Uchaguzi 2020 Star TV hamvitendei haki Vyama vya Upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu

KAYABOMBICHI

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
296
142
Kuelekea Uchaguzi Mkuu nimekua nikifuatilia matangazo ya taarifa za habari kwa vituo vyote vya TV za hapa nyumbani nakushangazwa na Kituo cha Television cha Star TV cha jijini Mwanza.

Kimekuwa na taarifa za upande mmoja zaidi kwa kuonyesha zaidi mikutano ya CCM lakini CHADEMA hawaoneshi kabisa labda litokee tukio negative kwao

Hii sii sawa kabisa nyinyi ni jicho la wananchi jifunzeni kwa ITV wako vizuri kwa kuonyesha kwa usawa kabisa vinginevyo mtapoteza mvuto kabisaaa
 
MKUU MI NAHISI WATU WANACHANGANYA MAMBO, STAR TV WALE WANARUSHA MIKUTANO NAHISI KWA KULIPWA NA SIO BURE
Au kama ni bure basi hawafanyi vizuri
 
Kwanza unatakiwa ujue, mmiliki wa hiyo media ni mwanaccm damu, then tambua hawawezi kushadidia chama tofauti na alicho mmiliki na mwisho media inapumulia mashine haina pesa so mpaka hapo unaweza kupata picha.
 
Wajielewe tu kua wao ni wafanyabiashara sio watoa huduma
Wataelewa baada ya uchaguzi. Nakumbuka uchaguzi uliopi
Baada ya uchaguzi ndio watatenda haki. Nakumbuka uchaguzi uliopita walikua wakionesha mikutano ya mgombea fulani mwanzo mwisho. Baadae naona walijitenga kanakwamba hakuendana na kasi hivyo naona waachwetu nimuda kidogo watajirudi
 
Kwanza unatakiwa ujue, mmiliki wa hiyo media ni mwanaccm damu, then tambua hawawezi kushadidia chama tofauti na alicho mmiliki na mwisho media inapumulia mashine haina pesa so mpaka hapo unaweza kupata picha.
Waliomfikisha hapo ni haohao kwanini asijifunze kwa ITV
 
Yes ITV nimewakuwabali sana mwanzo nilikuwa naangalia taarifa za AZAM nimekuta kuna upumbavu mwingi sijui wanashida gani lkn Itv Mabele makubi anaieleta habari kama ilivyo Safi sana
 
Bora vyama vingine kuliko Chadema

Chadema hawafai kuwepo hata na diwani moja
 
DQD2rzdWsAAeXHz.jpg


Anaitwa Anthony Mwandu Diallo, mwanachama wa CCM na mmiliki vituo kadhaa vya redio na television ikiwemo StarTV
 
Waliomfikisha hapo ni haohao kwanini asijifunze kwa ITV
Alikuwa anaweza kujifunza ila amechelewa ndiyo maana hana watangazaji wamemkimbia, unakuta mtangazaji mmoja anarudia vipindi zaidi ya vitani (5) kwa siku.
 
Start TV, Radio Free Africa & Kiss FM ni kutoka Sahara Media Group ya jijini Mwanza(Ilemela) ni vyombo vya Anthony Mwandu Diallo ambae mmiliki huyu ni CCM damu..
 
Kuelekea uchaguzi mkuu nimekua nikifuatilia matangazo ya taarifa za habari kwa vituo vyote vya Tv za hapa nyumbani nakushangazwa na kituo cha television cha Star tv cha jijini Mwanza kimekuwa na taarifa za upande mmoja zaidi kwa kuonyesha zaidi mikutano ya CCM lakini CHADEMA hawaoneshi kabisa labda litokee tukio negative kwao hii sii sawa kabisa nyinyi ni jicho la wananchi jifunzeni kwa ITV wako vizuri kwa kuonyesha kwa usawa kabisa vinginevyo mtapoteza mvuto kabisaaaa!!
Watavuna wanachopanda
 
Back
Top Bottom