Star Tv Kwa nini Namna Hii?

Star Tv Kwa nini Namna Hii?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,278
Mimi ni mtazamaji mzuri wa startv hasa saa za mchana. Kinachoniudhi
ni mtindo uliozuka hivi karibuni wa kurudiarudia vipindi fulani ambavyo havina
umuhimu wa kurudiwa kila siku.Vipindi hivyo ni:
1.Kilimo cha kahawa. Katika kipindi hiki wanaonekana wakulima wa kahawa Bw. Simplis Salakana
na Mama Nyaki wakilalamikia kilimo hiki.Kila siku mchana lazima waoneshe!
2.Ugumu wa uvuvi wa samaki mto Kilombero.Kila siku!
3. Matibabu ya mtoto wa jicho.
Nawauliza startv, hivi vipindi vina umuhimu gani wa kurudiwa kila siku? Mnachosha sana jamani,pengine hamjui hilo.
 
Hivi mkuu huna kazi au shughuli yoyote ya kufanya? acha kushinda kutwa home unaangalia tv naamini ukifanya hivyo hutawachukia StarTv.
 
Hivi mkuu huna kazi au shughuli yoyote ya kufanya? acha kushinda kutwa home unaangalia tv naamini ukifanya hivyo hutawachukia StarTv.
Koma kunipangia cha kufanya weee Sir Good. Muda wangu nautumia nitakavyo na ni haki yangu. Wewe ni nani kwangu kuniambia niache kuangalia tv mchana? Kama hujui nilichokilalamikia ungefanya la maana kusepa kama wafanyavyo watu wenye akili timamu wanaojua linalowahusu na lisilowahusu. Jifunze kukaa kimya!
 
Last edited by a moderator:
Eeeh, umekuwa Paul Kagame? ni ushauri tu mkuu kama nimekuudhi naomba nisamehe ila tambua kwamba hao waliokaa kimya ambao wewe unawaona wana akili wamekudharau ndiyo maana wamekupotezea baada ya kuona umeandika pumba!
 
Kama unapenda kushauri watu, jifunze namna zake. Ulioniambia sio ushauri bali ni kebehi Sir Good.
 
Last edited by a moderator:
Kama unapenda kushauri watu, jifunze namna zake. Ulioniambia sio ushauri bali ni kebehi Sir Good.
Basi nimekoma mkuu, sirudii tena naomba niwie radhi mkubwa mwenzangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom