Star TV Tuongee Asubuhi Sunday 06 June 2011: Mivutano ya wanasiasa ina tija kwa Watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Star TV Tuongee Asubuhi Sunday 06 June 2011: Mivutano ya wanasiasa ina tija kwa Watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Jun 2, 2011.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mada hii itajadiliwa Jumapili 06 June 2011 kuanzia saa 1 na dk 30 asubuhi Star TV. Baada ya kimya kirefu na majukumu mengine ya Kiofisi tutakuwepo wiki hii kuwezesha mjadala pamoja na Watanzania juu ya Mada husika. Toa mtazamo wako na utapata nafasi ya kusomwa hewani kwa manufaa ya umma wakati wa Kipindi.

  Nawasilisha.
   
 2. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu Yahya uliingia mitini. Any way karibu tena jamvini. Wageni waalikwa watakuwa kina nani?
   
 3. M

  Masuke JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu ni tarehe 05 au 06?
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Ni tarehe 05 mkuu, huyo amejichanganya tu. Ok, Yahya hatuwezi kuchangia kitu hapa ka sababu mada yako haiko wazi. mfano Mukama na Nape nao wana mvutano huyu akisema hivi huyu anasema vile tena mbele ya waandishi wa habari, kwahiyo fafanua vizuri mada yako ili ueleweke.
   
 5. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Majukumu yaligongana Mkuu. Tumerejea Rasmi
  Mwanza atakuwepo Kada wa CCM Mzee Emannuel Rutalaka na
  Mchungaji Mwandamizi Emmanuel Kutoka KKTT Iringa

  Dar atakuepo Mbatia na Mpiganaji mmoja kutoka CDM atakayethibitishwa baadaye
   
 6. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumeshuhudia hoja binafsi za kurishiana makombora wanasiasa binafsi kuliko agenda na ilani za vyama vyao, je hayo ndo watanzania wanataka kusikia. Au kama upo ulazima, matazamo na maono yattaoka kwa wachangiaji
   
 7. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Tarehe 5 mkuu. kosa la uchapaji
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kimsingi mivutano ya wanasiasa haina tija kwa watanzania kwa sababu mkiwa katika marumbano hamu wezi kufikiria masuala ya maendeleo badala yake ni kujaribu kuhujumiana kwa hali yoyote ile.
   
 9. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Oky..,Kama mivutano inahusu ustawishaji wa Maisha ya Watanzania itakuwa na tija kubwa..!
  Mfano:-
  1. Mvutano unaohusu kuhoji mali alizonazo mtoto wa Kigogo..,Una tija kwani watanzania wana haki ya kujua huo uatajiri amepata vipi,kwa hiyo..,Una Tija-100%.
  2.Mvutano Unaohusu suala la mauaji ya Watanzania kwa kupigwa Risasi-Tija 100%.
  3.Mivutano kuhusu Unafiki wa Viongozi wanaodaiwa kuanzisha Chama Marehemu(CCJ) ndani ya Chama Cha Magamba(CCM)..,una tija kwani unafiki wa kujifanya unapigania masrahi ya jamii kumbe una masrahi yako binafsi si vyema..,so tija-89.99%.
  4.Mivutano yoote ambayo ina masrahi kwa jamii..,mi nimetaja hiyo michache ..,wadau mtanisaidia mingine..!Ina tija kwani watu wanapambana kwa masrahi ya UMMA..!
  Nawasilisha..!
   
 10. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Thanks Mkuu mawazo yako yamefika
   
 11. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unadhani chanzo kikuu cha malumbano haya ambayo baadhi yana hoja binafsi ni nini hasa Mkuu?
   
 12. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Acheni udini.
   
 13. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fafanua Mkuu
   
 14. M

  Mindi JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Heshima mkuu,
  Awali ya yote nina tatizo na kichwa cha habari cha mada: Mivutano ya wanasiasa. kunaweza kuwepo na mivutano, lakini kuna kitu kinaitwa maslahi ya taifa. ipo hali ya hatari sana katika duru mbalimbali, ambapo mijadala serious ya maslahi ya taifa letu inawekwa rehani kwa kulinganishwa na "mivutano ya wanasiasa". kama anajitokeza mtanzania ambaye kwa kutumia forum aliyonayo, ama ni mbunge ama ni diwani au ni kiongozi wa chama cha siasa, kutangaza namna ambavyo taifa letu linahujumiwa. sasa ili kupoteza lengo na kuondoa tochi isimulike uozo huo, anajitokeza kiongozi mwingine kutoka kambi inayotuhumiwa, na kumzulia kashafa huyo aliyeibua hizo kashfa. na hiyo ni mbinu rahisi tu inayojulikana. sasa katika jitihada za huyu wa mwanzo kujibu mapigo kuweka rekodi sawa, ndio zinajitokeza hoja kama hizi za "mivutano ya wanasiasa".

  Mimi nadhani tutakuwa hatulitendei haki taifa letu, kama tutaacha kuangalia mambo yenye maslahi kwa taifa ni yepi, tukaingia kwenye mtego wa kuwaweka anayeibua tuhuma na anayetuhumiwa katika mizani moja na kusema wana "mivutano ya wanasiasa". kwa hiyo taifa letu linatetewa na nani? halina mwenyewe? nadhani halina mwenyewe. maana ukiangalia linavyoliwa kiroho mbaya! na unaweza kumwelewa Mtikila alivyowahi kumtuhumu Mkapa kwamba sio raia wa Tanzania, kwa jinsi alivyouza nchi hii kwa mikataba ya ajabu kabisa ya madini. mpaka leo ni watanzania wangapi wanajua undani wa mikataba hiyo, na kwamba kiasi gani kama taifa tunapoteza kutokana na kuingia mikataba mibovu, dhahabu iko bei juu. wawekezaji wetu watukufu wana-cash in kiasi gani, Tz inaambulia kiasi gani. watanzania wanaelewa hayo?

  Je, ni watanzania wangapi wanajua kwamba viongozi wetu wamegundua njia nzuri ya kula pesa za taifa hili ni katika uwekezaji wa nishati? kwamba kuanzia IPTL, AGGRECO, SONGAS, DOWANS, RICHMOND, nk. tunaliwa juu na chin, kulia na kushoto.

  Ni watanzania wangapi wanajua kwamba serikali yetu haitakubali kuingia kwenye serious projects za kuondoa kikwelikweli tatizo la umeme, maana watakosa mahali pa kula?

  kuzungumzia "mivutano ya wanasiasa" ni kukejeli msiba tulionao hapa nchini, wa Tanzania kuendelea kuliwa wakati iko ICU
   
 15. M

  Masuke JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Yako malumbano ambayo yana tija kwa wananchi, na kwa kiasi kikubwa yana tija, kwanza yanasaidia kuwafumbua macho wananchi na kujua ni wanasiasa wepi wako upande wa wananchi na wepi kwa ajili yao wenyewe.

  Ukiangalia yaliyotokea Nyamongo hivi karibuni kuna mambo ambayo yamewekwa wazi kwa nini mauaji yanatokea, na kama serikali yetu ingekuwa ni ya kujali wananchi wake pengine mauaji haya yangekomeshwa lakini watu wa upinzani wangekaa kimya usingemsikia waziri wa mambo ya ndani
  akitoka kwenye tv na kutaja baadhi ya mambo yanayosababisha mauaji yale.

  Yanayotokea kwenye operation kama iliyofanywa na viongozi wa chadema hivi karibuni nyanda za juu kusini yataifanya serikali ijitazame upya pamoja na kwamba mengine walikanusha kama la serikali kuishiwa fedha lakini nina uhakika kwa viongozi makini lazima siku za usoni wataangalia kwa umakini maamuzi yao.

  Alichoongea naibu katibu mkuu wa CCM bara na mbunge mwenzake wa zanzibar (sikumbuki jimbo) dhidi ya mapendekezo ya bajeti ya kuondoa posho za vikao ni dhahiri kabisa viongozi hawa si kwa ajili ya wananchi wangekaa kimya tusingejua wanavyojifikira wenyewe kuliko kuwafikiria mamilion ya watanzania ambao walio wengi vipato vyao kwa mwezi ni sawa hiyo posho ya vikao.

  Malumbano mengine ndani ya vyama kwa viongozi makini yanasaidia kuimarisha demokrasia ndani ya chama, mfano CCM walivyokuwa wanalumbana wao kwa wao wamefikia hadi kujitazama upya wao wanaita kujivua gamba, hii inaweza kuwa chachu ya ama kupunguza ama kuondoa ufisadi kama dhamira yao ni ya dhati.

  Maoni yangu acha walumbane ili wafichue mambo mengi, na hayo mambo yakishawekwa wazi basi ni juu yetu wananchi kujua nani anatufaa kwa ajili ya mstakabari wa taifa letu na nani hatufai na tuweze kufanya maamuzi sahihi kwenye chaguzi mbalimbali ili kuleta ustawi wa taifa letu changa.
   
 16. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  KKTT ni nini?
  Ni vyema kuheshimu dini za watu boss!
  Sijui kama ni bahati mbaya au ni makusudi umefanya
   
 17. m

  mbiktiraa Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  malumbano haya ni muhimu sana kwani mfumo wa chama kimoja uliwapumbaza watu na kuwaacha viongozi kama waamuzi wa kila kitu . Matokeo yake viongozi wakajisahau na matokeo ndio hapa nchi ilipofikia. Ila sasa viongozi watajirekebisha kwani malumbano haya yanarudisha uwezo wa wananchi kuelewa ukweli wa mambo na kuchagua lipi wanasiasa wawajibikenalo kwa manufaa yao
   
 18. M

  Masuke JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Nadhani alikuwa anamanisha KKKT.
   
 19. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yahya,
  Awali ya yote yatupasa kuelewa juu ya siasa husika, ni vema tukatofautisha baina ya SIASA (MASLAHI BINAFS)I dhidi ya ile SIASA (KWA MASLAHI YA UUMA).

  Katika taifa letu hili la Tanzania, majority ya wanasiasa wetu wapo mahsusi kwa niaba ya SIASA BINAFSI:
  · Kwamba wapo radhi kutumia nguvu binafsi kufanikisha azma yake/zao katika jambo Fulani lenye taswira ya utaifa wa Mtanzania.
  · Kwamba wapo tayari (kwa gharama yoyote) kuhakikisha dhamira zao kimaslahi zinafikiwa (tupende au tusipende).
  · Kwa mara kadhaa hudiriki kutumia mamluki kuwahadaa wananchi kwa mithili ya uguswaji wao na hali dhalili walizonazo wananchi, tena huwa ni wenye nyuso na matamshi mazito kanakwamba hawakujua matatizo yaliyopo tangu awali.
  · Kwamba matamshi yao hayaendani kamwe na matendo yao, machungu ya wanasiasa hayaendani na ukataaji wa ruzuku wapewazo katika kuendesha aidha vyama vyao au kwa nyadhifa zao majimboni…kwa kupinga na kukataa kodi ya watanzania kutumika ndivyo-sivyo, bali huwa ni werevu na watulivu tena wasiothubutu kurejea hoja zenye kugusa maslahi yao.
  · Uroho,umaskini, ufedhuli na ufisadi huwashamiri hawa wanasiasa,, hujisahau kama ni wanaadam na wameumbwa…wajue watahukumiwa kwa wayatendayo.

  Katika upande wa pili juu ya siasa nikimaanisha SIASA MASLAHI YA UMMA:
  · Ni aghalabu kuwapata wafasaha wa kundi hili, ni wachache sana wenye imani ya dhati kwa watamkayo na watendayo kwa wananchi mithili yam zee Madiba, hayati Ghandi wa India…ni sura pekee ambazo hazikuegemea ubinafsi zaidi ya wananchi kuwatumikia.
  · Miongoni mwa wanasiasa wa kundi hili aidha huwa ni wenye kuegemea upande Fulani wa imani zao kidini na kusahau zingine, japo huleta usawa wa kuridhisha wa maendeleo kwa jamii nzima.
  · Kundi hili huwa na ufinyu wa fitna, mara nyingi huwasikiliza wananchi wanataka nini.
  Kiujumla kwa siasa za Tanzania, hazina taswira nzuri huko siku za usoni. Wanasiasa hawaendani kabisa na matamshi yao, watamkacho sicho watendacho, hawaaminiani kabisa, wapo tayari hata Amani ivurugike kwa muda ili ‘ukombozi’ upatikane, ndani ya hao wanasiasa wakombozi…bado malumbano yashamiri, wao kwa wao kunyimana fursa za kiushawishi miongoni mwao, na yote haya husababishwa na kuporomoka kwa miiko ya kiuongozi shauri ya uchu wa MASLAHI SIASA BINAFI.

  Nawasilisha,
  Yousuph .M.
  DSM
   
 20. M

  Mindi JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Nimekupata Yousuph, lakini kwangu mimi napenda kuangalia hoja zinazotolewa na wanasiasa wetu, kwanza kabisa anachozungumza ni kweli?, na kama ni kweli, kinaathiri vipi taifa letu? na tufanye nini ili tuweke mambo sawa? nadhani tukienda hivyo tutakuwa katika msitari. lakini tukiwaona wote kuwa ni watu tu wanaolumbana wao wenyewe, hatutakuwa na mahala pa kusimamia, kwamba tunalinda maslahi ya taifa, au tunaongea tu kama kupiga umbeya kwamba huyu alisema hivi na yule akasema vile. hutokea pia hasa kwa viongozi wa chama cha CCM, wakawazushia wale wanaoibua kashfa, kwamba wanavuruga amani na utulivu. au wanawachanganya wananchi. kwamba uchaguzi umepita na wasubiri mpaka kipindi kingine cha uchaguzi! tuki-entertain nonsense kama hizo tutakuwa hatujalitendea haki taifa letu.

  kwa hiyo Star tv iangalie namna ya kuweka balance hapo, kwamba ijue inalinda maslahi ya taifa, na kwa hiyo kujikita kwenye yale yanayozungumzwa ambayo yana maslahi ya taifa, badala ya kuongea juu juu tu kwamba huyu alisema hivi yule akajibu vile
   
Loading...