Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Nimegundua king'amuzi cha Star times ni kizuri sana na kina vipindi vingi vizuri kulinganisha na vingine. Nilinunua kingine juzi juzi nimeangalia ila bado kwakweli sijakifurahi nimerudi zangu startimes
 
Habari zenu wanaJamiiForums

Je, una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

kumbuka namba zetu za huduma kwa wateja ni 0764700800 au 0677700800

Ahsanteni sana na karibuni nyote.
Mimi nilikuwa natumia king'amuzi Cha antena ilikuwa inashika vizuri lakini nikahamia sehemu nyingine saiv nimeshindwa kupata channel. Naomba msaada.
 
Habari zenu wanaJamiiForums

Je, una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

kumbuka namba zetu za huduma kwa wateja ni 0764700800 au 0677700800

Ahsanteni sana na karibuni nyote.
Mbeya Hapa Sae sizipati channel zenu
 
Nimehamia Majengo, jiji la Arusha mkoa wa Arusha ni mjini tu maana kwenda city center nauli ni 400
Majengo visimbuzi vyote (dish na antena) vinafanya kazi, tafadhari fika katika maduka yetu (Florida au Friends corner) utapatiwa namba za mafundi wetu watakushauri namna bora ya kufunga dish/antena.
 
Kero kubwa ni pale unapotaka kubadili kifurushi hadi upige customer care, kumbukeni kuna mama zetu vijijini hawalijui hela na matokeo yake mtu alikuwa na kifurushi cha juu anataka arud cha chini mnamhesabia siku. Huu ni wizi uliotukuka. Rekebisheni hapo ili mtu akiweka anaenda automatically kwenye kifurushi husika kulingana na pesa aliyoweka.
Mwisho kabsa hakuna channel ya mieleka, kulikoni?
 
Habari yako. Hatuwezi weka mfumo wakubadili kifurushi automatic; wateja wengine wanalipa hela zaidi kwa ajili ya miezi mawili sio kwa ajili ya kulipia kifurushi cha juu

Kubadili kifurushi peke yako pakua app ya startimes on au piga *150*63#
 
Nimegundua king'amuzi cha Star times ni kizuri sana na kina vipindi vingi vizuri kulinganisha na vingine. Nilinunua kingine juzi juzi nimeangalia ila bado kwakweli sijakifurahi nimerudi zangu startimes
Startimes wapo vizuri, nimeshindwa kuhamia Azam kwa sababu huwa naenda kuangalia ligi kuu ya Tanzania katika vibanda umiza.

Kitu ambao wameniudhi mpaka leo Startimes ni kuongeza gharama ya bundle na kupunguza channel za michezo katika kifurushi cha nyota. Kifurushi cha nyota kilikuwa na Sports Arena ambayo imeondolewa na kupelekwa kwenye kifurushi cha mambo. Siku hizi hata siangalii kickboxing tena. Dah! Umaskini huu!

Pia, Chonde chonde, naomba Startimes mrudishe Startimes kids katika kifurushi cha nyota mana watoto wanakosa katuni katika kifurushi cha nyota.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ofa za msimu wa sikukuu mnatoa lini?
Ofa zinaendelea tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii utapata taarifa ya ofa mbalimbali. Kwa kukujuza tu ofa ya Leo na kesho

Lipia TZS 100/= kisha unapewa kifurushi cha uhuru siku 5 (Dec 18 -23). Hii kwa wateja ambao hawajawahi kulipia mwaka mzima.

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom