Star TV Tuongee Asubuhi: Tumejifunza nini katika Historia ya Majanga na Maafa yake Nchini?

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Tumejifunza nini katika Historia ya Majanga na Maafa yake Nchini?

Tanzania imekuwa na historia ya maafa tangu mwaka 1872. Maafa hayo yamesababisha vifo, uharibifu wa mali na mazingiraAina ya majanga nchini Tanzania ambayo yameleta madhara ni magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na mifugo, ukame, moto, ajali za vyombo vya usafiri na za viwandani, mafuriko, wadudu/ndege na wanyama waharibifu wa mimea.

Mengine ni ya wakimbizi, vimbunga na upepo mkali, migogoro ya jamii; tetemeko la ardhi, milipuko na volkano.
Wakati mwingine maafa yanaweza kuwa makubwa na yenye madhara makubwa. Makali ya madhara ya maafa katika jamii yanategemea jinsi gani ilivyojiandaa kukabiliana nayo.Kutokana na kuongezeka kwa matukio na madhara ya maafa nchini, Serikali ilipitisha Sheria Namba 9 ya mwaka 1990 ya Uratibu wa Utoaji Misaada ya Maafa. Katika Sheria hiyo, Kamati ya Maafa ya Taifa (Tanzania Disaster Relief Committee - TANDREC) ilianzishwa ili kuratibu misaada yote ya Maafa Nchini.

Kamati za maafa kama hii zilitakiwa kuanzishwa katika ngazi za Mikoa na Wilaya. Sera hii ya Maafa inazingatia masuala muhimu katika mzingo (cycle) wa menejimenti ya maafa yaani kuzuia, kupunguza athari, kujiandaa, kukabiliana nayo yanapotokea na urudishaji wa hali ilivyokuwa kabla ya maafa kutokea au kuiboresha zaidi. Moja ya Kipengele muhimu cha sera hiyo kinasomeka kama ifuatavyo:

2.1.2 Kujiandaa Kukabiliana na Maafa:

(a) Hoja:

Kujiandaa kukabiliana na maafa kunahusisha kuandaa hatua muhimu za kiutawala, kisheria na kiufundi zenye lengo la kupunguza madhara kwa wanaokabiliwa na maafa. Hizi ni pamoja na utoaji wa tahadhari ya awali, mafunzo, mfumo wa mawasiliano, mipango ya uokoaji, na utafutaji wa rasilimali. Zoezi hii linahitaji kurudusiwa mara kwa mara mifumo na mipango, urekebishaji, na kufanya majaribio. Kwa sasa mifumo iliyopo bado haijaendelezwa na mingine muhimu haipo kabisa. Pale inapokuwepo, haifanyiwi majaribio kuona ufanisi au dosari zake ili zirekebishwe.

(b) Madhumuni:

Kuhakikisha asasi zote zenye jukumu la menejimenti ya maafa zinajiandaa, ziratibiwa na zinakuwa na rasilimali na nyenzo za kukabili maafa; mfano hospitali na vikosi vya zima moto.Maswali ya Msingi:Tumekwama wapi?Nini kifanyike?Shiriki Mjadala huu utakaoonyeshwa hapo kesho (Jumapili tarehe 2 Oktoba 2011) kuanzia saa 1:30 asubuhi kwa kutoa maoni na yatasomwa live wakati wa kipindi ambapo update za zoezi la Upigaji kura huko Igunga zitatolewa.

Nawasilisha.
 

oldonyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
549
86
hakuna cha kujifunza hila yanapotokea majanga ni furaha kwa wakubwa kwani ujineemesha kwa kula pesa za rambirambi na kuwekwa kwenye tume zisizo na tija ambazo hata matarajio yake kwa watanzania huwa ni zero tu.
 

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Pamoja na Uchaguzi Igunga hapa tatizo ni sugu naungana na mleta thread, napita kwa sasa nitarudi tena na details katika mikasa hii ili kupaza sauti zetu. Tufikishie salam zetu juu ya Tanzania we want. Mlituweka Solemba hatimaye nauona mdahalo sasa. Ntarejea baada ya mdahalo kwisha
 

Laurence

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
3,104
414
Mkuu Yahya, hapa kuna tatizo uwajibikaji(Responsibility) kwa serikali kwa sababu sheria zipo wazi za kusimamia usalama wa Raia lakn kwa sababu ya ulafi wa viongozi kunapelekea kutokuwa na Uwajibikaji kwa kwa viongozi wa nchi hii mfano Polisi ambao ni watu wa usalama wanapokea rushwa hadharani kwa mabasi/daladala/malori yanayokiuka taratibu zilizowekwa kwa hyo hapa tusitegemee haya majanga kwisha mfano jana Kongwa basi lililokua linatoka Mpwapwa to Dar limeua watu 23 tatizo mwendo kasi je hawa madereva wamepata leseni kihalali?
2.Kuna tatizo hata kwenye misaada itolewayo wakati wa matukio mfano mabomu ya Gongo la mboto tumeshuhudia mashirika na makampuni mbalimbali yanatoa misaada ili iwafikie wahanga lakn juzi waathirika wameilalamikia serikali kua imewatupa mfano wengine yale maturubai yanavuja sasa,pia hela wanayowafidia haiendeni na thamani ya nyumba zao.
Kwa kumaliza tutegemee ajali kutokea zaidi na mimi namshukuru Mungu bora mwezi wa 9 umepita maana ulikua wamajanga tupu.
 

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Pamoja na Uchaguzi Igunga hapa tatizo ni sugu naungana na mleta thread, napita kwa sasa nitarudi tena na details katika mikasa hii ili kupaza sauti zetu. Tufikishie salam zetu juu ya Tanzania we want. Mlituweka Solemba hatimaye nauona mdahalo sasa. Ntarejea baada ya mdahalo kwisha

Umekuwa mchangiaji mkubwa kwa kipindi hiki Mkuu sina shaka utarejea, endelea kufuatilia mdahalo
 

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Duuh! inamaana Yahya kaingia choo cha kike??

Ha ha ha ha! kaka ilete mada hii tena baada ya wiki mbili tutaijadili maana kuanzia kesho ni balaa kama uchaguzi haitaenda vizuri.

Wakuu Mwakimoge na Bora Kufa,

Kwa hakika tulipenda sana tuizungumze mada ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga bahati mbaya sana ama nzuri pengine sheria ya Uchaguzi inakataz hilo kwani ni kinyume na muda wa kawaida wa Kampeni, Tamshi lolote kuhusu Kampeni litamaanisha uvunjwaji wa sheria. Jambo ambalo ni harati kwa masilahi ya Kituo chetu.

Ila patakuwa na Updates on every top of the hour, Timu ya uhakika ipo Igunga kuwafahamisha watanzania. So msikose kutazama Star TV hapo kesho kwa update za Igunga mpaka saa sita Usiku.

Pamoja na hayo maisha yanasonga, wekeni michango hapa tuendeleze Siasa takatifu
 

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Mkuu Yahya M

Majanga si haya tu ambayo yumekuwa tukishuhudia yakitokana na sababu za kimaumbile, wanyama au uzembe wa Binadamu. Chombo kama Chomo au asili(nature) haikuumbwa kumuathiri binadamu bali apate mahala pa kuzaana na kuijaza Dunia.

Kinachotokea sasa ni ushabiki mkubwa wa kisiasa na Ahadi zisizotekelezeka haingii akilini kuona matukio ya Moto Mbeya yanafululiza kama Sinema ya Kuigiza na hakuna mpango mkakati wowote wa kukomesha tatizo hilo.

Janga jingine ambalo hasa ndio linanisukuma kuandika mchango wangu ni utitiri wa Vipindi vya kimagharibi, nichukulie mfano hapo hapo kwenu '' Sporah Show'' kwa namna ambavyo wanafundisha vijana maisha ya kimagharibi na kusahau maadili ya mwafrika, tunatengeneza kizazi potovu kabisa katika siku za usoni na hili ni janga kubwa sasa.

Nasisitiz hili nikimaanisha Media pia ni janga jingin kwa kuwa TCRA wameshindwa kabisa kuregulate content, sitaki kuzungumza kabisa yaliyotokea hivi karibuni huko Pemba na namna media ilivyochukua jukumu lake.

Natia Nukta hapa, tutakutana hewani kama Mgao wa Giza hautatukumba.

ADIOS
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,330
Tena inabidi tushukuru Mungu kwamba majanga hayatokei kila siku through lack of responsibility na uzembe wa kila namna...

Ajali nyingi zile za meli, gongo la mboto n.k. ni through uzembe, ubovu wa vyombo na matumizi mabaya ya vyombo (inabidi taasisi husika ziwe zinafanya checks za haya mambo yanayohusu jamii takriban kila mwaka..)

Tumeshajifahamu kwamba sisi ni wazembe hivyo basi chonde chonde ni bora tukadeal na mambo ambayo hayaitaji uangalizi mkubwa.. mfano suala la umeme wa nuklia tusahau (tutauana na kumalizana) pia issue mfano ya kuleta bomba la gesi ya kutengenezea umeme mpaka Dar huku ni kuongeza risk kwanini umeme usifuliwe kule kule kwenye Gesi....

Sisi ni wazembe na hatuna responsibility tukubali tu.., sababu majanga yanayotokea mpaka sasa sio sababu ya kukosekana uokoaji au ku-react baada ya majanga bali ni uzembe unaosababisha haya majanga..., na ni vipi tunaweza kujifunza kwamba sisi ni wazembe zaidi ya kuzuia uzembe wetu?
 

kitiku

Member
Mar 9, 2011
15
0
ni hivi uozo uliopo hasa kwa matrafiki ndo unatumaliza kwann huwa wanakutana nyuma ya gari?
 

Baba Ziro

Senior Member
Apr 15, 2011
130
30
Majanga TZ Mungu anatupenda sana, maana ingekuwa kama nchi za wenzetu tungeisha wote. Majanga ya TZ mengi ni ya kujitakia kwa kutokuwa na uongozi na viongozi wazalendo dhabiti. Serikali iwasimamie wasimamizi wa sheria kwa dhabiti.
 

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Majanga TZ Mungu anatupenda sana, maana ingekuwa kama nchi za wenzetu tungeisha wote. Majanga ya TZ mengi ni ya kujitakia kwa kutokuwa na uongozi na viongozi wazalendo dhabiti. Serikali iwasimamie wasimamizi wa sheria kwa dhabiti.

Ujumbe wako umefika Mkuu na utafanyiwa kazi Punde...Ahsante kwa kushiriki
 

Edson Zephania

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
517
112
Tanzania majanga mengi husababishwa na waliopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao, mfano: 1. Ajali nying ni uzembe wa Trafki kwa kuona hatari lakin akipewa chochote analiachia gari hata kama lina kasoro, 2. Ajali Melini, huu ni uzembe toka kwa waliopewa dhamana pale bandari, wanajali matumbo yao kwa kupata chochote. Watanzania tuwe na uzalendo kwanza kwa kujali maisha ya wengi kuliko maslah binafsi.
 

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,922
1,617
Ili kupunguza au kumaliza tatizo la majanga yanayosababisha maafa sisi kama taifa yatupasa tubadilishe mtazamo wetu.Taifa limekuwa linafanya vizuri sana kwenye councelling kuliko guidance.Vitu kama kufanya maziko ya kitaifa,kutoa rambirambi kwa wahanga,raisi kuwatembelea wahanga,kuunda tume za kutafuta kiini e.t.c ni machache tu kuonesha how we're good in councelling.Ni rahisi zaidi kupoteza maisha Tanzania kama ukitumia huduma za uma kama usafiri au hospitali!Hakuna hatua madhubuti za kulinda(guide)taifa lisiingie kwenye majanga kizembe.Ni gharama sana kudeal na councelling kuliko guidance ambayo tumeipuuzia.Watu wote wanaohusika watimize majukumu yao kwa kutii ethics zao.Ni bora kuingia gharama kulinda uhai kuliko gharama mara mbili ya kunyakua/kuopoa maiti au majeruhi.
 

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Tanzania majanga mengi husababishwa na waliopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao, mfano: 1. Ajali nying ni uzembe wa Trafki kwa kuona hatari lakin akipewa chochote analiachia gari hata kama lina kasoro, 2. Ajali Melini, huu ni uzembe toka kwa waliopewa dhamana pale bandari, wanajali matumbo yao kwa kupata chochote. Watanzania tuwe na uzalendo kwanza kwa kujali maisha ya wengi kuliko maslah binafsi.

Ahsante kwa kushiriki, mchango wako utasomwa punde
 

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Ili kupunguza au kumaliza tatizo la majanga yanayosababisha maafa sisi kama taifa yatupasa tubadilishe mtazamo wetu.Taifa limekuwa linafanya vizuri sana kwenye councelling kuliko guidance.Vitu kama kufanya maziko ya kitaifa,kutoa rambirambi kwa wahanga,raisi kuwatembelea wahanga,kuunda tume za kutafuta kiini e.t.c ni machache tu kuonesha how we're good in councelling.Ni rahisi zaidi kupoteza maisha Tanzania kama ukitumia huduma za uma kama usafiri au hospitali!Hakuna hatua madhubuti za kulinda(guide)taifa lisiingie kwenye majanga kizembe.Ni gharama sana kudeal na councelling kuliko guidance ambayo tumeipuuzia.Watu wote wanaohusika watimize majukumu yao kwa kutii ethics zao.Ni bora kuingia gharama kulinda uhai kuliko gharama mara mbili ya kunyakua/kuopoa maiti au majeruhi.

Ahsante kwa kushiriki, mchango wako utasomwa punde
 

Mwera

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
964
88
Ndugu yahya maohd, majanga yanayolikumba taifaletu kwa asilimia 80 yanatokana na uzembe au hujuma,mfano ajali yakuzama kwa meli ya mv spice ni uzembe wa ku over load mizigo na abiria kupita kiasi ndio sababu kuu yakuzama kwameli ile,pia ajali za mabasi kunatokana na uzembe na kutozingatiwa sheria za usalama barabarani,tukifata sheria na taratibu tutaepuka majanga haya,pia kiundwe kitengo maalum cha uokozi majini na nchi kavu chenye vifaa vyakisasa na wataalam waliobobea itasaidia sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom