Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,677
Akichangia hotuba ya Rais,Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula amesema kosa walilolifanya watu wa Nyamagana kwa miaka mitano ni kuchagua Mbunge mkimbizi ambaye hajui matatizo ya Jimbo lake kwa ugeni wake na ukaazi wake wa Kenya na Rorya
Hapo Mbunge mkimbizi aliyekuwa nalengwa ni Mh.Ezekia Wenje ambaye toka mwanzo wa uchaguzi wa 2010 na hizi za 2015 zilijawa na Ukabila na lugha za kibaguzi kuwa ni mtu wa Kenya na mjaruo wa Rorya hawezi kuja kuwaongoza wasukuma.
Hali hii imedhihirishwa na Mbunge wa sasa wa Nyamagana ambaye aliamua kutoa kauli hiyo ya kibaguzi ndani ya bunge.Tabia hii ya siasa za kibaguzi zilitawala sana ktk uchaguzi wa wabunge ktk Mkoa wa Mwanza,ambapo hata baada ya uchaguzi huo kuisha bado zinaendelezwa.
Tukemee mbegu hizi za ubaguzi wa kikabila ktk siasa za bunge na nje ya bunge.