Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

logframe, Fanya hivi, Startimes kigeuze kuwa cha kuangalia local free channels. Then nunua DStv kwa ajili ya kupata kilicho bora kabisa, Mimi hawa Wachina tangu walivyoshindwa kulipa mkataba mpya na Nat Geo Wild na Fox sioni cha maana tena kwenye hicho king'amuzi chao, sana sana nitakitumia kuangalia local channel's tu, silipii ng'oo.
 
Matola, Yaani hapo umenena. Nikisikia matangazo yao na wanachokifanya kwenye uhalisia napata kwikwi kabisa.
Hiyo ndiyo dawa yao. Nitaangalia free zao incase DStv sijalipia. Bora nigharamike kwa kitu kizuri na kinapatikana.
 
Tatizo la yote hayo ni TCRA, wanashindwa kusimamia mikataba kati ya watoa huduma na wateja ambayo ni vifurushi. Startimes ni kituo kinachogopwa sana na serikali ndiyo sababu wanakuwa wajeuri, wao picha wanazoonesha miaka nenda miaka rudi ni zilezile kila siku. Hawa startimes wamekuwa kila mara wanapandisha bei za vifurushi huku unacholipia ndani ya kifurushi hakipo.
 
Hawa jamaa wamekuwa wahuni sana. Mimi mwenyewe nipo njiani kuwakimbia. Chanel zote nzuri na ambazo tulikuwa tunapenda kuziangalia wanazitoa, ukipiga simu kuwauliza wanakupa majibu ya kijinga sana.
 
Naona moderators mmeedit uzi wangu na kuondoa baadhi ya maneno, sawa tu, sisi tunaumia na makampuni ya kijangili.
 
Naona hawa jamaa wamwpita huku jana leo wame updats system ila hawaja leta chanel za maana zaidi ile chanel ya Nollywood ambayo wanalaliana kila wakati
 
Naona hawa jamaa wamwpita huku jana leo wame updats system ila hawaja leta chanel za maana zaidi ile chanel ya Nollywood ambayo wanalaliana kila wakati
Bado mnalipia startimes? Kuna mna roho ngumu kwelikweli, Mimi nitaitumia startimes kwa local channel's tu.
 
Kuwa mjanja pata DSTV full burudani hivo vingine hakuna burudani
Sijawahi ona usanii kama wa Startimes.

Channel kifurushi cha uhuru Tshs 18,000 World Football na Sports nyingine kwangu siku hizi hazionyeshi na nimelipia.
Na matangazo yenu mnajigamba kuwa zinaonekana kwa bei hiyo. Sasa nina kama mwezi na zaidi nilkuwa naangalia mmetoa.

Wametoa channels kama:
1. Nat Geo Wild
2. Clouds Tv
3. Fox Sports na nyinginezo kama 4 sizioni.

Sasa mateso ya nini? Mwezi huu nahamia Multichoice (DStv) au Azam Tv
 
Mimi channels kama Aljazeera, Ze Cinema, TVC news, Star Rise, ST baby ,hazitoi sauti. Nilitembelea ofisi zao kuuliza hawakuwa na majibu ila wakawasiliana na makao makuu wakadai eti wameboresha tech ya urushaji wa matangazo kwa hiyo ving'amuzi vya zamani ndio maana baadhi ya channel zinasumbua kutoa sauti.
Suluhisho; Eti ninunue kinga'amuzi cha kisasa zaidi ndio zitatoa sauti.
Sasa maswali ni haya;
1. Hicho kinga'muzi nilitengeneza mimi?
2. Kwa nini wasitoe taarifa kuwa wenye ving'amuzi aina fulani wanapaswa ku update ili wapate huduma nzuri?
3.Je hizo gharama za ku upadate ziwe za mteja wakati ving'amuzi ni vya kwao?
Walichonichefua zaid ni kuondoa channelsle zenye akili kama Nat Geo Wild, Nat Geo Explorer, Fox Movies, na Fox News na kutuachia matakataka. Yaani sina hamu na Startimes.
 
Back
Top Bottom