Mhoja
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 207
- 24
Ndugu Wana JF, tarehe 1 may Kampuni ya Startimes inayojihusisha na masafa ya kurusha matangazo ya television kwa njia ya digital ilifungua mtambo wake wa kurusha masafa hayo mkoani Mbeya, cha ajabu mamia ya wananchi wa mkoa huu leo walijazana kurudisha ving'amuzi hivyo baada ya kushindwa kufanya kazi. Wengi wanalalamika kuwa wanaposcan channels inaandika channel empty list, na wengine wanapata channel moja badala ya 38. Nilichokishuhudia asubuhi mawakala wa StarTimes walikuwa wanawasisitiza wateja wao kununua antena ya nje kwa gharama ya sh. 19000/= kitu ambacho wananchi walilalamika kuwa ni wizi. Watu walitarajia unaponunua na kuanza kupata matangazo. Inavyoonekana wameamua waweke signal ndogo kwenye mtambo wa kurushia masafa ili waweze kuuza antena za nje kwa bei juu. Na cha ajabu hata waliolazimika kununua antena za nje walipoenda kuzifunga hawakufanikiwa na hivyo kutaka kuleta rapsha na hasa katika ofisi ya Main dealer.
Wana JF tusaidieni je tumeibiwa?
Wana JF tusaidieni je tumeibiwa?