu ruzukuu kwa vyama vya siasa?
 
Kwa ufafanuzi wa Nape ni kuwa wanataka kuwapa vijana jukwaa la kusemea ndani ya CCM.

Je, unaonaje kuwa ndani ya upinzani wanapewa madaraka? Mfano: Mkosamali, Zitto, Silinde, Mnyika, nk.

Je, ni lini vijana wa chuo watapata nafasi ndani ya CCM kugombea ubunge na kuchaguliwa bila kutumia hela?
 
Muulize Nape,

CCM inatoa mapendekezo kana kwamba haikujua hayo inayopendeza ni mazuri kiasi gani, kwa nini hawakufanya marekebisho ya katiba kuingiza hivyo vifungu wanavyopendekeza na walikuwa na wabunge wengi kipindi chote cha uhai wa taifa letu.
 
Namuuliza Nape: Kwanini anatumia sana huu msemo wa kudai wakikubali mgombea binafsi wapinzani ndio watakaoumia?

Sisi hatutaki kujua ni vyama gani vitakavyofaidika sisi tunataka Tanzania iliyo na neema, inayojali wananchi wake.

Yeye inaonyesha anaiogopa CHADEMA kuliko anavyoogopa mafisadi na wahujumu uchumi. Tunataka watu wanaosema Tanzania kwanza na si CHADEMA wala CCM.
 
Kuna vitu viwili inawezekana Nape hajui ki-ukweli au anafanya makusudi, CCM kimepoteza kabisa mvuto kama chama tawala, inawezekana hukai sana na watu wa kada ya kati na vijana wenzio, fungua macho Nape, huku mtaani mambo yamebadilika sana.
 
Sasa kama suala la mgombea binafsi litawaumiza wapinzani kuliko CCM, nadhani CCM ingeliacha kwa wananchi ili ifaidike na maumivu hayo kwa wapinzani, kuliko kulitolea maoni na kuwekea tahadhari, vinginevyo itaonekana kuwa CCM ndio itapata pigo.
 
CCM kwa sasa ni sawa na meli inayojaribu kuendelea na safari jangwani.

Kimsingi ni chama kilichoifikisha nchi hii katika umasikini mkubwa. Usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi chini ya utawala wa chama hiki umesababisha mali nyingi ya nchi kupotea kwa mikataba mibovu. Tukiachana na usimamizi mbovu wa mali ya nchi,

Swali dogo kwa Nape: Ni kwanini CCM imekuwa ikijipendekeza kwa muungano usio na faida yoyote?
 
Si kweli kwamba mgombea binafsi hatasaidia ama chama tawala au vile vya upinzani. Kuwa na mgombea binafsi ni dalili nzuri kwa ustawi wa demokrasia kwa nchi yetu.

Mimi naomba mambo haya yasije yaka-influence maoni yatakayokusanywa na tume kwani mengi kati ya mambo haya yamo katika masuala ambayo kimsingi yatakuwa yakikusanywa na tume
 
NAPE ni kwanini huwa unatumia propaganda chafu za kukiita CHADEMA ni chama cha kikanda? Hujui kama huo ni uongo kuna watu wengi ambao sio kanda ya kaskazin na wapo CDM, pia tunaomba Nape leo afafanue kwanini anasema CDM ni ya ukanda? Otoe hoja na sio maneno.
 
Back
Top Bottom