Starehe za Fukayosi weekend

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Kwa wanaokujua Fukayosi au wanaopita njia hii ya Bagamoyo Msata watajua ninachotaka kusema. Kama unakwenda Fukayosi ukitokea Bagamoyo, mara baada ya kuvuka daraja la mto Ruvu upande wa kushoto, kuna akina mama wanachemsha mahindi mabichi pale.

Sikuamini macho yangu,kuna ka-foleni katamu ka ma-vx ya watu wanaotafuna mahindi ya wale akina mama. Pale watu wanakandamiza mahindi kama hawana akili nzuri, vitu vya kiasili ni vitamu havina usomi,sijui cheo cha mtu au nini sijui.

Masufuria ya mahindi yanamalizika moja baada ya jingine. Halafu kuna kambale wa kubanikwa. Jamani wasio na ajira wachangamkie hii fursa.

Kama atatokea mtu akaiboresha ile huduma pale( hakuna choo,hakuna mifuko ya kubebea mahindi, maji ya kunywa hakuna,vinywaji baridi hakuna,sipendi maji ya Ilala yawepo,mchemsho ungekuwepo ingekuwa poa, nk), naamini kinaweza kuwa kituo kikubwa sana cha burdani siku chache zijazo hasa week end. Raha nyingine pale Fukayosi ni kwamba, kama unataka kulala pale ( kuna ka-guest house bubu), inabidi usiende na gari, ukienda na gari bei inapanda mara mbili !!
 
Fukayosi nilitapeliwaga shamba mwaka juzi,
Sina hamu na huko, we kula tu hayo mahindi.
Labda kama unaweza kunibebea niyapokee pale Mwenge mkuu wangu Malila!!
 
Pole, hata mimi sijanunua shamba pale ila nilikwenda kupima shamba la mtu pale Mwavi, sasa wakati tunarudi ndio nikakuta starehe za kulamba mahindi. Jumamosi ninapoenda huko nitaku-PM ili ninaporudi nikubebee kiasi ili uyapokee mwenge !!!!!!
 
Nitashukuru ndugu yangu.
Wajua nlikua nataka heka 5 na nikapimiwa from Point A (to Point B).

Kumbe mwenzangu mmoja hivi nae alikua anataka Heka 6, nae alishapimiwa from Point B (to Point A).

Kichekesho ni kua from Point A to Point B kuna heka 7 tu, so heka 7 hizi zitoe za jamaa 6 na zangu 5, mathematically nikaona haikuji na jamaa hakutaka tu-prorate nikamuachia zote na zangu achukue, bahati mbaya nlikua nimelipia laki 2 kwa heka mara heka 2 kama advance, nazo nika-surrender.
 
Hilo tatizo kwa sasa linaongezeka sana, kila siku kuna mtu analizwa mahali fulani. Ila usikate tamaa kabisa.
 
Hii ni fursa ya kuchangamkia. Mtoa mada naona umeangalia mbali zaidi. Hii sehemu ya mahindi hata mimi niliwahi kujipatia mmoja wakati tunaenda kuangalia mashamba Fukayosi.
 
BWAZ-DRJ.jpg

BWAZ.jpg
 
hata na mm nahitaji hayo mahindi

Back
Top Bottom