Stanslaus Mabula: Nyamagana msirudie kuchagua wakimbizi

Stanslaus Mabula: Nyamagana msirudie kuchagua wakimbizi

kw
View attachment 320192

Akichangia hotuba ya Rais,Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula amesema kosa walilolifanya watu wa Nyamagana kwa miaka mitano ni kuchagua Mbunge mkimbizi ambaye hajui matatizo ya Jimbo lake kwa ugeni wake na ukaazi wake wa Kenya na Rorya

Hapo Mbunge mkimbizi aliyekuwa nalengwa ni Mh.Ezekia Wenje ambaye toka mwanzo wa uchaguzi wa 2010 na hizi za 2015 zilijawa na Ukabila na lugha za kibaguzi kuwa ni mtu wa Kenya na mjaruo wa Rorya hawezi kuja kuwaongoza wasukuma.

Hali hii imedhihirishwa na Mbunge wa sasa wa Nyamagana ambaye aliamua kutoa kauli hiyo ya kibaguzi ndani ya bunge.Tabia hii ya siasa za kibaguzi zilitawala sana ktk uchaguzi wa wabunge ktk Mkoa wa Mwanza,ambapo hata baada ya uchaguzi huo kuisha bado zinaendelezwa.

Tukemee mbegu hizi za ubaguzi wa kikabila ktk siasa za bunge na nje ya bunge.
kwanza tuanze na wale nyumbu waliogeuka nyuzi 180 kufuata nini 'kabila yetu bwana' halafu kuna wale wamangi wanajidai eti wanajitambua wakati ni ukabila mtupu.
 
Sasa si aende akawasaidie uhamiaji kutumbua jipu na ushaidi anao kwamba Wenje ni mkimbizi ?
 
Aina ya mbunge ndio picha halisi na uelewa wa Watu wa eneo Husika waliomchagua...
 
Mabula mwenyewe japo ni msukuma lakini si mzaliwa wa Nyamagana kama alivyo Wenje. Mabula ni mzaliwa wa Busega mkoani Simiu , hivyo hata yeye ni mgeni pia kama alivyokuwa Wenje ambaye ni mzaliwa wa Rorya mkoani Mara

Mwanza jiji limeshavuka siasa za ukabila ni kama ilivyo Dar huwezii kusema mbunge mpaka awe Mzaramo . CCM chezeni siaSa zisizo za kibaguzi kwani waTz tunategemeana. Ajabu kubwa mtu akigombea kwa tiketi ya CCM hata akiwa Mhindi, Mwarabu Chotara etc ataonekana KADA & MZALENDO. Kosa ni pale anapogombea ktk vyama vingine ataanza kuulizwa kabila na dini yake.

Mabula anajua vizuri bila magari ya deraya na curfew ya kijeshi asingepita. Kama anadhani anaweza kumshinda wenje kuwe na fair by election aone
''
Mwanza jiji limeshavuka siasa za ukabila ni kama ilivyo Dar huwezii kusema mbunge mpaka awe Mzaramo''
Uko sahihi mkuu.. ila kwa Moshi na Monduli naona bado..Hata Rorya nako bado..lazima uulizwe unatoka wapi.
 
Kaka nililinganisha jiji na jiji sasa we unapolinganisha majimbo yayohusisha na vijiji e.g. Rorya na Monduli ulinganishe na Mwanza (nyamagana) ni vitu viwili tofauti na ndio maana hata Mabula amechaguliwa pamoja na kuwa naye ni mgeni Mwz.
 
Kwa sasa siyo rahisi kutokana na utawala wa ukoo wa ccm unaomilikiwa na uvccm umeshaanza kutupeleka siko wazee wao wameshachoka kila linalotamkwa kwao ni kicheko ndiyo maana sasa hivi hawaheshimu hata wazee wao katika akili za kawaida Mh. Karume na Membe ni wa kukejeliwa wajitathmini
 
Haingii akilini kumuita mwenzio mkimbizi ili hali anaishi akiwa ni raia na si kwa vibali maalum. Siasa km hizi zitaisha lini Tz?! Ndo maana Wazungu wanatumonitor kwa kila kitu kwa kutuona hatujitambui. Wao wakiisha maliza uchaguzi basi ni kujenga nchi. Sisi tunamaliza uchaguzi majungu ndo yanaanza.
mmezoea kilakitu kutolea mfano wazungu,yani hata la ubaguzi unawatolea mfano kwamba wao hawana ubaguzi na kukosoana?
tabia ya kusifusifu wazungu kilajambo yanikera Sana.
kwa taarifa yako sisi Ni wastaarabu kuliko wazungu na maserayao ya ushoga
ndowale walisemwa majuzi mitandaoni,kunavitabia vya ubaguzi na kujititimua kwawengi wao. tizama hata mb.wa geita (msu...) yaani hana lolote lakini ana dhihaka za kuudhi.wajifunze uungwana bhana
 
Sidhani km umenielewa ni nini nilichokitolea mfano!! Mimi nimetolea mfano siasa zao baada ya uchaguzi hakuna tena yale madongo km kipindi cha kampeni..mara huyu mkimbizi sijui huyu nani! Kuhusu ushoga it was none of my concern. Labda nikuulize tu, kwa nini unawachukia watu?
 
Wakati tunalaumiana wenyewe kwa wenyewe juu ya ukabila kwenye chaguzi na kadhalika tukumbuke pia kuwatupia lawama viongozi wa awamu tatu zilizopita ambao hawakuendeleza juhudi zikizofanywa na uingozi wa awamu ya kwanza. Moja ya kazi iliyofanywa kwa mafanikio ni kufifisha ukabila nchini. Leo hii mchagga na msukuma wako kila mkoa na wilaya kutokana na kazi ya kujaribu kufuta ukabila. Tunaomba kazi hiyo ianze upya ili tuondokane na ushamba huu wa ukabila.
 
View attachment 320192

Akichangia hotuba ya Rais,Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula amesema kosa walilolifanya watu wa Nyamagana kwa miaka mitano ni kuchagua Mbunge mkimbizi ambaye hajui matatizo ya Jimbo lake kwa ugeni wake na ukaazi wake wa Kenya na Rorya

Hapo Mbunge mkimbizi aliyekuwa nalengwa ni Mh.Ezekia Wenje ambaye toka mwanzo wa uchaguzi wa 2010 na hizi za 2015 zilijawa na Ukabila na lugha za kibaguzi kuwa ni mtu wa Kenya na mjaruo wa Rorya hawezi kuja kuwaongoza wasukuma.

Hali hii imedhihirishwa na Mbunge wa sasa wa Nyamagana ambaye aliamua kutoa kauli hiyo ya kibaguzi ndani ya bunge.Tabia hii ya siasa za kibaguzi zilitawala sana ktk uchaguzi wa wabunge ktk Mkoa wa Mwanza,ambapo hata baada ya uchaguzi huo kuisha bado zinaendelezwa.

Tukemee mbegu hizi za ubaguzi wa kikabila ktk siasa za bunge na nje ya bunge.
Uh mwenyewe nikikuangalia kama vile ni mtoto wa jirani zetu fulani waliotaka tugombane siku siyo nyingi...PM kazini!
 
Hili sasa gundu, MTU mchango wake wa kwanza Bungeni unakumbana na mashambulizi namna hii? Haijapata kutokea.
Na ukiona hata Lumumba boys wamegoma kutia timu walao kwa utetezi hata kidogo ujue kweli jamaa kachemsha.
Mabula, umechemsha bwana mdogo na hii i aonyesha umeingia vibaya
 
Sidhani km umenielewa ni nini nilichokitolea mfano!! Mimi nimetolea mfano siasa zao baada ya uchaguzi hakuna tena yale madongo km kipindi cha kampeni..mara huyu mkimbizi sijui huyu nani! Kuhusu ushoga it was none of my concern. Labda nikuulize tu, kwa nini unawachukia watu?
Kwasababu walituchukia kabla...nimesoma historia vizuri na sijapata mahali rohoni mwangu pa kusamehe uchafu wao...
vuta picha unapigwa viboko ukiwa mtupu,mbele ya familia yako huku wakimbaka mkeo na watoto Wako na upo nnchini mwako etikisa hujawafanyia kazi nahivyo umeshindwa lipa kodi!
ningumu Sana mm kumsifu mtuhuyu hata agundue njia ya paradiso
 
Walikuwa wakibaka? Hiyo sijawahi sikia. Hayo mengine ya viboko ni kweli lkn me nafikiri Saikolojia za watu kwa kipindi hicho zilijaa ukatili sana coz hata watemi nao ambao walikuwa ni waafrika wenzetu walitenda ukatili kiasi fulani kwa mfano watemi wa kikerewe walikuwa na mashamba ya miti yao, mti wa mtemi ulipokatwa haukutakiwa kuanguka chini bali kulikuwa na watu maalum ambao walilala chini ili mti uanguke juu yao!
 
Kwasababu walituchukia kabla...nimesoma historia vizuri na sijapata mahali rohoni mwangu pa kusamehe uchafu wao...
vuta picha unapigwa viboko ukiwa mtupu,mbele ya familia yako huku wakimbaka mkeo na watoto Wako na upo nnchini mwako etikisa hujawafanyia kazi nahivyo umeshindwa lipa kodi!
ningumu Sana mm kumsifu mtuhuyu hata agundue njia ya paradiso
Walikuwa wakibaka? Hiyo sijawahi sikia ila ya viboko sawa. Mi nafikiri watu wa zama hizo walijawa ukatili coz hata watemi waliokuwa ni waafrika wenzetu pia walitenda ukatili. Kwa mfano watemi wa kikerewe walikuwa na mashamba yao ya miti, mti wa mtemi ulipokatwa haukutakiwa kugusa ardhi hivyo kulikuwa watu maalum wakulala chini ili wadondokewe na mti wa mtemi uliokatwa.
 
Chochote anachoongea mbunge bungeni ana Kinga, huwezi kumfanya chochote kile

Naona watu wamelishikia BANGO issue ya Kubenea kuhusu shanga lakini serious issue kama hii tunatwanga tu twende.Lakini bado nitasema kama VIONGOZI ndani ya Bunge hii ni pamoja na wapinzani hawakumuonya akiwa ndani ya Bunge basi kama TAIFA tumekwsiha.

Hata kama anakinga lakini issue ya UBAGUZI ikiongelewa ndani ya BUNGE inaashiria nini?
 
Madaraka yanatafutwa mpaka Kwa ushoga na akina jeni musssooorooo sembuse ukabila

Hawa ni viongozi washamba na primitive kutoka kolomije na nchi tumewapa washamba na malimbukeni in zitto voice
 
Back
Top Bottom