Star times waache ubabaishaji

Star times waache ubabaishaji

mfereji

Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
13
Reaction score
1
Kwa muda sasa Star Times wanacheza mchezo mchafu. Stesheni za bure - yaani ITV, TBC, Star TV, EATV na Channel Ten zinaonekana vizuri kwa muda mfupi na kuanza kuganda picha au kusikia sauti tu.Wakati hizi za bure hazionekani, zile station nyingine za nje zinaonekana vizuri bila tatizo lolote. Ina maana wanalazimisha wateja kulipia ili waone TV la sivyo ubaki na hizi zinazoganda! TCRA waingilie kati kwani tunanyanyaswa.. . . ,
 
Nimehama na kisimbuzi chao kutoka dar kufika moro akifanyi kazi nawapigia huduma kwamteja wanasema natakiwa kununua kifurushi cha elfu sitini ili kiwe activated! Nimekiweka tu nyumbani naangalia tu cd ..ingekuwa makaratasi ningefungia maandazi...
 
Pole mkuu, hata hicho unaweza kukigeuza kuwa toy la kuchezea mtoto.

Mimi kisimbusi changu kilianza na kujipandisha na kushusha sauti chenyewe mpaka nikahisi labda nyumbani kwangu kuna wachawi. Wakati mwingine kinajibadili stesheni chenyewe nikakimwagia maji ya baraka wapiii...ikabidi nitafute cha Bakhresa - Azam tv
 
Kwa muda sasa Star Times wanacheza mchezo mchafu. Stesheni za bure - yaani ITV, TBC, Star TV, EATV na Channel Ten zinaonekana vizuri kwa muda mfupi na kuanza kuganda picha au kusikia sauti tu.Wakati hizi za bure hazionekani, zile station nyingine za nje zinaonekana vizuri bila tatizo lolote. Ina maana wanalazimisha wateja kulipia ili waone TV la sivyo ubaki na hizi zinazoganda! TCRA waingilie kati kwani tunanyanyaswa.. . . ,

Mkuu wakati mwingine ikiganda, we amisha Antena tu, itakua poa kabisa.

mi nina sehemu zaidi ya 20 tofauti tofauti, natumia ile ile antena ya ndani.
 
Mimi cha kwangu kinajizima na kujiwasha mda wote siwezi hata ona kitu, nimepeleka ofisi kwao wananambia ninunue kingine
 
Dah mkuu Mimi hilo limeaza karibuni inawiki sasa zinazingua kichizi
 
Kwa muda sasa Star Times wanacheza mchezo mchafu. Stesheni za bure - yaani ITV, TBC, Star TV, EATV na Channel Ten zinaonekana vizuri kwa muda mfupi na kuanza kuganda picha au kusikia sauti tu.Wakati hizi za bure hazionekani, zile station nyingine za nje zinaonekana vizuri bila tatizo lolote. Ina maana wanalazimisha wateja kulipia ili waone TV la sivyo ubaki na hizi zinazoganda! TCRA waingilie kati kwani tunanyanyaswa.. . . ,

habari yako Mfereji, sio kweli kuwa tunafanya hivyo, tatizo kubwa la chanel za ndani ni matatizo toka 'SOURCE' ya chanel husika, kiukweli kunabaadhi ya chanel za ndani tumekosa ushirikiano wa kutosha toka kwa wamiliki wa vyombo husika na hivyo kutulazimu kutumia njia nyingine mbadala kuzipata ili kuhakikisha zinapatikana kwa watanzania. Tunajitahidi sana kufanya kila linalowezekana ili kupatikana chanel hizo. kwa chanel za nje nyingi tunapata ushirikiano toka kwa wamiliki na hivyo hata 'SOURCE' ya chanel hizo kupatikana kirahisi.

hata hivyo pamoja na hayo yote chanel hizi za ndani muda mwingi zinakuwa zinaonekana vizuri kabisa, na nimara chache tu huwazinasumbua. endapo antena yako itakuwa inapokea mawimbi hafifu basi kunauwezekano mkubwa ukasababisha tatizo hili na kwa kuwa chanel zote za ndani zinaingia kwa frequency moja basi zote zitasumbua kwa pamoja.
 
Mimi cha kwangu kinajizima na kujiwasha mda wote siwezi hata ona kitu, nimepeleka ofisi kwao wananambia ninunue kingine

habari yako Wizzo, pole sana kwa tatizo, hilo ni tatizo dogo sana 'BOOTING' na linarekebishika ndani ya muda mfupi, tafadhari fika na king'amuzi chako katika ofisi zetu zilizokaribu nawe, na kama utapata majibu usiyoridhika nayo wasiliana na supervisor wa kituo husika au piga simu yetu moja kwa moja toa malalamiko yako 0764700800.
 
Halafu hivi we StarTimes Tanzania, tafsiri yenu ya mwezi ni nini?

Hebu acheni wizi, mtu unajiunga na scheme yenu ya 20,000/= hazipiti hata 20 days unakuta unaambiwa ufanye subscription....

Hebu jipangeni bana mnatukera
 
Last edited by a moderator:

Na hili la kutakiwa kununua kifurushi cha elfu sitini kuactivate kisa tu umehama mkoa mmoja kwenda mwingine unalizungumziaje?
 
Halafu hivi we StarTimes Tanzania, tafsiri yenu ya mwezi ni nini?

Hebu acheni wizi, mtu unajiunga na scheme yenu ya 20,000/= hazipiti hata 20 days unakuta unaambiwa ufanye subscription....

Hebu jipangeni bana mnatukera

habari yako Cathod Ray, tafadhari kama umelipia pia inatakiwa ubadilishe kifurushi, kunauwezekano ulikuwa unatumia kifurushi kikubwa na ulipofanya malipo ya 20000 hukubadilisha kifurushi na hivyo kuendelea kufurahia chanel za kifurushi kikubwa, hivyo pesa yako kuchajiwa kwa kifurushi husika
 
habari yako Peter, pole sana, je unaishi wapi na unatatizo gani? tafadhari wasiliana nasi tukupatie msaada, namba yetu ya huduma kwa wateja 0764700800

Haaa mm nimepiga simu jana hiyo namba nikawaambia tatizi langu wakaniambia napata shida ya jupata channel kwa sababu nimeweka waya mweusi. startimes cna hamu nao.
 
na mmetoa hata stesheni ya dtv mwenyewe nililipia ili nione mechi ila ovyo kabisa, mnaboa sana
 
habari yako Wizzo, pole sana kwa tatizo, hilo ni tatizo dogo sana 'BOOTING' na linarekebishika ndani ya muda mfupi, tafadhari fika na king'amuzi chako katika ofisi zetu zilizokaribu nawe, na kama utapata majibu usiyoridhika nayo wasiliana na supervisor wa kituo husika au piga simu yetu moja kwa moja toa malalamiko yako 0764700800.

Nimekwenda ofisini hapa Arusha wakanambia haifai kutengeneza eti ninunue kingine
 
Mimi cha kwangu kinajizima na kujiwasha mda wote siwezi hata ona kitu, nimepeleka ofisi kwao wananambia ninunue kingine
Mkuu wizzo inaonekana una dekoda ya continental na startimes pia zote za Terestrial, ungejaribu na dekoda ya satellite ulinganishe ubora wa picha.
Mi kwa mtazamo wangu picha bora zinapatikana kwenye dekoda za satellite kama zuku na azam.
Tatizo ni channel contents ambazo ina bidi uchangue wapi uende.
 
Suala lingine ktk star times kuna channels zingine hazionekani mpaka ulipie ikiwa pamoja na DTV.CTN.SIBUKA.wakati channels hizi zimo ktk orodha ya local channels. Tunahitaji maelezo tafadhari.
 
Mkuu hawa jamaa sijui wanamatatizo gani Mimi waliniimbia docoda ya star time toka mwaka Jana.nilienda kuripoti kwao wakanipa matumaini.itapatikana mpk Leo hii hamna kitu cjui zile zauwizi. Wanazifungua wanachukua pesa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom