Startimes tuoneeni huruma, kifurushi kinakaa wiki 2?

Startimes tuoneeni huruma, kifurushi kinakaa wiki 2?

Sasa kama king'amuzi ni elf 71, si ujiunge na dstv tu
 
Jamani hawa wanaboa unalipa kifurushi kinakaa wiki 2 yaani sijui mpaka uwapigie simu
Local channel ndo mmepotezea kbs halafu kingamuzi chenu mwakiuza 71000
Hovyo sana
Halafu mmeingia ubia na tbc mnatumia mitambo ya kodi za watz huku mnatukatia local channel
Jipangeni upya
Hadi continental majanga wanawashinda
Tulishahama huko wenzio siku nyiiingii
 
mkuu unalalamika nini sasa??

wiki 2 = sh 6,000
mwezi = sh 12,000
sawa tu
UMEME 15000
MAJI 8000
KODI 25000
KINGAMUZI 12000
USAFI 2000
SIJALI VOCHA SABUNI NKB MAPATO LAKI NITAFIKA KWELI?
 
sina hamu kabisa na startimes , na mtu akitaka hicho king'amuzi nampa bure.Nilikuwa nalipa 30,000/ vipindi vya ovyo kabisa siku zenyewe baada ya kumi wamekata mpaka TBC na kukuachia TV 1 pekee. sasa niko Taifa kubwa AZAM TV nalipa 28,000/ vipindi bwerere na siku mpaka unapata na za motisha.
Mimi nakitaka nakiomba bure kama ulivyosema
Nna TV tuu sina king'amuzi ili na mimi nijionee kero zake
 
WAFANYA BIASHARA WA MADISHI, NA WATAALAMU WA ISLALATION YA FTA DISH NI FURSA HIYO,,,,, MMEISHIA WAPI WAZEE WA LNB, EAST, WEST HUKU TUNAIBIWA JAMENI, TUNAUZIWA CHANNEL ZA FREE ON AIR TUOKOENI TUKISHANUNUA BASI HAKUNA KULIPIA KWA MWEZI NI KERO ASIKUAMBIE MTU
 
local channel inabaki Tbccm na tv1 hili liking'amuzi shida tupu
Mbona hata azam ni hivyo hivyo endapo kifurushi kikiisha unabakiwa na TBC na TV 1 pekee kama free channel kwa sasa.
 
Angalia ulichagua kifurush gan ..usikute umejiset kwenye uhuru ww unaweka wlfu 12 lazima uone wik mbili badil kwanza kingamuz chake kiwe cha mambo
Mkuu unawezaje kuset kifurushi cha mambo?
 
Ni kweli ndugu amia kwingineko maana hata Mimi kingamuzi cha star times kiliniboa nikakidump madogo wanachezea tu sasa.
 
Hivi star times bado wapo. Pole sana Mkuu hamia azam tv burudani kwa wote
 
6000 ni nyingi sana kwa channel 20
 
dishi channel 20 wanalipa 9000
 
Back
Top Bottom