Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Jamani channel gani unaweza kuiangalia endapo ujalipia king 'amuzi cha star times?
 
STARTIMES, mliniambia nikija na kingamuzi chanu cha antena huku mpanda kitafanya kazi mbona hakifanyi kazi?
 
Hivi mbona huku Musoma njini mnakatika sana, tatizo ni nini? Je, muda ambao mnakata na ukifika mwisho wa mwezi mbona hamfidii? Nikisema mna tutapeli wateja wenu nitakuwa nimekosea?
 
Kuhusu kujirudiarudia kwa movies na tamthilia kwenye starswahili
Kusema ukweli mnatuboa wateja wenu, mfano, tamthilia ya forever more, na If only, kingine ni kuonyesha movie za zamani tu, kwanini msituwekee na tamthilia ambazo ni current? mi binafsi naipenda starswahili na kung ful,ila mmenitolea na kuniwekea Tv E ambayo hata siitaki kuiona, je mnaweza kunibadilishia?
 
habari yako

tunaving'amuzi vya aina mbili, vinavyotumia antenna na vinavyotumia Dish

vinavyotumia Antena viko vya aina mbili

kuna vile ukinunua unafurahia chanel zaidi ya 75 mwezi mmoja kinauzwa tshs 59000
na kuna vile ukinunua unapata chanel 17 kwa muda wa miezi 7.5 vinauzwa tsh 34000 (kingamuzi na malipo humo humo)

vingamuzi vinavyotumia Dish

hivi vinauzwa TSHS 139000 pamoja na ufundi unapata na dishi lake
kama unadishi kinauzwa Tshs 96000

Ahsante
Mimi ni mkazi wa CHANIKA dar, naomba ushauri ni nunue kisimbuzi kipi ambacho kinaendana na mazingira haya ya chanika kati ya hicho cha dishi na hicho kisicho na dishi? Naomba ushauri wenu kwanza!
 
Mimi ni mkazi wa CHANIKA dar, naomba ushauri ni nunue kisimbuzi kipi ambacho kinaendana na mazingira haya ya chanika kati ya hicho cha dishi na hicho kisicho na dishi? Naomba ushauri wenu kwanza!

ninacho sema hapa mbona ninacho hico cha antena na hakifanyi kazi huku mpanda nadhani ni hicho cha 34,000?
 
Naomba kujuwa tatizo ni Chanel za nyumbani pesa ikiishàsizipati kwa nn jamani naomba mnisaidie kadi namba hii 01819453104 Niko tabata Dar.
 
Hivi nikiwa kwenye kifurushi cha mambo kwa nn mmeondoa mfumo wa kununua kifurushi kidogokidogo MF nikilipia elfu 6 mnachaji daily chaji want in nusu mwezi?
 
Back
Top Bottom