STAR TV Tuongee Asubuhi 24th July 2011 - Mjadala Nidhamu Bungeni Part 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

STAR TV Tuongee Asubuhi 24th July 2011 - Mjadala Nidhamu Bungeni Part 2

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Jul 24, 2011.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumeonelea ni vema tukaurejesha tena mjadala huu kutokana na kuendelea kuyumba kwa usimamizi wa shughuli za kila siku Bungeni na hivyo kupelekea mizozo na kurushiana maneno kwa wabunge mara kwa mara.

  Tafiti za karibuni zinaonyesha kuongezeka watazamaji wa Bunge hata wale ambao walikuwa hawalitazami, wanafanya hivi si kwa kufuatilia masuala muhimu ya kitaifa bali kujua leo nani kapewa mipasho na mwenzie ( kama tujuavyo hulka ya watanzania wengi kushabikia mambo ya hovyo hovyo)

  Michango iwasilishwe kupitia 0685 358973 (Live Text zitasomwa wakati wa Kipindi ) kipindi kinaanza saa 1 na DK 30 hadi 3 kamili asubuhi
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ok, ubarikiwe sana kwa kutujulisha!
   
 3. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  wekeni link yenu pia tuweze kupata online
   
 4. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunapatikana online kupitia jumptv.com...Isipokuwa ni pay service kwa members Only. Katika mpango huu wa Digitali tunategemea kuwa Online baada ya ukarabati kukamilika. Vuteni subira
   
 5. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amen Mkuu
   
 6. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shukrani kwa nyote mnaoendelea kuchangia kupitia text...So far two texts received
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  umesomeka
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Malipo kiasi gani kwa hao members? Na huo ukarabati unategemewa kukamilika muda gani?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Natarajia kuwemo kwenye kipindi hiki dakika chache zijazo...
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Naona najitahidi kuingia huko inakuwa ngumu.
   
 11. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umeme umetatiza jitihada zote: 8:40 EAT Jaribu tena Mkuu Mambo yametengemaa sasa
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Yahya naamini sasa unaelewa kwanini wengi wanashindwa kushiriki mjadala huu.

  Wabunge wetu ni wasanii. Wanasinzia sana, wapo kwa maslahi binafsi walio wengi.

  Unafiki zaidi nauona pale mbunge anapothamini chama badala ya taifa, tatizo hili lipo pande zote, chama tawala na vyama pinzani.

  Kuna wabunge tunawaona kuwa wapo kwa maslahi yetu wananchi, ni wazi wanapotoa hoja za msingi wakati mwingine hawaeleweki kwa wananchi kwakuwa wana maono mapana na hivyo wanaeleweka visivyo (japo baadae tunakuja kuelewa walimaanisha nini).

  Narejea pa awali, viti maalum ni gharama kwa taifa, wengi wapo kupaza sauti za NDIYOOOOOO
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Pouwaaaa
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Yahya,

  Shukrani kwa kusoma maoni yetu na kuonyesha kuwathamini watanzania watumiao mtandao huu wa JF. Nimefahamishwa umeyasoma.
   
 15. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Viti maalum havina manufaa yoyote sijawahi ona mbunge wa viti maalum ametoa hoja ya msingi
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nadhani next time...
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Viti maalum hasa wa CCM wamekuwa na kazi maalum bungeni ni mipasho mwanzo mwisho. Lakini chimbuko la lote ni CCM, badala ya kuchagua Spika wakachagua mwanamke! From the outset Mama Anne Makinda, alionekana kabisa ametumwa kuuwa mawazo tofauti kulinda maslahi ya wakubwa zake. Na kwa kuanzia alibadili kanuni za kudumu za bunge ili neno kambi rasmi ya upinzani liwe kama wakubwa zake walivyotaka.

  Sasa hivi huyu mama amekuwa ni msemaji wa serikali na sio mwongoza majidiliano ya wawakilishi wa wananchi katika kusimamia serikali. Kero za wananchi zimesahulika kabisa chini ya Makinda. Hana academic qualifications kuongoza chombo cha kutunga sheria at the same time hana interpersonal skills za kuwa kiongozi hata wa kata let alone bunge la Jamhuri. Kama wanataka kuokoa jahazi wampe huyu mama tuition but my worry is she thinks she is doing well.
   
 18. n

  nsami Senior Member

  #18
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio mkuu tunashukuru sana kwa kutujali na kuthamini mchango wetu.
  Infact, sababu za malumbano bungeni ziko katika makundi mawili tu!

  1. Tofauti ya mitazamo baina ya wabunge,

  Hili sio baya, ni zuri na ni lazima kuwe na tofauti ya mawazo ili kuleta chachu ya mijadala. Hakuna cha kujadili kama wote wakiwa na uniform ya ufikiri na inakuwa mbaya zaidi kama mnafikiri sare na mnafikiri vibaya kuhusu jambo fulani yaani wote mmefikiri sawa na mmekosea. Cha kushangaza ni kuona hata jambo ambalo liko wazi kwamba wenzetu wataunga mkono! Mitazamo na ifanane kama wote mko sahihi.

  2. Ulimbukeni wa kisiasa,
  Wabunge wanaweka pembeni maslahi ya taifa na kuweka mbele maslahi ya vyama. Hoja ikitolewa na mbunge wa chama flani hiyo si hoja! wenyewe sifa yao ni kuona mbunge wa chama chake tu akizungumza, chochote atachozungumza yeye ni hoja ya kuungwa mkono! utakuta kwa mfano, mbunge wa upinzani akisimama tu uatasikia miongozo kibaaaaao! katika bunge hili linaloendelea mbunge mmoja kama sijakosea alikuwa Mhe. Lembeli akichangia katika wizara ya nishati alimtaja mtu mmoja ambae alipunjwa stahiki zake mgodini alimtetea sana, ni vizuri, lakini mwishoni akasema "......tena mtu mwenyewe ni mwana-CCM angekuwa hata mpinzani hata nisingesema lakini ni CCM." hapo nikapata hisia kumbe kama mimi ni mpinzani nisimpelekee mbunge wangu wa CCM kwa kuwa yeye hatetei watanzania bali wana-CCM, ndipo akamaliza kwa kusema "...wacha niishie hapo nisije nikasema jambo ambalo halilingani na busara zangu" akamaliza.

  Wakuu nawasilisha!
   
 19. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  Mkuu wale wa CCM sio viti maalum, ni VITU maalum. Chakla ya walafi ile.....
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu si wote wa viti maalum hawana hoja, wapo wenye hoja za msingi sana. Lakini asilimia kubwa (tukiri ukweli) hawana manufaa kwa taifa, wanawajibika kwa vyama si taifa na ni mzigo kwa taifa!
   
Loading...