Star Tv mjadala wa leo: Haikuwa sahihi kwa Makonda kuita watuhumiwa kwa majina ya mitaani(a.k.a)

K M S

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
524
424
DOTTO BULENDU anaendesha mjadala wa namna ya kampeni alioanzisha Makonda juu ya madawa ya kulevya na kubwa ni namna majina yalivyowasilishwa hayakua majina halisi ni kama yaliwasilishwa kimzaha mwingi kiasi cha kuitana majina ya mitaani aka kiasi mtu anaweza kukataa lkn hata majina waliopewa waandishi hayakua rasmi kwani hayakua na kitu chochote kilichodhihitisha kuwa yalitoka ofisi ya mkuu wa mkoa hakuna muhuri hakuna sahihi hakuna nembo hii ni hatari katika vita kubwa kama hii
 
Endelea kutujuza mkuu mbona kimyaa tena? Wengine tupo mbali na tv
 
Wengine jina moja tu nalo limekosewa. Mwandishi wa majina hayo hata mwandiko wake na majina yalivyoandikwa vinaacha maswali mengi. Tuwe serious na masuala mazito ya nchi
 
Ni mpuuzi na mtu asiye na uzalendo pekee atampinga Mkuu wa Mkoa katika vita hii, Ila ni werevu na wenye akili tuu watapinga mbinu/approach iliyotumika, kwani ikiwa tunaamini tutazingatia UTAWALA WA SHERIA, basi ni kuwa vita hii itashia mahakamani na kama itaishia mahakamani Criminal Procedure Act Cap 20 RE 2002, Evidence Act cap 6 Re 2002, Haki za binadamu zilizomo katika katiba na Sheria mpya ya Madawa ya Kulevya No 5 ya mwaka 2015, na Police General Orders zifuatwe ili kusinusuru kesi hizo zikiwa mahakamani, ukiangalia vita hii inavyoendeshwa hauhitaji kusoma sheria kujua kinachofanyika hapa kuwa kimekuwa kikiendeshwa kwa utashi wa kisiasa zaidi kuliko sheria, kuendesha vita hii kisiasa kuliko kisheria zaidi kunadidimisha na kufifisha zaidi vita hii.
 
Nilivyosoma 'Noliega' nakafikiri labda ni wa Panama lakini baadae nikawaza anaweza kuwa Twaha Hamidu ndio nikakumbuka alishatangulia mbele za haki pia! Baada ya kutafakari zaidi ya ya Division Five na jinsi Profesa alivyoamua kurudisha mfumo wa zamani wa Division zero na shule moja ikapata Four mbili na zero 120 ndio nikajua kuwa hii ndio Tanzania tuliyonayo hata kama hatuitaki!
 
Tumefanya uchunguzi wa kina tunawajua zaid ya wanavojijua, kisha unataja a.k.a ya mtu, jamaa anatuzingua
 
DOTTO BULENDU anaendesha mjadala wa namna ya kampeni alioanzisha Makonda juu ya madawa ya kulevya na kubwa ni namna majina yalivyowasilishwa hayakua majina halisi ni kama yaliwasilishwa kimzaha mwingi kiasi cha kuitana majina ya mitaani aka kiasi mtu anaweza kukataa lkn hata majina waliopewa waandishi hayakua rasmi kwani hayakua na kitu chochote kilichodhihitisha kuwa yalitoka ofisi ya mkuu wa mkoa hakuna muhuri hakuna sahihi hakuna nembo hii ni hatari katika vita kubwa kama hii
Ma dealer wengi wanafahamika kwa a.k.a.!!!!
 
Kingine ni huo muswada wa sheria wa habari na ya makosa ya kwenye mtandao yanawanyima waandishi uhuru wa kuyafuatilia haya kwa kina kwani kesho yanaweza kuwageuka na kujikuta wako mahakamani kwa vikaratasi kama vivyo visivyo na nembo wala muhuri wala sahihi ya mkuu wa mkoa au chombo chochote rasmi cha serikali.
 
FB_IMG_1486804666464.jpg
 
Back
Top Bottom